Uenyekiti wa UWT: Ni Vita Kati ya Ukweli na Ubatili!

Si kweli kwamba sipendwi na wanaume – Sophia Simba
Mwandishi Wetu

Toleo la 130
21 Apr 2010


  • Anaanika mahusiano yake na Kitwana Kondo
  • Asema UWT ya sasa ni ya dot com
  • Asema mkataba na mwekezaji wa jengo la UWT aibu tupu


Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), amekuwa akisemwa wakati mwingine kwa mafumbo kuhusu masuala ya mahusiano ya kimapenzi aliyopata kuwa nayo. Katika mahojiano na gazeti hili, mama huyo, miongoni mwa mambo mengine, aliamua kuwa muwazi juu ya mahusiano hayo na pia masuala kadhaa yanayohusu UWT.

Raia Mwema: Wasomaji wetu wangependa kukufahamu kwa sababu mengi yamekuwa yakisemwa na yakinong'onwa hususan kuhusu elimu yako; labda kwa vile hawaifahamu vizuri. Unaweza kutupa CV yako kwa kifupi?

Mama Sophia Simba: Asante kwa kunipa nafasi hii adimu. Nimefurahi kwamba umeweza kufika ofisini kwangu na kuweza kuongea na mimi. Nashukuru kwamba umeona upo umuhimu wa watu kunijua mimi Sophia ni nani hasa.

Ni kweli maneno mengi yamekuwa yakisemwa ambayo hayapendezi, lakini nitafanyaje? Kwa hiyo, kwa kifupi sana ningependa nikufahamishe labda pengine kwa kupitia wewe watu watanifahamu. Mimi naitwa Sophia Simba. Ni Sophia Mathew Simba. Nyambi ni jina langu la nyumbani. Wazaramo wana majina yao ya ukoo, kwa hiyo mimi ni Nyambi na mdogo wangu alipewa jina lingine. Nilipokuwa mdogo baba yangu akasema huyu ni Nyambi.

Kwa kifupi sana, mimi ni mtoto wa mfanyabiashara. Baba yangu alitokea Kisarawe, kijiji kinachoitwa Sungwi. Baba yangu alisoma Minaki. Alipomaliza Minaki alirudi hapa Dar es salaam. Baba yangu aliwahi kufanya kazi mpaka ya uvuvi. Aliacha shule kutokana na umbali kutoka kijijini kwake Sungwi kwenda Minaki.

Watoto waliokuwa wakitoka bara walikuwa wanasoma boarding, lakini watoto wa Kisarawe wenyewe walikuwa wanatakiwa watembee umbali mrefu. Kwa hiyo, kutokana na hiyo alifikia mahali haikuwezekana. Baba yangu mwanzoni alikuwa Mwislamu. Alikuwa anaitwa Omari Simba. Kutokana na kusoma pale Minaki, aliamua kubadilisha dini. Baba yangu alibatizwa katika Kanisa la St. Albans - hili la hapa mjini. Na baada ya hapo baba yangu aliondoka akaenda Morogoro kufanya shughuli za biashara.
Kule alikutana na mama yangu, mwanamke wa Kiluguru ambaye naye historia yake alikuwa Sister wa Roman Catholic. Kwa hiyo walikutana na wakaoana.

Katika maisha yetu yote tumeishi kama Wakristu wa Roman Catholic. Mpaka leo mimi ni Mroman Catholic ingawaje kila mtu ananipa dini ambayo anaitaka. Kwa hiyo, mimi ni mmoja wa watoto tisa. Mimi ni wa pili.

Raia Mwema: Makazi yenu hasa yalikuwa wapi?

Mama Sophia Simba: Makazi yetu yalikuwa Dar es salaam na Morogoro. Dar es Salaam tuliishi Bungoni, Ilala. Lakini tukiwa wadogo kabisa baba yangu alijenga nyumba yake ya kwanza kabisa Morogoro, Kwa Kingu.
Alifanikiwa sana kwa shughuli za baa. Mimi ni mtoto ambaye nimesomeshwa kwa pesa za pombe. Baba yangu alikuwa na baa inayoitwa Uzaramo Bar, Morogoro lakini pia alikuwa na baa inayoitwa Simba Bar. Kwa hiyo, mimi kufungua vizibo vya bia najua.
Nikiwa bado mdogo nilikuwa nauza mishikaki. Siku zote nyumba yetu ilikuwa upande baa, upande tunaishi sisi. Kwa hiyo, baba yangu aliendelea na shughuli za baa muda mrefu.

Raia Mwema: Ulianza shule wapi?

Mama Sophia Simba: Mimi nilianza shule Morogoro katika shule inayoitwa Kilakala, baada ya hapo nikapelekwa shule ya boarding inayoitwa Ilonga Middle School, Kilosa. Baada ya hapo nikasoma Forest Hill Secondary School. Sisi ndiyo waanzilishi wake.
Ule mwaka ambao wanafunzi wengi tuliambiwa hatukuchaguliwa tuliunganishwa darasa la saba na la nane. Kwa hiyo sisi tulimalizia darasa la nane. Huo ulikuwa mwaka 1965. Shule nyingi (za binafsi) zilianzishwa mwaka huo. Shule za Kibohehe, Forest Hill, Mzizima na Kinondoni, zote zilianza wakati huo.

Baada ya pale nikaenda Kibosho Secondary School. Kwa bahati mbaya baba akafariki, wakati huo nikiwa nafanya kazi NDC. Kabla hajafariki, baba alitaka sana nifanye shughuli za biashara, niendeleze biashara ya familia. Baada ya kumaliza shule nilichaguliwa nikasomee ualimu lakini sikwenda, na badala yake nikapata kazi NDC. Hapo NDC nilianza kazi 1971 hadi mwaka 1979.
Baada ya hapo nikaingia Lonrho Group of Companies baada ya kuacha kazi NDC. Kutoka pale nikaanza kazi Metal Engineering Industries Development Association (MEIDA) ambayo ilianzishwa na Waswedish. Nikiwa hapo nikaamua kwenda kusoma. Nilianza mafunzo ya Certificate of law mwaka 1985. Nilipenda sana kusomea sheria.

Mwaka 1987 nilianza kusomea shahada ya sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na nikahitimu mwaka 1992 au 1993. Kuna mwaka hapo katikati chuo kilifungwa kwa sababu ya kuwapo mgomo. Baada ya kuhitimu Chuo Kikuu nikarudi kufanya kazi Metal Industries; kwani wakati nasoma walikuwa wamenipatia likizo isiyokuwa na malipo. Baada ya kurudi walinipandisha cheo kuwa legal and administrative officer; kwani kabla ya kwenda chuo kikuu cheo changu kilikuwa administrative officer tu.
Wakati niko NDC nilikuwa katibu wa tawi la UWT la NDC na Mama Anna Mkapa alikuwa mwenyekiti wetu, tulifanya mambo mengi mazuri.

Nilipokuwa MEIDA niliomba pia kuwa diwani wa viti maalumu. Kulikuwa na uchaguzi mwaka 1993 au 1994. Nikawa diwani hadi 1995. Mwaka 1995 wakasema kuna viti maalumu vya ubunge kwa akina mama. Mimi nikagombea vitu maalumu. Mwaka huo wa 1995 nilipata invitation ya kwenda Beijing, China kuhudhuria mkutano wa wanawake duniani. Nikakataa, nikampa mwenzangu nikamwambia mimi siendi nitabaki hapa kwa ajili ya kampeni za ubunge. Sikwenda mimi Beijing kwa sababu ya kampeni hiyo. Kwa hiyo mwaka 1995
Nikashinda, na hivyo nikaingia bungeni.

Mwaka 1995 nilifanya mafunzo ya Post Graduate Diploma on Women Law kwenye Chuo Kikuu cha Zimbabwe na mwaka 2005 nilifanya Masters ya Community Economic kwenye Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Thesis yangu ilikuwa Women and Economic Empowerment in Tanzania. Mwaka 1972 mimi niliolewa. Mume wangu alikuwa ni mwanasheria wa Chama cha Ukombozi cha Afrika Kusini cha ANC. Siku zile walikuwa wakiwaita wakimbizi, lakini wenyewe walikuwa wanataka waitwe freedom fighters.

Mume wangu aliruhusiwa pia kufanya kazi za uanasheria nchini. Kabla ya kufariki aliwahi kufanya kazi pia benki. Alikuwa anaitwa Clifford Zex Senge. Wengi walikuwa wanamwita kwa jina la Cliff. Wanasheria wengi wanamjua. Kwa hiyo, niliolewa na Cliff na nikazaa naye watoto wawili. Watoto hao walikwenda Afrika Kusini kwa baba yao lakini sasa wote wamerudi. Maisha ya Afrika Kusini ni magumu hayako that easy. Kuna watu wanasema mimi ni kituo cha polisi, wanaume wananikimbia. Nilisoma kwenye gazeti (eti) wanaume hawanitaki. Lakini I was married.

Raia Mwema:Uliolewa na Msouth Afrika na kwa bahati mbaya akafariki dunia. Lakini nasikia ulikuwa na mahusiano na ulionekana mwaka 1995 ukiwa na Kitwana Kondo, Meya wa zamani wa Dar es Salaam na mbunge wa zamani wa Ilala. Uhusiano wako na yeye ulikuwa wa aina gani?

Mama Sophia Simba: Sawa, mimi nilikutana na Mzee Kondo… Kwanza nakubali nilikuwa na mahusiano naye, na nimezaa naye mtoto wa kiume. Nilikuwa na Mzee Kondo kutoka mwaka 1975. Nilikutana naye wakati akigombea ubunge; mimi nikiwa kama mpiga debe wake. Kwa hiyo tulikutana mwaka 1975 na tukaachana mwaka 1983.

Siyo kama tulioana, hapana, alikuwa boyfriend. Yeye siku zote amekuwa na mke wake. Kwa hiyo, nilizaa naye kweli mtoto mmoja na mpaka sasa hivi mimi namuheshimu Mzee Kondo. Na baada ya hapo, mwaka 1983, ameshaoa mara mbili au mara tatu lakini mimi bado namheshimu mpaka watu hawaelewi mahusiano yangu mimi na yeye yakoje. Hata tulipokwenda bungeni watu wengine walidhania ni mtu na mkewe, lakini mimi sijaolewa na Kitwana Kondo. Namheshimu sana, ni baba wa mtoto wangu.

Raia Mwema: Sasa tuje kwenye nafasi yako ya uenyekiti wa UWT. Wewe katika miaka yako hii mitano unataka UWT iwe ya namna gani baada ya kuvaa kofia iliyovaliwa na wanawake wazito huko nyuma kama Bibi Titi Mohammed, Sophia Kawawa na Anna Abdallah?

Mama Sophia Simba: Asante kwa swali hilo. Kwanza nishukuru walionitangulia kwamba wamefanya kazi kubwa. Wao ni role models ambao tulikuwa tukiwatizama na sisi kufanya kazi chini yao. Nikiri kwamba nimefanya kazi chini ya Mama Sophia. Alipokuwa mwenyekiti, mimi nilikuwa katibu wa tawi. Mama Abdallah alipokuwa mwenyekiti wa taifa, mimi nilikuwa mwenyekiti wa UWT tawi la kata ya Upanga Magharibi. Kwa hiyo, hawa wote wamekuwa viongozi wangu na nimewaona walivyokuwa wakifanya kazi.
Mimi katika kipindi hiki cha miaka mitano nitaendeleza yale yote ambayo nimejifunza kutoka kwao, lakini pamoja na hivyo; mambo yamebadilika. Itabidi na sisi UWT tubadilike.

Ukumbuke kwamba hapo nyuma mimi nilipoinga UWT nilikuwa mfanyakazi. Sasa hivi baada ya matawi ya kazini ya chama kuvunjwa, kumekuwa na gap hapo. Wafanyakazi wengi wapo wapo tu. Wanawake wengi hawapo katika chama, hawapo katika jumuiya, wapowapo tu. Wapenzi wengi wa CCM wako kama vile wa Simba na Yanga - hawana kadi, hawana nini. Kwa hiyo, mimi mkakati wangu mmoja mkubwa ni kuhakikisha nawapata hawa akina mama. Nitawafuata hukohuko waliko katika maeneo yao kuwahamasisha kuinga UWT.

Hadi sasa tunaendelea vizuri. Tuna kitengo kizima kinachoelezea jinsi ya ku-capture na kuwahamasisha akina mama na kuwaambia; na wewe pia unaweza kuwa mwanachama wa UWT, unaweza kuwa mwanachama wa CCM, usikae tu bure hivi hivi.
Kwa kufanya hivyo, UWT itakwenda na wakati. Tunawahitaji hawa young generation twende nao tusiwaache nyuma. UWT isiwe jumuiya ya wazee na watu wazima tu.

UWT iwe ni jumuiya ya wanawake vijana pia, kwa sababu naamini ukishirikiana na vijana kuna mengi ambayo utaweza kujifunza. Tunaweza tukaifanya UWT ikawa hatua moja zaidi kutoka hapa tulipo. UWT tumejipanga kuanzisha tawi la UWT makao makuu. Na lingine ambalo tumesema tutafanya ni kuifanya UWT isiwe tegemezi kiasi hicho. UWT ina mali zake nyingi ambazo zimekuwa dormant kwa muda mrefu. Kwa hiyo, tunataka tuzitumie ili tuweze kwa kiasi fulani tujitegemee.

Hivi sasa watendaji wote UWT wanategemea ruzuku kutoka CCM. Kwa hiyo, tunakipa mzigo mkubwa sana Chama cha Mapinduzi. Lazima tuangalie ni jinsi gani tunaweza tukatumia raslimali tulizokuwa nazo, nadhani tutaipunguzia mzigo CCM. Kama nilivyosema siku yangu ile ya kwanza, ni lazima twende na wakati. Nilitumia maneno: ‘UWT iende na dot com.' Generation ni dot com, tusirudi nyuma.

Raia Mwema: Lakini baadhi ya watu wanasema kwamba labda umeanza na gea ngumu kidogo baada ya Katibu Mkuu wako, Husna Mwilima kuwa amewajibishwa na Baraza Kuu. Huoni kwamba kitendo hicho cha kumwondoa ni hatua ngumu kwako?

Mama Sophia Simba: Kwanza nikiri kwamba si jambo zuri kwamba katibu mkuu wangu imebidi Baraza Kuu limwondoe. Mimi binafsi siyo kitu ambacho nilitarajia, kwa sababu mimi ndiye niliyemtafuta yeye na jina lake kulipeleka kwenye vikao vya chama ili lipitishwe.
Kwa hiyo, hiyo imeonyesha kwamba ni udhaifu kwa upande wangu. Nikiri kwamba sikulifanyia kazi vizuri lile jina. Pengine nilikuwa sikujiandaa vizuri. Binadamu kufanya makosa ni kawaida, na pale nilikosea.

Hata hivyo, nilijitahidi sana kufanya naye kazi vizuri. Nimekaa naye kipindi cha mwaka mmoja. Unapopewa madaraka inabidi kwanza ujifunze, kwa hiyo nilijitahidi sana kuhakikisha kwamba katibu mkuu huyu, ambaye mimi mwenyewe nilimtafuta, aweze ku-cope na ile ofisi. Lakini kukawa kuna matatizo ya… Kwanza huwezi kumfananisha huyo na akina Thecla Mchauru, Kate Kamba, Dk Msimu ambao kiwango cha elimu yao kidogo ilikuwa zaidi. Hata Halima Mamuya elimu yake iko juu zaidi ya huyu.

Huyu alibebeshwa mzigo ambao hakustahili, tulifanya makosa. Tulimbebesha mzito mkubwa wa kiutendaji. Pengine kisiasa kazi nyingine angeweza kuzifanya, lakini kiutendaji… Kuna kazi za utendaji zina miiko yake ambayo kiwango cha elimu yake ilikuwa kidogo kina matatizo.

Raia Mwema: Sawa kulikuwa na makosa, lakini wewe ulimpataje pataje hadi akaukwaa ukatibu mkuu wa UWT?

Mama Sophia Simba: Huyu alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu la UWT, ndicho kitu kimoja ambacho kilinifanya nimteue. Nimekuwa naye kwenye baraza tokea mwaka 2003. Mimi nimemjua Husna wakati nikigombea ujumbe wa Baraza Kuu. Kwa hiyo, nilipokwenda Arusha yeye ndiye aliyenisaidia kutafuta kura, siyo campaigner, lakini ndiyo nilianza kumfahamu. Lakini nikamfahamu pia ndani ya vikao. Kwa hiyo nilimjua kwa hivyo. Na kwa bahati mbaya sana, sikujaribu kuomba ushauri kwa mtu yeyote kutaka kujua habari zake zaidi. Ndiyo maana nasema nakiri makosa. Hakuna mtu aliyenishawishi kuhusu yeye.

Raia Mwema: Eneo lile la Maria Hostel kulikuwa na mpango wa kujenga jengo kubwa kuondoa hali ya utegemezi ya UWT ambayo umekwishaieleza. Je mpango huu bado upo?

Mama Sophia Simba: Mpango wa kuendeleza kiwanja cha mtaa wa Lindi cha Maria Nyerere Hostel upo. Tumekuta mpaka na ramani zimeshachorwa, lakini sisi kamati yetu ya utekelezaji tunataka tujiridhishe, tutumie utaalamu zaidi. Lile jengo tulilolikuta pale linataka kujengwa lilikuwa haliendani na wakati.

Kwa hiyo, tulichokuwa tukingojea kwanza ni kupata Baraza la Wadhamini kwa sababu lile baraza la wadhamini lililopita la UWT, limemaliza muda wake. Sasa limepatikana jipya. Majuzi walikuwa na kikao chao cha kwanza cha Baraza la Wadhamini. Mwenyekiti wao ni Mzee Said El Maamry ambaye ni mwanasheria. Tumelizindua baraza letu na sasa tunachotaka ni kupata hati ya pale Maria Nyerere. Maria Nyerere ilikuwa trusteeship ya Tanganyika Women, sasa hivi ni Tanzania Women. Jina limeshabadilishwa, na sasa tunangojea hati mpya. Tukishapata hati tutaweza kuwekeza pale na kujenga kitu kizuri.

Raia Mwema: Kitu kizuri namna gani, kwani mnataka kujenga kitu gani?

Mama Sophia Simba: Tunataka tujenge office blocks na apartments, na sisi wenyewe tutakuwa na floor moja kwa ajili ya ofisi zetu. Tutakuwa na ukumbi wetu mkubwa wa mikutano, ni vitu kama hivyo.

Raia Mwema: Sasa hebu tuelezee kuhusu jengo jipya lile ambalo lilikuwa makao makuu. Nini mnachotarajia kupata kutoka hapo kwa sababu nalo lilileta minong'ono.

Mama Sophia Simba: Jengo jipya limekwisha, linangojea kufunguliwa. Lakini kwa kifupi sana niseme kwamba jengo hilo jipya haliko chini ya management ya UWT. Jengo jipya mkataba uliosainiwa ulikuwa ni mkataba wa UWT kulipwa certain amout of money kwa mwaka, hakuna percentage.

