Ufisadi ATCL: Mkurugenzi wa Fedha, Steven Kasubi asimamishwa kazi

SERIKANI imebaini wizi wa takribani shilingi Milioni 715 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Komoro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.

“Kufuatia upotevu huo Serikali imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi cha polisi kitengo cha usalama mtandaoni ili kubaini mtandao mzima uliohusika ” alisema Prof.Mbarawa.

Aidha aliongeza kuwa kwa utaratibu wa kawaida wa shirika hilo wakala anapewa ruhusa ya kuuza tiketi za ndege kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na pale anapomaliza mauzo anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa tena.

Prof.Mbarawa anasema kwa sasa wameanza na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo la kulifufua kwa kununua ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi na waadilifu.

“Siku mbili zilizopita nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini mapungufu mengi na hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika hii linarudi kutenda kazi kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote wanaoenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma” alisema Prof.Mbarawa.

Vilevile aliongeza kuwa Serikali imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.
escrow ni vipi?
 
ENZI ZA SEREKALI KUFANYA BIASHARA YA UASAFIRI WA NDEGE UMEPITWA NA WAKATI KABISA.ATCL HAITAMUDU USHINDANI .SEREKALI NI BUREACRACY ISIYOWEZA BIASHARA HII KABISA
Mkuu ata mimi anasubiri kwa hamu sana kuona jinsi serikali itakavyoweza kuirudisha ATCL barabarani.Biashara ya Airline sio lelemama.
 
Pia ikumbukwe huyu Dogo alipokea majuzi tu baada ya mwingine kufukuzwa...waangalie wasijewakambebesha madeni ya yule alieondolewa NA wizi
 
Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Mh.Prof Makame Mbarawa amemsimamisha kazi meneja wa fedha wa shirika la mdege la taifa ATCL Bw.Steven Kasubi kwa kuhusika na upotevu wa fedha zaidi ya million 700,

Hivi hii ATCL haina board ya wakurugenzi wakusimamia shuhuri zake? Inakuwaje shirika linaibiwa left,right and centre bila Mwenyeki wa board na wajumbe wake kujua? Haya ndio matatizo aliyotuachia Kikwete kwa kuwateua maswahiba wake kuongoza mashirika hata pale ambapo hawakuwa na uwezo!! Angalia hata kule TANTRADE alimpa ukurugenzi mkuu wa shirika binamu yake ambae hakuwa na sifa mwisho wa yote akaliibia shirika na hivi sasa ana kesi ya jinai mahakamani!!
 
sasa hivi ukitembelewa tu na waziri ujue kuna watu vibaru vinaota nyasi
 
Ati Serikali "imebaini". Mpaka huruma yaani.

CAG na TAKUKURU walikuwa likizo awamu iliyopita? How about hizi kamati za Bunge?

Kule China huwa wanawanyonga watu hawa. Tungehang wawili au watatu hivi, watu wangeogopa kidogo. Ngoja next week tutasikia Serikali imebaini ubadhirifu mwingine Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza and so forth..
 
Nafikiri tuwekeze kwenye usafiri wa anga ili turudi tena kwenye Grid, njia zetu wamechukua jirani na walipiga vigeregere sana sasa tuboreshe IA zetu na tutumie ICAO no 6 watajuta onyango
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom