UFISADI Kila Kona: Baraka za CCM KINGA ya Ufisadi BoT na Viongozi Mafisadi

Baada ya habari za kifisafi kuenea kila kona na hata kuonyesha kwamba CCM na Serikali walitumia pesa za wananchi kuwapa wabunge wao Ubunge leo naelewa kwa nini kila mara ni watiifu kwa CCM na hasa EL akiwaita sirini na kurudi Bungeni wakiwa wana CCM na si Bunge la Nchi tena .

Wabunge wa CCM wako bungeni kwa maslahi yao binafsi, sio kwa maslahi ya wananchi waliowachagua. Vitendo vyao vinadhihirisha hivyo.
 
Wacha wale basi lakini yale ya Kenya hayako mbali.Mawasiliano sasa yapo na mwaka 2010 hakutakuwa na kulala.
 
Kuna wakati huwa nakaribia kukata tamaa ila nikisoma maandishi ya vichwa makini kama hiki basi nafarijika kuwa kuna watanzania wanaweza kuona moto katikati ya ukungu mzito wa theluji.

CCM ndio mhimili mkubwa wa matatizo yote hapa. Wabunge wa CCM wapo tu kama hawapo na wengi wao wamelala usingizi pono kama vile hawajui kinachoendelea. Wanaojaribu kusema kidogo wanaitwa kwenye vikao vya chama na mzee wa kasungura na ndege ya kupaa ya richmonduli na kufungwa midomo.

CCM inabidi waondolewe na wajengewe gereza lao la kiguantanamo kule ukara katikati ya ziwa victoria ili mzimu huu ututoke. Kama vijana nao (kina Lugaza) wameanza kuingia kwa kasi katika hii list ya kifisadi? kama watoto wa mafisadi Ridhiwani na January nao sasa ni part ya serikali hii ya kifisadi? Kama watoto wa wakubwa ndio wanajazwa BOT kulinda siri za kifisadi? Hii nchi inabidi kitu kikubwa sana kifanyike kuvunja hii circle.


only thing we have to fear is fear itself
Tamko hilo la Roosevelt la “ogopa woga kwa moyo wako wote” Leo hii katika sanyansi na dhana mpya kabisa (1998/2000) ya kutathmini Ustawi wa jamii Emotional Intelligence (EI) au Ukomavu wa utu linachambuliwa hivi;

WOGA unatizamwa katika njia tofauti kabisa na ile inayofahamika kwenye Psychology na psychiatry. Woga, wasiwasi na Mashaka, (negative emotions/hisiahasi) vinaweza kutumiwa kama nguvu maalum ya kusaliti ustawi wa jamii iliyopevuka na kujitawala kiuchumi na kibinadamu. Mnapokuwa kwenye kundi na mkashituliwa na "Mbwa makali…" yule atakaye zalisha au kusambaza woga zaidi ya wenzake ndiye atakaye kuwa wa kwanza kuwa kitoweo cha mnyama huyo mkali. fuatilia. http://www.duniahai.com/Uharibifu wa Hisia Hasi.html
Atakaye zalisha woga zaidi atashambiliwa, atakuwa mnyonge na atakaye fedheheshwa na mnyama huyo. Atajulikana kama “With low EI”. Yaani aliye duni katika kuerevuka kihisia. Ili kuelewa vizuri dhana hii , Kwenye neno mbwa liondoe na weka neno FISADI, ndipo utelewa vema Roosevelt anasema nini. Yaani fisadi akutishe kwa kukumwagia tindikali usoni na wewe utishike, fisadi akutishe na wewe uogope pale anaponyofoa vipengele muhimu kwenye maagano, maazimio na nyaraka muhimu za kitaifa. Fisadi atoe tafsiri za kifisadi za kitu kama azimo la Arusha na wewe ukae kimya unatetemeka kwa woga! Hakika Fisadi atakufanya kitoweo muafaka. Atatafuna jamii nzima kupitia kodi za walalahoi zilizoko bank kuu, mikataba hovyo ya uchumi wa taifa, miradi muhimu ya kitaifa, kuyumbisha makusudi dira ya taifa kwa faida yake etc. Lakini yote haya ni kwa kuwa mwananchi kajitakia mwenyewe ;kawa mkarimu wa woga tu kwa fisadi. Kimsingi Kama wewe ni Mtanzania wa kweli: Kamwe Usimuogope fisadi. Hasa unapopigania na kutetea haki ya wanyonge waliowengi. “Milele usimwezeshe Fisadi” kwa Hisia hasi! Erevuka kuhusu hisa zako sasa!Na uziwajibikie.

Woga na hisia hasi anasema Roosvelt havituwezeshe kamwe kusonga mbele na kujitokeza kutetea taifa kwa kusema Ukweli kama Ulivyo mioyoni mwetu au kama tunavyoujua na kuuamini.”This is preeminently the time to speak the truth, the whole truth, frankly and boldly. Nor need we shrink from honestly facing conditions in our country today. This great Nation will endure as it has endured, will revive and will prosper. So, first of all, let me assert my firm belief that the only thing we have to fear is fear itself”

Shime tumnyime Fisadi kile anachotaka kutoka kwetu “ngvu ya hisia hasi”. Bila sisi kumpa woga, wasiwasi, unyonge na kunywea hovyo mbele yake, fisadi hana Nguvu peke yake ya kutunyonya nakutufanyia michezo inayoendelea sasahivi ndani ya taifa letu!

Bila kumpa Mbwa woga , anauweka mkia sehemu inayostahili .. katikati ya miguu yake na kurudi alipotoka kwa unyonge mkubwa. Huo unakuwa ni ujembe tosha kwa Fisadi wa aina yeyote toka kwa wale anaowafisadi. Maana anajua Nguvu ya fikra toka kwa Mtanzania asiye ujua woga wa kijinga. Fikra Pevu zilizojikita kwenye kiwango cha juu cha EI sio IT; Ni silaha tosha ambayo inaweza kumtingisha fisadi na kufuatiwa na hatua ACTION NOW!!!Ambazo lazima... , lazima Zitakuwa Productive!!
 
Kuna wakati huwa nakaribia kukata tamaa ila nikisoma maandishi ya vichwa makini kama hiki basi nafarijika kuwa kuna watanzania wanaweza kuona moto katikati ya ukungu mzito wa theluji.

CCM ndio mhimili mkubwa wa matatizo yote hapa. Wabunge wa CCM wapo tu kama hawapo na wengi wao wamelala usingizi pono kama vile hawajui kinachoendelea. Wanaojaribu kusema kidogo wanaitwa kwenye vikao vya chama na mzee wa kasungura na ndege ya kupaa ya richmonduli na kufungwa midomo.

CCM inabidi waondolewe na wajengewe gereza lao la kiguantanamo kule ukara katikati ya ziwa victoria ili mzimu huu ututoke. Kama vijana nao (kina Lugaza) wameanza kuingia kwa kasi katika hii list ya kifisadi? kama watoto wa mafisadi Ridhiwani na January nao sasa ni part ya serikali hii ya kifisadi? Kama watoto wa wakubwa ndio wanajazwa BOT kulinda siri za kifisadi? Hii nchi inabidi kitu kikubwa sana kifanyike kuvunja hii circle.

MM.KIKE;

Hii post iko mahali pengine ... but it worth this thread too!!!

only thing we have to fear is fear itself
Tamko hilo la Roosevelt la “ogopa woga kwa moyo wako wote” Leo hii katika sanyansi na dhana mpya kabisa (1998/2000) ya kutathmini Ustawi wa jamii Emotional Intelligence (EI) au Ukomavu wa utu linachambuliwa hivi;

WOGA unatizamwa katika njia tofauti kabisa na ile inayofahamika kwenye Psychology na psychiatry. Woga, wasiwasi na Mashaka, (negative emotions/hisiahasi) vinaweza kutumiwa kama nguvu maalum ya kusaliti ustawi wa jamii iliyopevuka na kujitawala kiuchumi na kibinadamu. Mnapokuwa kwenye kundi na mkashituliwa na "Mbwa makali…" yule atakaye zalisha au kusambaza woga zaidi ya wenzake ndiye atakaye kuwa wa kwanza kuwa kitoweo cha mnyama huyo mkali. fuatilia. http://www.duniahai.com/Uharibifu wa Hisia Hasi.html
Atakaye zalisha woga zaidi atashambiliwa, atakuwa mnyonge na atakaye fedheheshwa na mnyama huyo. Atajulikana kama “With low EI”. Yaani aliye duni katika kuerevuka kihisia. Ili kuelewa vizuri dhana hii , Kwenye neno mbwa liondoe na weka neno FISADI, ndipo utelewa vema Roosevelt anasema nini. Yaani fisadi akutishe kwa kukumwagia tindikali usoni na wewe utishike, fisadi akutishe na wewe uogope pale anaponyofoa vipengele muhimu kwenye maagano, maazimio na nyaraka muhimu za kitaifa. Fisadi atoe tafsiri za kifisadi za kitu kama azimo la Arusha na wewe ukae kimya unatetemeka kwa woga! Hakika Fisadi atakufanya kitoweo muafaka. Atatafuna jamii nzima kupitia kodi za walalahoi zilizoko bank kuu, mikataba hovyo ya uchumi wa taifa, miradi muhimu ya kitaifa, kuyumbisha makusudi dira ya taifa kwa faida yake etc. Lakini yote haya ni kwa kuwa mwananchi kajitakia mwenyewe ;kawa mkarimu wa woga tu kwa fisadi. Kimsingi Kama wewe ni Mtanzania wa kweli: Kamwe Usimuogope fisadi. Hasa unapopigania na kutetea haki ya wanyonge waliowengi. “Milele usimwezeshe Fisadi” kwa Hisia hasi! Erevuka kuhusu hisa zako sasa!Na uziwajibikie.

Woga na hisia hasi anasema Roosvelt havituwezeshe kamwe kusonga mbele na kujitokeza kutetea taifa kwa kusema Ukweli kama Ulivyo mioyoni mwetu au kama tunavyoujua na kuuamini.”This is preeminently the time to speak the truth, the whole truth, frankly and boldly. Nor need we shrink from honestly facing conditions in our country today. This great Nation will endure as it has endured, will revive and will prosper. So, first of all, let me assert my firm belief that the only thing we have to fear is fear itself”

Shime tumnyime Fisadi kile anachotaka kutoka kwetu “ngvu ya hisia hasi”. Bila sisi kumpa woga, wasiwasi, unyonge na kunywea hovyo mbele yake, fisadi hana Nguvu peke yake ya kutunyonya nakutufanyia michezo inayoendelea sasahivi ndani ya taifa letu!

Bila kumpa Mbwa woga , anauweka mkia sehemu inayostahili .. katikati ya miguu yake na kurudi alipotoka kwa unyonge mkubwa. Huo unakuwa ni ujembe tosha kwa Fisadi wa aina yeyote toka kwa wale anaowafisadi. Maana anajua Nguvu ya fikra toka kwa Mtanzania asiye ujua woga wa kijinga. Fikra Pevu zilizojikita kwenye kiwango cha juu cha EI na sio IT; Ni silaha tosha ambayo inaweza kumtingisha fisadi na kufuatiwa na hatua ACTION NOW!!!Ambazo lazima lazima Zitakuwa Productive!!
 
Hi! administrator. Pamekuwa na power flactuation...HECE the post imetokea mara mbili!!
 
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake vi mtegoni, na itabidi kuamua kusuka ama kunyoa kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba fedha zilizochukuliwa kutoka Benki Kuu (BoT) chini ya Mpango wa Ununuzi Madeni (EPA), ziliingizwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, uliokipa chama hicho ushindi wa kishindo, Raia Mwema imedokezwa.

Vyanzo mbalimbali vya habari vimeiambia Raia Mwema kwamba kiasi cha Shilingi bilioni 40 kilichochukuliwa na kampuni ya Kagoda Agricultural Limited (KAL) ili zikafanye kile kinachoelezwa kuwa ni kazi “nyeti za usalama wa nchi” sehemu yake iliingizwa katika uchaguzi.

Baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na Raia Mwema, wamesema kwamba wana taarifa kwamba baadhi yao walipata “msaada” ili kufanikisha uchaguzi wao majimboni japo kwamba “msaada” huo ulitofautiana kati ya mbunge na mwingine, kulingana na mhusika ni nani.

Kwa mujibu wa wabunge hao, ambao kwa sababu za wazi hatutawataja majina, walikuwa wakipata kati ya Shilingi milioni moja hadi milioni 20, na kwamba katika matukio kadhaa baadhi yao walilalamika Makao Makuu ya chama kuhusiana na kwa nini “msaada” huo haukutolewa kwa kiasi kinacholingana kwa wote.

Aidha, Raia Mwema imefahamishwa kwamba kwa jinsi fedha hizo zilivyokuwa nyingi, baadhi ya wajanja ndani ya CCM waliunda mpango wa kupora sehemu yake. Kati ya matukio hayo ya uporaji lipo moja la Dar es Salaam ambako kiasi cha Shilingi milioni 600,000 taslimu zilichukuliwa lakini taarifa za wizi huo hazikufikishwa Polisi.

Aidha, vyanzo hivyo vya habari vinasema katika tukio jingine, mjumbe aliyetumwa apeleke fedha kiasi cha Shilingi milioni 200 Kanda ya Ziwa, badala ya kufikisha kiasi chote, aliwasilisha Shilingi milioni 80, na aliyekabidhiwa hizo 80 naye akawasilisha milioni 20.

Ni suala hilo, kati ya mengine, vyanzo hivyo vya habari vinasema, lililosababisha mvutano mkubwa wa uongozi hasa katika Mkoa wa Mwanza, ambako viongozi kadhaa waliwajibishwa, na wengine kuhamishwa kutokana na utata katika mgao wa fedha hizo

Tayari CCM, kwa kuhisi unyeti wa suala hilo, kimekanusha kuwako kwa uwezekano wa fedha hizo kuingizwa katika kampeni. Katika mahojiano na baadhi ya vyombo vya habari vilivyochapisha habari za kuhusiana na fedha hizo mwishoni mwa wiki iliyopita, vilivyowanukuu vigogo kadhaa wa chama hicho, akiwamo Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, CCM kimesema hakikutumia fedha hizo.

Alisema Makamba katika mahojiano ya simu na gazeti moja wiki iliyopita: "Kwanza, siijui kabisa kampuni hiyo ya Kagoda, na chama changu huwa hakipokei fedha kutoka kwenye makampuni, zikija za Msamaria mwema kama wewe, nazipokea na ninatoa risiti. hesabu zetu ziko wazi, zimekaguliwa na juzi tu tumezipeleka kwa Msajili wa Vyama.”

Akijibu gazeti jingine juu ya habari hizo Makamba alisema:"Sisi tuna wanachama, ruzuku na mali zinazokifanya chama kijitosheleze. Ballali ana ofisi yake na mimi nina ofisi yangu, mlango wa kuingilia kwake siujui na wala alivyokuwa akinunua magari sifahamu."

Aliendelea Makamba: "Hatuna deni lolote, wala hatuzijui hizo hela, wanaosema hivyo walizipitishia wapi? Wanaotaka kuja kutuchunguza waje wakati wowote".

Alipoulizwa iwapo CCM haihusiki na mtandao uliochota fedha BoT ni kwa nini imekuwa ikihusishwa na kutajwa mara kwa mara, alijibu:

"Watu wanaotaja chama changu mimi sina tatizo nao, wewe mbona mke wako anakutaja taja kwani umemkosea nini?", alihoji huku akisisitiza kuwa ofisi ya Ballali na ya CCM ni vitu viwili tofauti.

Alisisitiza kuwa CCM ina vyanzo vya mapato vinavyojulikana na anayetaka kujua hayo aende akachunguze ripoti ya mapato na matumizi ya chama hicho iliyokwisha kuwasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ya kipindi cha mwaka 2005 hadi 2007.

"Hesabu za CCM zimekaguliwa na ziko wazi, tunaendesha chama kwa ruzuku na tuna rasilimali za kutosha," aliongeza Makamba.

Makamba, kwa mujibu wa gazeti hilo, alionyesha mshangao kwa wanaohoji matumizi ya chama hicho ambayo aliyaita kuwa "ni ya kawaida," wakati vipo vyama, alivyodai vina matumizi makubwa lakini watu hawavihoji.

"Hebu niambie CCM inatumia helikopta? Lakini (Chama cha Demokrasia na Maendeleo) Chadema, wanatumia helikopta, mbona hamuwaulizi walitumia Shilingi ngapi? CCM mnaitakia nini," alihoji.

Mwingine aliyezungumzia suala hilo ni Katibu wa Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati. Alisema Chiligati: "Mimi hilo silijui na wala sina taarifa nalo."

Kwa upande wake, Katibu wa Uchumi na Fedha, Amos Makalla ambaye alishika nafasi hiyo Oktoba mwaka jana, akimbadili Mbunge wa Igunga na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rostam Aziz, alisema: "Suala hilo ni uzushi unaofaa kupuuzwa. CCM ina utaratibu wa kupata mapato kupitia vitega uchumi vyake vilivyoko nchi nzima".

Aliongeza Makalla: "Hao wanaodai kuwa CCM inahusika na ubadhirifu wa fedha BoT ninawashangaa sana. Watu husema kama hujafanya utafiti, huna takwimu, huna haki ya kuongea na wanaosema hivyo ni wababaishaji wanaotaka kukipaka chama matope.

"CCM inampongeza Rais Jakaya Kikwete kwa ujasiri aliochukua wa kuweka mambo wazi na kwamba ujasiri huo ndio ambao unawafanya wananchi waendelee kumwamini katika utendaji wake wa kazi".

Mwingine aliyezungumzia suala hilo kwa mujibu wa magazeti hayo ya wiki iliyopita ni Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Phillip Mangula, aliyekuwa mtendaji mkuu wa chama hicho hadi mwishoni mwaka 2005.

"Suala hilo uongozi wa sasa unaweza kulizungumzia zaidi, lakini ninavyofahamu kwa mwaka 2005 chama kilikuwa na uwezo wa kujiendesha chenyewe bila kutegemea mtu.

"Tuna wanachama zaidi ya milioni 3.6 nchi nzima. Hao kama kila mmoja angechanga sh. 1000 tu unaweza kuona tungekuwa na fedha nyingi," alisema na kuongeza:

"Mwaka 2005 tulijipanga na tulikuwa na kamati mbalimbali ndani ya chama kama za Uchaguzi, Fedha, Vifaa na pia kuna wanachama na mashabiki wetu walijitolea kuchangia vitu kama kofia na fulana, kwa hiyo suala la chama kujitosheleza lingewezekana kabisa," alisema Mangula.

Vyanzo vya habari vilivyozungumza na Raia Mwema vinasema kwamba kujitokeza kwa vigogo hao wa CCM kuzungumzia suala lilelile, kwa wakati uleule, ni ishara kwamba hilo si jambo la kupuuza, na kama CCM haitacheza karata zake vizuri, litaibukia kuwa kashfa kubwa kwa chama hicho na Serikali kwa ujumla.

“Wako (CCM) katika harakati za kujaribu kufunika mambo. Wanazima moto. Na inaelekea hata nyinyi wenye vyombo vya habari mnataka suala hili liishe hivi hivi. Lakini hili si jambo la kumalizika hivyo. Mwaka 2010 kutakuwa na uchaguzi hapa. Mkiliacha yatajirudia hayahaya na huenda wengine wakachota tena BoT,” anasema mmoja wa vyanzo hivyo.

Vyanzo vya Habari pia vimeliambia Raia Mwema kwamba Kagoda Agriculture Company ilianzishwa kwa maelekezo ya Rais Benjamin Mkapa, na kwamba sababu za “usalama wa taifa” zilizotumiwa kuhalalisha kuchukuliwa kwa pesa hizo ndizo alizoambiwa Ballali na ndizo pia alizomwambia Meghji.

Aidha, nyaraka za kuuziana deni kati ya BoT na Kagoda zilisainiwa katika ofisi ya mwanasheria mmoja wa Dar es Salaam na katika kusaini huko, kulikuwa na Ofisa wa BoT na mmoja wa viongozi wa fedha katika kamati ya kampeni ya CCM.

Raia Mwema limeonyeshwa na mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi huo wa BoT nakala ya hundi ya malipo kwa Katibu Mkuu wa CCM.Habari zaidi zinasema pia kwamba kampeni za uchaguzi wa mwaka huo zilikuwa zikiendeshwa nje ya ofisi ya makao makuu ya CCM, na hivyo kumfanya aliyekuwa Katibu Mkuu, Mangula asijue kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

“Kampeni ziliendeshwa katika ofisi binafsi ya mmoja wa wajumbe wa sasa wa Kamati Kuu ya CCM na huko ndiko fedha zote za kampeni zilipelekwa, na hivyo CCM kutaka kujiaminisha kuwa haihusiki na fedha chafu ni kujaribu kuficha ukweli,” kilisema chanzo hicho cha habari.

“Fedha zilizochotwa BoT na Kampuni ya Kagoda zililipwa kupitia benki moja ya ndani na hii inarahisisha sana kazi ya uchunguzi kwani ni rahisi sana kujua ni nani alikwenda kuchukua fedha hizo Benki,” kilisema chanzo hicho cha Habari.

Aidha baadhi ya watu ndani ya vyombo vya dola waliohojiwa na gazeti hili wanasema, kama kweli Serikali ina nia ya dhati kushughulikia wahusika, kamati inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, haipaswi kusubiri kufikisha kundi la watuhumiwa mahakamani na badala yake kufikisha wale ambao ushahidi wa jinai dhidi yao uko wazi kabisa kama ule wa Kagoda.

Katikati ya sakata hili la BoT ni Dk. Daudi Ballali - Gavana wa zamani wa BoT aliyetimuliwa kazi hivi karibuni na Rais Kikwete. Dk. Ballali, ambaye amekuwa akijiuguza nchini Marekani, ndiye anayeonekana kutwishwa mzigo wote wa ubadhirifu ndani ya benki hiyo mhimili wa uchumi wa Tanzania.

Taarifa za karibu na yeye zilizoifikia Raia Mwema, zinasema amekuwa akishangazwa na jinsi ambavyo vigogo wanavyojitahidi kumgandamiza katika suala hilo.

“Bado anaumwa. Anahisi kuwa ugonjwa wake, pamoja na sababu nyingine, umetokana na sumu, walau madaktari bingwa wa Marekani anakotibiwa wamemwambia kuwa alikula sumu. Kwa hiyo amefanyiwa operesheni ya tumbo. Haijulikani itachukua muda gani kupona, na ndiyo maana aliandika barua ambayo haikujibiwa ya kujiuzulu. Lakini Mungu si Athumani. Akijalia Mwenyezi atapona. Akipona, kama ambavyo wote tunaomba kwa Mungu, atakuja kuzungumza.

“Ana kila ushahidi. Ana kila aina ya nyaraka zilizokuwa zikimtaka afanye nini. Hakika akifanikiwa kuzungumza watu wataumbuka. Si kuwa yeye ni malaika, lakini madhambi mengi wanataka kumbebesha yeye,” alisema.

“Na hicho ndicho vigogo nchini wanachokiogopa. Akiweza kusema tutashangaa, na tutawashangaa viongozi wetu. Hivyo ili asiweze kusema ndiyo kila mara unasikia mara kafukuzwa kazi, mara visa yake imetenguliwa na mara anakaribia kufa.

“Wanataka afe ili siri isifichuke. Kuna uongo mwingi. Na mwenye ufunguo wa uongo huo ni yeye. Anajua na hata baadhi ya wafanyakazi wa BoT wanajua nani alikuwa akishinda ofisini kwake, kwa mfano, kushinikiza malipo ya kampuni ya Kagoda.”

Ndugu huyo wa karibu wa Dk. Ballali amesema Gavana huyo aliyepita wa BoT anataka afikishwe Mahakamani ili ukweli wa nani alishiriki vipi uweze kuanikwa huko.

“Ametuambia kwamba anataka sana kwenda Mahakamani. Huko anatarajia jina lake litasafishwa. Na wanaombeza leo nao sheria ichukue mkondo wake juu yao,” anasema ndugu huyo wa Dk. Ballali ambaye anazungumza naye mara kwa mara.

Baadhi ya wakongwe katika fani ya sheria wanasema endapo kweli Serikali italifikisha suala hilo Mahakamani, itasaidia kuibua mambo mengi ambayo pengine yakafungua ukurasa mpya wa demokrasia na utawala bora.





Source: raiamwema.co.tz

Kwa habari hii na kwa gazeti hili na kwa kujifunga na kauli niliyoi-bold na kui-color; sina shaka CCM wanahusika na ufisadi wa BoT.
 
Nilisha sema hakuna kesi JK anatishia tu hana pa kwenda sasa kaunda Tume kuzima issue ama kujua how big is damage till now . Hana lolote bwana .
 
Ukitizama habari ifuatayo katika gazeti la East African ambayo nanukuu hapa chini hakuna haki tutakayopata wananchi kutokana na CCM hatokubali kula matapishi yake.

Nanukuu:
Tanzania ruling party in danger over $133million EPA scandal
Monday, 07 April 2008
By Daniel Said

DAR ES SALAAM, TANZANIA — Suspicion that the ruling Chama cha Mapinduzi (CCM) was one of beneficiaries in the US$133 million External Payments Arrears (EPA) account of the Bank of Tanzania (BoT), have placed the Presidential investigating team into a dilemma.

Recent reports have it that in its efforts to investigate and take “appropriate measures” as ordered by President Jakaya Kikwete, the team which comprises the Attorney General, Johnson Mwanyika, Inspector General of Police Said Mwema and the Director of Prevention and Combating of Corruption Bureau Edward Hosea has met a hitch.

“Our investigations is like opening up a Pandora Box because all the 22 companies involved in the EPA scandal have issued written statements that implicate the ruling CCM,” said a source close to the committee, who spoke on condition of annonimity.

The Committee which started its job by tracing the accounts of the suspects, has to a large extent managed to freeze some of them including those of their beneficiaries. “The only beneficiary, who has severally been mentioned by the 22 companies and appears to be ‘unreacheable’, is CCM,” the source said.

But the one-million-dollar question remains: “Who’s going to freeze CCM’ accounts despite the fact that all the 22 companies involved in the EPA scandal have issued written statements which show that the companies disbursed some of the money to the ruling party? Indeed, the team is in a dilemma,” said the source.

“The written statements have worried the team. The suspects have severally mentioned the ruling party and its top leadership and sometimes giving evidence of letters and related correspondences,” she said adding that, at times, some senior government officials have also been implicated.

But although the statements directly mention some of the CCM top brass in the previous government and the current one, all of them are yet to appear before the presidential investigating team.

The East African Business Week has reliable information that about four key suspects and witnesses were yet to be summoned by the Presidential investigating team despite their “role and direct involvement in the scandal.”

Some of them, the source said, were the architects of the scam.

A new revelation is now showing that that some of the EPA funds were used in financing the 2005 general elections, including campaigns and other related activities.

Last week, East African Business Week, learnt that about Tsh 108 million (US$87,000) was “offered” by one EPA scandal suspect to retain the Kigoma Urban Constituent which was under the opposition party, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) for 10 years.

The money, a source said, was used to woo both CCM and CHADEMA voters to vote for the CCM candidate. Eventually, the Kigoma Urban seat went to CCM and the former CHADEMA candidate defected to CCM -- he is now a member of the EA Legislative Assembly for Tanzania (CCM).

Apart from using the EPA money in Kigoma Urban, it has been established that part of the money went to Songea Urban whereby a CCM candidate was facing a tough challenge from an opposition member.

East African Business Week is informed that one of the former staunch members of CHADEMA in Kigoma is a surety to one of the EPA scandal suspects.

Also, a substantial amount from one of the companies was paid to an influential sheikh who was campaigning against the ruling party. “The money was reportedly given to the sheikh to contain Moslems who had shown direct opposition to the ruling party,” a source said. The sheikh is now deceased.

East African Business Week has also been informed of the key suspect who has been all the time available but was yet to be interrogated by the presidential investigating team. The suspect, whose documents show that he is the director of the controversial Kagoda Agriculture Ltd which in eight weeks dished away more than $ 30 million from the EPA account may not appear before the team, for fear that he may “spill the beans.”

Although Kagoda was paid $ 30.7 million, a source said, the money that went into the elections was about $20 million due to the fact that “one of the party’s financiers had deducted the money he used in the 1995 and 2000 general elections.”

Again, although one of the committee’s top priorities has been to recover the monies involved, East African Business Week was told last week that some of the suspects had managed to transfer the monies before the committee took action.

As of last week, reports have it that some Tsh 60 billion ($48million) had been recovered although it was yet to be established if it was cash money or pledges.

Apart from the money, the investigation committee also targets property purchased from the transactions and steps have been taken to prevent sales of the assets especially those immovable property.

Following the discovery of the loss of about $133 million from the Bank of Tanzania (EPA Account) recently, President Kikwete fired the BoT Governor Daudi Ballali. About five senior staff of the bank had also been suspended in connection with the scandal.

However one of the BoT senior officers who was implicated in the Control and Auditor General’s Report was not suspended for reasons that he was “close to the authorities.”
 
Thanks for your beautiful ideas. Lakini umasikini wa watanzania ni zao la ujinga tuliopandikizwa ambao utaendelea kututafuna kwa vizazi kadhaa. Maendeleo duni kwa mtanzania imekuwa ni kama hadithi za alfu lela ulela, hatuamini kama tuna umasikini ama kwa lugha nzuri hatufahamu kama tu maskini. Labla twafahamu, lakini hatuoni madhara yake. Je mtu mwenye akili timamu, mkamilifu wa fikra anaweza kushuhudia mwingine akichukua mkungu wake pekee wa ndizi (chakula), akachekelea? "Mafisadi na watanzania". CCM imelitia taifa katika umasikini uliokithiri, kwa miaka 40 tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele kutokana na sera mbovu za chama hicho. Lakini watanzania hilo kwao ni sawa na utani wa Simba na Yanga (Mimi yanga tu hata tufungwe milele, mi Yanga asili bwana).
Mustakabali wa maisha yetu tumeugeuza ushabiki wa michezo, mfano hai uchaguzi wa ubunge Kiteto, " walioipa ushindi CCM ni wafugaji masikini wa vijijini ambao hawajui hata harufu ya chai yenye sukari. Pato lao kwa mwaka halizidi Tshs. 3,000,000/-. Masikini watu hao, licha ya kutengwa kwa takriban miaka 40 na utawala waliounenzi wa CCM lakini bado wanaonyesha utiiifu kwa utawala huo?
Rais wetu tuliyemchagua kwa kura nyingi amekuwa wa kwanza kutupa mgongo licha ya uaminifu wa hali ya juu wananchi wake tuliomwonesha. Ajabu na kweli tuliamini ni rais wa watu, mchapakazi wa kweli, mtumishi wa taifa lake. Loh!!!! Kumbe alivaa ngozi ya kondoo tu ndani, walewale. Yatasemwa mengi sana, lakini langu ni moja tu, ni rais wa aina yake ambaye serikali yake imeungana na wahalifu, kuwasaidia, kuwalinda na kuwatetea, wakati huo huo kuwashughulikia wanaodai haki dhidi ya uhalifu (vijana wanaosadikiwa kuwazomea wenye tuhuma za ufisadi).
Rais wakati anaapishwa alitamka kuilinda na kuitetea "KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA". Pengine ipo katiba nyingine inayohalalisha uvunjaji wa sheria, wanasheria naomba msaada wenu hapa. Nionavyo mimi katiba ni sheria kuu ya nchi ambayo kwayo sheria nyingine zote nchini zinaitegemea kama si kutokana nayo. Je mtu akiapa kuilinda, si ni pamoja na zinazoitegemea? Au ni yenyewe tu basi zingine shauri yake?
Mnisaidie vizuri ufafanuzi na uchambuzi wa tamko au ibara au nini sijui kwenye katiba yetu isemayo, nukkuu yangu si rasmi "Sisi tumedhamiria kuanzisha jamhuri ya muungano wa Tanzania, ambayo itafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea". Nimejaribu tu kukumbuka ilivyoandikwa, sikunakili. Naomba msomaji unisaidie usahihi wake.
Je, tunafuata siasa hiyo kwa mujibu wa katiba, au kipengele hicho kimebadilishwa?
Je, rais anapoapa huwa inamaanishwa kama katiba hiyo inavyosomeka wakati huo, au vinginevyo?
Napenda kuishia hapo. Asante.
 
Hawahawa na watoto wao sasa hivi wanaiba kwa vitisho, utekaji, utesaji, upotezaji na mauaji.
 
Back
Top Bottom