Ufisadi:mfumo Mpya Wa Maisha Ya Binadamu?

Augustoons

JF-Expert Member
Oct 31, 2007
409
30
Tunasoma katika historia ya mwanadamu kuwa amepitia katika vipindi vikuu vitano vya maisha vinavyoitwa mifumo au modes of production.Mfumo wa kwanza kabisa unaitwa primitive communalism(ujima) mfumo wa pili unaitwa ukabaila(feudalism) na mfumo wa tatu unaitwa utumwa(slavery) na mfumo wa nne unaitwa ubepari(capitalism) ambao msingi wake ni mtaji yaani capital,na mfumo wa tano ni ujamaa(socialism) ambao msingi wake ni utu na usawa wa binadamu,wenzetu warusi walienda mbali zaidi na kuunda mfumo wao ambao unaitwa ujamaa uliokomaa(communism) ambao hata hivyo haukufua dafu mbele ya ubepari japo bado vipande vyake vipi.

Kwa sisi waafrika mifumo yetu miuwa ilikuwa african socialism na huo ujima,lakini badala ya sisi kuamua kwenda kwenye ubepari moja kwa moja au ujamaa uliokithiri tumeunda mfumo mpya wa maisha uitwao Ufisadihata sijui kwa kiingereza neno sahihi ni lipi maana unainclude egoism,corruption,embellezlement,nk.
Mfumo huu ni mbaya kabisa na hatari zaidi duniani,ni hatari hata kuliko ubepari wenyewe.Kwani ubepari wenyewe hauna egoism sana kama huu mfumo wetu sasa.Na kwakuwa umeshakuwa mfumo basi kila mtu ameambukizwa mfumo huu sio sisi wana jf tunaojadili hapa wala hao viongozi na watu mbalimbali tunaowajadili hapa.wote ni mafisadi katika level moja au nyingine.Tinachotofautiana hapa ni degree ya huo ufisadi ambao mimi huita degree of chumpability,that all human beings are chumperble but we differ in te degree of chumperbility
Usiniulize hiyo lugha ina maana gani,tafakari message yangu na kama utatafakari kwa kina sana utagundua namaanisha nini ila ukidandia gari kwa mbele waweza jikuta unajadili usichokijua.Nasema huu mfumo umeathiri watanzania kiasi kwamba hata watoto wanaozaliwa wanavuviwa ufisadi.Maana mtoto anazaliwa katika mazingira ya ufisadi,anahudumiwa katika mazingira ya ufisadi hadi anakua mkubwa.Kutokana na mfumo huu mtu anajifunza kutoa rushwa akiwa chekechea,kwani akitaka kuwahi shue lazima atoe rushwa ili awahi,na kila huduma.Sio kwamba anapenda bali mfumo unamlazimisha kwa kuwa ndio njia ya maisha.Inashangaza sana kuona hata wanafunzi wa shule za msingi kwa sasa wanawafuata walimu wanawabembeleza kuwaongezea maksi,au kuwashawishi kupitia alama za miili yao(paralinguistic features),sasa kisheria hakuna kitu kinachoenda bure,kilatini tunasema quid pro quoyaani kwa kiiingereza nothing goes for nothing.Mwalimu naye hawezi kutoa maksi bure atataka kulipwa in kindambapo ni moja ya malipo yaliyokuwepo kwenye mfumo wa ukabaila.In kind kwa sasa maana yake ngono,lakini awapo mwanaume atalipa in cash,ambayo pia ni mfumo wa maisha ya ukabaila.Kwani mwalimu huyu huenda kwake hela si shida sana,sasa akimwambia demu huyo ampe laki moja ni wazi atashindwa njia ilobaki ni ngono basi.Hivi ndivyo tunavyoanza kuharibika.
mfumo huu hauishii hapo unaenda hadi kwenye shule za sekondari,high schools, na vyuo vikuu.Siku hizi hata kugombea uhead prefect tu lazima uwe na kampeinazi ambao lazima uwalipe na uwaahidi feva ukiingia madarakani.Humo DARUSO na serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu ambao tunawategemea waje kuwa viongozi wetu waadilifu tena na wao wenyewe wanaongoza maandamano kupinga ufisadi kuna ufisadi kibao.Hivyo nachokiona sasa ni kulalamikiana kwamba aah bwana wewe umechukua kingi kuliko mimi haiwezekani rudhisha bwana.Kila mtu anapiga debe bovu mwenzie atoke aingie yeye naye aibe aende.Huo ndio mfumo tulionao sasa.
Kwa mantiki hii hakuna mtu msafi serikalini wala walionje ya serikali bali waliopo wana afadhali kidogo kuliko hao wa serikalini.Msingi mkubwa wa mfumo huu wa ufisadi ulipo sasa ni mtaka cha uvunguni sharti ainame

Kwa mantiki hiyo kila mtu akijichunguza hapa jf hata kama dhamiri yake inamsuta atagundua kwamba katika hali moja au nyingine katika maisha yake amewahi kutoa ama kuomba rushwa ama upendelea fulani.Si kwakuwa anapenda kwakuwa tu alilazimishwa na mazingira.Huyo mbowe tunayemjadili hapa ndio ni mtu mahiri lakini si msafi kwa 100% wala kiongozi yeyote tutakayempigia debe hapa hatakuwa 100% pure.Analau basi tupate wale ambao tukiwarate watapata above 75% hapo ndio tutakuwa tumefikia lengo.

Lakini kikubwa nani katufikisha hapa? hili wala sio la kubishaniwa ni baba mwenye nyumba,na ninaposema baba mwenye nyumba sio jk namaanisha chama kinachotawala.Kwakuwa hicho ndicho chenye dhamana ya kushikilia mfumo wa nchi na kuandaa sera,basi kinawajibika moja kwa moa na hali hii na pia kama wakikubali hili wao wenyewe pia wanawajibika kutuondoa hapa tulipo.Kama wanayo nia wanaweza kama hawana hata watawale miaka 200 ijayo hatutafika popote.Imefikia hatua serikali zetu za kiafrika kwa sasa ni hatari kuliko hata ukoloni.Adui yetu mkubwa kwa sasa sio IMF wala WORLD BANK ni serikali zetu ambazo.World bank sawa watatupa dola milioni mia moja tujenge daraja na masharti magumu na riba ya kurudisha lakini pamoja na hayo tukishapokea huko kwenye daraja nangurukuru zitafika milioni ishirini.Je,hapa tuwalaumu world bank?

Ukitaka kujua ufisadi ni mfumo basi test ni ndogo sana ni hii hapa,leo teuliwa kuwa waziri kaa miaka kumi afu usijenge nyumba ya maana jenga bangaloo moja tu linaloendana na mshahara wako na nunua kasuzuki kamoja kakutembelea baada ya kuacha uwaziri.Watu watakucheka watakwambia mmh lile ndo jinga kweli yaani limekaaa pale kisimani limeshindwa kuchota pesa na ona sasa si bora angekuwa mkuu wa shule ya msingi tu.What does that mean,we everuday encourage people who go to power to continue with maladministration na ufisadi.

Naomba kuwasilisha hoja
 
Back
Top Bottom