Mkataba uliosainiwa haukuwa mzuri. Kwa hiyo, sisi UWT hatuna eneo lolote. Sisi tutakuwa tunapata kodi ndogo tu. Kiwanja bado ni cha kwetu, lakini lile jengo wale tumeingia nao mkataba wa miaka 33. Kwa hiyo they will run that thing kwa muda wa miaka 33. Sisi tutapata pesa kidogo. Naona aibu hata kuzisema. Pesa tutakazozipata kwa mwaka hazisaidii hata kuwalipa mishahara makatibu wetu wote wa jumuiya lakini ndiyo hivyo tumejifunza kutokana na makosa.

Raia Mwema: Hivi hakuna namna ya kuweza kukutana na waliowekeza mkajadiliana nao kurekebisha huo mkataba?

Mama Sophia Simba: Mkataba uliopo ni binding, mkataba umeshaingiwa. Hiyo amount ambayo imefikiwa ni ambayo baada ya kuzungumza nao wakaongeza. Lakini sisi tunasema tumeshajua pale yeye anakodisha kwa kiasi gani, basi tunataka tumwambie, basi, na sisi tuongezee kigogo, lakini hiyo ni subject ya mazungumzo ya sisi na yeye.

Raia Mwema: Bunge linalokwisha kwa sasa lina wanawake wanaowakilisha majimbo 17. Je, mnao mkakati wowote wa kuweza kuwasaidia wanawake kuwa na ushindani wa kutosha na wanaume kwenye majimbo?

Mama Sophia Simba: UWT tayari tumeshatengeneza mkakati wetu wa kuhakikisha wanawake wengi zaidi wanajitokeza kugombea kwenye majimbo. Majimbo siyo ya wanaume, majimbo ni yetu sote kwa hiyo kuna ziara tumeshajipanga. Tutazunguka nchi nzima kuhakikisha wanawake wanajitokeza kugombea kwenye majimbo. Tutahakikisha wanakwenda kupiga kura na kuhamasisha wanawake kuipigia kura CCM. Kwa hiyo tunakwenda kupiga ndege watatu kwa jiwe moja.

Naamini itakapofika mwaka 2015 wanawake watakaokwenda kwenye majimbo watakuwa wengi zaidi kwa sababu tumeshawawekea ukomo. Wengine wamekuwa wabunge wa vitu maalumu kwa miaka 15 na wengine hivi sasa wameshaingia miaka 20, na bado hawajathubutu kugombea kwenye majimbo. Lakini kwa sasa mkakati tulionao ni kuhakiksiha wanawake wengi wanajitokeza.

Raia Mwema: Halmashuru Kuu ya CCM imekubaliana na pendekezo la Baraza Kuu lako juu ya ukomo wa viti maalumu, lakini baadhi ya wabunge waliopita wa muda mrefu ambao wanadhani mlikuwa nao, wanadai mumewatosa. Hayo manung'uniko yao wewe unayajibuje?

Mama Sophia Simba: Nafurahi kupata nafasi hii nijibu hilo. Suala la ukomo wa viti maalumu halikuanza na mimi. Suala la ukomo wa vitu maalumu tumeanza kulizungumzia mwaka 1998 au 1999. Lakini kwa sababu sisi wenyewe tuko mle mle kwenye baraza Kuu, likaminywa. Likarudi tena 2000 hadi 2005. Likazungumzwa tukiwa Arusha, likazungumzwa tukiwa Moshi. Watu wanalipooza kwa sababu kila binadamu tuna kitu kinaitwa choyo, unajifikiria wewe. Kwa hiyo, lile jambo ni jambo la siku nyingi. Hao wote wanaolalamika wanalijua, wanaiongopea jamii.

Suala la ukomo halikuletwa na Sophia Simba, suala la ukomo lililetwa na Baraza Kuu, isipokuwa kwenda kwenye NEC ndiyo limepelekwa safari hii. Tatizo ni kwamba siku zile tulikuwa tunalizungumza kwenye Baraza Kuu lakini halitoki kwenda NEC. Hivi sasa limekwenda kwenye NEC, na kwa bahati mbaya sana hao wanaolalamika wengine wameshakuwa wabunge miaka 15, wengine miaka 10. Baraza Kuu lilisema kuwa nafasi za vitu maalumu ambazo ni za upendeleo, siyo wapendelewe hao hao tu kila siku. Ziliwekwa ili kumuwezesha mwanamke aweze kupambana na vile vigezo ambavyo tumesema vinatufanya wanawake tushindwe kuingia kwenye majimbo nao kwa sababu ya kuwapo mfumo dume.

Tumesema wanawake kwa sababu ya mfumo dume tuna aibu, hatuwezi kuongea kwenye majukwaa. Kwa sababu ya mfumo dume wanatutukana (eti) tunaogopa lakini tunasema pia kwamba mwanamke hana pesa za kwenda kwenye kampeni.
Sasa Baraza Kuu linasema huyu mwanamke au mama baada ya miaka kumi amekaa bungeni amekwenda kwenye mikutano, ana pesa anashindwa nini? Aende zake kwenye jimbo. Hiyo ndiyo concept tuliyozungumza kwamba tayari ile kazi ya upendeleo imeshafanya kazi. Imeshamtengeneza huyu mwanamke kuwa mwanasiasa.

Sisi shida yetu tunakata tuwe na wanawake wanasiasa wengi. Sasa hawa wanakuwa kama selfish, wanaona wao. Kuna mwingine anathubutu anasema ‘he mimi kule kwangu nikitoka mimi, sina jimbo kule. Lakini kama huna jimbo wewe ukitoka mwanamke mwingine atachukua nafasi yako, kaa pembeni. Kwa hiyo mimi wananionea kusema kwamba nimewacha kwenye mataa. Na hao kwanza waliokaa wanaosema kwamba nimewatosa, mimi UWT nimechaguliwa na wanawake wa Tanzania yote.

Na nimechaguliwa; hivyo siyo kazi yangu kulipa fadhila. Nimechaguliwa niwahudumie wanawake wa Tanzania na kwa kufanya hivyo, kwa kuweka ukomo baada ya miaka kumi tutaona majimbo mangapi wanawake watachukua. Watajitokeza tu, sisi wanawake tunapenda sana kusukumwa. Sasa nenda hapa, sasa nenda pale. Mama Anna Abdallah aliweza mwaka 2005 kutusukuma. Aliniambia Sophia nenda Ilala, wewe fulani nenda pale. Isitoshe siku hiyo kwenye Baraza Kuu ajenda ya kuwe na ukomo haikutoka kwenye kamati yangu ya utekelezaji, ilitoka pale pale barazani.

Hilo ndilo lililotokea kwa hiyo kina mama popote walipo naomba wasilichukulie hilo kama ni langu binafsi isipokuwa hofu ya wale wanaotaka waendelee na wasiotaka wenzao wengine wapata hizo nafasi ndiyo iliyofanya waende wakapeleke hadithi hizo.
Lakini siku moja wataniona shujaa. Kwa suala hili kulipeleka kwenye NEC ilikuwa kazi kubwa, lakini imewezekana. Hata hivyo, NEC imesema lisianze mwaka 2010, litaanza mwaka 2015. Mwaka 2015 ni keshokutwa tu panapo na uhai. Kwa hiyo tutaona sura mpya zinaingia.
 
Wanabodi,
Kipenga cha kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UWT kimepulizwa na wa kwanza kukimbilia fomu ni Mwenyekiti wa sasa Mhe. Sofia Simba akijiaminisha atapata kwa mteremko wa kupita bila kupingwa maana CCM inatawaliwa na nidhamu ya woga kwa jina la "utii", lakini hali haikuwa hivyo kwani Mhe. Mama Anne Kilango Malecela ametia timu kumpinga Mama Simba ambae "she is good for nothing"!. Mama Kilango ni just an opportunist mpiga kelele kila anapoongea as if ana uchungu wa kweli na anachopigia kelele!.

Ila kumlinganisha na mama Simba, Kilango ni mpiganaji wa kweli kwani baada ya kubebwa pale mwanzoni, sasa amejibeba na kubebeka zaudi wakati Simba yeye ni kubebwa tuu mwanzo mwisho!.



K
Mark my words!.

Pasco!.

.

I have marked your contradictory words about Mamas Simba and Kilango.

Thank you for being a good campaigner! vijana oyeee!
 
Hizi ni changamoto kwa sisi CDM members especially viongozi wakae chini na kutafakari strategies ambazo zitakuwa bora ktk kuikuza BAWACHA ili tuendane vizuri na hii political competition.

FEAR NOT.
 
CV ya Mayrose Kavura Majinge: ana Masters ya Public administration; an exposure kubwa kwenye mambo ya uongozi;

Nimesoma CV ya Maryrose it is relatively impressing when comparing to her competitors i.e Sophia Simba and Anna Kilango.

As far as ni Gamba don't expect too much from her.

On serious note Mayrose kama msomi angeto fautisha papers za kwenye conference proceedings na PUBLICATIONS. Naomba asahihishe hapo!
 
CV inakubalika kabisa. Nafikiri CCM wameishabadilika na wanajua changamoto zilizombele yao. Wakijua hilo hawatachukua watu kwa mazoea. Kila la kheri.
 
Mkuu Wa Ukenyenge, sina CV yake rasmi ila ni msomi mwenye masters. Sifa yake kuu ni kitabu fulani alichoandika kuhusu vita dhidi ya umasikini!.

Huyu Mayrose she is real good ambaye anaweza kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya CCM kwa ku invoke changes from within!.

Kwa vile huyu ni mdada wa ukweli, bado anaamini a dying CCM can be revived kupitia UWC!. Kumbe bado hajajua, uwongo, fitna na majungu ni mtaji mkubwa wa ushindi kwenye uchaguzi wowote wa ndani ya CCM.

Huyu Mayrose ana tatizo moja kibwa, she is too genuine hivyo kuwa too good kwa CCM, I hope baada ya uchaguzi huu wa UWT, she'll realize she is in a wrong party, anapoteza bure time, money na her very promising potentials to try reviveing a dying CCM!.

I wish her all the best!.
we gamba vp hujagundua kuwa uko kwenye wrong party?poor you
 
Nimesoma CV ya Maryrose it is relatively impressing when comparing to her competitors i.e Sophia Simba and Anna Kilango.

As far as ni Gamba don't expect too much from her.

On serious note Mayrose kama msomi angeto fautisha papers za kwenye conference proceedings na PUBLICATIONS. Naomba asahihishe hapo!

Bobuk,

..nimeshangaa Maryrose ameweka kabila ktk CV.

..Sophia Simba ana LLB na PG Dip ya masuala ya kina mama. sasa ukichanganya hiyo na uzoefu wake ndani na nje ya siasa anaweza kuwa na CV "kubwa" zaidi ya Maryrose.

..kinachotakiwa kuangalia ni link kati ya CV, ahadi za mgombea, na matamanio ya wanachama wa UWT[CCM].

NB:

..sometimes CV is not everything. Hillary Clinton alikuwa na CV "kubwa" kuliko ya Obama lakini alishindwa.
 
Pasco, Nimependa Lips zake

Mkuu Pasco, ningeomba utuwekea profile ya huyo mwanamama Bi. Mayrose Kavura Majinge, wengi hatumfahamu kiasi cha kubaki tunajiuliza ni nani haswaaa hadi awe tumaini jipya kwa UWT?
2.JPG
 
Mkuu Mamndenyi, very unfortunately waalimu sio wanasiasa!, hawa ni watu wa wito hivyo ni wa kupelekwa pelekwa tuu!.

Umesema kwa vile waalimu wengi ni wanawake, na kwa vile wamedhalilishwa hivyo watajitoa CCM?!. Hivi kumbe waalimu wengi ni CCM?!. Mimi nilifikiri waalimu ni just professionals hivyo have nothing to do with CCM!.

Mpaka leo katiba ya CCM inasema CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi, hawa wafanyakazi ni wepi???? Unajua sisi wanachama tunapoanza kukatishwa tamaa na ujuha kama huu ndani ya CCM na kuonekana ni wasaliti, liwalo liwe, kwani tunafanywa wapuuzi sana! Vinginevyo Inawezekana wewe unajua wafanyakazi hao ni wepi, na ingekuwa bora utuelimishe, vinginevyo ukubali tu kwamba CCM kama chama haina dira wala mwelekeo!

Enzi za TANU na hata CCM kabla ya mwaka 1992, ili upate ajira ya aina yoyote ile, hata dereva wa UDA, ilikulazimu kwanza uwe mwanachama wa CCM. Hii ni kwa sababu nchi yetu ilikuwa ni ya wakulima na wafanyakazi walioamua kushikamana pamoja nyuma ya CCM na kufanya kazi kwa bidii, huku fedha zao zikitumika kuleta maendeleo ya kijamii (elimu, afya, maji) na vile vile maendeleo ya kiuchumi kwa kuendeleza kilimo na viwanda kwa faida yao. Baada ya hapo, ghafla mambo yakabadilika bila taarifa rasmi jinsi gani wajiandae na transformation. Kilimo chao, viwanda vyao, vyote vimehamishiwa kwa wafanyabiashara ambao hawapo kweney equation inayozungumzia nani ni mmiliki wa chama kikatiba i.e. Mpaka leo katiba inasema CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi, lakini jasho lao lote linafaidisha wafanyabiashara ndani ya chama. Suala la ualimu kuwa wito lilikuwa relevant katika mazingira ya awali kwani waliona faida ya jasho lao katika ujenzi wa taifa - kulikuwa na mishahara inayokidhi haja zao, kulikuwa na vitendea kazi, na zao la kazi yao lilionekana kwani vijana wengi waliendelea na elimu mpaka ya juu na kupata ajira.

Katika mazingira ya sasa, wito unajengewa hoja gani wakati kwanza mwalimu hana thamani tena, kwani watoto wa watunga sera na watendaji wa sekta hii muhimu wapo shule binafsi za ndani na nje ya nchi. Pili walimu hawaoni zao la kazi yao kwani vijana wenye elimu hawana pa kukimbilia tofauti na miaka ya nyuma ambapo private returns to education kwa mtu ilikuwepo. Tatu hakuna vitendea kazi, sana sana ni wazo la shule la kata ambalo limejaa siasa zaidi na mbaya zaidi linalenga maendeleo ya sekta ya elimu in terms of quantity at the expense of quality.

Hoja ya Mamndenyi ni hoja ya msingi sana, sijui kwanini haulioni hilo. Ushindi wa CCM hasa mikoani umekuwa unachangiwa sana na walimu kwani hawa ndio wasimamizi wa chaguzi, lakini muhimu sana ndio wanao influence watoto ambao ndio wapiga kura wa baadae wawe na mtazamo gani kuhusu maendeleo ya nchi yao kisiasa, kiuchumi, na kijamii. Kumbuka, socialization process ya mtoto ipo through maeneo makuu mawili: malezi nyumbani (wazazi) na mazingira ya shule (walimu),lakini sote tunakubali kwamba watoto wetu wanatumia muda wao mwingi sana katika maisha yao ya utoto na walimu kuliko wazazi. Sasa kwanini tusiwaheshimu watu hawa????? Repercussions siku za mbeleni zitakuwa kubwa sana. Time will tell.

Mimi ni mwana CCM, let me declare my interest but still nakubaliana na hoja ya Mamndenyi kwamba walimu watahama CCM - kuhama aina maana kwamba walikuwa wanachama wa CCM wenye kadi za uanachama, bali wengi walikuwa watanzania wenye imani na mapenzi na CCM tangia enzi za TANU, hivyo walikiunga mkono CCM kwa wingi sana.
 
Bila shaka Pasco, atakuwa kampeni mananger wa Mayrose, maana unavyo watisha wana CCM kuhusu kuwapitisha Mama Kilango na Simba eti ndio utakuwa mwisho wa CCM...





Hata wakimpitisha huyo Mayrose aliyekutuma uje upingie debe hapa Safari ya CCM kuelekea kaburini iko pale pale, CCM ni kama mgonjwa wa Cancer ambaye yupo kwenye hatua ya mwisho hivyo hakuna miuzijiza ya kupona tena hapo.
 
Wanabodi,
Ila wale mnao amini mimi ni gamba, endeleeni kuamini hivyo kwa sababu kuwa mwana CCM sio dhambi wala kuishabikia CCM sio kosa!.
Tofauti na wewe Pasco, mimi naamini kabisa kwamba adui mkubwa wa Tanzania, ni CCM na hivyo kuendelea kuwa mwana CCM ni dhambi kubwa na kuishabikia ni kosa lisilosahemeka...kwangu mimi;

  • Uanachama CCM ni hatua ya awali katika ujenzi wa tabia za kifisadi,
  • Ubunge CCM ni hatua ya pili inayotoa fursa ya kutetea tabia za kifisadi,
  • Uwaziri ni tuzo kwa kuwa mtiifu katika kuimarisha tabia za kifisadi na
  • Uraisi ni hatua ya mwisho ya heshima kwa kulinda na kusimamia tabia za kifisadi...liwalo na liwe!
Kwa hapa tulipofikia, yeyote anayekubali kuhusishwa kwa namna yoyote na hiki chama ni mbinafsi, mnafiki na fisadi na moja kwa moja ni msaliti wa taifa...hayo sitachoka kuyasema.
 
Ukweli na Ubatili...! Wagombea Maryrose,Sofia na Anne...! Utata mtupu. Mkuu Pasco siku hizi najitahidi kusoma thread zako lakini sikupati kabisa.
 
Pasco, ndo huyu unayenpigia debe? Mbona amechoka sana jamani. Hebu tuwekee cv yake maana wife wangu ni mpiga kura huko UWT naweza kumshawishi

ayrose Kavura Majinge is founder and chairperson of the Registered Trustees of the Community Development Services(RTCDS).The Trustee is hosting the Mayrose TV talk show program which is aired by star TV and Mayrose is the moderator for the program.



Mayrose is an expert in leadership, management of civil society organization and good governance issues, she is a holder of Masters in public administration Mzumbe University, Bachelor degree in Business Management (India) Diploma in strategic leadership (USA.


© 2010 RTCDS Copyrights


slogan.gif

FAQ

 
Huyu ni mtoto wa Mfanyakazi wa Tanzania katika maana ya Wafanyakazi. ana umri wa miaka arobaini na ni mwanaharakati za maendeleo yanayotokana na bidii za kujituma na siyo kutumwa. Ameendesha kipindi chake kwenye Star TV kilichojulikana kama Mayrose Show. Anaendesha NGO inayojulikana kama Registered Trustee of the Community Development Services. Ameandika mawazo yake juu ya maendeleo kwenye kitabu chake kinachoitwa: DIRA YA MAENDELEO. She is a rare type of independent women Thinkers in Tanzania. She believes in what she does and she is not easily manipulated. Ni vigumu kwa wanasiasa wetu kuweka mawazo na maoni yao wazi kwa maandishi kama alivyofanya mama huyu. My doubt is: being so independent can she enter the race of the type we are used to?
Join Date : 3rd April 2012
Posts : 2
Rep Power : 0
Likes Received1
Likes Gi


Karibu Maryrose, naona umeamua kuingiza timu mwenyewe- ni vizuri zaidi kuliko kuachia wapambe!
 
Mkuu Pasco data za kwamba wanawake ndo wengi zaidi kati ya wapiga kura umezitoa wapi?Kwasababu huo ndo msingi wa hoja yako,then ni vyema ungetuwekea uthibitisho wa data(statistical) if possible.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom