UDSM watishia kugoma

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wametishia kugoma kuingia darasani, wakati wowote ili kuishinikiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini (HESLB), kuwapatia mikopo.
UDSM wanatarajia kufanya hivyo siku chache baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kugoma kuingia madarasani wakipinga kile walichodai kuwa HESLB imewachelewesha mikopo wanayostahili kupata.

Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa wanafunzi kwa sharti la kutotajwa jina kwa kuwa si msemaji wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho (DARUSO), alisema wanatarajia kugoma kama walivyofanya wenzao wa UDOM baada ya taratibu za kistaarabu zilizofanywa na viongozi wao kugonga mwamba.

“Kwa kifupi tunatarajia kugoma wakati wowote kuanzia Desemba 27 mwaka huu (jana)…maana tumechoshwa na bodi ya mikopo ambayo inatucheleweshea fedha zetu, hatuwezi kama ni wao ama ni serikali kuu ila itajulikana siku ya mgomo,” alisema mwanafunzi huyo.

Mwanafunzi huyo alisema mbali na madai ya fedha, bado wana matatizo mengine yanayowakabili ambapo wanaweka wazi siku watakayogoma ili uongozi wa chuo uweze kuyatatua.

Hata hivyo Tanzania Daima ilifanya jitihada za kuutafuta uongozi wa DARUSO ili kuzungumzia mgomo huo lakini haukuweza kupatikana.

Mwanzoni mwa mwezi huu polisi walilazimika kutumia nguvu ya ziada kutuliza mgomo wa wanafunzi wa UDOM baada ya wanafunzi hao kuandamana kuelekea katika Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma kuwasilisha madai yao.
 
Back
Top Bottom