Ufisadi GEPF na NIDA

Savimbi Brown

New Member
Aug 26, 2016
1
1
Mtafiti binafsi wa

haki za wanyonge

S.L.P 318

Mkuranga Pwani

22/08/2016

Raisi wa Jamhuri ya Muungano

Wa Tanzania,

Ofisi ya rais,

Ikulu,

1 Barabara ya Barack Obama,

11400 Dar es salaam,

Tanzania

YAH: UTUMBUAJI WA MFUKO WA “GEPF” KWA KUDHULUMU WATUMISHI NA KWA KUVUNJA SHERIA INAYOONGOZA MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII KWA UBABE. (HASA WATUMISHI WA “NIDA” WALIOAJIRIWA).

Mheshimiwa Raisi pole na majukumu ya kuiongoza Nchi. Napenda kutumia fursa hii kukufahamisha kuhusu Uozo unaofanywa na Mfuko wa hifadhi za jamii wa “GEPF” kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa ofisi kuwadhulumu Watumishi haki zao kwa maslahi binafsi.

Siku kadhaa zilizopita takribani miezi mitatu nilipata malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa “NIDA” kuhusiana na sakata lao la kutopewa fedha zao za kazi ya mkataba walizochangia GEPF licha ya kuwa na ruhusa ya kisheria ya kupewa fedha hizo.

Niliamuamua kuingia ndani zaidi na kufanya utafiti binafsi juu ya swala hili na baada ya miezi miwili nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukamilisha utafiti wangu na nikaona niuwasilishe kwako kwa hatua zaidi.

SSRA ndiye mwenye mamlaka ya kusimamia mifuko ya hifadhi za jamii hasa pale inapokiuka haki za wanachama na pia zinapovunja sheria. Lakini kwa masikitiko makubwa swala hili ni kama wamelipuuzia na hata hivyo hawatoi msaada bali wameonekana wamekua wakiendelea kutetea mifuko ya hifadhi za jamii.

Sheria ziko wazi na nitachambua vile vipengele vinavyohusika moja kwa moja na swala hili ili kutoa ufafanuzi zaidi. Na kama kuna wanasheria ambao wangependa kusaidia kwa kwenda kufungua kesi mahakamani dhidi ya GEPF.

1. TATIZO

(a). Tatizo ni Watumishi wapya wa nida kunyimwa fedha zao walizochangia mfuko wa GEPF za kazi ya mkataba kama walivyokubaliana hapo mwanzo kati ya NIDA, Wafanyakazi na GEPF kwamba mkataba ukiisha watapewa fedha zao walizokatwa kama zilivyo.

(b). Kuingizwa kwa lazima katika mfuko huo wa GEPF baada ya kupata ajira ya kudumu bila ya kufuata sheria

2. MAELEZO NA MATOKEO YA UTAFITI.

Wafanyakazi hao ambao walikua wameajiriwa kama Data entry hapo awali kwa mkataba wa mwaka mmoja moja. Waliingia mkataba halali na GEPF wa kuchangia asilimia 10 ya mishahara yao na mwajiri kutoa asilimia hizo hizo kwa makubaliano kwamba mkataba ukiisha watapewa michango yao.

Kwa bahati nzuri zilitokea ajira za kudumu za ndani na baada ya Utumishi wa Uma kujiridhisha na sifa za wafanyakzi hao wa mkataba kwa kukagua vyeti vyao, Utumishi ulifuata taratibu zote za kiutumishi ikiwa ni pamoja na kutangaza kazi hizo na kuendesha usaili (interview) wa watu hao kisha kuchambua waliofaulu na wenye vigezo vya hali ya juu wakapewa ajira mpya ambazo sasa zilifanya mkataba wa kazi za muda kama data entry kufa na kuanza mkataba wa masharti ya kudumu kwa mujibu wa sheria za utumishi wa uma.

Kama inavyofahamika katika sheria ya utumishi wa uma kwamba mfanya kazi anapoajiriwa kwa masharti ya kudumu ni lazima ajiunge na mfuko wa hifadhi na mafao ya pensheni. Kwa mujibu wa sheria, hivyo basi wafanyakazi hawa ambao walikua na mikataba ya mwaka na walichangia katika mfuko wa GEPF walipovunja mkataba wao walikwenda GEPF kuchukua fedha zao walizochangia na kama walivyokubaliana hapo mwanzo kwamba wakati wowote mkataba ukiisha watapewa fedha zao.

Sasa mambo hayakwenda kama walivyokubaliana. GEPF waligoma kutoa fedha hizo kwa madai kwamba hawajapewa uthibitisho kutoka NIDA. Waliporudi NIDA wakakutana na kikwazo kwamba barua hazitolewi japo hapo mwanzo kwa mujibu wa kijana huyu niliyefanya nae mahojiano kwa masharti ya kutomtaja jina lake, alisema, “Afisa tawala aliefahamika kwa jina la Warda alikua tayari amewaandikia barua za kusitisha mkataba wa ajira ya Data entry ili wachukue fedha zao. Lakini kwa bahati mbaya amri kutoka juu ilitoa onyo na kusitisha zoezi hilo na kupiga simu GEPF kuwataka wasipokee na wasitishe kufanyia kazi barua ambazo tayari wamezipokea”.

Kijana huyu Aliendelea kusema “Kikao kikaitishwa na kiongozi wao ambaye amemtaja kwa jina moja tu la Ufoya. Kiongozi huyo ambae pia ni afisa tawala wao aliwataka wafanyakazi hao wapya kuacha kufuatilia fedha hizo na kuwaambia wale wote ambao wapo GEPF hakuna ruhusa ya kuhama kwa sababu sheria ya serikali hairuhusu na pia wakapewa mkwara mkubwa na bwana Ufoya kuhusu ajira zao kwamba ni za ndani na waache kiherehere. Na kwa uoga wao katika kutetea ajira yao walikubali kukaa kimya”.

Maskini waajiriwa hawa wananyimwa haki yao kwa ubabe wa viongozi wao na wa gepf.

Nilipomuuliza sasa itakuwaje.. akasema GEPF wamewaambia fedha zao za mwanzo zitaunganishwa na kua kitu kimoja hivyo wasijali lakini tayari wamekwishapewa vitambulisho vipya ambayo vina namba mpya ya uanachama.

Kwa masikitoko makubwa nilimuonea huruma Yule kijana na wenzake wote kwani hayo yote walioambiwa ni uongo.

Kwa sababu katika ajira hasa hizi za serikalini Barua ya kazi inasema pensheni ya mwajiria itaanza kukalkuletiwa pale alipoanza ajira ya kudumu na pale alipoaanza kuchangia katika ajira ya kudumu. Nilipomwuuliza kijana huyo lini umeajiria aaksema Tarehe moja mwezi wa 10 ndio ajira yake serikalini imeanza.

Sasa nasikitika kwa sababu mafao yake yataanza kupigiwa hesabu tarehe iyo aliopewa ajira na mwezi alioanza kuchangia ambayo ni tarehe 1/10/2015.

Katika sheria za Nchi kuhusu mifuko ya hifadhi za jamii hakuna sheria inayoruhusu mfuko wa jamii kuunganisha Fedha za kazi ya mkataba na fedha za ajira ya kudumu kisha kuzipigia hesabu za mafao. Utaratibu huo haupo na ndio maana Hao GEPF kwa kujua hilo walitoa namba mbili za uanachama Ile ya Mkataba na Hiyo mpya ya ajira ya kudumu hivyo vijana wakawa na vitambulisho viwili ambavyo alinionyesha cha kijani cha zamani kazi ya mkataba na cheupe cha ajira ya kudumu.

Walipoenda kuulizia statement zao walipewa mbili ya zamani na mpya, Lakini baadae GEPF wakafanya manuva katika Excel kwamba wakachanganya michango yote ya zamani na mipya kisha kutoa kama moja iliyounganika na kuwapa waajiriwa hao. Lakini bado ni akaunti mbili tofauti katika system ya GEPF. (Hii ni kwa mujibu wa mfanyakazi wa GEPF ambaye katika utafiti wangu aliweza kunipa ushirikiano katika ofisi zao zilizoko jirani Victoria).

Mheshimiwa raisi sheria iko wazi na katika sheria ya Hifadhi ya mifuko ya jamii kuhusu usajili wa wanachama.

“THE SOCIAL SECURITY SCHEMES (MEMBERSHIP REGISTRATION GUIDELINES 2013)”

Made under section 5 of the Social Security (Regulatory Authority). Act no. 8 of 2008 (as amended)

Sehemu ya pili

MEMBERSHIP REGISTRATION PROCEDURES.

namba 6, 7, na 8.

Imezungumzia na kuweka wazi mambo matatu ya msingi na vipengele vyake, naomba ninukuu kwa kiingereza kama ilivyo ili nisikosee kuandika kwa Kiswahili.

PART II

Membership registration requirements

6. (i). It shall be the duty of employer to accord all schemes equal opportunity to meet with employees for the purpose of providing public education on their benefit plans to employee

Mheshimiwa raisi baada ya kumhoji kijana huyo niligundua kua sheria hii hapo juu haikufuatwa. Ambayo tafsiri yake ni kwamba mwajiri anapaswa kuitisha mifuko na sio mfuko mmoja kwa ajili ya kutoa sera zao kwa wafanyakazi. Lakini swala hili halikufuatwa kwa sababu bwana Ufoya tayari alikwisha wachagulia kwa lazima mfuko wa GEPF hivyo hakuna mfuko mwingine uliopewa nafasi ya kufika NIDA kunadi sera zao kwa waajiriwa wapya na ushahidi wa hili nilifika katika mifuko mingine na kuuliza kama wamewai kuitwa NIDA na wakasema hawajawai kuitwa katika swala la ajira mpya za kudumu huko NIDA lakini wamewahi kwenda kwa ishu nyingine.

Jambo ambalo ni kinyume kabisa na sheria hii ya mifuko ya jamii kusajili wanachama. Na wamekiuka sheria namba: 7 (1) (a) mpaka (d) ambayo inasema ….. nanukuu kwa kiingereza.

7. (1) in respecting the right to employee to choose a mandatory scheme under which an employee shall be registered,

The employer;

(a). shall not choose scheme for any of its employee

(b). shall not force an employee to join a scheme which is not of his choice

(c). shall not be allowed to issue policies or circulars requiring an employees to be member of particular scheme

(d). shall not have employment contracts indicating specific scheme membership registration requirement

Sasa nikirejea maelezo ya uyo kijana ni wazi kwamba kiongozi wao bwana Ufoya alikiuka sheria hasa namba 7 (1) na vipengele vyake kwa kuwachagulia GEPF mfuko ambao sio chaguo lao lakini kwa sababu ni bossi na aliweza kuwafool kwa kushirikiana na GEPF walitulia.

Pia kitendo cha GEPF kuhamisha watu kutoka mkataba wa muda kwenda wa kudumu bila kujaza fomu wala kusaini mkataba mpya wa kudumu ni kinyume na sheria. Kwani mtu alipokua na kazi ya mkataba alijaza fomu labda alikua hajaolewa ama kuoa hivyo yawezekana next of kin anataka ajaze mwenzi wake mume ama mke lakini hawakupewa nafasi hiyo. Kilichotokea ni ubabe na GEPF kwa kushirikiana Na NIDA walichukua picha za waajiriwa kutoka katika database ya nida na kuwatengenezea vitambulisho vipya bila ya kujaza fomu wala mkataba wowote wa GEPF kama sheria inavowataka kufanya gafla tu wakaletewa vitambulisho vipya.

Mheshimiwa rais mchezo huu ni mchafu na haukubaliki kisheria kwani kila kilichofanyika ni ubabe na waajiriwa hao hawakupewa nafasi ya kuchagua mfuko wanaoutaka walilazimishwa na kudanganywa ili tu wabakie GEPF pamoja na vitisho vingi. Kijana huyo anaendelea kusema pia wapo wengine waliitwa na wakuu na wakatulizwa kuhusu swala hili kwamba watulie.

Lakini baada ya kuchunguza niligundua Mke wa mfanyakazi wa NIDA ambaye anacheo Ni afisa wa GEPF hivyo pana uwezekano mkubwa kwamba ulikua mchezo mchafu wa kupeana chochote kitu ili idadi ya wanachama iwe kubwa GEPF.

Kwa sababu haiwezekani ofisi moja waajiriwa wapya wakaenda wote GEPF sasa nawaachia Takukuru wachunguze hilo kwamba huyo mke wa afisa wa NIDA ambae anafanya kazi GEPF je ni amemshawishi mumewe kulazimisha waajiriwa wapya kubaki GEPF na kuhakikisha anaweka mazingira magumu na kutumia cheo kuhakikisha amefanikiwa kwa maslahi yao binafsi..?.

3. MAKOSA YALIYOFANYIKA WAZI.

Ø GEPF kutoa namba mbili za uanachama kwa mtu mmoja.

Ø GEPF kudanganya kwamba wataunganisha fedha za mchango wa mkataba na zile za ajira ya kudumu huku wakijua ni jambo ambalo halipo lakini wameendelea kuwablackmail waajiriwa hao.

