Ufisadi mkubwa uuzwaji wa (UDA)

Lua

JF-Expert Member
May 19, 2011
704
305
katika uuzaji wa shirika la usafiri dar es salaam UDA, shirika hili limebinafsishwa kwa kampuni ya Simon Group Limited kwa bei ya kutupwa ya shilingi milioni 285 badala ya shilingi bilioni 1.4. Kibaya zaidi , shirika hilo limebinafsishwa kwa kampuni hiyo bila ya kuwashirikisha wanahisa kwa sababu zisizojulikana.

Wanahisa wa shirika hilo linalokadiriwa kuwa na mtaji wa sh bilioni 12, ni jiji la DSM 24.5%, serikali 23% na asilimia 52.5 zimechukuliwa na mwekezaji mpya ambaye ni Simon Group Limited. Ambapo katika suala zima la ufisadi huo Mbunge wa Ubungo Mh: John Mnyika aliweza kuhoji zaidi juu ya uhalali wa mkataba huo kwani wakati unaingiwa haujawashirikisha baraza la madiwani wa jiji kwani wao ndio wadau wakuu wa shirika hilo.
 
simon group ni mali ya fisadi chipukizi riziwan kikwete

ila kuna mtu kampandikiza pale
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom