UDSM: Ukweli Ni Huu

na kwa kuwakumbusha tu ni kuwa wazungu hawajengi mtaro, ila wanaziba pale maji yanapotoka.
kwa hiyo kuwasimamisha masomo wanafunzi au kuwaitia FFU ni sawa na kujenga mtaro.
ila kama watakaa chini na kusikiliza wanachokitaka then wakubaliane itakuwa ni sawa na kuziba maji yanapotoka.

Nakubaliana nawe kabisa lakini kitendo cha kuvunja mageti na kuleta fujo katika makazi ya viongozi halikuwa jambo la busara haswa tukitegemea kuwa hawo vijana ndio viongozi wa kesho
 
Parapanda Litalia parapanda - Hii ndio nyimbo iliyokuwa inaimbwa na wanafunzi waliokuwa wanaandamana kutokea UDASA wakapita Hall 6 mpaka kuelekea utawala , watu waliokuwa upande wa hall 6 na 7 walikuwa wanasikia vilio vya watu tu huko juu utawala , baadhi ya wanafunzi walikuwa nyumbani mwao wengine katika korido , wengine njiani wakiwashangaa wenzao , wale waliokuwa wanaandamana wengine walishika matawi ya mili , wengine vitambaa na hata wengine walibeba maji maji haya ni ya kujiandaa kama polisi wakivurumusha mabomu ya machozi tena waweze kujiosha nyuso zao .

Mbele kabisa kulikuwa na wanafunzi kama 6 hivi wote walikuwa wamebeba bango moja lilioandikwa kwa mkaa inaonyesha wanafunzi hawa hawakujiandaa ndio maana wanakuwa na bango ambali halisomeki vizuri wala nini , pamoja na wanafunzi kuandamana hivi sikuona vyombo vyovyote vya habari pembeni yao au nyuma yao kuweza kuhoji au kudadisi ni nini haswa wanafunzi wanachotaka .

Pia wapiga picha za televisheni hawakuwa pamoja na wanafunzi hawa waandishi wengi walikaa upande wa askari wa kuzuia fujo upande ule wa utawala , wengine walikuwa hall 7 wakihoji wanafunzi ambao hawajaandamana , sijaelewa kwanini haswa waaandishi hawataka kuwahoji wale wanaoandamana nao waongee chao , tatizo lengine ni kwamba hawa wanaoandamana hawana msemaji wao kwahiyo inakuwa ngumu sana kuweza kufuatilia au kukaa meza moja na uongozi wa chuo

Binafsi nilijaribu kumtoa mwanafunzi mmoja niongee nae kujua nini kinaendelea yeye akabaki kusema tu hatumataki mkandara , ukiuliza kwanini hajui jibu kwa nini , lakini pia kuna tatizo lingine kubwa baadhi ya wanafunzi wanasema wengi wanaoandamana wamekuwa na matatizo na chuo kwa muda mrefu wengi wao hawajamaliza kulipa adda zao wanazodaiwa na chuo kwahiyo nao wanajiingiza katika mgogoro huu .

Mpaka namaliza kuandika ukurasa huu hali ya chuo kwa sasa imetulia wanafunzi wanangoja kusikia chochote kutoka kwa uongozi wa chuo watasema nini waende nyumbani au wafanye nini , kuhusu mauaji yaliyotokea jana hapa chuoni , ni kwamba bomu hilo lilikuwa ni la machozi na lilipigwa katika mghahawa wakati wanafunzi wanapata mlo na kufanya mambo mengine ya kiafya

Hakuna upande wowote unaosema kwanini polisi waliamua kurusha bomu la machozi ndani ya kafteria au mule ndani kulikuwa na nini haswa lakini bomu hilo lilianguka karibu na mama mja mzito huyu mama akakosa kupumua vizuri na ndipo mauti yake yalipomkuta , maajabu ilikuwa hata watu wa msaada wa kwanza hawakuwa pale wanafunzi wachache walijaribu kumuokoa ikashindikana kweli kazi ipo humu ndani .

Na mwisho kabisa , maandamano haya yanayoendelea katika eneo la chuo ni batili hayajarihusiwa na mtu wowote yule , na hata kama yangeruhusiwa kuna sehemu zake za kupitia katika maandamano yoyote ili kuepusha fujo au uvunjaji wa amani kwa njia yoyote ile lakini maandamano ya wanafunzi haya ni tofauti kabisa wanapita katika mabweni ya wanafunzi wenzao ambao hawajagoma , wanatishia kupiga baadhi ya watu na wamesababisha hasara kwa baadhi ya biashara ndani ya eneo la chuo hayo ni makosa je watakuwa tayari kulipa hasara hii siku wakitakiwa kufanya hivyo ?

Hii nyingine sijui ni tatizo la mawasiliano au ni hujuma tu inayoendelea kutokana na maandamano haya huduma za mawasiliano ndani ya chuo zimekuwa za taratibu au hazipatikani kabisa mfano wale wanaouza kadi za simu hawauzi ingawa wako katika biashara zao huduma ya internet iko slow sana au kuna kipindi ilikatwa kabisa watu walishindwa kuwasiliana na ndugu na jamaa zao ndio maana usishangae kwanini habari hizi ziko kimya sana watu hawachangii katika blogu na forum zingine ni kuhusu uslow down wa huduma hii
 
Swala la mwanafunzi asiye Mtanzania kuongoza Serikali ya Wanafunzi ina nikumbusha yaliyotokea hapo mlimani 1970/71 wakati Bwana Akivaga mwanafunzi raia wa Kenya alipojitokeza kugombea Uongozi wa DUSO - Dar es Salaam University Students Organization. Vice Chancellor wa wakati huo Bwana Pius Msekwa na TANU Youth League walichukua hatua za ku frustrate hii effort na hata kumfukuza Bwana Akivaga kutoka chuoni. Pia DUSO ilipigwa marufuku na nafasi yake kuchukuliwa na TYL. UDSM then was reduced almost to a branch of Kivukoni College. Matters were made even worse when political Vice Chancellors like Mr. Kaduma took over including the tragic purge of academic staff which occured in 1975/76 - Professor Arnold Temu; Kassim Guruli etc who were purged and transferred to parastatals as Personell Managers/officers etc in many cases to serve under their former students whom they had taught many years before. Some could not stand this humiliation and left the country for greener pastures and others persevered and drowned themselves in alcohol - committing academic and physical suicide.

I hope and pray that UDSM is not going back to this era!. This was a tragic period when academic excellence was sacrificed at the altar of largely political expediency.

The current President of Tanzania Jakaya Kikwete and the Minister of Education Jumanne Maghembe were both active student leaders in the TYL then. One hopes that they will spare our children the agony of going through a similar experience. Please respecty academic freedom - including the right of young men and women to elect whoever they feel should lead their organization without political interference. Kudi Shauri.
 
Asante Kudi Shauri kwa historia hii muhimu.

Inaonekana Mkandara anataka kurudisha chuo kwenye miaka ya 70
 
Sasa ni saa moja za usiku saa za afrika mashariki , kwa wakati huu wanafunzi wamepungua sana katika maeneo kadhaa wengine wameenda makwao wengine wako sehemu zisizo eleweka kwa kweli hali ya amani ndani ya eneo hili sio nzuri na sio ya kujivunia kama ilivyo muda mwingi ninepokuwa huku .

Muda wa saa 9 hivi nilivyotoka hapa kuelekea mjini kulikuwa na kundi kubwa la wanafunzi sehemu ya mgahawa wa chakula kwa juu kulikuwa na wanafunzi waliovalia jeans inasemekana hao ndio viranja na viongozi wa migomo hii wanafunzi wale walikuwa wanatoa hutuba pale kwa wenzao .

Waliwaambia na kuwasisitizia kwamba kesho pia mgomo uko pale pale , lakini sasa wamebadilisha kauli wanasema hawawezi kuingia darasani kutokana na mwenzao mmoja kufariki dunia ni siku ya huzuni kwao na majonzi mpaka hapo taarifa itakapotolewa zaidi .
Hawa ndio wasomi ambao wiki hii walivamia nyumba ya mkuu wa chuo kuvunja geti na kufanya fujo zingine , hawa hawa jana walitaka kupambana na wanafunzi wenzao ambao walikuwa wakiwaangalia tu hawakutaka kuungana nao katika maandamano hawa hawa ndio wasiotaka kusema haswa tatizo ni nini .
 
Mkuu shy hivi hizi habari ni za kweli? kwani nasikiliza BBC muda huu (Internet), Mkandara na Dkt wa Mwananyamala wanasema hakuna aliyekufa. Wanadai huyo mjamzito ni mzima au hata BBC ni kimeo siku hizi?
 
Kuna uwezekano mkubwa kuwa mmoja wa wanafunzi wa mlimani amekufa kwa kipigo cha FFU. Cha kusikitisha zaidi ni habari kuwa huyo mwanafunzi ni mama mjamzito aliyekuwa amejikalia zake kwenye cafe ya chakula kabla hajakutana na kipigo kikali cha FFU ambao walikuwa na ruhusa toka kwa dikiteta na fisadi Mkandara.

Nikiconfirm hii habari, nitamwita rasmi mkandara kama double murderer kwa kuua mama na mtoto wake bila sababu yoyote ile.
 
Mkuu shy hivi hizi habari ni za kweli? kwani nasikiliza BBC muda huu (Internet), Mkandara na Dkt wa Mwananyamala wanasema hakuna aliyekufa. Wanadai huyo mjamzito ni mzima au hata BBC ni kimeo siku hizi?

Nziku, hii habari haijathibitishwa bado lakini watu wengi wanakiri kuwa imetokea. Bado nafuatilia kujua hili.
 
Nziku, hii habari haijathibitishwa bado lakini watu wengi wanakiri kuwa imetokea. Bado nafuatilia kujua hili.

Mama/Dada Mwafrika heshma Mkuu, inawezekana wanaogopa kutangaza, hii ni mbaya sana (kama ni kweli) ITABIDI VYAMA VYA KIRAIA NA WANAHARAKATI WANAWAKE KWA WANAUME KUDEMOSTRATE. Mbaya sana kumuua mama mjamzito tena akiwa cafeteria siyo kwenye maandamano. Mkandara hafai kwa lolote, mzushi tu, na REDET zake hazina maana sasa, utawala bora gani huo sasa.
 
Unajua Hao Bbc , Na Vyombo Vingine Vya Habari Haviko Karibu Na Wanafunzi Hawa Na Wanaripoti Upande Mmoja Wa Shilingi Tatizo Ndio Hilo
 
Pia Kuna Madai Mengine Kwamba Jana Usiku Kuna Baadhi Ya Wanafunzi Walitekwa Katika Mabweni Ya Wanawake Lakini Hii Haijadhibitishwa Rasmi Kama Kitendo Hicho Kilitokea
 
Mama/Dada Mwafrika heshma Mkuu, inawezekana wanaogopa kutangaza, hii ni mbaya sana (kama ni kweli) ITABIDI VYAMA VYA KIRAIA NA WANAHARAKATI WANAWAKE KWA WANAUME KUDEMOSTRATE. Mbaya sana kumuua mama mjamzito tena akiwa cafeteria siyo kwenye maandamano. Mkandara hafai kwa lolote, mzushi tu, na REDET zake hazina maana sasa, utawala bora gani huo sasa.

Nziku,

Hapa nilipo roho inauma sana kusikia hili. Ngoja tufuatilie zaidi hii habari. Ni siku ya majonzi makuu sana hasa itakapothibika kuwa hili limetokea na kina Mkandara wanaleta siasa kwa kupinga kwenye media.
 
Hata mimi sitaki kuamini kuwa kuna vifo vilivyotokea, ila najiuliza kama jana jeshi la polis lilikamata wanafunzi 39. Mbona waliosomewa mashtaka leo ni 38?
 
Hata mimi sitaki kuamini kuwa kuna vifo vilivyotokea, ila najiuliza kama jana jeshi la polis lilikamata wanafunzi 39. Mbona waliosomewa mashtaka leo ni 38?

Yote haya yatajulikana muda si mrefu. Naona Kibaki na Mugabe wanapata rafiki na mfuasi mwingine hapo Tanzania - Kikwete.
 
Back
Top Bottom