Ø GEPF kuwahamisha watu kutoka mfuko wa mkataba na kwenda mfuko wa kudumu bila ya ridhaa ya waajiriwa kwa kisingizio kwamba tayari wana taarifa zao.

Ø GEPF kuwalaghai wajiunge na kudanganya waajiriwa kwamba watapewa fedha zao mkataba ukiisha lakini hawakufanya hivyo

Ø Afisa Ufoya kulazimisha na kuwachagulia waajiriwa mfuko wa GEPF

Ø NIDA kutoipa nafasi mifuko mingine ya hifadhi za jamii kufika na kutoa sera zao kwa waajiriwa wapya kama sheria inavyotaka.

Mheshimiwa raisi kwa kuangalia makosa hayo apo juu pamoja na uvunjaji mkubwa wa sheria ni dhahiri kwamba mkataba wa GEPF na waajiri hao sio halali ni batili na kama sheria ya mikataba inavyosema mkataba wenye udanganyifu ama ulaghai ni batili hivyo huu wa hawa vijana GEPF ni batili.

Ninaomba mkataba wa hao waajiriwa na GEPF ufutwe na mchakato uanze upya kwa kufuata sheria na waajiriwa hao waweze kuchagua mifuko wanayoipenda na kwa kuwa sheria inawalinda basi fedha ambazo washaweka GEPF kwa muda wa tangu ajira mpya zitahamishiwa kwa mfuko mtu aliochagua kama sheria inavyosema.

Na zile fedha za awali za kazi ya mkataba wapewe fedha zao ni haki yao hazina uhalali wa kungojea adi wastaafu kwani kazi hiyo ya mkataba imekwisha tayari na haikua na makubaliano ya kufika uzeeni kama GEPF wanavotaka kulazimisha. Kwa maelezo ya huyo kijana NIDA wanapaswa kuwaandikia barua ya kusitisha mkataba wa kazi zile za muda kama kibarua kabla ya kuajiriwa (termination latter).

Pia GEPF ishtakiwe mahakamani kwa kuvunja sheria nakutumia loop hole ya kukingiwa kifua na bwana shemeji na kwa kutokujua sheria kwa waajiriwa hao.

Baada ya kusema hayo mheshimiwa raisi naomba kuwakilisha kwa hatua za kinidhamu ninaamini utalifanyia kazi na hao vijana wapate haki yao kwa sababu wasipoipata leo pesa yao hiyo ya mkataba ni wazi kwamba itapotea na wakija kuidai uzeeni hakuna ushahidi wa kutosha walio nao hao.

Bob Marley aliwai kusema.

“You can fool some people for some time but you cannot fool all people all the Time”

ASANTE
 
Ni ndefu lakini umechambua with concrete evidence imekaa vizuri kiongozi
 
Acha kukurupuka, hakuna sheria inaruhusu mtu kuchukua michango yake akiwa katika ajira hiyo hiyo..? hata kama terms zimebadilika. Polisi wanakaaga kwenye mkataba miaka 12 ndiyo wanaingia permanent and pensionable ushawahi kusikia wanadai mafao ya kipindi wakiwa katika mkataba..? Na hiyo ndo sababu SSRA walikupuuza kwa sababu huna hoja ya msingi.
 
Mtafiti sijui kama ulufuatilia physical au umedownload masheria na kutuletea hapa.Mfuko ni wa pensheni sasa unatakaje uchukue hela katikati ? Hata migodini ni shida hii hii.Navyojua mm mfano police na magereza wanaanza kwa mikataba ya miaka mitatu mitatu ikifika wa kumi na mbili anakuwa pensionable au kabla ya hiyo akifika cheo cha assistant inspector.mbona hawadai hela za hiyo miaka ?Hujaeleza hapo maana ya social security kwa mapana yake.Suala la kubadili namba lipo kama labda mnaingizwa ktk utaratibu wa malipo ya hazina.muhimu hapa ni kama ukikuta michango haipo kwenye namba mpya.Umesikia suala ka vitambulisho vya taifa kwa kuwa unajidai kutafta kiki kwa kuwatetea.Nakuutaarifu kwamba mchakato ukimalizika desemba kwa kutoa namba kwa kila mtanzania namba zote za wanachama ktk mifuko yote zitasomeka kwa national id.unasemaje hapo ?
 
Back
Top Bottom