Ufisadi HAZINA (Treasury)

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Mfanyabiashara maarufu akabidhi mil 700/-

Mwandishi Wetu

February 22, 2008

BAADHI ya waliochota mabilioni ya fedha serikalini chini ya mpango wa kuagiza bidhaa mbalimbali nje ya nchi yaani Commodity Import Support (CIS), wameanza kulipa madeni yao baada ya serikali kutishia kuanika majina yao.

Habari za uhakika kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi zilizoifikia HabariLeo zimethibitisha kuwa watu kadhaa ambao walichukua fedha za CIS lakini baadaye wakaacha kwa makusudi kulipa wamejisalimisha Hazina mara tu baada ya serikali kutishia kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuanika hadharani majina yao kama hawatalipa madeni yao ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Miongoni mwa wadaiwa hao wamo wafanyabiashara maarufu nchini na wanasiasa.

HabariLeo imethibitishiwa na maofisa wa Hazina kwamba mara tu baada ya tangazo la kudaiwa kutoka magazetini, baadhi ya wadaiwa walijitokeza haraka na kusema sasa wako tayari kulipa.

“Kuna huyu tajiri (jina tunalo) ilipotangazwa tu akaja na hundi ya Sh milioni 700,” Ofisa mmoja wa Hazina alisema na kuongeza wengine kadhaa wenye viwango vya chini pia wamejitokeza.

Inaaminika kwamba baadhi ya wadaiwa walitumia kampuni bandia kujipatia fedha na kutoagiza bidhaa kama ilivyotarajiwa na serikali.

Kampuni 980 zilikopeshwa mabilioni hayo kuanzia miaka ya 1980 mpaka mwaka 1993. Fedha hizo zilitolewa na wahisani mbalimbali chini ya mpango huo ili kuipa uwezo serikali wa kuimarisha uchumi wake.

Miongoni wa nchi hizo ni Japan ambayo imekuwa inatoa misaada mingi kwa Tanzania.

Lengo la wahisani kutoa fedha hizo ilikuwa kuzipatia taasisi, kampuni, viwanda na biashara mbalimbali uwezo wa kuagiza bidhaa na mali ghafi kutoka nje kwa kuwa wakati huo nchi ilikuwa na upungufu mkubwa wa fedha za kigeni.

Hata hivyo wafanyabiashara wengi waliochukua fedha hizo ambazo zilitolewa kama mkopo wa masharti nafuu ambao hauna riba, lakini kinyume cha matarajio wafanyabiashara hao walishindwa kuagiza bidhaa yo yote kutoka nje kama ilivyokusudiwa na serikali badala yake wakazitumia fedha hizo kwa manufaa binafsi.

Kuanzia mwaka 2002 serkali ilikabidhi mpango huo wa fedha chini ya Benki ya Raslimali (TIB), lakini tangu wakati huo wadaiwa wameshindwa na wengine wamekataa kwa makusudi kulipa madeni hayo.

Mwaka huu benki hiyo ililazimika kupeleka wakusanya madeni mjini Dodoma kwa ajili ya kushauriana na baadhi ya wadaiwa walioko bungeni.

Kwa mujibu wa maofisa wa Hazina uchotwaji wa mabilioni hayo ya CIS ulikuwa ufisadi wa mwanzo wa aina yake kufanyika nchini na tangu wakati huo baadhi ya wafanyabiashara walijineemisha hali iliyowafanya waendelee kujichotea fedha zingine serikali kwa kutumia mianya mbalimbali na udhaifu wa watendaji.

Kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na serikali wakati huo, mkopaji akishindwa kulipa kwa kipindi cha miezi 18 tangu achukue mkopo alilazimika kulipa riba ya asilimia 17.

Fedha hizo zilizokuwa zinakusanywa kutokana na deni hilo zilikuwa zinachangia mapato ya Serikali pamoja na miradi maalum ya maendeleo baada ya makubaliano na wahisani husika.

Kwa mujibu wa tangazo la Serikali la kuwataka wakopaji warejeshe fedha hizo, wafanyabiashara wengi walikacha kurejesha licha ya Serikali kufuatilia.

