Ufisadi ofisi za kilimo mifugo arusha

felista.

Member
Jul 4, 2011
8
0
Salamu! Nimekerwa na hii tabia ya baadhi Ya wateneaji au watu wenye mamlaka au dhamana iwe ni sehemu yoyote ya umma uliyokabidhiwa kuiendesha au kuisimamia halafu unaanza kuigeuza mradi binafsi hii ni aina ya ufisadi mdogo mdogo na unaoendelea kukua na ndio maana taifa letu halipati maendeleo, mfano ni mradi unaoendesha na ofisi ya kilimo mifugo mkoani arusha mradi huu ulibuniwa na wajanja flani kwa lengo la kujipatia fedha kutoka serekalini na kuziweka kwenye mifuko yao binafsi mradi huu wa ufugaji wa kuku, ngombe na samaki uliopo kwenye viwanja vya maonyesho ya kilimo nanenane njiro arusha unafaa uchunguzwe uanzishwaji wake na endeshaji wake kwani baadhi ya watendaji wa ofisi hiyo waliuanzisha wakijidae eti ni shamba darasa kwaajili ya kufundishia wafugaji lakini mwenendo wake sio hivyo. Mradi huo unapata fedha kutoka wizara ya mifugo kwaajili Kuuanzisha na kuuendesha na mradi huu una mazao kama samaki, mayai, maziwa pamoja na kuku ambayo huuzwa inabidi kujua fedha zinazotokana na mauzo ya mazao hayo zinaingia mfuko gani ilihali gharama za uendeshaji zinapatiwa pesa na wizara? Gharama hizo ni pamoja na ununuzi wa mifugo hiyo kama kuku samaki, ngombe, chakula cha mifugo hiyo, pamoja na ujenzi wa mabanda. Kukt hutaga na mayai huuzwa na kuku hao awamu xa kwanza walipozeeka waliuzwa kama nyama na ofisi ilipelekewa taarifa kuwa kuku hao wamekufa kwa ugonjwa na hapo walinunuliwa kuku wengine na mradi wa kuku unaendelea mayai yatauzwa na wakiishakoma watauzwa sijui kipindi hicho watasema wamekufa kwa ugonjwa tena, samaki nao mradi uliendelea na walipokuwa wakubwa waliuzwa na taarifa zilizopelekwa ofisini ni kuwa bwawa la samaki limebomoka na samaki wamekufa kitu ambacho sio cha kweli na sasa pesa zinaandaliwa kwaajili ya kukarabati bwawa pamoja na ununuzi wa samaki wengine tayari kwa mradi wa awamu ya pili. Ngombe walinunuliwa wakazaa maziwa yanauzwa fedha haijulikani inapokwenda ndama haijulikani walipo eti sijui kuna wakulima wanapewa ndama kwa mpango gani? Ngombe hao kuna siku utasikia walikufa kwa ugonjwa na watanunuliwa wengine. Mradi huu ni ufisadi nambari wani ni watu wamekaa wakafikiri jinsi ya kuchukua fedha zinazotolewa na wizara kwaajili ya maendeleo mbalimbali yanayohusu ufugaji na wafugaji ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo na kuwawezesha lakini imekuwa sivyo inaishia mikononi mwa watu najua hata wakipeleka report wizarani wanaitaja sehemu hiyo kama shamba darasa kwa wakulima / wafugaji lakini wenyewe wanajua jinsi inavyoingia matumboni mwao na fedha kutoka wizarani zikiendelea kuingia kwenye mfuko uliotoboka. Ombi langu kwa muheshimiwa waziri wizara ya mifugo chukunguza mradi huu juu ya haya niliyokueleza hapa na wizara yako isiishie kuletewa report ya uwepo wa shamba darasa linalonyonywa na hao wafanyakazi wa ofisi ya kilimo mifugo arusha na ujue haswa mapato yanayotokana na mradi huo yanaenda wapi na je gharama zilizowekweza zinaendana na zilizoandikwa kwenye riport kama ujenzi wa mabanda n.k gharama za uendeshaji na faida inayopatikana kwa kuwepo na mradi kama huo usiishie kudanganywa kuwa wanatoa mafunzo kwa wakulima kumbe wanashibisha matumbo yao. Naomba hili lifanyiwe kazi sio na waziri tu bali wizara nzima pamoja na serekali kuu na serekali ya mkoa, pamoja na wapenda maendeleo na wote wenye mapenzi mema na nchi hii bila kusahau makamanda wa kupigana na ufisadi wakiwemo vyama vya upinzani na mbunge wa arusha.nitakuja tena kuendelea na mradi mwingine unaobuniwa na ofisi hiyo wa kifisadi hivyo hivyo pamoja na miradi mingine mbalimbali ya ofisi na taasisi mbalimbali.
 
Back
Top Bottom