Ufaransa yakataa tangazo la uhuru wa Tuareg

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Ufaransa imetupilia mbali tangazo la kujitangazia uhuru la waasi wa kabila la Tuareg nchini Mali ambao wameanzisha taifa lao wenyewe katika eneo kubwa sana kaskazini mwa nchi hiyo. Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Gerard Longuet ameliambia Shirika la Habari la Uingereza Reuters kwamba tangazo hilo la kujitangazia uhuru ambalo halitambuliwi na mataifa ya Afrika halitakuwa na maana yoyote kwa Wafaransa.Waasi hao wa Tuareg wamejitangazia rasmi uhuru wa taifa lao la Azawad mapema leo asubuhi.Wakati huo huo Shirika la Kimataifa Kutetea Haki za Binaadamu la Amnesty lenye makao yake mjini London limeonya kuwa taifa hilo la Afrika ya Magharibi lenye machafuko ya kisiasa liko katika hatari ya kupata maafa makubwa ya kibinaadamu licha ya tangazo la kusitishwa kwa mapigano la waasi hao, lililotolewa hapo jana baada ya kufanikiwa kutwaa miji muhimu ya Kaskazini mwa nchi hiyo kutoka katika mikononi mwa wanajeshi walioupindua utawala wa kidemokrasia nchini humo. (Mapigano katika nchi hiyo yamesababisha kuzidi kudhoofika kwa hali ya kibinaadamu iliyotokana na ukame wa hali ya juu. Kwa mujibu wa shirika hilo, usambazaji wa chakula na dawa umezorota wakati wafanyakazi wengi wa misaada wamekimbia eneo hilo.Shirika la misaada la Oxfam limesema kuwa raia wapatao milioni 3.5 tayari wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
 
Back
Top Bottom