Kwa sasa Serikali imewataka wadaiwa kuwasiliana na taasisi mbalimbali kama Mamlaka ya Mapato (TRA) na Benki ya raslimali (TIB) au Wizara ya Fedha na Uchumi kwa ajili ya kupata kumbukumbu ya madeni.
 
Ingekuwa vizuri majina ya hao walioanza kurudisha mapesa hayo yakawekwa hadharani na kiasi walichorudisha pia kikawekwa hadharani. Isije ikawa mtu karudisha shilingi 10,000 mwingine 5,000 kukaitwa huko nako ni kurudisha. Katika wizi wa mabilioni kurudisha shilingi 10,000 ni usanii wa aina yake.
 
Bubu hapo umesema.... KWanza lazima ijulikane kuwa walikopeshwa kuanzia miaka ya 80 mpaka 1993, sasa hapo kuna vitu kama interest, penalties nk...

Mimi ni Mhandisi na sio mchumi wala mhasibu lakini nina uhakika kuwa kutokana na mikataba yetu ya kula vumbi jamaa akichelewa kufanikisha mkataba lazima atulipe (tukatane mapesa) kwa kufuatia vifungu vya mikataba vikiwemo "liquidated damages"

sasa hao wakuu kule hazina lazima waliangalie hili manake kama mtu amekopa miaka ya 90 akaweka fixed deposit tu tayari ameweza kutulipa kwa pesa yetu wenyewe, tunataka walipe/warudishe ghamara zote, interest, usumbufu, penalties... na wakishindwa ni kutaifishiwa mali kisha kama kawaida, LUPANGO!!!

Viva vita dhidi ya MAFISADI!!!+

By the way, walikuwa wanangoja nini kulipa toka miaka ile????
 
Kwa nini Serikali inasita kutaja majina ya hao wadaiwa ilhali fedha walichukua na wakakataa kurudisha kama ilivyokubaliwa?. Hii hali ya kuoneana aibu ndiyo inayodumaza maendeleo ya Taifa na kufanya watu wengine kujifanyia mambo jinsi watakavyo wao. Kwa hili nashauri Serikali iweke majina ya wadaiwa hao hadharani ili jamii ijue ni watu gani wananeemeka kwa fedha za walipa kodi kwa njia ambazo sio halali. Kwa woga huu wa kutotangaza majina ya wadaiwa hao inanipa wasiwasi kuwa huenda wengi wa wadaiwa hao ni wakubwa Serikalini hivyo wanaogopa kuanika uovu walioufanya. Majina yatangazwe tuwajue (pamoja na kiasi wanachodaiwa) na hatua kali zichukuliwe dhidi yao ikiwa ni pamoja na kufilisi ama kutaifisha mali wanazomiliki.
 
Mimi naona cha muhimu hayo majina yatajwe tu. Hakuna haja ya kuficha...

Mimi kwanza siamini kama pesa zinarudi ila naona ni mbinu ya kudhoofisha harakati zetu za kujua kulikoni.Tutajuane kama wanarudisha ?Kwa nini waandikwe kwamba wanaanza kurudisha lakini wakiwa wana kopa hawa kuandikwa ? Pesa wa wajasirimali zina kumbukumbu kuanzia bank na tuna wajua wengine na hawa walio jichotea kwa nini isiwe hivyo ? Wametukosea sana, kuchota na kukaa nazo kimya .Mzindakaya atakosa kwenye dirty deals kama hizi jamani ? RA je na washikaji zake ? Mimi nasema siamini kama wanarudisha ila wanatafuta namna kututuliza .Kama wanataka tu waamini wasema nani alichukua ngapi karudisha ngapi na interest kwa kuanzia muda ule na penalties. Je hakuna aliyekufa ? Kama kesha kufa pesa hizo nani adaiwe ? Makubaliano yalikuwaje ina case of death kwa mkopaji ?
 
Ahsante JK uzi uo uo mpaka usafishe uozo wote ulioachwa na waliokuwepo kabla yako.
 
Ahsante JK uzi uo uo mpaka usafishe uozo wote ulioachwa na waliokuwepo kabla yako.

Ndug Dar kwa karibu karibu sana hapa . Pia umesema asante JK .JK kafanya nini kwenye hili ? Tunataka ukweli maana kutaja jina la alieykopa si dhambi wala siri .Nia ni kujua kama kweli wanarudisha na si kusema asante JK na kwamba yeye hahusiki. JK yuko kweney Serikali miaka kibao na maamuzi ya kutoa hizo pesa mara nyingi wakubwa wa aina yake huwa wanajua ama walijua .What did he do kusema pesa zirudi ? Kama si kafsha za EPA , BOT nk je kuna mtu angeweza kurudisha pesa ? Mbona nyumba hawajarudisha akiwemo JK mwenyewe ?Asante ya nini unampa ?
 
Ahsante kwa kunikaribisha na maswali kibao, kifupi:

Ahsante JK kwa kuwa kwa sasa tunaona tume zinaundwa, tunaona watu wanaanza kuwajibika, tunaona watu wanaanza kurudisha fedha. Kwa hayo inabidi tumpe ahsante, tena nyingi tuu.

Kuhusu jina au majina ya aliyekopa, naungana nawe hiyo inaweza ikawa ni siri ya Bank kwa wateja wake na inaweza ikawa si siri iwapo fedha hizo zilizokopwa zina mizengwe kama ilivyo kwa wakati huu. Nadhani muandishi wa makala hiyo kama ameweza kujua fedha zimeanza kurudishwa basi nina uhakika pia atakuwa anajua na majina ya waliorudisha, sijui kwanini kaamua kuyabana?

JK yuko kwenye serikali kwa miaka kibao kama usemavyo, lakini kumbuka nyadhifa aliokuwa nazo, kwa jinsi nchi yetu ilivyo, ma-raisi wana madaraka makubwa sana kiasi cha kuwa waziri hana nguvu yeyote mbele ya raisi na akijidai mjanja anawachishwa kazi bila taarifa, nadhani yameshatokea huko nyuma. Hapo lawama hana, alikuwa akilinda kitumbua chake na sasa kafika pale alipokuwa akipataka na hapa ndipo tunapoanza kuona mabadiliko ya kweli.

Kuhusu kashfa uzisemazo zote, bila JK usingeziona kufichuka, na hata kama zingefichuka zisingefanyiwa kazi yoyote, kwani ni mangapi yaliyokuwa yakiibuka kabla hajachukua urais na hatukuona kikifanywa chochote na waliomtangulia? namna afanyavyo kazi JK ni ya kutenda bila kukurupuka. Hayo masuala yote yote uliyoyataja, kila linapoibuka, JK aidha ameliundia tume au amelichukulia hatua zinazoonekana wazi wazi. Mfano, swala BoT? au hujui kilichotokea na kinachoendelea mpaka watu tunasikia wanaanza kurudisha fedha? Mfano mwengine, Buzwagi, Spika Sitta alifanya madudu makubwa pale mpaka ikafikia kumsimamisha kijana Zitto, lakini alichofanya JK si unakijua? kamchuua huyo kijana Zitto na JK kaonyesha kumpinga Sitta waziwazi kwa kumuweka Zitto kwenye tume hiyo ya kuchunguza mikataba ya Buzwagi! au hilo nalo hafai kupewa ahsante? Nyumba si tatizo wala si kitu cha kukushtuwa sana, na kama ni madudu basi yalifanywa na waliomtangulia. Hili la nyumba halina hoja wala uzito.

Nadhani umeelewa kwa nini nampa JK ahsante. Na wewe pia ahsante kwa kutaka kuelewa kwa nini nimetowa ahsante.
Ahsante.
 
Ndugu Dar
Bora umekuja na Serikali imepata msemaji .Haya ndiyo tunataka siku zote kwamba wasemaji wa hawa jamaa muwe mnakuja hapa .Now here you are .Karibu sana .Nawaachia wenzangu wakusome n wakupe maswali zaidi lakini tutaendelea tu .Umetaja mambo nimeshangaa .Unasema kwamba yote yanayo julikana sasa ni kwa ajili ya JK kukubali ? Unaleta mchezo sana . JK is only being smart anataka sifa na the same time he feels sorry for his old folks na anajua Dunia sasa ni ndogo lakini JK si mkweli hata kidogo .
 
