TANleaks imepata taarifa za wazi zenye uthibitisho kuwa mradi wa uwekezaji uliopo Nairobi uliopaswa kufadhiliwa na NSSF umesimama. Kusimama kwa mradi huo kunatokana na NSSF kukataa kutoa fedha sambamba na kile unachoweza kukiita cha juu (rushwa) kwa mmoja wa vigogo waliopo Wizara ya Mambo ya Nje. Kugoma huko kwa NSSF kumesababisha sasa mazungumzo mapya yaanze safari hii yakifanyika kupitia mfuko mwingine wa hifadhi PPF ambao huo unaelezwa kuwa na viongozi ambao wako karibu na wahusika wa kuchonga deal ambayo ni makampuni ya ujenzi sambamba na lile la consultancy. Kufuatia kushindikana nchini Kenya, mazungumzo ya sasa yanalenga mradi huo kuhamishiwa nchini Msumbiji. Kuhamishiwa ujenzi huo Msumbiji kunatokana na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji kuwa na ushirikiano na makampuni hayo ambayo yanatajwa kuwa ndiyo hutumika kupiga deal za wizara ya Mambo ya Nje, na pia Balozi huyo wa Tanzania nchini Msumbiji ameonyesha ushirikiano wa kutoa pacenti inayotakiwa kama mradi huo utapitishiwa mkononi mwake. Balozi huyo swahiba wa Waziri wa Mambo ya nje, pia ana uhusiano wa karibu wa mabosi wa PPF, hali inayoashiria kuwa deal hili litapita kirahisi.
Taarifa zetu zinaeleza makampuni yanayofahamika kwa upigaji deal MOFA ya Tanzania ni QD Consults na Undi Engineering. Makampuni haya sasa yanasubiri kwa hamuBalozi wa Tanzania Msumbiji kukamilisha hatua za kazi ya ujenzi kuhamia Maputo, baada ya Balzoi wa Tanzania nchini Kenya kuwawekea ngumu. Taarifa zetu pia zinaeleza kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya hadi kuweka ngumu kunatokana na kunuswa sikio na kigogo mmoja wa NSSF ambaye alimtahadharishwa juu ya ushirika wa makampuni hayo mawili QD na UNDI na mpango wao wa kuchota fedha kwa ajili ya KIGOGO wa wizara ya Mambo ya Nje. Mtoa taarifa huyo kwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya alimhakikishia Balozi wetu huyu Mzalendo kuwa, kama atakubaliana na deal hili wao NSSF wameshalistukia na hawako tayari kutoa fedha na kama wataleta fedha kutoka eneo jingine akumbuke yaliyomkuta Balozi Mahalu. Balozi wetu Mzalendo baada ya kuona deal hili ni chungu huku akihakikishiwa kuwa makampuni hayo yamekuwa yakitumika kukusanya fedha zinazowekwa sehemu fulani aliamua kukataa mradi huo, hali iliyoufanya kusimama hadi sasa mjini Nairobi. Mkakati uliobakia inaelezwa kuwa ni huu wa kuuhamishia mradi nchini Msumbiji na kazi inafanyika kwa uharaka sana.