Tatizo la Muwasho Sehemu za Siri: Chanzo, Matibabu na Namna ya Kujikinga

Yo Yo

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,217
1,702
itching 1.jpg

BAADHI YA MASWALI YA WADAU KUHUSU HALI HII:
Habari waungwana,

Mie nina tatizo limenitokea hivi karibuni. Ninapofanya mapenzi na mke wangu,baada ya shahawa kutoka nasikia muwasho ndani ya mrija wa kukojolea.

Muwasho huo uendelea kwa siku mbili kisha upotea, niikifanya tena unarudi. Sasa sijui hilo ni tatizo gani.

Naomba ushauri wenu tafadhali.

View attachment 164427View attachment 164428View attachment 164460

===================
Hv ukiwashwa sehem za siri muda mrefu kama fangasi hivi tiba yake ni nini? Maana kama vidonge na dawa za tube sijui cream nimepaka sana hadi basi. Inafika time unaona kama umelogwa hivi.

Wadau nijuzeni labda kuna tiba nyingine zaidi ya tube na vidonge?
Kuwashwa sehemu za siri na kuota vinyama nyama kwa nje husababishwa na nini? Na ni nini tiba yake?

Ni sehemu za siri za mbele yaan sehemu ya haja ndogo kwa ndani inawasha na kuota vinyama nyama kwa nje husababishwa na nini?

Pia muwasho huu unakuja kupotea?

UFAFANUZI WA TATIZO
Idadi kubwa ya watu wanasumbuliwa na tatizo la kuwashwa sehemu za siri bila kujali jinsia na umri. Tatizo hili laweza kusababishwa na matatizo mbalimbali lakini kubwa ni fangasi.

Watu wanapaswa kufahamu kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani ndani ya mwili kama vile mzio, matatizo ya ngozi au sumu ya mimea au wadudu ambao wanakawaida hiyo.

Mara nyingi muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu huisha wenyewe au muda mfupi baada ya kitu hicho kikiondolewa. Kuondolewa kwa kitu hicho kunakuwa ni matibabu sahihi na kuendelea na njia bora za kujikinga kutopata maambukizi tena.

Vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu. Ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari.Kukaa na ugonjwa kwa muda mrefu kunaweza sababisha ugonjwa kusambaa mwilini na kuongeza hatari ya kifo.

KISABABISHI
Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu zingine za mwili. Maradhi ya fangasi husababisha muwasho kwa wanaume wengi, sababu zingine ni kama ugonjwa wa upele, kuwepo kwa chawa, mzio na maambukizi mengine ya bakteria. Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo cha kuwashwa uume.

FANGASI SEHEMU ZA SIRI
Maradhi ya fangasi (Candidiasis) husababishwa na vimelea viitwavyo Candida albicans. Vimelea hivi hushambulia jinsia zote ingawa hushambulia zaidi jinsia ya kike kutokana na maumbile yao na hali ya kuwa na unyevunyevu mara nyingi. Mazingira hayo husababisha fangasi kumea vizuri. Watu wengi wana vimelea hivi katika miili yao kwa kiwango kidogo. Kinga ya mwili ikisaidiwa na bakteria walinzi wa mwili huweza kupambana na vimelea hivi.

Mtu anapokunywa dawa za kuua bakteria kutokana na ugonjwa mwingine wa bakteria kama kuhara damu,husababisha bakteria walinzi wa mwili kufa hivyo kuongeza hatari ya mwili kushambuliwa na ugonjwa wa fangasi.Ikiwa kinga ya mwili itashuka kutokana na maradhi kama VVU au lishe duni mwili utakuwa katika hatari zaidi ya kupata maradhi ya fangasi.
Hata hivyo maradhi ya fangasi yanaweza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kuchangia nguo au vifaa vya kuogea na kujamiiana na mwathirika.Wanaume wengi wanasumbukiwa na fangasi sehemu za siri huishi maeneo yenye joto sana kama pwani, Lindi, Mtwara, Tanga na Dar es Salaam.

Kuishi sehemu yenye joto pamoja na kuvaa nguo za kubana hasa zisizotengenezwa na pamba kwa asilimia 100kunafanya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu hivyo kutengeneza mazingira mazuri kwa fangasi kuzaliana na kuongezeka.

DALILI ZA FANGASI SEHEMU ZA SIRI
Sehemu za siri mara nyingi hutumiwa kama maficho ya fangasi.Hizi ni kama vile uume, korodani, katika mapaja, uke,na sehemu za katikati ya makalio. Wakati mwingine fangasi husambaa hadi kwenye mapaja. Kwa wanaume fangasi huweza kusababisha sehemu za siri za mwanaume kubadilika na kuwa nyekundu na hata kuwasha. Ngozi inayozunguka sehemu hizo huwasha ,kukakamaa na kutoa majimaji ambayo hutoa harufu mbaya.

MATIBABU YA FANGASI
Ikiwa una dalili za ugonjwa wa fangasi ni vyema kufika kwa daktari kwa ajili ya matibabu na ushauri zaidi. Kutumia dawa bila ushauri wa daktari kunaweza kusababisha kutopona kabisa, kutopona vizuri au ugonjwa kujirudia baada ya siku chache. Vimelea pia vinaweza kujenga usugu wa dawa.

Kumwona daktari kutasaidia kujua kama una maradhi mengine yanayosababisha upate fangasi sehemu za siri.Ugonjwa wa fangasi usipotibiwa husambaa kwenye damu na kusababisha madhara makubwa mwilini kama kwenye ubongo na mapafu.

Baadhi ya magonjwa mengine yanayotibiwa na dawa hii ni pamoja na;saratani ya ngozi,vidonda vibichi,vidonda visivyopona kwa namna yeyote ile, bawasiri, majipu, vimbe mbalimbali, maumivu ya magoti kwa kuchua, nywele kukatika, mabaka na michirizi mwilini, kucha kung'ooka kwaajili ya fangasi kuota tena (ni nzuri sana kwa watu wenye ulemavu wa ngozi), mba n.k

Kwa wale ambao ugonjwa wa fangasi umetapakaa mwili mzima ikiwa ni pamoja na kuenea kwenye damu tunayo dawa iitwayo LMTM/J19 ambayo ni yakunywa inayotibu fangasi zote pamoja na magonjwa mengine yaliyo ndani ya damu. Baadhi ya magonjwa hayo ni; fangasi ya njia ya chakula, saratani ya koo, saratani ya utumbo, saratani ya njia ya haja kubwa, minyoo, mzio, kufunga choo, vidonda vya tumbo, magonjwa ya zinaa (uti, kisonono nk)

JINSI YA KUJIKINGA
Ili kusaidia kuepuka kupatwa na fangasi sehemu za siri ni vyema kuosha vizuri. Kwa wale wanaume ambao hawajatahiriwa wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani ya govi. Kwa kifupi ni vizuri sehemu za siri kubaki wakati wote katika hali ya usafi na ukavu, kwa maana ya kutokuwa na unyevunyevu unaweza kusababisha maambukizi.

Matumizi ya poda maalum yanaruhusiwa hasa kipindi cha joto kali ili kuzuia unyevunyevu. Vaa nguo isiyobana, iliyotengenezwa kwa vitu asilia kama pamba. Badili nguo ya ndani angalau kila siku na tumia kinga pale unapokutana kimwili na mtu ambaye hujui hali yake kiafya.

MICHANGO YA WADAU MBALIMBALI WA JF:
MUWASHO WAWEZA KUWA DALILI YA MARADHI FULANI
KUWASHWA sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani kujumuisha maradhi ya uke kwa wanawake au muwasho na kuvimba kwa sehemu za siri za wanaume (jock itch). Bila kujali jinsia muwasho unaweza kusababishwa na ugonjwa wa ngozi, magonjwa ya zinaa au mzio (allery).

Kuwashwa makalioni hutokea pale ngozi inayozunguka njia ya haja kubwa inapokereketa ikiambatana na hamu ya kutaka kupakuna, muwasho huongezeka pale unapokaa na kukiwa na unyevunyevu. Aidha, sababu kuu za kuwashwa kwenye makalio ni kutojisafisha vizuri, kula vyakula vyenye viungo vingi sana, kuhara, vidonda kwenye njia ya haja kubwa, maambukizi ya fangasi, bawasiri (hemorrhoids), minyoo na kadhalika.

Watu wengi wakiwemo wasomaji wa FikraPevu wamekuwa na tatizo la muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu flani na huisha wenyewe baada ya kitu hicho kikiondolewa, vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi, ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari.

Nini husababisha muwasho sehemu za siri za Mwanaume?

Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu zingine za mwili. Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo kikuu cha kuwashwa uume. Sababu zingine ni maradhi ya fangasi, ugonjwa wa upele (scabies), kuwepo kwa chawa, mzio, maambukizi ya bakteria n.k

Nini hupelekea muwasho wa sehemu za siri kwa Mwanamke?

(i) Maambukizi ya Fangasi Ukeni (Vaginal Yeast Infection), Ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosababishwa na fangasi waitwao Candida. Dalili kuu ni uwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.

(ii) Ugonjwa wa kuvimba uke (Vulvovaginitis), Ni ugonjwa unaoathiri kwa kuvimbisha sehemu za nje za uke na uke wenyewe. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, mkojo kuuma na kukereketa wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu ukeni.

(iii) Kuvimba Uke baada ya hedhi kukoma (Postmenopausal Atrophic Vaginitis), Ni ugonjwa wa kuvimba kwa uke baada ya hedhi kukoma. Hali hii huongeza maambukizi ukeni na huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

(iv) Maambukizi ya Trikomonasi (Trichomonas Infection), Ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na kimelea aitwaye Trichomonas vaginalis. Dalili kuu ni muwasho katika uke au uume na kutokwa na uchafu ukeni.

(v) Ugonjwa wa Minyoo (Pinworm Infection), Ni maambukizi ya minyoo wadogo sana wenye umbo la pini wanaoweza kuambukiza utumbo na kusambaa maeneo mbalimbali. Ugonjwa huu huwatokea sana watoto wa kati ya miaka 5 na 10.

(vi) Inflamesheni ya Urethra (Urethritis), Ni maambukizi kwenye urethra (ujia wa kutolea mkojo nje) yanasababisha kuvimba kwa urethra. Dalili kuu ni mkojo kuchoma, maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kutokwa uchafu.
UNDERSTANDING VAGINAL YEAST INFECTION
Me nadhani kuwasha kwa sehemu za siri nako kwatakiwa kufafanuliwa maeneo ya siri napo kumegawanyika kuna ndani ya eneo la siri na nje ya eneo la siri.

Me nta base kwa dada zangu na kuwapa hiki kifungu wakisome na kitawasaidia sana pia dada yangu pretty kipitie pia na uwaelimishe wengine

Yeast Infection Causes
Sometimes, taking antibiotics can cause yeast infection. One prime factor of the cause of yeast infection in pregnant women is the course of hormone changes as well as women undergoing menopause. Not only the women experience this infection, even men can contract the disease by engaging on sexual intercourse with women who are infected with it.

At times, overdoing the personal hygiene can be a major cause for this infection to occur.

Feminine washes and douches can sometimes cause fungal infestation. Too much cleanliness tends to kill the beneficial bacteria that normally protects and shields the body from the disease. Another factor when looking up the causes of yeast infection is clothing. This cause is often overlooked, but it also plays a big part in causing the symptoms to occur. Tight clothes tend to keep away the cold in the body; thus the fungus creates their environment.

Vaginal Yeast Infection
Yeast infection is better prevented than cured. That is why it is important to know its causes. Reading and researching can be a big help when it comes to preventing the disease occurrence. The most common yeast infection is the one which occurs at the vagina. This is caused by the organism Candida Albicans. During sexual intercourse, with or without the use of a protective item, the organism can be transferred.

Irritating soaps can be a candidate for causes of yeast infection. These are bubble baths, douches, and some feminine liquid wash. Although it is meant to clean you from the fungus, they can sometimes trigger and cause the infection themselves. Having proper hygiene can help prevent this kind of infection, but overdoing it can possibly be the cause of infection instead.

The overuse of antibiotics is also an agent to the cause of vaginal fungal infection, so are dairy products and beef. There are also foods that can cause yeast infection; here are some to name a few: grain, corn, apples, and peanuts. So it is better to know the causes of this disease so we can easily prevent them from happening. Bear in mind that prevention is always better than cure.
SI LAZIMA UWE UGONJWA WA ZINAA
Kuwasha sehemu ya siri kuna sababishwa na vitu vingi, huo sio ugonjwa wa zinaa.

- Inawezekana hao ni fungus, hivyo inabidi akamuone daktari ampe vidonge vya kuingiza sehemu ya siri au cream ya kupaka.

- Vile vile inawezekana anapenda kuvaa chupi wakati sehemu ya siri sio kukavu, anapomaliza kuoga ahakikishe ajifute vizuri ndipo avae chupi, unyevu nyevu sehemu za siri unaweza kusababisha kuwashwa.

- Ahakikishe anajisafisha vizuri sehemu za siri, wanawake wana utoko sehemu zao za siri, hivyo ahakikishe kila siku kujisafisha hadi ndani ili utoko wote utoke. Kama akiwa na utoko nao unaweza kusababisha kuwashwa.

- Azingatie usafi wa hayo niliyotaja hapo juu, kama muwasho unaendelea akamuone daktari na achukuliwe kipimo cha mkojo.
HAKIKISHA UKAVU WA NYETI
Mi nadhani usafi hayo maeneo kwa wanaume wengi huwa hatuzingatii. Maanake unakuta mtu kamaliza kukoga anajifuta maji mwilini,lakn katikati ya mapaja na chini ya pumbu huwa watu wanasahau sana. Pia usivae nguo yaan boxer hadi hizo sehem ziwe kavu kabisa. Pia kama una mafuta ya nazi wakati wa kulala inabid uwe unapakaza, epuka kuvaa chupi zinazobana.
YAWEZA KUWA NI UCHAFU. MAZINGIRA YA JOTO PIA YAWEZA KUWA SABABU

Hiyo ni chronic fungal infection. Inasababishwa mara nyingi na unyevu wa mara kwa mara wa meneo hayo, na pia hali ya uchafu kama vile kutumia boxer moja kwa muda mrefu bila kubadilisha, hasa maeneo yenye joto kama Dar.

Matibabu:

1. Kitu kikubwa cha kwanza, kabla ya matibabu yoyote yale ni kuzingatia usafi wa maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na kutovaa boksa kwa zaidi ya siku moja hasa kwa maeneo yenye joto kama Dar, pamoja na kuhakikisha kuwa unapomaliza kuoga, umejifuta vyema maeneo hayo, na pia unapomaliza kujitawaza kwa maji baada ya haja kubwa, unajifuta majimaji na taulo au toilet paper na kuhakikisha kuwa maeneo hayo ni makavu kabisa.

2. Pili, kama unatumia chupi, nashauri uachane na chupi uwe unatumia boksa ambazo ni pana, zinapitisha hewa na ni za COTTON kwa 100% (hizi ni expensive zaidi, but ndizo ambazo zinashauriwa kiafya kwa usalama wa nyeti zako).

3.Tatu, wakati unatumia dawa, hakikisha kwamba boksa zako zote umeziloweka kwenye maji ya moto kabisa kwa muda wa dakika 15-20 kisha uzifue kwa sabuni, na kuzianika kwenye JUA, halafu kabla ya kuzivaa tena uzipige pasi vizuri.

4. Usivae boksa mbichi au yenye unyevu, pia hakikisha boksa zako unazianika kwenye JUA (sio ndani chini ya kitanda); Na hakikisha UNAPIGA PASI boksa kabla hujaivaa.

5. Kama una mpenzi wako ambae mnakutana kimwili, hakikisha pia na yeye anatumia dawa KABLA hujakutana nae tena (dawa za fungus za sehemu za siri kwa wanawake ni tofauti); Otherwise, utajitibu wewe, halafu ukirudi tena kwa mpenzi/mke wako, anakuambukiza tena, fungus zinarudi tena UPYA! Haya maelezo niliyokupatia ni muhimu sana ukayafahamu na ukayafuata,kabla na wakati unakunywa dawa, la sivyo kila siku wewe utakua ni mtu wa kunywa dawa za fungus.

Pole sana

da viper

PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HII
- Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake
 
Yo Yo,
Tiba yake ni kuzingatia usafi wa mwili hasa sehemu yeti,kama muwasho ni wa mara kwa mara ni heri ukaenda kumuona daktari.
 
Yo Yo,

Ndio tatizo la wagonjwa, hawatoi maelezo ya kutosha. Kuna muwasho tu au pia kuna discharge yeyote? Pia kuna changes zozote katika skin ya sehemu hiyo inayowashwa? Vipi haja ndogo ipo fresh? Umri wa mgonjwa?

Toa maelezo ya kutosha tumpatie msaada.
 
Last edited:
Yo Yo,

Hahaha shem mademu zako bwana unaniacha hoi. Inawezekana ni venereal diseases amabo nyingi ni sexually transmitted infections, sasa mazee usiuze naye mechi atakuachia mikuno. Tiba...awaone madaktari na kuchukua vipimo.
 
Ndio tatizo la wagonjwa,hawatoi maelezo ya kutosha.Kuna muwasho tu au pia kuna discharge yeyote?pia kuna changes zozote katika skin ya sehemu hiyo inayowashwa?vipi haja ndogo ipo fresh?umri wa mgonjwa?

toa maelezo ya kutosha tumpatie msaada
Hana dalili zingine zaidi ya kuwa na muwasho sehemu za siri, haja ndogo ipo fresh tu umri wake ni kati ya 23-30.

Hahaha shem, Inawezekana ni venereal diseases amabo nyingi ni sexually transmitted infections, sasa Mazee usiuze naye mechi atakuachia mikuno. Tiba awaone madaktari na kuchukua vipimo
Shem nakula vitu classic bana, hana STI yoyote maana ningejua si unajua kwa jinsia ya pili haichukui muda kujitokeza kawaona madktari kapewa vidonge kuweka huko chini bado nasikilizia kama muwasho utaendelea. Aaaah shem kuna sehemu kuuza mechi hakukwepeki.
 
Hana dalili zingine zaidi ya kuwa na muwasho sehemu za siri, haja ndogo ipo fresh tu umri wake ni kati ya 23-30....
Basi hiyo hali itakuwa inasababishwa na chemicals such as soap, cream, feminine spray ect

Hamna tatizo hapo mjomba, we endelea tu kuuza mechi.
 
Basi hiyo hali itakuwa inasababishwa na chemicals such as soap, cream, feminine spray ect

hamna tatizo hapo mjomba,we endelea tu kuuza mechi.
Wewe ni moja kati ya madktari bora nuilio wahi kukutana nao. Ubarikiwe mkuu.
 
Kuwasha sehemu ya siri kuna sababishwa na vitu vingi, huo siyo ugonjwa wa zinaa.

- Inawezekana hao ni fungus, hivyo inabidi akamuone daktari ampe vidonge vya kuingiza sehemu ya siri au cream ya kupaka.

- Vile vile inawezekana anapenda kuvaa chupi wakati sehemu ya siri sio kukavu, anapomaliza kuoga ahakikishe ajifute vizuri ndipo avae chupi, unyevu nyevu sehemu za siri unaweza kusababisha kuwashwa.

- Ahakikishe anajisafisha vizuri sehemu za siri, wanawake wana utoko sehemu zao za siri, hivyo ahakikishe kila siku kujisafisha hadi ndani ili utoko wote utoke. Kama akiwa na utoko nao unaweza kusababisha kuwashwa.

- Azingatie usafi wa hayo niliyotaja hapo juu, kama muwasho unaendelea akamuone daktari na achukuliwe kipimo cha mkojo.
 
Dada Yangu Pretty,

Ulicho kisema ni sawa na ninadhani kati ya wakina dada wanao jipiga mausafi wewe ni namba wani.

Me nadhani kuwasha kwa sehemu za siri nako kwatakiwa kufafanuliwa maeneo ya siri napo kumegawanyika kuna ndani ya eneo la siri na nje ya eneo la siri.

Me nta base kwa dada zangu na kuwapa hiki kifungu wakisome na kitawasaidia sana pia dada yangu pretty kipitie pia na uwaelimishe wengine

Yeast Infection Causes
Sometimes, taking antibiotics can cause yeast infection. One prime factor of the cause of yeast infection in pregnant women is the course of hormone changes as well as women undergoing menopause. Not only the women experience this infection, even men can contract the disease by engaging on sexual intercourse with women who are infected with it.

At times, overdoing the personal hygiene can be a major cause for this infection to occur.

Feminine washes and douches can sometimes cause fungal infestation. Too much cleanliness tends to kill the beneficial bacteria that normally protects and shields the body from the disease. Another factor when looking up the causes of yeast infection is clothing. This cause is often overlooked, but it also plays a big part in causing the symptoms to occur. Tight clothes tend to keep away the cold in the body; thus the fungus creates their environment.

Vaginal Yeast Infection
Yeast infection is better prevented than cured. That is why it is important to know its causes. Reading and researching can be a big help when it comes to preventing the disease occurrence. The most common yeast infection is the one which occurs at the vagina. This is caused by the organism Candida Albicans. During sexual intercourse, with or without the use of a protective item, the organism can be transferred.

Irritating soaps can be a candidate for causes of yeast infection. These are bubble baths, douches, and some feminine liquid wash. Although it is meant to clean you from the fungus, they can sometimes trigger and cause the infection themselves. Having proper hygiene can help prevent this kind of infection, but overdoing it can possibly be the cause of infection instead.

The overuse of antibiotics is also an agent to the cause of vaginal fungal infection, so are dairy products and beef. There are also foods that can cause yeast infection; here are some to name a few: grain, corn, apples, and peanuts. So it is better to know the causes of this disease so we can easily prevent them from happening. Bear in mind that prevention is always better than cure.
 
Sidhani kama ana ugonjwa wa zinaa kwa sababu ingekuwa ni ugonjwa ungeshapata dalili. Azingatie tu usafi na choo anachotumia kiwe safi ahakikishe amemwaga maji ya kutosha kabla ya kukitumia maana sisi kina dada tunachuchumaa, halafu anapoenda haja ndogo ajisafishe na maji na ajifute siyo kutumua toilet paper, na anapokuwa nyumbani ajisafishe kwa kutumia maji ya uvuguvugu aweke dettol ya maji ajaribu kuingiza kidole ajisafishe mpaka ndani hata kama kitauma ili kama ndani kuna uchafu unatoka uishe wote.
 
Ni Vizuri kutoa maelezo zaidi. Kuna kuwashwa kwenye ngozi inayozunguka sehemu za siri (perenial region) mara nyingi ni kwa sababu ya fungal infection au chawa (Phthirus pubis). La sivyo kuna kuwashwa ndaniiiii ambayo mara nyingi inakuwa na discharge ya iana fulani na pia vidonda. Sijui ni lipi linakusibu ndugu yangu?

Willy
 
Sidhani kama ana ugonjwa wa zinaa kwa sababu ingekuwa ni ugonjwa ungeshapata dalili. Azingatie tu usafi na choo anachotumia kiwe safi ahakikishe amemwaga maji ya kutosha kabla ya kukitumia maana sisi kina dada tunachuchumaa, halafu anapoenda haja ndogo ajisafishe na maji na ajifute siyo kutumua toilet paper, na anapokuwa nyumbani ajisafishe kwa kutumia maji ya uvuguvugu aweke dettol ya maji ajaribu kuingiza kidole ajisafishe mpaka ndani hata kama kitauma ili kama ndani kuna uchafu unatoka uishe wote.

Naweza sana kufanya hii kazi kuna dada yeyote anayehitaji msaada wangu? Hakuna malipo!
 
na anapokuwa nyumbani ajisafishe kwa kutumia maji ya uvuguvugu aweke dettol ya maji ajaribu kuingiza kidole ajisafishe mpaka ndani hata kama kitauma ili kama ndani kuna uchafu unatoka uishe wote.

Huu ni upotoshaji Joyce.

Dettol ni antiseptic disinfectant, tena strong germ killer. Kuitumia sehemu hizo kila mara kutasababisha kuondoa hata normal flora ambao ni muhimu katika eneo hilo.

Tumia Dettol eneo hilo kama tu umeshauriwa na daktari tena aliyebobea katika maswala hayo, sio general doctor.
 
Naweza sana kufanya hii kazi kuna dada yeyote anayehitaji msaada wangu? Hakuna malipo!

Masa ndugu yangu, to be honest kila nikimuona huyo dogo [AVATAR] anavyopata dhoruba ya hiyo miba na mimi nahisi muwasho na maumivu... msaidie basi maana huwa hayo majani yenye miba yanavimbisha sana asije akajaza monitor.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom