MJADALA: Kwanini Wanawake wanaongoza kuwa na majini/mapepo kwa kasi kuliko Wanaume?

Teamo

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
12,272
1,034
MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU:

Salaam wakuu wangu!

It's been long time since i posted a thread herein lakini haina mbaya kiviile manake makamanda mnawakilisha kama ilivyo ada!

STRAIGHT TO THE TOPIC:

Nimeangalia sana kwa uchunguzi wangu wa muda mrefu nikagundua kuwa:


1) Asilimia kubwa sana ya wanawake wanaandamwa na majini/mashetani/mizimu/mapepo....! Hii nimeifuatilia sana kuanzia makanisani, misikitini, hadi uraiani kwenye maisha ya kawaida ya kiswazi.

2) Wanawake ndo watu pekee wenye hofu ya mwenyezi Mungu..(makanisani wamejaa wao, misikitini, mikutano ya injili, jumuiya ndogondogo n.k)


Sasa mi nashindwa kuelewa wala kuziunganisha hizo hoja mbili hapo juu..

Mnisaidie wakuu!

ANGALIZO: Sina nia yoyote ya kuwa-humiliate wanawake

Wana JF habari!

Kuna tukio nimelishuhudia likanifikirisha sana. Tukio lenyewe ni la Binti aliyekua anapiga makelele kama aliyepata wazimu. Jambo lililonifanya kusogea karibu ili kujua kulikoni. Mara baada ya kufika karibu niliwasikia baadhi ya mashuhuda wachache waliokua eneo la tukio wakisema " Ni mashetani hayo, atakua amepandisha" na mwingine alipendekezwa akaitwe msomaji ili aje amsomee.

Baada ya kushuhudia hilo tukio nikakumbuka mtiririko wa matukio mengine mengi yanayofanana na hilo nililokua nalishuhudia. Ndipo maswali ambayo hunijia kila ninaposhuhudia matukio yanayofanana kabisa na hilo yakaanza kujirudia.

Maswali ambayo hujirudia katika kichwa changu;
  • Jini awezaje kukaa na kuishi katika kichwa cha mwanadamu?
  • Je, kwa nini kila niliyemwona akipandisha mashetani alikua/ huwa MWANAMKE?
  • Ni kwa nini matukio haya nimeyashuhudia tu maeneo ya pwani?
  • Kuna ukweli wowote juu ya uwepo wa majini yanayowaingia wanadamu?
Hayo ni maswali makuu katika maswali mengi ambayo nimepata kujiuliza juu ya jambo hilo.

Ni matumaini yangu kuwa humu ndani JF kuna magwiji wengi ambao wanayajua mambo hayo vizuri na watanipatia majibu mujarabu.

Naomba kuwasilisha!
1579845518447.png

=====
BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU:

Kama ni kwenda mdogomdogo basi tuanzie mwanzo kabisa from the bible sawa?
1. Eve alishawishiwa na shetani akala tunda na kumgawia Adam - huu ulikuwa muingiliano wa kwanza kabisa kati ya shetani na binadamu
2. Muingiliano wa pili mkubwa utauona ukisoma genesis (Kitabu cha mwanzo) sura ya 6:mstari wa 1 tunaona mashetani walivyofanya kazi kubwa zaidi. Kama una idea ya bible utakuwa unajua kuwa wale malaika walioasi walifukuzwa mbinguni katika vita kuu na kutupwa. I will quote in extenso:

GENESIS 6:1 When men began to increase in number on the earth and daughters were born to them, 2 the sons of God saw that the daughters of men were beautiful, and they married any of them they chose. . . . 4 The Nephilim were on the earth in those days – and also afterward – when the sons of God went to the daughters of men and had children by them. They were the heroes of old, men of renown. (NIV)

After the angels sinned by marrying human women, they bore them gigantic hybrid children. The Bible calls these offspring nephilim, the "mighty men of old, warriors of renown" (Gen. 6:4). When they appear again later in the Scriptures, they are called by a variety of names, including Rephaim, Zumim, Emim and Horites (Gen. 14:5), Anakim (Deu. 2:11), Zamzummim (Deu. 2:20), and Avim (Deu. 2:23)........