Sipo hapa kutetea serikali au kutetea ovu lolote litalotokea au lilitokea na pia sipo hapa kuponda tu watu hata kama wamefanya ya maana na yanayoonekana.

kuhusu JK kutaka sifa, nadhani hilo si kosa na nadhani ni njia nzuri sana ya kuongoza kwani ikiwa anayafanya mema kwa wananchi ili wampe sifa, sidhani hapo kama kuna tatizo. Na kama ni kutafuta sifa bila kufanya lolote jema basi wakati utam-hukumu. lakini mpaka sasa "being smart" na "sifa" alizojitafutia zina-stahili.

Kuwa sorry kwa "his old folks", hili sidhani kama lina ubaya, ubaya ni kuwalinda madudu waliyofanya, tumeona kwa yaliompata swahiba wake mkubwa EL, Karamagi na Msabaha of course he may feel sorry for them but "being sorry" did not stop him short of executing his duties as required.
 
Mwandishi Wetu
Daily News; Friday,February 22, 2008 @10:05

.....Miongoni mwa wadaiwa hao wamo wafanyabiashara maarufu nchini na wanasiasa ........ Inaaminika kwamba baadhi ya wadaiwa walitumia kampuni bandia kujipatia fedha na kutoagiza bidhaa kama ilivyotarajiwa na serikali.... Kampuni 980 zilikopeshwa mabilioni hayo kuanzia miaka ya 1980 mpaka mwaka 1993.

Kuanzia mwaka 2002 serkali ilikabidhi mpango huo wa fedha chini ya Benki ya Raslimali (TIB), lakini tangu wakati huo wadaiwa wameshindwa na wengine wamekataa kwa makusudi kulipa madeni hayo.

Mwaka huu benki hiyo ililazimika kupeleka wakusanya madeni mjini Dodoma kwa ajili ya kushauriana na baadhi ya wadaiwa walioko bungeni.

Kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na serikali wakati huo, mkopaji akishindwa kulipa kwa kipindi cha miezi 18 tangu achukue mkopo alilazimika kulipa riba ya asilimia 17.

Kwa mujibu wa tangazo la Serikali la kuwataka wakopaji warejeshe fedha hizo, wafanyabiashara wengi walikacha kurejesha licha ya Serikali kufuatilia.

Kwa sasa Serikali imewataka wadaiwa kuwasiliana na taasisi mbalimbali kama Mamlaka ya Mapato (TRA) na Benki ya raslimali (TIB) au Wizara ya Fedha na Uchumi kwa ajili ya kupata kumbukumbu ya madeni.

Hapa kuna mambo mengi yanayoonyesha udhaifu wa serikali, uliopelekea kuliwa kwa mafedha hayo. Kampuni zilizotumika kukopa fedha hizo zilikuwa ni feki. swali ni je, kampuni feki italipa deni?

Kuanzia mwaka 2002, serikali iliikabidhi TIB kufuatilia deni hilo bila mafanikio kwani wanadiwa walishindwa!! au walikataa kwa makusudi kulipa!!

Kinachoshangaza ni serikali (kupitia TIB) kwenda Dodoma kushauriana na wadaiwa ambao ni Wubunge. Kwanini kushauriana? mkataba unawataka walipe deni na riba ya asilimia 17.

Ni vugumu kwa Mbunge anayetafuna fedha za umma bila huruma, akaacha kutafuna fedha zinazotolewa kupitia ofisi ya bunge kwa ajili ya maendeleo kwa ya jimbo. Watajwe hawa ili wananchi wawaondoe kwa kura.
 
Mchango mzuri wana JF.

Na vita ni mbele kwa mbele.

NAFIKIRI CHA MAANA NI KU-NOTE WHAT HAS HAPPENED HERE. WAKATI WAFADHILI WANATUPA HIZI HELA, SERIKALI KUPITIA WIZARA YA FEDHA HUWA WANA-SIGN HUO MKATABA HADHARANI NA WANANCHI WOTE TUNAFURAHIA KWAMBA MFADHILI KATOA HELA SASA MADAWATI NA MAJI SAFI YATAPATIKANA. WAKATI FEDHA ZINATOKA, WANANCHI TUNAKUWA GIZANI HATUJUI HELA ZIMEENDA KWA NANI KUTIMIZA MIRADI ILIYOKUSUDIWA.

SINA UHAKIKA KAMA KUNA SHERIA YEYOTE KWA SASA YA KUJUA NANI KAPEWA HIYO MIRADI ZAIDI YA KUTANGAZA ZABUNI. MAONI YANGU NI KWAMBA, BUNGE LINGIPITISHA SHERIA YA KUHAKIKISHA HELA ZINAZOTOLEWA NA WAFADHILI ZIKO HADHARANI KWA MAKAMPUNI YANAYOPEWA HIZO KAZI NA KIASI CHA HELA WANAZOPEWA. PIA KAMATI ZA BUNGE ZIFUATILIE HIZO KAZI NA SIO KUTEGEMEA MAJIBU KUTOKA WIZARA HUSIKA KWANI MUDA MWINGI WANAKUWA HAWAJUI KINACHOENDELEA.

SHERIA NDIO NJIA PEKEE YA KUANZA KUWABANA WABADHIRIFU WA MALI ZA UMMA, BILA HIVYO WATAKIMBILIA MAHAKAMANI. HUKO UNAJUA TENA NINI KINAENDELEA, ANOTHER WHOLE DIFFERENT BOOK!
 
Dar -es Salaam,

Mkuu shukrani sana kuwepo kwani si vizuri kuona upande mmoja tu wa shilingi hii tulokuwa nayo..
Umezungumzia swala la Being sorry - did not stop him short of executing his duties as required.

Hapa mkuu sijakuelewa maanake ulowataja wote wamejiuzuru wao na sio matakwa ya JK kama alivyosema ktk kikao cha chama..

Hadi sasa hivi pamoja na kamati kuwakilisha report yake as President hajachukua hatua yeyote zaidi ya kukubali kujiuzuru kwa hao viongozi...which serve his interest na sio za Taifa kwani Mkataba huo bomu bado tunaendelea nao na kila siku inatugharumu millioni 152. Hivyo basi alichofanya ni feelings zake kwa washikaji wake na pengine chama chake bila ku excute wajibu wake kwa Taifa. Na hata kubadilishwa kwa baraza la mawaziri lina serve chama chake zaidi ya Taifa kwa sababu mawaziri hao ni uchaguzi wake kama ule uliotangulia.

Dhahiri vita ya JK ni viongozi wanaoharibu jina la chama sio Uhujumu Uchumi na labda nikwambie kuwa kila case za Corruption zinavyozidi kuibuliwa ni advantage kwa JK kwa sababu nchi za Ulaya zinazotoa misaada zinamwona akifanya kazi safi regardless of what action amechukua kuhakikisha fedha hizo zinarudi kupitia njia za kisheria.

Mkuu Mwizi akisha iba na report ikisha fika Polisi, basi huyo mtuhumiwa anatakiwa kuwa wanted hata kama atapenda kurudisha mali aliyoiba. Anachojaribu kukifanya JK ni kulikosha jina la mwizi kiasi kwamba wananchi tutaendelea kuishi na majizi majirani zetu kwa sababu ID zao zimesirtiriwa.

Hakuna confidentiality kati ya mwizi na benki hasa ktk treaty ama mutual legal assistance lenye lengo la kufadhili criminal intent..
 
karamagi232bspottedus4.jpg

Karamagi anapeta tu baada ya kusaini mikataba kinyemela na kulihujumu taifa mamillioni ya pesa lakini wezi wa kuku na mayai wanasota Keko. Hata muuaji Dito naye yuko huru.

lowass435anandegeum0.jpg

Waziri mkuu aliyejiuzulu naye ati hana hatia kwa sababu tu ni rafiki wa rais. Uhujumu alioufanya kwenye Richimonduli sio neno wabongo tulipie kwenye gharama za umeme. Kwani yeye alizaliwa na malaika hadi aishi kwa pesa ya walipa kodi hadi afe? Hawa vibaka ambao wameshirikiana na MAFISADI ni lazima wafunguliwe mashitaka na kufilisiwa mali zao.

Ati anapokewa kwa nderemo, anastahili kushitakiwa haraka inavyowezekana na mafisadi wenzake.
 
Mimi naona cha muhimu hayo majina yatajwe tu. Hakuna haja ya kuficha...

Hawa wasanii wetu ukiwaomba majina ya waliorudisha pesa hizo na kiasi walichorudisha utaanza kupingwa kalenda. Hiki kitu ni simple kabisa kama kweli pesa zinarudishwa basi wananchi tungependa kujua majina ya hao wanaorudisha pesa hizo na kiasi hicho, lakini kama mnavyojua mambo katika nchi yetu kila kitu ni SIRI KALI!
 
Hao wanaopokea feza inayorudishwa wajue tunajua idadi yake ,sasa wasilete hesabu ambayo itakuwa na mapungufu.
Lakini fedha imechotwa ,je hivi wanavyokaa na kutuambia kuwa fedha imeanzwa kurudishwa ,kweli hivi ndivyo au ndio katika kuwaburuza wananchi ,kama wameanza kurudisha je uchotaji wao ulikuwa sahihi ? Na wenye kukubalika ? Serikali usifanye mazingahombwe hawa walioanza kurudisha wasweke jela tu ,kwa kweli wanastahili adhabu ya kifo bila ya huruma na iwe fundisho kwa wengine ,maana kusema fedha imeanzwa kurudishwa ni kuwaruhusu wengine nao kuchota wakiamini hata wakifika kujulikana hukumu yao ni ndogo ,kuzirudisha tu utakuwa umemaliza kazi na unapeta na cheo kingine kubarikiwa.
Wananchi ni lazima watake sheria kufuata mkondo wake na sio kusameheana na huku ndiko kutakako fanya Serikali ya mh.Kikwete kujisafisha na sio kutueleza kuwa feza imeanza kurudishwa upumbavu gani huu mnataka kuuonyesha.
 
Asante Dar es salaam kwa kuwa msemaji mkuu wa wakuu wako wa kazi. Tuna maswali mengi sana,huu usafi wa JK sjiu huko wapi?

1: Mkataba wa IPTL,JK alikuwa wapi?by that time alikuwa waziri wa nishati na madini. Pesa ngapi zinapotea kutokana na the most stupid contract?

2:Vipi kuhusu rada ambayo tuliingizwa mjini,na JK akatuambia siye siyo deparment ya World bank?Billion ngapi zimepotea na JK kama waziri wa mabo ya nje alitakiwa kutuhakikishia kampuni husika ilikuwa ni mdau wa kampuni ya British.

3:Jk katumbia pesa zetu za hiyo rada lazima zitarudi,zimerudi,muda wazidi eda atii. Nasi twahitaji majibu juu ya pesa zetu. Kama JK ni mwamba kwanini ajamuuliza Mramba kilitokea nini tukaiingizwa mkenge kwenye manunuzi ya rada na ndege ya rais

Dar es salaam, mwambie JK twahitaji majibu
 
Mkuu Mwizi akisha iba na report ikisha fika Polisi, basi huyo mtuhumiwa anatakiwa kuwa wanted hata kama atapenda kurudisha mali aliyoiba. Anachojaribu kukifanya JK ni kulikosha jina la mwizi kiasi kwamba wananchi tutaendelea kuishi na majizi majirani zetu kwa sababu ID zao zimesirtiriwa.

Hakuna confidentiality kati ya mwizi na benki hasa ktk treaty ama mutual legal assistance lenye lengo la kufadhili criminal intent..

Ahsante sana kwa kuweka wazi kwa namna uonavyo. Na ntajaribu kukufahamisha kwa kadri ya uwezo wangu, mimi kwa kifupi sipo upande wowote wa shilingi na ninacho kieleza au kukiktolea maoni ni kwa kuwa nakiona ni sawa na sahihi kwa upande wangu, maoni na muono wa kila binadamu hutofautiana na hasa zaidi zinapokuja hisia za "ikiwa samaki mmoja kaharibika basi wote wameharibika". Naomba kama binadam wenye uwezo wa kujua zuri na baya tusiwe na mtazamo huo, kwani binadam hata wanaozaliwa tumbo moja huwa tofauti, mmoja akawa Sheikh, mwingine akawa Padri, mwingine akawa Mwema na mwingine akawa Muovu.

Kuhusu la JK kuwa sorry, nilikuwa naelezea kuwa sorry haimaanishi kuwa asitimize majukumu yake.

Kuhusu kujiuzulu hawa waheshimiwa, nadhani tunaelewa kuwa hata walipojiuzulu lakini ilibidi JK akubali au akatae kujiuzulu kwao. Na JK alikubali na hapo ndipo alipo execute his duties as required. Nadhani tutakubaliana nikisema kuwa alikuwa na uwezo wa kukubali kujiuzulu kwao au kukataa.

Kuhusu kutokuchukua hatua yeyote kuhusu kujiuzulu kwao, nadhani unafahamu kuwa MP (Mizengo Pinda) ameunda task force ya kushughulikia hilo, na nadhani ni busara njema kwa Rais kungoja mchujo utaofanywa na task force ili atoe uamuzi au akubali au akatae uamuzi utaotolewa na task force. Na pili ukumbuke kuwa hili suala bado lipo bungeni na si vyema kabla ya bunge kutoa uamuzi wake Rais akaingilia. nadhani ni busara kungoja task force ya MP na Bunge litaamua nini. Na hapo ndipo JK ataonekana msimamo wake kwa hili. Mfano mdogo kwa haya, ukitazama kuhusu mkasa uliompata Mhesimiwa ZK (Zitto Kabwe), Rais hakuingilia maamuzi ya Bunge bali alichofanya ni kumuingiza ZK katika kamati ya kuchunguza Buzwagi baada ya bunge "kumshughulikia" na huo nadhani ulikuwa ni uamuzi mzuri na umeonyesha wazi kuwa JK hakupendezewa na maamuzi ya Sitta na ndio maana akafanya hivyo. Jingine la kutizama ni kuhusu Balali, Rais alikataa ombi la Balali kujiuzulu na badala yake akam-fire (faya. Na hapo pia inangojwa tume inayochunguza. Naomba ukumbuke kuwa maamuzi anayofanya JK ni ya kisheria na kikatiba na kidemokrasia na si udikteta (kama ilivyokuwa zamani).

Siona wapi alipofanya JK "kilikosha jina la mwizi" labda mwenzangu umeona pahali ambapo mimi sijapaona.

Sentence yako ya mwisho ni sahihi kabisa na sipingi hilo na wala sijaona ni wapi JK kaenda kinyume na hilo.
 
By definition ufisadi si kuiibia tuu serikali bali ni pamoja na kuikosesha mapato na kuchelewesha kwa kusudi miradi ya maendeleo ambayo ishapitishwa

Kwa taarifa yenu tuuu ni kuwa hakuna idara ya serikali inayoongoza kwa urasimu kama HAZINA, miradi mingi ya maendeleo imekwama na hasa ya elimu kwa sababu kuna baadhi ya waheshimiwa kama 6 hivi ambao wao wanaona sifa kubwa mafaili kukaa kwao mwezi mzima kwa nia ya kuonyesha kuwa wao ni wachapakazi sana na wako thorough wakati ukweli ni kuwa wao ni opposite,hali inachangiwa zaidi na boasi wao ambaye kusema ukweli naye si madhubuti na mwepesi katika kutoa maamuzi na hii inafanya kila idara ya inayodeal na treasury kuwachukia with passion.

anyway hiyo ndio treasury yetu hiyo...sasa mnapo piga vita mafisadi mkae mkijua kuwa hawa jamaa ni wanatisha kwa ufisadi kuliko Benki ya Posta, TBC,wizara ya Ardhi na TAMISEMI
 
Back
Top Bottom