Ufisadi huu mpaka lini?

Aug 10, 2011
81
9
Kwa takiribani miaka kumi sasa nchi yetu imekuwa ikigubikwa na kashifa mbalimbali za ufisadi na hasa zikiwahusisha maafisa waandamizi au wakuu wa serikali je hali hii mpaka lini?

Hatuna maendeleo makubwa tuliyofikia katika nyanja za elimu,kilimo na afya, bajeti zetu zimekuwa za kubabaisha zikitegemea zaid misaada ya wafadhili huku tukishindwa kutumia rasilimali zetu vizuri kama madini, bandari, misitu, mbuga na nyinginezo nyingi kuweza kujiongezea mapato, wadau tupeane mawazo hali hii mpaka lini?
 
Ni mpaka pale tutakapo tambua nguvu ya maamuzi tuliyonayo watanzania na namna ya kuitumia kwa ustawi wa Taifa letu!
 
Wadau kwanini tusiamue jambo moja kama jamii moja na taifa moja.tuprotest watu hawa watoke madarakani kwa nguvu yetu sisi(wananchi) na wachunguzwe na kufikishwa mahakamani?

Mimi binafsi nimechoka na niko tayari kwa lolote.najua ugumu wa maisha individualy serikali haiwezi kusaidia ila kwa kuweka vipaumbele muhimu kwa jamii na uzalendo kwa nchi yetu, kama taifa it wont take us 10years we will be flying our economy na maisha ya mtu mmoja mmoja yatabadilika.wizi umekuwa mkubwa sanaaa,hata usiye mdhania naye ni mwizi kama Msekwa.

Hawajali maisha ya vizazi vijavyo vitarithi nini, labda sababu wao wamesha walimbikizia watoto na wajukuu na vitukuu vyao,ole wao maana tukiamka kama Taifa tutawafuata mpaka vilebwe vyao na watawajibika kwa dhambi za mababu na mababa zao.

TUAMKE JAMANI NA TUAMUE KUANDAMANA HATA KAMA WANATAKA KUREKEBISHA SHERIA YAO ILI IWALINDE WAO TUENDE NA TUPUNGUZE UOGA JAMANI.HII NCHI NI YETU SOTE NA TUNA HAKI SAWA KAMA WALIVYO WAO.

TUKISUBIRI WACHUNGUZANE NANI ATAMCHUNGUZA MWINGINE MAANA HATA ANAYEMCHUNGUZA NAE NI MWIZI TUUU NA NDIYO MAANA HAKUNAGA MAJIBU ZAIDI YA KUTAFUTWA MBUZI WA KAFARA HALAFU WANAKAAA KIMYA HUKU PAPA AKIWA ANAKULA KWA MRIJA.
ENOUGH IS ENOUGH,LETS WAKE UP AND PROTES.

NAWAKILISHA, mkimind kivyenu na ndiyo mjue tuko tayari kwa lolote.nchi inwezi kila kona mpaka maofisini sababu wameubariki wao kwa wizi wao.
 
Shida yetu sisi Watanzania ni kwamba bado hatujajua tuna nafasi gani katika uongozi. Unajua kama leo tutaamu kuandamana kwa ajili ya umeme tu naamini tutapatiwa umeme. Lakini mbona tumenyamaza.
 
Mkuu nakushukuru sana kwa swali lako linalotukumbusha mengi yanayoendeleakutokea katika nchi hii ya watu wachache.
Katikanchi hii sidhani kama ufisadi utafikia kikomo hasa kwa vizazi hizi za enzi hizi. Ila ikitokea wote tukawa na mawazo ya kuyatatua matatizo ya nchii bila kulalamika pasi na matendo, hakika tunaweza tukauondoa ufisadi huu na hatimaye kumwona kila mtu akishughulika na shughuli zake badala ya kuendelea kuishangaa nchi. Ufisadi kwa kweli ni kikwazo kwa maendeleo ya jamii yeyote ile tupilia mbali nchi.

Ninashauri tuache kulalamika pasipo vitendo. Tulalamike huku tukitenda jambo.
 
Back
Top Bottom