UFISADI Kila Kona: Baraka za CCM KINGA ya Ufisadi BoT na Viongozi Mafisadi

Nchi imegawanyika katika makundi mawili: mafisadi wa wazi (Manji, Mgonja, RA, Lowassa, Balali, Rutabanzibwa) ambao wanaiba hela yetu hivi hivi tunawaona na kuna mafisadi wa kimya kimya ambao kwasababu hawako jikoni kwenye hela wanafanya ufisadi wa namna nyingine kama vile ugoni na ushirikina (hapa namhusisha Slaa, Mbowe, Liumba, Zito (Amina Chifupa saga), Reginald Mengi, Sheikh Khalifa). Tatizo la kundi hili la pili ni unafki jambo ambalo ni baya kuliko sisi mafisadi wa wazi.
 
Sasa una mkejeli nani kwa kujiita fisadi mtoto!? Unadhani ufisadi ni sifa nzuri!? :confused:

Baba yako nani katika mafisadi hawa!? Mkapa, Ballali, Mzindakaya, au Mkono.

Utaonaje ubaya wakati wewe ni fisadi mtoto? Tangu lini BOT ikatoa mikopo kwa watu binafsi na siyo benki za biashara?

Moderators hili jina kwa maoni yangu lipigwe marafuku hatuhitaji watu kutumia majina kuwakejeli Watanzania katika hii vita ya kupambana na mafisadi.

kwanza hujui atan unachoongelea,majiyatanga hakupewa mkopo na BOT bali serikali ndio ilimdhamini,na serikali ikimdhamini mtu kwa utaratibu hailipi wizara bali BOT.Kuhusu jina ni matatizo yako binafsi na udikteta uliokubuu kama mie nkejeli ufisadi na wewe unaotumia jina la watu wenye ulemavu?hio si kejeli?swala la kumjua baba yangu halikuhusu mbona mie sina shida ya kujua baba yako analima mahindi au viazi huko kwenu mwanarumango?
 
Tafakuri butu -ve kama hii ktk jamii hii yetu ya Taifa Changa kama hili lenye Umri wa Miaka arobaini na ushee ni hatari kua na watu kama wewe.

Kauli hii yako na nikiangalia Kibwagizo chako inanionyesha kua chadema ni chama cha watu wenye mawazo butu na waliokata tamaa ya maisha ni hatari.

Ila kazi yetu sisi CCM ni kuleta mapinduzi ya Fikra ambayo tunajitahidi kuyaleta.

Jitahidi kuacha kutafuta majibu rahisi na tafakuri rahisi kama hivi na UGUNDUZI unaodai umegundua ni hatari kwa Afya ya chama chako.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Hapana.Tuache mambo ya UCCM na UCHADEMA na tuangalie hoja hapa ni nini.Hapa tunaona kuwa nchi au inji kama mzee wa Kiraracha anavyoita inaishia kwa Mafisadi.Awe CCM au Chama kingine chochote.Ufisadi hauna chama.Wapo watu ambao ni mafisadi lakini hawana UCCM au Uchadema. Kuondoa hili tatizo ni kuwa na Rais ambae yuko fiti katika maamuzi yake na awe serious na kauli pamoja na vitendo.Mimi naona kuna mambo mengi tu yanafoka moshi na moto utakapolipuka hakuna wa kuuzima. Ishu kama za mahakama ya kadhi ambayo mambo kama hayo yamepitwa na wakati lakini yanapewa nafasi ya kujadiliwa sasa wakati tulishasema nchi yetu haina dini ila watu wan dini zao ni kupoteza wakati.Napenda kuuliza hivi kuna mambo gani ya kisheria au fursa gani ambazo hazipatikani kwenye mfumo huu mahakama zinazotumika sasa hivi mpaka mtu atake mahakama ya kadhi? .Kama ni fursa ya kuoa hata wake wanne si ipo ? .nagalia kinachotokea Kenya ni vita ya Ukabila na Uchaguzi huu umetumika kama chambo tu au njia ya kupitia tu lakini ukweli ni ukabila ambao haukukemewa tangu huko nyuma.Viongozi walizembea na matokeo yake tumeyaona. Mimi naona kama tumeshindwa kupata viongozi ambao ni committed basi tunaweza tukabinafisisha Urais kwani nini mbona tumbinafisisha mashirika yetu yote? HATA NA URAIS HAYA !
 
Nchi imegawanyika katika makundi mawili: mafisadi wa wazi (Manji, Mgonja, RA, Lowassa, Balali, Rutabanzibwa) ambao wanaiba hela yetu hivi hivi tunawaona na kuna mafisadi wa kimya kimya ambao kwasababu hawako jikoni kwenye hela wanafanya ufisadi wa namna nyingine kama vile ugoni na ushirikina (hapa namhusisha Slaa, Mbowe, Liumba, Zito (Amina Chifupa saga), Reginald Mengi, Sheikh Khalifa). Tatizo la kundi hili la pili ni unafki jambo ambalo ni baya kuliko sisi mafisadi wa wazi.

Nimependa jina lako FISADIST, linatamkika kama FISI vile halafu kuna kaneno SAD. Jina lako lina maana gani?

Asha
 
Mimi sioni ubaya wa yeye kuchukua mkopo mkubwa kwa kuwa kwanza ni njia halali na pia ukumbuke kuwa ni njia ya kuwasaidia na wananchi wengine mbao kwa uwekezaji wake wamepata ajira na zaidi ya yote wananchi wamepata elimu ya ufugaji wa kisasa kwa vitendo.Nadhani tatizo ni wale viongozi kama Sani Abacha,Mobutu na wengineo ambao wanaiba na kwenda kuwekeza ktk mabenki ya nje.Winzi wa Mzindakaya ni sustainable.

Nafikiri kwa sababu wewe ni mtoto wa FISADI utakuwa unaelewa hili vinginevyo badilisha jina.

Hivi hao MAFISADI wengine wa BoT wamewekeza wapi? Tanzania au Ulaya.

Kwa hiyo MAFISADI waliowekeza Tanzania unatushauri tuachane nao?
 
Tafakuri butu -ve kama hii ktk jamii hii yetu ya Taifa Changa kama hili lenye Umri wa Miaka arobaini na ushee ni hatari kua na watu kama wewe.

Kauli hii yako na nikiangalia Kibwagizo chako inanionyesha kua chadema ni chama cha watu wenye mawazo butu na waliokata tamaa ya maisha ni hatari.

Ila kazi yetu sisi CCM ni kuleta mapinduzi ya Fikra ambayo tunajitahidi kuyaleta.

Jitahidi kuacha kutafuta majibu rahisi na tafakuri rahisi kama hivi na UGUNDUZI unaodai umegundua ni hatari kwa Afya ya chama chako.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Mpe shule kaka huyo mkatie kiu kijana apate kuelewa
 
kwanza hujui atan unachoongelea,majiyatanga hakupewa mkopo na BOT bali serikali ndio ilimdhamini,na serikali ikimdhamini mtu kwa utaratibu hailipi wizara bali BOT.Kuhusu jina ni matatizo yako binafsi na udikteta uliokubuu kama mie nkejeli ufisadi na wewe unaotumia jina la watu wenye ulemavu?hio si kejeli?swala la kumjua baba yangu halikuhusu mbona mie sina shida ya kujua baba yako analima mahindi au viazi huko kwenu mwanarumango?


Jamani hii Mbaya?

Kijana fisadi Mtoto,usijisifie kwa pesa ya mzazi wako wala nini,simama kama wewe.Mbona kuna watu hapa JF wako safi zaodo ya hao Mafisadi.

Kata ishu na wala sio kuuza chai.NA KWA TAARIFA YAKO,UFISADI NI DHAMBI NA NAKUSIHI SANA MWANA WA KITANZANIA ULIYE FUKARA WA MAWAZO UKASOME KATIKA MAANDIKO.
 
Nafikiri meneja wa kampeni za Kiteto kwa upinzani aanze kazi yake kwa kutoa nakala nyingi iwezekanavyo za makala haya na kuhakikisha kuwa kila nyumba na hasa kila kijana katika jimbo hilo anaipata. What a superb piece of work!
 
Jamani ngoja nijitolee kuipamba na kuiweka kwenye pdf ili iweze kuchapwa vizuri... nadhani hii ni makala inayotakiwa itolewe wakati wa uchaguzi mkuu..!!

Superb!
 
Nafikiri meneja wa kampeni za Kiteto kwa upinzani aanze kazi yake kwa kutoa nakala nyingi iwezekanavyo za makala haya na kuhakikisha kuwa kila nyumba na hasa kila kijana katika jimbo hilo anaipata. What a superb piece of work!
natamani sana Chama Changu CCM kishinde,Hili Nimekewlwa na jinsi nchi inavyoongoza na viongozi hawa ambao Mwalimu hakuwataka ,matahalani Mamvii..

kama JK anasoma hapa,naomba uwang'oe hawa ila kama sivyo mie niko mstari wa mbele kuongozana na Dr. slaa Mpaka kiteto na kumwaga sumu.nitaandaa vipeperushi kama usipowang'oa kina

1.Msola
2.Mramba
3.Meghji
4.Karamagi,
5.Masha,
6.Mungai
7.Gray Mgonja
8.Komba
9.mama Kabaka
10.Ritta Mlaki
11....

uchaguzi ni tarehe 24th February,Muungwana unao Muda..Tafakari na chukua hatua.

hawa si viongzoi w akarne hii bali umewarecyle na wanaon ekana ni sumu
 
Ushabiki umekujaa mpaka chini yako. Lady JD huwa anasema 'wanaume kama mabinti'. Endelea tu FISADI MTOTO. Hivi wewe ni fisadi wa kiume au wa kike?

Asha
SIna aja nyan kusema jinsia yangu maana kuna mtu kasema unataka kumtongoza nadhani alikuwa ni fisadist,sasa sijui na kwangu wanitakia nini
 
Nafikiri meneja wa kampeni za Kiteto kwa upinzani aanze kazi yake kwa kutoa nakala nyingi iwezekanavyo za makala haya na kuhakikisha kuwa kila nyumba na hasa kila kijana katika jimbo hilo anaipata. What a superb piece of work!
WATASOMA LAKINI HAWATAELEWA,WAANGALIA LAKINI HAWATAJUA,WAPOKWEA LAKINI HAWATAJALI NA WAKA HAWAJUI KAMA KILIMO CHAO KINA UHUSIANO NA CCM,WAMERIDHIKA NA HAWANA SHIDA ZAID YA KUFURAHIA KUPUNGA MKONO KWA BABA ZETU WAKIWA WANAPITA NA MA VX,MWISHOWE WATACHAGUA CCM INDALILE
 
Fisadi Mtoto kwa mara ya kwanza yawezekana umesema kweli, ndio maana tunataka kuhakikisha "baba zenu" watakapopita na VX wanazomewa hasa baada ya CCM kubwagwa Kiteto..
 
Ufisadi BoT: CCM matatani

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake vi mtegoni, na itabidi kuamua kusuka ama kunyoa kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba fedha zilizochukuliwa kutoka Benki Kuu (BoT) chini ya Mpango wa Ununuzi Madeni (EPA), ziliingizwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, uliokipa chama hicho ushindi wa kishindo, Raia Mwema imedokezwa.

Vyanzo mbalimbali vya habari vimeiambia Raia Mwema kwamba kiasi cha Shilingi bilioni 40 kilichochukuliwa na kampuni ya Kagoda Agricultural Limited (KAL) ili zikafanye kile kinachoelezwa kuwa ni kazi “nyeti za usalama wa nchi” sehemu yake iliingizwa katika uchaguzi.

Baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na Raia Mwema, wamesema kwamba wana taarifa kwamba baadhi yao walipata “msaada” ili kufanikisha uchaguzi wao majimboni japo kwamba “msaada” huo ulitofautiana kati ya mbunge na mwingine, kulingana na mhusika ni nani.

Kwa mujibu wa wabunge hao, ambao kwa sababu za wazi hatutawataja majina, walikuwa wakipata kati ya Shilingi milioni moja hadi milioni 20, na kwamba katika matukio kadhaa baadhi yao walilalamika Makao Makuu ya chama kuhusiana na kwa nini “msaada” huo haukutolewa kwa kiasi kinacholingana kwa wote.

Aidha, Raia Mwema imefahamishwa kwamba kwa jinsi fedha hizo zilivyokuwa nyingi, baadhi ya wajanja ndani ya CCM waliunda mpango wa kupora sehemu yake. Kati ya matukio hayo ya uporaji lipo moja la Dar es Salaam ambako kiasi cha Shilingi milioni 600,000 taslimu zilichukuliwa lakini taarifa za wizi huo hazikufikishwa Polisi.

Aidha, vyanzo hivyo vya habari vinasema katika tukio jingine, mjumbe aliyetumwa apeleke fedha kiasi cha Shilingi milioni 200 Kanda ya Ziwa, badala ya kufikisha kiasi chote, aliwasilisha Shilingi milioni 80, na aliyekabidhiwa hizo 80 naye akawasilisha milioni 20.

Ni suala hilo, kati ya mengine, vyanzo hivyo vya habari vinasema, lililosababisha mvutano mkubwa wa uongozi hasa katika Mkoa wa Mwanza, ambako viongozi kadhaa waliwajibishwa, na wengine kuhamishwa kutokana na utata katika mgao wa fedha hizo

Tayari CCM, kwa kuhisi unyeti wa suala hilo, kimekanusha kuwako kwa uwezekano wa fedha hizo kuingizwa katika kampeni. Katika mahojiano na baadhi ya vyombo vya habari vilivyochapisha habari za kuhusiana na fedha hizo mwishoni mwa wiki iliyopita, vilivyowanukuu vigogo kadhaa wa chama hicho, akiwamo Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, CCM kimesema hakikutumia fedha hizo.

Alisema Makamba katika mahojiano ya simu na gazeti moja wiki iliyopita: "Kwanza, siijui kabisa kampuni hiyo ya Kagoda, na chama changu huwa hakipokei fedha kutoka kwenye makampuni, zikija za Msamaria mwema kama wewe, nazipokea na ninatoa risiti. hesabu zetu ziko wazi, zimekaguliwa na juzi tu tumezipeleka kwa Msajili wa Vyama.”

Akijibu gazeti jingine juu ya habari hizo Makamba alisema:"Sisi tuna wanachama, ruzuku na mali zinazokifanya chama kijitosheleze. Ballali ana ofisi yake na mimi nina ofisi yangu, mlango wa kuingilia kwake siujui na wala alivyokuwa akinunua magari sifahamu."

Aliendelea Makamba: "Hatuna deni lolote, wala hatuzijui hizo hela, wanaosema hivyo walizipitishia wapi? Wanaotaka kuja kutuchunguza waje wakati wowote".

Alipoulizwa iwapo CCM haihusiki na mtandao uliochota fedha BoT ni kwa nini imekuwa ikihusishwa na kutajwa mara kwa mara, alijibu:

"Watu wanaotaja chama changu mimi sina tatizo nao, wewe mbona mke wako anakutaja taja kwani umemkosea nini?", alihoji huku akisisitiza kuwa ofisi ya Ballali na ya CCM ni vitu viwili tofauti.

Alisisitiza kuwa CCM ina vyanzo vya mapato vinavyojulikana na anayetaka kujua hayo aende akachunguze ripoti ya mapato na matumizi ya chama hicho iliyokwisha kuwasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ya kipindi cha mwaka 2005 hadi 2007.

"Hesabu za CCM zimekaguliwa na ziko wazi, tunaendesha chama kwa ruzuku na tuna rasilimali za kutosha," aliongeza Makamba.

Makamba, kwa mujibu wa gazeti hilo, alionyesha mshangao kwa wanaohoji matumizi ya chama hicho ambayo aliyaita kuwa "ni ya kawaida," wakati vipo vyama, alivyodai vina matumizi makubwa lakini watu hawavihoji.

"Hebu niambie CCM inatumia helikopta? Lakini (Chama cha Demokrasia na Maendeleo) Chadema, wanatumia helikopta, mbona hamuwaulizi walitumia Shilingi ngapi? CCM mnaitakia nini," alihoji.

Mwingine aliyezungumzia suala hilo ni Katibu wa Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati. Alisema Chiligati: "Mimi hilo silijui na wala sina taarifa nalo."

Kwa upande wake, Katibu wa Uchumi na Fedha, Amos Makalla ambaye alishika nafasi hiyo Oktoba mwaka jana, akimbadili Mbunge wa Igunga na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rostam Aziz, alisema: "Suala hilo ni uzushi unaofaa kupuuzwa. CCM ina utaratibu wa kupata mapato kupitia vitega uchumi vyake vilivyoko nchi nzima".

Aliongeza Makalla: "Hao wanaodai kuwa CCM inahusika na ubadhirifu wa fedha BoT ninawashangaa sana. Watu husema kama hujafanya utafiti, huna takwimu, huna haki ya kuongea na wanaosema hivyo ni wababaishaji wanaotaka kukipaka chama matope.

"CCM inampongeza Rais Jakaya Kikwete kwa ujasiri aliochukua wa kuweka mambo wazi na kwamba ujasiri huo ndio ambao unawafanya wananchi waendelee kumwamini katika utendaji wake wa kazi".

Mwingine aliyezungumzia suala hilo kwa mujibu wa magazeti hayo ya wiki iliyopita ni Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Phillip Mangula, aliyekuwa mtendaji mkuu wa chama hicho hadi mwishoni mwaka 2005.

"Suala hilo uongozi wa sasa unaweza kulizungumzia zaidi, lakini ninavyofahamu kwa mwaka 2005 chama kilikuwa na uwezo wa kujiendesha chenyewe bila kutegemea mtu.

"Tuna wanachama zaidi ya milioni 3.6 nchi nzima. Hao kama kila mmoja angechanga sh. 1000 tu unaweza kuona tungekuwa na fedha nyingi," alisema na kuongeza:

"Mwaka 2005 tulijipanga na tulikuwa na kamati mbalimbali ndani ya chama kama za Uchaguzi, Fedha, Vifaa na pia kuna wanachama na mashabiki wetu walijitolea kuchangia vitu kama kofia na fulana, kwa hiyo suala la chama kujitosheleza lingewezekana kabisa," alisema Mangula.

Vyanzo vya habari vilivyozungumza na Raia Mwema vinasema kwamba kujitokeza kwa vigogo hao wa CCM kuzungumzia suala lilelile, kwa wakati uleule, ni ishara kwamba hilo si jambo la kupuuza, na kama CCM haitacheza karata zake vizuri, litaibukia kuwa kashfa kubwa kwa chama hicho na Serikali kwa ujumla.

“Wako (CCM) katika harakati za kujaribu kufunika mambo. Wanazima moto. Na inaelekea hata nyinyi wenye vyombo vya habari mnataka suala hili liishe hivi hivi. Lakini hili si jambo la kumalizika hivyo. Mwaka 2010 kutakuwa na uchaguzi hapa. Mkiliacha yatajirudia hayahaya na huenda wengine wakachota tena BoT,” anasema mmoja wa vyanzo hivyo.

Vyanzo vya Habari pia vimeliambia Raia Mwema kwamba Kagoda Agriculture Company ilianzishwa kwa maelekezo ya Rais Benjamin Mkapa, na kwamba sababu za “usalama wa taifa” zilizotumiwa kuhalalisha kuchukuliwa kwa pesa hizo ndizo alizoambiwa Ballali na ndizo pia alizomwambia Meghji.

Aidha, nyaraka za kuuziana deni kati ya BoT na Kagoda zilisainiwa katika ofisi ya mwanasheria mmoja wa Dar es Salaam na katika kusaini huko, kulikuwa na Ofisa wa BoT na mmoja wa viongozi wa fedha katika kamati ya kampeni ya CCM.

Raia Mwema limeonyeshwa na mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi huo wa BoT nakala ya hundi ya malipo kwa Katibu Mkuu wa CCM.

Habari zaidi zinasema pia kwamba kampeni za uchaguzi wa mwaka huo zilikuwa zikiendeshwa nje ya ofisi ya makao makuu ya CCM, na hivyo kumfanya aliyekuwa Katibu Mkuu, Mangula asijue kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

“Kampeni ziliendeshwa katika ofisi binafsi ya mmoja wa wajumbe wa sasa wa Kamati Kuu ya CCM na huko ndiko fedha zote za kampeni zilipelekwa, na hivyo CCM kutaka kujiaminisha kuwa haihusiki na fedha chafu ni kujaribu kuficha ukweli,” kilisema chanzo hicho cha habari.

“Fedha zilizochotwa BoT na Kampuni ya Kagoda zililipwa kupitia benki moja ya ndani na hii inarahisisha sana kazi ya uchunguzi kwani ni rahisi sana kujua ni nani alikwenda kuchukua fedha hizo Benki,” kilisema chanzo hicho cha Habari.

Aidha baadhi ya watu ndani ya vyombo vya dola waliohojiwa na gazeti hili wanasema, kama kweli Serikali ina nia ya dhati kushughulikia wahusika, kamati inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, haipaswi kusubiri kufikisha kundi la watuhumiwa mahakamani na badala yake kufikisha wale ambao ushahidi wa jinai dhidi yao uko wazi kabisa kama ule wa Kagoda.

Katikati ya sakata hili la BoT ni Dk. Daudi Ballali - Gavana wa zamani wa BoT aliyetimuliwa kazi hivi karibuni na Rais Kikwete. Dk. Ballali, ambaye amekuwa akijiuguza nchini Marekani, ndiye anayeonekana kutwishwa mzigo wote wa ubadhirifu ndani ya benki hiyo mhimili wa uchumi wa Tanzania.

Taarifa za karibu na yeye zilizoifikia Raia Mwema, zinasema amekuwa akishangazwa na jinsi ambavyo vigogo wanavyojitahidi kumgandamiza katika suala hilo.

“Bado anaumwa. Anahisi kuwa ugonjwa wake, pamoja na sababu nyingine, umetokana na sumu, walau madaktari bingwa wa Marekani anakotibiwa wamemwambia kuwa alikula sumu. Kwa hiyo amefanyiwa operesheni ya tumbo. Haijulikani itachukua muda gani kupona, na ndiyo maana aliandika barua ambayo haikujibiwa ya kujiuzulu. Lakini Mungu si Athumani. Akijalia Mwenyezi atapona. Akipona, kama ambavyo wote tunaomba kwa Mungu, atakuja kuzungumza.

“Ana kila ushahidi. Ana kila aina ya nyaraka zilizokuwa zikimtaka afanye nini. Hakika akifanikiwa kuzungumza watu wataumbuka. Si kuwa yeye ni malaika, lakini madhambi mengi wanataka kumbebesha yeye,” alisema.

“Na hicho ndicho vigogo nchini wanachokiogopa. Akiweza kusema tutashangaa, na tutawashangaa viongozi wetu. Hivyo ili asiweze kusema ndiyo kila mara unasikia mara kafukuzwa kazi, mara visa yake imetenguliwa na mara anakaribia kufa.

“Wanataka afe ili siri isifichuke. Kuna uongo mwingi. Na mwenye ufunguo wa uongo huo ni yeye. Anajua na hata baadhi ya wafanyakazi wa BoT wanajua nani alikuwa akishinda ofisini kwake, kwa mfano, kushinikiza malipo ya kampuni ya Kagoda.”

Ndugu huyo wa karibu wa Dk. Ballali amesema Gavana huyo aliyepita wa BoT anataka afikishwe Mahakamani ili ukweli wa nani alishiriki vipi uweze kuanikwa huko.

“Ametuambia kwamba anataka sana kwenda Mahakamani. Huko anatarajia jina lake litasafishwa. Na wanaombeza leo nao sheria ichukue mkondo wake juu yao,” anasema ndugu huyo wa Dk. Ballali ambaye anazungumza naye mara kwa mara.

Baadhi ya wakongwe katika fani ya sheria wanasema endapo kweli Serikali italifikisha suala hilo Mahakamani, itasaidia kuibua mambo mengi ambayo pengine yakafungua ukurasa mpya wa demokrasia na utawala bora.

Source: Raia Mwema
 
"Bado anaumwa. Anahisi kuwa ugonjwa wake, pamoja na sababu nyingine, umetokana na sumu, walau madaktari bingwa wa Marekani anakotibiwa wamemwambia kuwa alikula sumu. Kwa hiyo amefanyiwa operesheni ya tumbo. Haijulikani itachukua muda gani kupona, na ndiyo maana aliandika barua ambayo haikujibiwa ya kujiuzulu. Lakini Mungu si Athumani. Akijalia Mwenyezi atapona. Akipona, kama ambavyo wote tunaomba kwa Mungu, atakuja kuzungumza.

"Ana kila ushahidi. Ana kila aina ya nyaraka zilizokuwa zikimtaka afanye nini. Hakika akifanikiwa kuzungumza watu wataumbuka. Si kuwa yeye ni malaika, lakini madhambi mengi wanataka kumbebesha yeye," alisema.

"Na hicho ndicho vigogo nchini wanachokiogopa. Akiweza kusema tutashangaa, na tutawashangaa viongozi wetu. Hivyo ili asiweze kusema ndiyo kila mara unasikia mara kafukuzwa kazi, mara visa yake imetenguliwa na mara anakaribia kufa.

"Wanataka afe ili siri isifichuke. Kuna uongo mwingi. Na mwenye ufunguo wa uongo huo ni yeye. Anajua na hata baadhi ya wafanyakazi wa BoT wanajua nani alikuwa akishinda ofisini kwake, kwa mfano, kushinikiza malipo ya kampuni ya Kagoda."

Haya maneno mbona kama yanatia kizunguzungu!!!! Enyi wafanyakazi wa BoT muliopo JF na jamaa zenu tuambieni pia ni nani aliyekua anashinda BoT kumshinikiza huyu mzee?
 
Jamani ngoja nijitolee kuipamba na kuiweka kwenye pdf ili iweze kuchapwa vizuri... nadhani hii ni makala inayotakiwa itolewe wakati wa uchaguzi mkuu..!!

Superb!


Mkjj:
Give us feedback on progress and how you intend to proceed with this.

I know for a fact that there are a few declared members from 'vyama vya upinzani' in this JF. (I need not list their names). Feb. 24? is not that far. It is my sincere hope and wish that arrangements to win the Kiteto seat are in full swing as we speak. If not, then please stop bothering us with lots of unmeaningful words, we need action NOW.
 
Baada ya habari za kifisafi kuenea kila kona na hata kuonyesha kwamba CCM na Serikali walitumia pesa za wananchi kuwapa wabunge wao Ubunge leo naelewa kwa nini kila mara ni watiifu kwa CCM na hasa EL akiwaita sirini na kurudi Bungeni wakiwa wana CCM na si Bunge la Nchi tena .
 
Back
Top Bottom