kanga
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,025
- 494
Wana jf katika kutafakari timbwili timbwili za elimu ya awali nashauri, UDSM irudishe utaratibu wa zamani kwa wanafunzi wote wanao chaguliwa kuanza shahada ya kwanza kufanya mtihani maalum kwa ajili ya kupima na kubaini uwezo wao kumudu masomo ya elimu ya juu waliyoomba bila kujali alimepata daraja la kwanza point tatu au daraja la tatu na wanapofaulu mtihani huo ndio waruhusiwe kujisajili kwa ajili ya kuanza masomo ya shahada ya kwanza.
Hii itasaidia kuendelea kulinda ubora na hadhi ya Chuo kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa kwa kutoa wahitimu wenye uwezo na ubora kukidhi viwango vya kimataifa.Kwa mtindo wa sasa wa TCU kupanga wanafunzi kwa kuangalia kozi mwombaji aliyoomba, UDSM imejikuta ikipokea wanafunzi vilaza kabisa ambao kwa kweli ni aibu baadae kwa chuo chenyewe kama hakutakiwa na mkakati makini wa kudhibiti wanafunzi wenye uwezo ndio wanachaguliwa na kuanza masomo.
Zamani kuingia UDSM kulikuwa na cuttoff points kulingana na aina ya shahada na alama za chini ili mwanfunzi achaguliwe katika kitivo au college, UDSM pamoja na kwamba inatakiwa kufanya kazi na TCU ,sera na malengo ya UDSM yazingatiwe ikiwa ni pamoja na kuchagua wanafunzi wenye ubora na uwezo na kwa kuwa vyuo vya elimu ya juu ni vingi wanafunzi wasio na sifa hizo wanaweza kujiunga na vyo vingine vya umma na binafsi.Hii itaendelea kukijenga chuo chetu cha Mlimani (UDSM).
Naamini sababu zifuatazo pia ni mjalabu wa kutaka mtihani wa mchujo wa kuingia MLIMAN urejeshwe.Maendeleo ya elimu yetu kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu ,madhila mengi yameonekana siyo kwa sektor yenyewe bali pia kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.Kuongezeka kwa shule za Kata na pasipo kuwa na huduma muhimu kumeathiri ubora wa elimu kwa kiasi kikubwa nchini.
Udanganyifu wa wakati wa matokeo kwa mitihani ya ngazi mbalimbali za msingi na sekondari pia ni tatizo la kupata wataalam waliobora kwa kiwango cha juu.Taarifa za mwaka 2012 zaidi ya wanafunzi 5,000 walichaguliwa kuingia kidato cha kwanza bila kujua kusoma na kuandika.Kulinda Heshima ya chuo kikongwe na alama ya Taifa letu,Bila UDSM Imara elimu ya Juu itakuwa goigoi na legelege.
Kuendelea kuandaa wakufunzi na wahadhiri waliobobea na weledi katika taaluma kwa ajili ya vyuo vya elimu ya juu vya umma na binafsi. Kwa sasa hakuna chuo chochote cha elimu ya juu cha binafsi au umma kisichofaidika na matunda ya mafanikio ya chuo cha Mlimani kwa kutoa wakufunzi waanzilishi.:clap2: