Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 11,324
- 17,829
Kumekuwa na sintofahamu kuhusu hii habari ya faru maaarufu aliye fahamika kwa jina la faru John. Watu wengi hasa sisi ambao hatukusoma baiolojia ktk elimu ya sekondari tumekuwa tukijiuliza hivi hii sababu ya kukwepa tatizo la animal inbreeding ndio nini hasa? Je ina mashiko. Sasa ilinibidi niende kufanya utafiti kujua hii animal inbreeding na majibu niliyoyapata yapo kama ifuatavyo:
Ni hivi kutokana na uchache wa faru ktk eneo lilojifunga kijiografia la creta faru wote walikuwa ndugu yaani faru John alikuwa anawazalisha dada zake na watoto wake na wajukuu zake. Sasa hii kibaiolojia sio nzuri kwani inaweza kuathiri mfumo wa uzaaji yaani kama kulikuwa na tatizo la kinasaba la kusababisha ulemavu au kupungua nguvu za kuzalisha au kufa mapema kwa ugonjwa flani au kuto kuzaa toka ktk faru John au wajukuu zake basi lilikuwa linarithishwa na kukuzwa (amplified kwa vizazi vyake) ingefika maali wangekuwa hawazaani au wanakufa kwa ugonjwa flani wa kurithi au wanalemaa kwa ugonjwa wa kurithi. Hii ndio inaitwa tatizo la inbreeding ya wanyama. Ni aina ya incest. Hii ndio sababu wewe binadamu hauruhusiwi kumuoa dada yako. au ndugu yako yeyote.
Tafadhari unaweza kuongeza au kukosoa chochote katika bandiko hili kwani mimi sio mwanasayansi wa baiolojia.