Also read ENOCH 7(1) And all the others together with them took unto themselves wives, and each chose for himself one, and they began to go in unto them and to defile themselves with them . . . And they (3) became pregnant, and they bare great giants, whose height was three thousand ells: Who consumed (4) all the acquisitions of men. And when men could no longer sustain them, the giants turned against (5) them and devoured mankind. And they began to sin against birds, and beasts, and reptiles, and fish, and to devour one another's flesh, and drink the blood. Then the earth laid accusation against the lawless ones.

Nitarudi tena.
===
Tuendelee.... huo mfano kutoka genesis unaonyesha ni kwa jinsi gani evils spirits waliwaingia wanawake na kuwezesha kutapakaza uovu duniani.

Haya tukija kwenye matukio ya kutoa pepo wachafu ( demons/evil spirits) kwanza nitakiri kuwa ni vigumu kuwa na takwimu sahihi/halisi zilizochambuliwa kijinsia kuonyesha kati ya hao ni wangapi wanawake na wangapi wanaume.Pia accounts za kwenye bible zinatumia "gender blind' language kwa kutumia maneno "watu/persons" na maa chache kutaja kama ni mwanamke au mwanaume.Nitakupa mifano michache:
In the bible we read that Jesus drove out demons from "persons" believing these to be the entities responsible for those persons mental and physical illnesses.
Mathew 4:23-25 Demon-possessed persons are healed by Jesus (see also Luke 6:17)-

Mathew 8:14-17: Jesus healed many demon-possessed

Mathew 8:28-34 Jesus sent a herd of demons from two men into a herd of pigs ("about two thousand" pigs; according to the account at Mark 5:1-20 it mentions only one man).

Mathew 15:21-28: Jesus expelled a demon from the body of the daughter of a Canaanite woman
MATHEW 17: 14-21: Jesus healed a lunatic by driving out a demon from him

Mark 16:9: Jesus had driven seven demons out of Mary Magdalene.

Luke 7:21: Many people are cleansed from evil spirits by Jesus.
Luke 13:10-17: Jesus expelled a spirit of disease from the body of a woman on the Sabath.
Acts 5: 16: The Apostles healed those tormented by evil spirits.
Acts 16:16-24 Paul and Silas were imprisoned for driving a future-telling spirit out of a slave girl.
Act 19:11-12: Handkerchiefs and aprons touched by Paul cured illness and drove out evil spirits.

In short haijalishi sana kama takwimu zinaonyesha wanawake au wanaume, lakini mtiririko wa matukio unaonyesha kuwa women are more prone.Ikumbukwe pia kuwa wanawake na watoto waliongoza kama ilivyo leo kuhudhuria mahubiri ambapo mapepo walitolewa enzi hizo.

Kwa siku hizi sihitaji kuku convince maana ukiangalia hata kwenye TV utaona ni nani wanaongoza katika kupagawa na mapepo.
===
Subiri nikujib kiiman yangu (Islam) kutokana na iman yangu , wanawake wengi wanasumbuliwa na Majini
1.majini wanapenda vitu vichafu mfano mikojo na haja Kubwa ( kwa ushahidi wa Huu majini wanapendelea kukaa sehemu za Chooni) unashauriwa ukitoka haja Kubwa na ndogo tawaza kwa maji mengi.
Kwa maumbile ya wanawake na wanawake walio wengi sikuhz hawanaw wanatumia toilets paper wanazurula mjini ikiwa miili yao ina najis hapa Majini ni rahisi kupata makaz Kwenye mwili wa huyu mtu kwa kukumbana naye hata barabaran.


2.Uchafu wa janaba Majini wanaupenda, unapotoka kufanya mapenzi unatakiwa ukoge mwili mzima kila kiungo chako kiingie maji kuanzia nywele hii ni kwa wanaume na wanawake, zoezi hili kwa wanaume ni rahisi Sana. Ukija kwa wanawake kuna vikwazo nywele kasuka hawez kutia maji, vidolen kabandika mikucha Kwahiyo na mwingine kaolewa Kwahiyo anaoga nusu mwili ule uchafu wa janaba anadhurula nao mtaani Chochote kibaya majini wanawakumba kirahisi kwa kuwa mwili wake unamvuto wa makaz ya Majini.

3.majini wanapenda damu, inashauriwa kidini mwanamke anapokuwa period atulie nyumban asidhurule, kudhurulula ilhali mwili mchafu Majini wanauwezo wa kukumba hapohapo inashauriwa ukimaliza hedhi unajitwaharisha unakoga Kama kule Kwenye janaba viungo vyotee vya mwili vipate maji, mtihan unakuwa uleule kasuka, amebondi, kasuka rasta, maji hayaingii anatembea ilhali ana uchafu wa hedhi mwanamke wa aina hii akipita njian ni rahisi Majini kumkumba.

4.Damu ya uzazi Majini Wanapenda, Ndio maana imeshauriwa kidini mwanamke aanze Shughuli zake pindi damu ya uzazi itakapokata,wengine wanakaa siku 40 ndani halafu ajitwaharishe kuoga mwili mzima Ndio aendelee na mambo yake. Wanawake walio wengi hawafanyi hivi kinachotokea Mwanamama huyu mwili wake unakuwa ni kivutio kwa Majini.

Ukiangalia Hizo sababu unakuta wanawake wengi wako hatarini ya kufikwa na Majini tofauti na wanaume Ndio maana Kwenye wanawake 100 unaweza kuta 90 wanamapepo 10 tu Ndio wamekoswakoswa au wako hatarini.
===
1.majini wanapenda vitu vichafu mfano mikojo na haja Kubwa ( kwa ushahidi wa Huu majini wanapendelea kukaa sehemu za Chooni) . Kwa mujibu wa Uislamu unashauriwa ukitoka haja Kubwa na ndogo tawaza kwa maji mengi.
Kwa maumbile ya wanawake na wanawake walio wengi sikuhz hawanaw wanatumia toilets paper wanazurula mjini ikiwa miili yao ina najis hapa Majini ni rahisi kupata makaz Kwenye mwili wa huyu mtu kwa kukumbana naye hata barabaran.


2.Uchafu wa janaba Majini wanaupenda, kwa mujibu wa Uislam unapotoka kufanya mapenzi unatakiwa ukoge mwili mzima kila kiungo chako kiingie maji kuanzia nywele mpaka unyayo hii ni kwa wanaume na wanawake, zoezi hili kwa wanaume ni rahisi Sana. Ukija kwa wanawake kuna vikwazo nywele kasuka hawez kutia maji, vidolen kabandika mikucha Kwahiyo na mwingine kaolewa Kwahiyo anaoga nusu mwili ule uchafu wa janaba anadhurula nao mtaani Chochote kibaya kinauwezo wa kumkumba kirahisi kwa kuwa mwili wake unamvuto wa makaz ya Majini.

3.majini wanapenda damu, uislam unashauri mwanamke anapokuwa period atulie nyumban asidhurule bila sababu za msingi , kudhurulula ilhali mwili mchafu Majini wanauwezo wa kukumba hapohapo inashauriwa ukimaliza hedhi unajitwaharisha unakoga Kama kule Kwenye janaba viungo vyotee vya mwili vipate maji, mtihan unakuwa uleule kasuka, amebondi, kasuka rasta, maji hayaingii anatembea ilhali ana uchafu wa hedhi mwanamke wa aina hii akipita njian ni rahisi Majini kumkumba.

4.Damu ya uzazi Majini Wanapenda, Ndio maana imeshauriwa kidini mwanamke aanze Shughuli zake pindi damu ya uzazi itakapokata,wengine wanakaa siku 40 ndani ,anajua siku hizo hata damu ya uzazi itakuwa imekata. halafu anatakiwa ajitwaharishe kuoga mwili mzima kila kiungo kipate maji Ndio aendelee na mambo yake. Wanawake walio wengi hawafanyi hivi kinachotokea Mwanamama huyu mwili wake unakuwa ni kivutio kwa Majini.

5.Kutia udhu unapolala usiku. Inashauriwa unapoingia kulala mwanamke au mwanaume uoge halafu utie udhu ulale (ukiwa msafi) hii inamaanisha hata ukifa huo usiku utakufa ukiwa msafi mwenye udhu ni swawabu na majini wanaoranda usiku hawawez kupata makazi kwako . Wanawake tunakumbana na mtihani uleule, wa nywele, kucha za kubandika mtu Huwez kutia udhu unalala ukijumlisha una uchafu wa hedhi, janaba Ambao unadhurula nao mchana kutwa basi mwili wako unazidi kuwa na mvuto wa majini .

Ukiangalia Hizo sababu unakuta wanawake wengi wako hatarini ya kufikwa na Majini tofauti na wanaume Ndio maana Kwenye wanawake 100 unaweza kuta 90 wanamapepo 10 tu Ndio wamekoswakoswa au wako hatarini na wao kupata.
===
Msiwalaumu wanawake bure, mnatakiwa mjue kwamba kiumbaji mwanaume amepewa uungu yani uwezo wa kuumba kitu, na ndio mana hata wanapokutana kimwili mwanaume anatoa mbegu ambazo mwanamke anazihifadhi hadi hapo mtoto atakapokuwa tayari kuzaliwa hivyo, Mapepo, shetani, mwanaume na viumbe vingi viliumba na mwenyezi Mungu ila mwanamke alitoka katika mwili/ubavu wa mwanaume.

Hivyo viumbe wengine huwa wanamwogopa mwanaume sababu ana uungu ndani yake na ana uwezo mkubwa kama walivyo mashetani, mapepo n.k.

Hii hali ipo hata kwa wanyama kama nyani wanapokula mazao shambani wanapomuona mwanamke hawaogopi ila wanapomuona mwanaume lazima waogope.

Hivyo jambo la mwanamke kutoogopwa na viumbe wengi ni la kiumbaji zaidi kuliko wadau wengine walivyoelezea.
Note:
mwanaume ana uwezo mkubwa sana ambao unaendana kidogo na nguvu za mashetani na mapepo kiumbwaji na ndio mara nyingi shetani anashindwa kumu attack mwanaume moja kwa moja hivyo anamtumia mwanamke kumvuruga mwanaume sababu anajua mwanaume ni mdhaimu kwa mwanamke kwa kuwa ametoka mwili wake au ubavu kama maandiko matakatifu yanavyosema.

Nitaendelea badae kwa mjadala zaidi..
 
Naomba nijaribu, (kama nakosea au kuwakwaza watu natanguliza kuomba msamaha!)

Shetani
anatumia udhaifu mwanamke tokea kuumbwa kwake! Nathibitisha; Kwanza naomba tuwe na Biblia kwenye majibu yangu. Tusome Mwanzo 2:18,12; Mwanamke aliletwa ili awe msaidizi(company) kwa mwanaume(koz ya kuwa weak no.1). Soma Mwanzo 3:1-6,13 Hapa inaonyesha, nyoka(ibilisi) anajua mwanamke ni dhaifu na hajiamini hivyo ndo alikuwa wa kwanza kufanikiwa kumdanganya!(weakness no.2), bado Soma Mwanzo3:15 kuwekwa uadui kati ya nyoka(ibilisi) na mwanamke (koz no3) Soma Mwanzo 3:16 haswa sehemu b, ananyimwa utawala so weakened even the more! (koz no.4).

Tuhame hapo, twende Mwanzo 6:1-3;' Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,wana wa Mungu waliwaona hao binti wa wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. BWANA Mungu akasema Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele!.............'

Hapa inaonyesha Mungu alichukizwa na mchanganyo huu maana watu wake(wenye maadili na kufuata sheria zake) wanaingia kwa mabinti wa wanadamu(wasiokuwa na hofu ya Mungu, hivyo ulinzi hawana kwa kufuata mila a matambiko yao, hivyo ni wazi wana mapepo) kwani huko mbele inaonyesha jinsi walivomuasi Mungu hata akakifutilia mbali kizazi hicho kwa gharika kasoro Nuhu tu na wanawe.

Hapa naonyesha shetani alipitia kwa watoto wa kike wa wanadamu. (Soma Kumbu 7:3,4 wanavyokatazwa kujichanganya. na sababu zake). Kwa kifupi ; kwa vile wanawake kwa ujumla wao hawana confidence hasa katika kumiliki, wamejikuta wanaingia mikataba mingi(kwa hiyari au kuingizwa aidha kwa kulazimishwa/ kulazimika ama wakiwa bado wadogo na wazazi wao na haswa wa kike awe mama,bibi, shangazi, nyakanga n.k) au yeye mwenyewe kwa kutaka kumiliki say mume, nyumba, utawala n.k) na yule muovu shetani!

Ikumbukwe kuwa Ibilisi amewekewa uadui na mwanamke, hivyo kila siku yuko bize kutaka kumuingia mwanamke, sasa anapojipeleka mwenyewe ili apate utawala, shetani anamuingia 'in four' tena mbaya zaidi anapitiliza mpaka ktk uzao wake.

Nijibu kuhusu wazungu au kwa ujumla walioendelea na wasomi, kwa kifupi hawa wengi wameachana na mila potofu, hivyo hawajiingizi kwenye mikataba hii, lakini akijiingiza tu shetani anaye haijalishi msomi, mzungu,wala mhindi, si tunawaona!

Kwa leo naishia hapa, narudia kama nimewakwaza wengine, naomba msamaha, lakini kama umeinuliwa nakukaribisha tukate huo mnyororo wa laana kwa ajili ya watoto wako wa kike! Kuna mkataba mwingine ni wa damu, hii somo lake siku nyingin.
 
Naangalia kipindi cha utakaso kwenye Emmanuel TV (monday service ya (T.B Joshua).

Kwa mtazamo wangu naona idadi kubwa ya viumbe wanaosumbuliwa na mapepo ni kina mama na mabinti. Sijui kwanini inakuwa hivi?

Wenye ufahamu tafadhali!
 
Huko Nigeria umeenda mbali sana mkuu, huwa nawaangalia 'mtume' na nabii' Mwingira, yaana asilimia kubwa ya wanaokutwa na mapepo ni kina dada na mama, huwa nashindwa kabisa na kituko huwa pale 'anapoamurisha' mpepo yatoke na watu kuanguka, wanaume wengi huwa hawaanguki ukilinganisha na kina mama na dada.

Inanichanganya sana lakini mwisho wa siku, ni fumbo la imani
 
Bado jibu langu halitakuwa tofauti lakini naomba kwanza kukuondolea shaka juu ya kubaki kwa fumbo la Imani.

Kila mtu awe dada au kaka kama ana pepo mara nyingi huanguka chini,kisha pepo humtoka. Swala la wadada wengi kuanguka ni kwa sababu wanatumia vitu vingi vya mapepo.

Mfano mzuri sana ni pafyum kali sana lakini pia nguo nyingi wanazovaa zina mvuto kwa majini-referring to Wanajimu watakueleza.
 
Naangalia kipindi cha utakaso kwenye Emmanuel TV (monday service ya (T.B Joshua).kwa mtazamo wangu naona idadi kubwa ya viumbe wanaosumbuliwa na mapepo ni kina mama na mabinti. Sijui kwa nini inakuwa hivi? Wenye ufahamu tafadhali!

Kwa kuongezea swali lako, mimi kwa Tanzania, sijawahi kuona watu waliotoka kwenye familia zenye kipato kizuri, wakiwa na mapepo/mashetani. Wote nilioshuhudia, wanatoka katika familia fulani ambazo zipo duni ama kwenye kipato au kwenye elimu. Sijui kama wengine wameona hivi.

Halafu dalili nyingi za watu wenye mapepo/mashetani zinafanana sana na psychiatric disorder inayoitwa "Dissociative Identity disorder-DID" au zamani ikiitwa "multiple personality disorder MPD".

Disorder hii kwa nchi za wenzetu, huwapata baadhi ya waliokuwa abused utotoni. Tiba zake ni Psychological treatment including hypnosis. Basically hata tiba ya imani (kwa maoni yangu) ni psychological treatment. Inawezekana pia wanawake wa kiafrika TZ ikiwemo, wengi wao kutoka kwenye familia duni have been abused in one way or another ambayo ndio inapelekea DID. Ila kwa vile tunaamini sana ushirikina katika jamii zetu, sisi tunaona ni mapepo.

Kwa shule zaidi kuhusu DID/MPD, get it from google.com.
 
wewe ni atheists sio?
huwezi elewa haya....
eti stuka,huachi kabisa naona ..

Boss hebu kuwa muwazi hueleweki

Wanawake wengi wanapata hysteria na kwa sie tusojua sayansi husika tunafikiri mapepo.

Hiyo ya wanawake wote wanavutia mapepo ndo naipata kwako......nieleweshe :]
 
Boss hebu kuwa muwazi hueleweki

Wanawake wengi wanapata hysteria na kwa sie tusojua sayansi husika tunafikiri mapepo.

Hiyo ya wanawake wote wanavutia mapepo ndo naipata kwako......nieleweshe :]

nilicho ongea ni according to 'some religious teachings'
ndo maana nikakuuliza wewe ni atheist?
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom