Ufisadi mwingine huu ndani ya serikali yetu ya tanzania

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,235
4,949
Jamani hivi mnajua kua ukimwalika Mkuu wa mkoa, Waziri, Mkuu wa wilaya au kiongozi yeyote serikalini aje kufungua Mkutano, warsha, semina au mafunzo Unamlipa hela.
1. unamlipa full perdiem kama vile ameenda kikazi nje ya kituo chake cha kazi,
2. unamlipa hela ya kufungulia mkutano au hiyo shughuli uliyoiandaa
3. unamlipa hela ya mafuta ya gari alilotumia kuja nalo
4. unamlipa na dereva wake
5. Hotuba anayokuja kuisoma wakati wa kufungua hiyo semina unaiandaa wewe uliyemualika
Sasa kinachotokea akifika hapo anaisoma hiyo hotuba akimaliza kuisoma anawatakieni semina njema then anachukua hela zake anarudi Ofisin kwake kuendelea na shughuli zake zingine
Hii ndo hali halisi tunayokutana nayo
 
Unalijua leo hilo suala?
Jamani taratibu. Inamaana unamkodi kiongozi sawa na jinsi utakavyokodi viti vya plastiki ukiwa na ugeni eeh???
Kumbe ndio maana wengi wao wanadharaulika na matajiri kualikwa hadi kwenye vi-bethidei vya vichanga kumbe hakuna cha bure hapo, duu haki ya kweli!!

Serikali ya MISHENTAUNI hao.
 
Jamani hivi mnajua kua ukimwalika Mkuu wa mkoa, Waziri, Mkuu wa wilaya au kiongozi yeyote serikalini aje kufungua Mkutano, warsha, semina au mafunzo Unamlipa hela.
1. unamlipa full perdiem kama vile ameenda kikazi nje ya kituo chake cha kazi,
2. unamlipa hela ya kufungulia mkutano au hiyo shughuli uliyoiandaa
3. unamlipa hela ya mafuta ya gari alilotumia kuja nalo
4. unamlipa na dereva wake
5. Hotuba anayokuja kuisoma wakati wa kufungua hiyo semina unaiandaa wewe uliyemualika
Sasa kinachotokea akifika hapo anaisoma hiyo hotuba akimaliza kuisoma anawatakieni semina njema then anachukua hela zake anarudi Ofisin kwake kuendelea na shughuli zake zingine
Hii ndo hali halisi tunayokutana nayo

Kabila ulichoeleza hapa ni kweli tupu! Swali! Je kuna stahili yeyote kwa watu hawa kulipwa hizo pesa? Tena kibaya zadi hili halijalishi kama wamealikwa ktk shuguli ya kiserikali au za kibinafsi. Nafikiri kuna haja ya kuangalia upya swala la kualika viongozi kufungua/kufunga semina na makongamano kama lina value yeyeto maana wengi utafuta publicity tu kuwa waziri fulani kafungua kikao fulani hivyo kuleta fikra fulani kuwa kikao hicho ni muhimu. Binafsi hii ni moja ya aina nyingi tu za ufujaji wa mali za umma.
 
Binafsi nilikuwa sijui. Ila siku nikimwalika na akanidai simlipi ng'o!!! Najua dawa ya serikali isiyo na masikio ni ukorofi tu. Tunawabembeleza ndo maana. Kama tunawakodi hizo fedha zinaingia serikalini au wanakula wenyewe. Kama wameacha kazi ni za serikali si kazi zao. Wangesema tuilipe serikali hapo sawa lakini kusema kwamba tumlipe mtu anayelipwa kwa kuwa ofisini huu ni ulimbukeni kabisaaa!!! Watanzania hatuna akili ndo maana tunakubaliana na upuuzi wa kila aina.:disapointed:
 
that is the way it has been, nashangaa kumbe kuna watu hawalielewi hili. Tukiwaambia hii nchi imeshachafuliwa na CCM mnaishia kututukana na kutuona ni wavunjifu wa amani tu.
 
Unalijua leo hilo suala?

Nimelijua hivi karibuni baada ya kuanza kuwaalika hao vigogo. Nimeshuhudia sehemu nyingine kwa siku kiongozi mmoja anenda kufungua mikutano minne kwa siku moja na hasa hizi semina za Afya maana hizi ni kila siku
 
Watanzania vilaza kwenye kila kitu, someni majarida na magazeti yenye kuongeza knowledge na sio magazeti ya ngono.
Wapi ulisoma kazi ya waziri mkuu au waziri yoyote wa serikali ni kufungua seminars?????? Na jingine semina ufanye wewe halafu akulipie nani??????
Shame on you people, fyi hizi ni taratibu za kawaida nchi sote na sio hata rais.
 
Ndio maana wakialikwa kwenye harambee za kuchangia maendeleo hutoa sababu nyingi zisizo za msingi za kutohudhuria kwa kuwa wamezoea vya bure.SHAME ON THEM!!!
 
Nimelijua hivi karibuni baada ya kuanza kuwaalika hao vigogo. Nimeshuhudia sehemu nyingine kwa siku kiongozi mmoja anenda kufungua mikutano minne kwa siku moja na hasa hizi semina za Afya maana hizi ni kila siku

Bora kama fedha hizo wanazo lipwa zinaingia serikalini maana wanatumia mda wa serikali kufanya shughuli binafsi
 
Inamaana hawa viongozi hawana Mishahara au??????? Wanafanya kazi kama MAEZEKI???????? Hii nchi hii?????
 
Watanzania vilaza kwenye kila kitu, someni majarida na magazeti yenye kuongeza knowledge na sio magazeti ya ngono.
Wapi ulisoma kazi ya waziri mkuu au waziri yoyote wa serikali ni kufungua seminars?????? Na jingine semina ufanye wewe halafu akulipie nani??????
Shame on you people, fyi hizi ni taratibu za kawaida nchi sote na sio hata rais.

Sasa kama sio kazi zao wanaachaje kazi za serikali na kwenda kutafuta per diem hizo? Waende basi siku zisizo za kazi na wasiende na magari ya serikali. wala wasiandike magazetini "waziri ...... kafungua tamasha, sermina au mkutano". Kutumia tu jina la ofisi kwa manufaa ya mtu binafsi ni ufisadi. Soma wewe habari za nchi zingine wanavyofanya uelimike. Juzi amehukumiwa kifungo engineer USA kwa kutoa ushauri wa kiufundi kwa China kwa manufaa yake binafsi wakati akiwa ndani ya kiapo. Tena alifanya kazi hiyo kwa wakati wake.

Hizo nchi unazozisema zinafanya kama wewe ni zipi kama sio ........., na sehemu zote zenye uozo kama wa kwetu.

Kwa taarifa yako, nchi zilizoendelea ukipewa gazi la kazi huruhusiwi kufanyia kazi zako za nyumbani kama vile kukupeleka kazini na kukurudisha nyumbani, kuwapeleka watoto wako shuleni, kukupeleka sokoni, au kumpa lift mpenzi au rafiki yako.

Sasa kwetu tunafanyaje: Gari za serikali zinawapeleka watu kwenye disko, semina, harusi, kanisani, misikitini, nyumbani, n.k. mradi tu uweke mafuta yako na wakati mwingine mnaiba mafuta ya serikali.

Mnatumia vyeo vyenu vibaya. Rais akiitwa kwenye birthday na akaenda pamoja na vyeo na mali za serikali ukijumuisha na watumishi wa serikali, ujue ameenda kikazi. kama sio kikazi aache mali zote za serikali na vyeo vyake. aende mwenyewe.

Hata wewe ukialikwa kwenda kufungua kongamano, usiende na VX au sijui gari gani ulilopewa, nenda mwenyewe na waambie umeenda kama wewe. sio waziri. Waziri kweli unaweza kupewa per diem na mwananchi! huu ni ufisadi. Sasa polisi na makarani ambao hawatakaa waitwe kufungua hizo washa watafanyaje? si wataishia kuomba rushwa na kujiunga na majambazi?

Ndio maana hawa jamaa hawaoni maisha yakiwa magumu. akiitwa birthday, sermina, washa, matembezi ya hisani, nk wanalipwa vizuri na mishahara yao haiguswi. Hawa sio wenzetu. Hata kama marekani na uchina, au ulaya wanafanya, haimaanishi kuwa ni kitendo kizuri. Haya marekani wameruhusu ushoga, kwa hiyo na wewe umekuwa shoga kwa vile nchi zingine zimeruhusu? Tuambie
 
Na akitoka ofisini anachukua zingine za serikali kwa dhumuni hilohilo

Sasa wakati unampa hizo hela ikaonekana imepungua kama sh 500 ndo utakapoona ukali wake.
Kwa wasiojua kufungulia kikao ni sh 100,000, na perdiem ni sh120,000
na anaweza akatumia kama dk 10 tu kazi ikawa imeisha
 
Ndio maana wazungu wanatufananisha na nyani
jamani hivi mnajua kua ukimwalika mkuu wa mkoa, waziri, mkuu wa wilaya au kiongozi yeyote serikalini aje kufungua mkutano, warsha, semina au mafunzo unamlipa hela.
1. Unamlipa full perdiem kama vile ameenda kikazi nje ya kituo chake cha kazi,
2. Unamlipa hela ya kufungulia mkutano au hiyo shughuli uliyoiandaa
3. Unamlipa hela ya mafuta ya gari alilotumia kuja nalo
4. Unamlipa na dereva wake
5. Hotuba anayokuja kuisoma wakati wa kufungua hiyo semina unaiandaa wewe uliyemualika
sasa kinachotokea akifika hapo anaisoma hiyo hotuba akimaliza kuisoma anawatakieni semina njema then anachukua hela zake anarudi ofisin kwake kuendelea na shughuli zake zingine
hii ndo hali halisi tunayokutana nayo
 
Hili ni tatizo na ni tatizo pana kuliko linavyoonekana.
Mambo kama haya ndio yanawavnja vijana moyo wa kujitolea.
Ila kuna jambo moja inabidi tuligusie hapa. Hizi warsha nyingi ziko kiulaji tu. Wala haziko kwa ajili ya capacity building etc. Kila mshiriki wa warsha hulipwa. Sasa kama washiriki wengine wote wamelipwa, waandaaji hujisikia nafsi zao zikijisuta kutokuwalipa wageni rasmi kwa sababu hata wao waandaaji wako kiulaji zaidi.
Tujnge utamaduni wa kuheshimu elimu. Nchi nyingine watu hulipa ada ili waweze kuudhuria warsha, hapa kwetu kukiwana warsha isiyolipa posho au inayolipa kidogo, wadau hawahudhurii! namna hii hatutafika popote.
 
Kinachosikitisha zaidi na kule serikalini anatoka na posho yake so anapata posho mara mbili...? Huu ni unyonyaji wa hali ya juu bila hata huruma ya kodi ya walalahoi wanaoumia usiku na mchana kutafuta mlo mmoja tu..!
 
Back
Top Bottom