UDSM ndio chanzo cha mfubao wa Elimu Tz

Ogah and TzPride,

nadhani mnaufahamau fika ule usemi

"do not argue with a fool because when people see you they ill not know the difference" I guess you get my drift,.............

Mkamap,

I am sorry maelezo yako toka mwanzo ni hafifu kitaaluma, kihoja, hata katika kujieleza haujatulia kabisa. Details zako na heading uliyoweka havilingani. Kama unataka kutoa changamoto ya kuendeleza elimu basi spend less time hating and more time contributing, Masua is a well respected Professor, be a better professor than him then challenge his choices and decisions that he once made there you will make a difference rather than spending time insulting people.

This is my last post to you. I need this energy more than you know!

PEACE

Unajua wewe hapa unatumia evidence na logic katika arguments zako wakati mwenzenu mkamap anatumia roho (emotions), sasa hapo mtakesha. Hata hivyo nafikiri shule uliyokwisha kuitoa ni kubwa na watakuwa wameshaelimika sema tu inabidi waendelee ili mjdala huu usife. Kudos sana and keep it up!
 
hawa ndio wasomi wa udsm kuita wenzao vilaza.
Aliyekupa akiri wewe ndiye aliyemnyima kilaza.Hivyo wa kumlaumu sio kilaza ila aliyemfanya yeye kua kilaza na wewe kua kupanga.

Na hata hivyo bado nashawishika kua hawa watu kama kweli wamemaliza udsm na wana watuhumu wenzao kua vilaza kuna viashilia vya kila namna kua tuhuma hizi ni ukweli mutupu.

Mimi bado naamini kwa mtu aliyefika chuo kikuu ktk mazingira ya tz sio mtu wa kumbeza ila ku DISCO kunaweza sababishwa na vitu vingi mfano mazingira hali halisi anakotoka ama ubabe wa uongozi wa wasomi wa udsm kulazimisha watu kusoma fani ama kozi wasizokua na hobby nazo.Sasa basi kama msomi kutoka udsm anamwita mwezake kilaza eti tu kwa vile ali disco kuna kila ushaidi wa mazingira kwa tuhuma zinazoelekezwa hapo kua udsm ndio chanzo cha kudumaza elimu tz. una ukweli hawa watu nima consecutives mno.

hakuna kitu kama hiki chuo kikuu chochote
 
hakuna kitu kama hiki chuo kikuu chochote

Niliijibu hoja hii hapo juu, lakini mmiliki wa thread hii akatoa naye utetezi wake wa hoja hii. Hebu soma alivyojibu hapo juu na uje na maoni yako hapa.
 
data tunazozijua ni kuwa WALTER RODNEY kafanya paper zake nyingi za kuwa professor, na kazibiwa na hao hao maprof. ila baada ya kufariki ndipo walipoona aibu na kumpa huo uprofessor. sio roho mbaya?. hii inatokea kwa wengi tu!.

kama mkuu wa nchi alienda kuomba wataalamu nje ya nchi akidai tanzania hamna wataalamu, wakati chuo kimeendelea kutoa sheria tandu miaka nenda rudi, hivi unataka jibu gani kuwa chuo hiki cha udsm hakijakidhi matatizo ya nchi.

all the efforts so made since independence have been futile na sasa tunahitaji njia nyingine ya watu kuja na mawazo mapya. hatusiti kuwashutumu hao wanaotetea ufisadi kuwa nao ni mafisadi. au tunahitaji kumtumia DR Slaa na mwakyembe autumie circumstancial evidence kuwaunganisha na hao mafisadi?

tusiuje na hoja moja tu ya degree feki kuover rule others. hii hoja imeisha kubalika na pande zote na hivyo it is not in dispute. sasa hoja nyingine je.......

mimi ninadhani kitendo cha Rais wetu kudai hatuna wataalam ni dhairi kuwa UDSM imefubaza elimu ya tanzania.

BIG UP!!!
Rais alipo sema tz inaiingia mikataba mibovu kwa sababu haina wataalamu watu walisema kawa shushia hadhi lakini ukweli ndio huo.
Tanzania ni nchi tajiri mno kila kitu imejariwa ila tatizo ni kufeli kwa udsm kulikopelekea kufeli kwa elimu ya juu tz na consequences zake ni kufeli kwa uchumi wa tz.

Nitarudia kusisitiza
Hakuna nchi inayoweza kuendelea kama haina wataalamu,wabunifu kutoka elimu ya juu ktk nchi husika, Nchi iliyo na kila sababu ya kua moja ya nchi tajiri lakini cha kushangaza ndio masikini karibu kuliko zote duniani na kinacholitafuna taifa hili ni kufeli kwake kwa elimu ya juu.
Na unapoongelea elimu ya juu kwa tz unaongelea udsm .
Udsm imefubaisha elimu yetu udsm inabidi iangaliwe kwa jicho kali ili nchi ipate kujinusuru kielimu pia kiuchumi.

Ndugu yangu ni kweli hili limekua tatizo wenda tuliita janga la kitaifa.
Na kama kweli tunahitaji kujikomboa kiuchumi na kielimu hatuna budi kubadili uelekeo huu uelekeo tulio nao ndio kabisa tunaelekea kaburini.
Hili swala ni gumu na wote tunaoishi saizi tukubali kubali kuumia kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Mimi binafsi ningeshauri hivi serikali kwanza lazima ikubali kuingia gharama na ifanye hivi-
1.Ijitoe mhanga ihakikishe kila kona ya nchi kuna umeme.
2.Ijitoe mhanga kuhakikisha kila kona ya nchi inapata mawasiliano hasa internet kwa bei rahisi .
3. ihakikishe inafuta ushuru wa kuingiza computer,printer na vifaa vya namna hiyo .
4.ijenge chuo kingine kipya kikubwa na wahadhiri wake iwatoe nje ya nchi kama vile INDIA,CHINA,ISRAEL,VIETNAM,KOREA,ULAYA ,MAREKANI,JAPAN hawa waachiwe hiki chuo wafundishe miaka kama 15 ama zaidi ndio baadae waanze kuwaingiza taratibu wa tz .
 
Unajua wewe hapa unatumia evidence na logic katika arguments zako wakati mwenzenu mkamap anatumia roho (emotions), sasa hapo mtakesha. Hata hivyo nafikiri shule uliyokwisha kuitoa ni kubwa na watakuwa wameshaelimika sema tu inabidi waendelee ili mjdala huu usife. Kudos sana and keep it up!

mkubwa
tunajua nawe u mmoja kati yao , nothing new!!!!!
 
4.ijenge chuo kingine kipya kikubwa na wahadhiri wake iwatoe nje ya nchi kama vile INDIA,CHINA,ISRAEL,VIETNAM,KOREA,ULAYA ,MAREKANI,JAPAN hawa waachiwe hiki chuo wafundishe miaka kama 15 ama zaidi ndio baadae waanze kuwaingiza taratibu wa tz

Yaani kweli unatuona sisi mazezeta kiasi hicho? Iko kazi.
 
Yaani kweli unatuona sisi mazezeta kiasi hicho? Iko kazi.

hapana mkuu sio kweli tuko mazezeta
ila mfumo na mentality iliyojikita ndani kwetu sio ,sasa basi badala ya serikali kusomesha watu udsm ,Mu,DIT harafu baadae inawatuma ktk nchi hizo kujifunza na kuona nini na kwa vipi wanafanya ni bora
Tujenge chuo waje watufundishe na tujifunze hapa hapa na kwa wingi zaidi.
Na pia kwa kuwepo chuo hicho nchini makosa yaliyofanyika kudumaza elimu yataonekana wazi na nafikiri marekebisho yatafanyika haraka na hatimaye elimu bora kupatikana.
 
Mkamap you aint lying bro!! UDSM wanabana especially Masuha, this guy did get the heat from DIT students.
 
Fundi,
Angalia posti ya Kitila hapo juu kabla jujaendelea kuandika.

Unajua tusiwe tunakimbilia ku cofirm vitu ndugu yangu.
Kwa hali iliyopo kwa elimu ya juu tz chachu ya elimu bora kupatikana lazima kiwepo chuo shindani na udsm.

Vyuo kama MU ,IFM,DIT kamwe haviwezi shindana na udsm hata kama vyuo hivi vinatoa elimu bora kuliko udsm (elewa hapo ) neno udsm(mlimani) ni tosha kabisha.
Na chuo chochote kitakachoanzishwa bila kua na chachu fulani fulani nacho hakitatoa ushindani wowote.
sina haja ya kuendelea nafahamu umefahamu ninachotaka kukuelezea .
 
Mkamap you aint lying bro!! UDSM wanabana especially Masuha, this guy did get the heat from DIT students.

KAZI IPO MKAMAP. KINACHOTUHARIBIA NI KITU KIDOGO TU. WATU HAPA HAWASOMI KWANZA HABARI ZILIZOISHA ANDIKWA NA WACHANGIAJI NA MATOKEO YAKE WANAROPOKA TU. HAWANA EVIDENCE TAYARI VICHWA VINAMAWAZI YAJANA. UVIVU HUO WA KUFIKIRIA TUUONDOE KWANZA KWENYWE VICHWA VYAO.
 
Lawyer nimekupa thanks kwa makosa, that was meant for Mkamap, it is true UDSM wanalazimisha, kuna mshkaji wangu alilazimishwa kusoma kozi asiyoitaka mpaka ikawa noma, alikuwa na daraja la kwanza kidato cha sita, so at the end of the day ikawa bora elimu badala ya elimu bora

Anyway mimi vyuo kama IFM na DIT navipa hongera sana, UDSM wanabana kisha wataachia soon na education itakuwa fair nchi nzima.

check balaa la DIT for instance from tanzania daima of today

DIT Taasisi ya kwanza Afrika Mashariki

Ratifa Baranyikwa

NCHI ambazo zina maendeleo makubwa duniani ni zile zilizowekeza katika elimu ya ufundi na ile ya teknolojia ya habari na mawasiliano, hapa nchini kwa sasa tunaizungumzia Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).
DIT imekuwa taasisi ya kwanza Afrika Mashariki isiyokuwa chuo kikuu kutoa shahada ya uhandisi huku ikijiimarisha kuwa mhimili wa elimu ya ufundi na uhandisi nchini, na mpaka sasa hakuna taasisi yoyote ambayo imeweza kufanya hivyo katika nchi za Afrika Mashariki.

Njia imeanza kuonekana mwanzoni mwa mwaka huu, na historia imeanza kujengwa na wahitimu wa kwanza wapatao 160 walitunukiwa shahada ya kwanza ya uhandisi, mbali na wahitimu wengine 140 ambao walitunukiwa vyeti na kufanya idadi yao kutimia 300 katika mahafali ya kwanza iliyofanyika Januari 26 mwaka huu.

Mkuu wa taasisi hiyo, Prof. John Kondoro, anasema kuwa sasa ni miaka kumi tangu taasisi hii ilipoanzishwa ikiwa imeendelea kukua na kuimarika na kuanzisha programu zake yenyewe, ambazo zina ithibati ya NACTE.

Prof. Kondoro anasema kuwa historia ya DIT inaanza Oktoba 21, 1957 wakati huo ikitoa mafunzo ya ufundi stadi na kujulikana kwa jina la Dar es Salaam Technical Institute (DTI) na baada ya Tanzania Bara kupata uhuru, serikali kwa kutambua umuhimu wa elimu ya ufundi katika ujenzi wa taifa ilipandisha daraja DTI kuwa Chuo cha Ufundi Dar es Salaam (Dar es Salaam Technical College au Dar Tech - DTC).

Anaelezea historia hiyo kuwa mnamo mwaka 1962, DTI wakati huo ilikuwa ni kielelezo cha hatua muhimu katika kutambua mchango wa elimu ya ufundi katika ujenzi wa taifa.

Prof. Kondoro anasema kuwa mabadiliko ya kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia duniani yakiambatana na utandawazi, yanahitaji elimu ya ufundi kuyakabili, kwa kulitambua hilo Serikali ya Awamu ya Tatu mwaka 1997, kwa kupitia sheria ya Bunge iliipandisha daraja iliyokuwa DTC kuwa Dar es Salaam Institute of Technology (DIT), ambayo kwa sasa yapata miaka 10 tangu kupandishwa kwake daraja na miaka 50 tangu msingi wa Taasisi ulipowekwa.

Anasema kuwa tangu kuanzishwa kwa DIT kwa maana ya kupandishwa hadhi kati ya mwaka 1997 na 2007, Taasisi hiyo (DIT) imeongeza udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa takriban asilimia 182.

Pamoja na mafanikio hayo mazuri, lakini pia Kondoro anasema kuwa ongezeko limeleta changamoto za aina mbalimbali kwa wanafunzi, wahadhiri na wafanyakazi waendeshaji wa taasisi na miundombinu ya taasisi.

Kwa mfano, maktaba iliyojengwa kuhudumia wanafunzi 250 kwa sasa inahudumia wanafunzi zaidi ya 2,000. changamoto nyingine kubwa ni uchakavu wa vifaa vya kufundishia na uchakavu wa miundombinu ya majengo kutokana na taasisi kuwa imehudumia muda mrefu bila kufanyiwa ukarabati wa kutosha kutokana na ufinyu wa bajeti.

“Karakana za kufundishia, hosteli za wanafunzi na bwalo ni majengo ya siku nyingi ambayo yamekosa ukarabati wa kutoha kiasi kwamba panahitajika fungu maalumu kwa ajili ya matengenezo,” haya ni maneno ya Prof. Kondoro.

Aidha, hafichi kutamka wazi kuwa mikakati ya kutatua baadhi ya changamoto za maendeleo ya taasisi imetokana na misaada wanayopata kutoka asasi za kitaifa na kimataifa na washirika wengineo wa maendeleo.

Anasema kuwa uboreshaji katika sekta ya ufundi na uhandisi, unahitajika kutokana na nchi kuwa na uhaba mkubwa wa wafanyakazi katika sekta hizo, na katika kupunguza makali hayo taasisi imekuwa ikiongeza udahili wa wanafunzi tangu ilipoanzishwa kama jukumu lake.

Lakini pia anasema kuwa taasisi imeweka mpango mkakati wa kuongeza idadi ya programu kulingana na mahitaji ya nchi, anazitaja programu hizo kuwa ni pamoja na multimedia Technology (Computer Graphics & Animation), Communication System Technology, Biomedical Engineering, Mechatronics Engineering, na Information Technology.

Hata hivyo anasema kuwa ongezeko la programu na udahili lina lengo la kuongeza uzalishaji wa rasilimali watu, ambapo kwa sasa halikidhi mahitaji ya nchi na hasa ukizingatia wahitimu watakaotokana na programu ya MES ambao watakuwa zaidi ya mara nne ya hawa wa hivi sasa.

“Kama hatutachukua hatua za makusudi kuongeza nafasi katika taasisi na vyuo vya ufundi, hatutakuwa na mafundi sanifu na wahandisi wa kutosha kuleta maendeleo tunayotarajia katika utekelezaji wa dira ya maendeleo ya 2025” anasema.

Anasema kuwa kwa upande wake DIT ili kukabiliana na ufinyu wa nafasi na changamoto ya kuongeza udahili inatafuta eneo kwa ajili ya kujenga kampasi ya pili ya taasisi, lakini hilo linahitaji mchango wa serikali, wamiliki wa ardhi na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Anaelezea majukumu mengine ya taasisi zaidi ya ufundishaji kuwa ni pamoja na kufanya tafiti na utoaji wa ushauri wa kitaalamu kwa jamii, kama tunavyojua, umuhimu wa utafiti wowote wa elimu ya juu katika kuipatia jamii maarifa mapya na hivyo kuleta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii.

Kwa mujibu wa mkuu wa taasisi hiyo, tafiti walizofanya mpaka sasa ni pamoja na kutafiti namna ya kuunganisha umeme majumbani kwa bei nafuu, utafiti huo unafanywa kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati, SIDA na Tanesco.

Aidha, anasema kuwa taasisi imefanya na inaendelea kufanya tafiti zinazolenga kupunguza kero mbalimbali kama anavyoainisha Prof. Kondoro kwa kusema:

“Kwa mfano utafiti mwingine, tunashirikiana na TANROADS, tunatafuta utatuzi wa msongamano wa magari mijini kupitia uundaji wa taa za barabarani, pia tunatafiti utengenezaji wa mashine ndogo za kusindika mazao ya kilimo, na tayari tumeshatengeneza mashine za kuangua vifaranga 1,000 kwa mara moja, mashine za kuweka vinywaji kwenye paketi kwa kasi ya paketi 25 kwa dakika moja.

Utafiti mwingine ambao taasisi inafanya ni pamoja na uundaji wa mitambo ya kurushia matangazo ya redio za FM kwa bei nafuu kwa stesheni ya redio hapa nchini.

“Taasisi pia imetekeleza kwa mafanikio majukumu yake yanayohusu utoaji huduma kwa umma (consultancy service) kupitia Instute of Consultancy Bureau. Taasisi imefanya mengi lakini kama kielelezo ni pamoja na utafiti wa udongo kwa ajili ya ujenzi wa barabara na majumba mbalimbali yakiwemo mashule.

“Usimamizi wa taka ngumu, yaani solid waste management kwa manisapaa zaidi ya 20 mbalimbali nchini chini ya mkataba kati ya taasisi na Shirika la Kimataifa la Kazi Duniani (ILO), lakini pia matumizi bora ya nishati (energy Management) viwandani na uwezeshaji wa matumizi ya TEKNOHAMA vijijini kupitia mradi wa Bunda-Mugumu na Miono –Chalinze kwa kushirikiana na COSTECH, Royal Swedish Institute of Technology na SIDA,” anaeleza.

Prof. Kondoro anaeleza kuwa kama sehemu ya mashirikiano katika tafiti, taasisi inashirikiana na Leeds Metroplitan University ya Uingereza kuendesha kozi ya shahada ya uzamili tangu mwaka 2004, ambako wahitimu wa kwanza walipata cheti cha kuhitimu kutoka Leeds Metropolitan University katika mahafali iliyofanyika mwaka huu.

Anasema kuwa programu hiyo ni sehemu ya mkakati wa kujenga uwezo wa kutafiti na pia kujipima ili taasisi iweze kuanzisha programu yake ya shahada ya uzamili mwaka 2009 kama ambavyo imejipanga.

Prof. Kondoro anaeleza historia ya watu mashuhuri na viongozi ndani ya nchi ambao ni chemchemi ya taasisi hiyo kongwe, anawataja baadhi ya watu hao ambao waliwahi kusoma au kufanya kazi katika taasisi hiyo kuwa ni Prof. Mark Mwandosya, mwanamazingira na kwa sasa ni waziri katika wizara ya Maji na umwagiliaji, mwingine ni Prof. Mathew Luhanga aliyewahi kuwa Makamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Idrissa Mshoro, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la DIT, Dk. Pius Ng’wandu, aliyewahi kuwa waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu katika kipindi cha utawala wa Awamu ya Tatu.

Katika hitimisho la maelezo yake hayo aliyoyatoa ofisini kwake hivi karibuni, Prof. Kondoro amekaribisha maombi ya kujiunga na masomo kwa wale wote wenye sifa kwa ajili ya mwaka 2008/09, ambapo fomu za kujiunga zinapatikana chuoni hapo na katika taasisi ya Sayansi na Teknolojia, Mbeya na Chuo cha Ufundi Arusha.

Prof. Kondoro amemalizia kwa kutoa rai kwa wanafunzi wa kike kujiunga na elimu ya ufundi, kwani wana uwezo mkubwa na historia za tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa wanafanya vizuri katika masomo hayo.

Amekaribisha yeyote mwenye maoni juu ya uboreshaji wa taasisi hiyo na elimu ya ufundi kwa ujumla kuzuru chuoni hapo na atapata mengi zaidi.

Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/2/14/makala5.php
 
Hiki ni kisa cha ajabu: I remember one day "DR" WA MZUMBE walitaka kumfanyia promotion ya kuwa Associate Prof. kwa hiyo wakaleta publications zake kwa jamaa azifanyie review pale UD....guess what? the guy had three published papers...(naomba nisiendelee maana anaweza kuwa anapita humu)..kifupi ni mbili alipublish Mzumbe na moja Dodoma chuo cha....!!! Yalaaaabiiiiii this is the guy who wanted to be Associate Professor!!! Well obvisous jamaa alimlima vibaya mno na AKAIKARIPIA BOARD ya Mzumbe kwa kutokuwa makini..The rest is history. Ingawa jamaa aliitwa mnoko..

Personally Iam a UDSM graduate, I do admit UD has its own probs. But as a nation we cant afford to proliferate "degree mills", jamani hawa ndo wanaenda kuwa wataalamu, kutuwakilisha huko duniani..au mnataka watu wawe na degree for the sake of degree? Camon people lets be real! wote humu ni wasomi. Jamani hii globalization mtu wa DIT AU IFM anashindana na Harvard na OXFORD....sasa tusipojizatiti, tutaambulia kitu kweli?

Bwana Mkamap nakusoma ila nadhani UDSM siyo chuo kibaya as we tend to think. Hivi vyuo vinahitaji kuinvest katika raslimali watu. huwezi kuwa na university yenye PhD tatu au tano ukaniambia kwamba hicho ni chuo kikuu! Its a disagrace.
 
Masanja:

Kuna msemo wa kiswahili unaosema nyani haoni .... Kuna chombo kinachoitwa Association of Commonwealth Universities. Kila mwaka kinachapicha kitabu cha Commonwealth Universities Yearbook. Ukichukua Commonwealth Universities Yearbook 1987 na kuangalia namba ya maprofesa na wenye Phd UDSM, utaona hakuna sababu za kimsingi za vyuo vingine visitoe digrii. UDSM haikuanza kama chombo chenye maprofessor na maPhd. walianza mwanzo kama vyuo vingine tu wakiwa na Phd za manati.

Na jinsi serikali ya Tanzania ilivyobahili katika matumizi, wengi waliopata Phd na kurudi kufundisha UDSM, walipata udhamini wa vyuo, mashrika na serikali kutoka nje. Na sababu kubwa ya udhamini huo kuanzisha chuo ambacho kitasaidia maendeleo ya nchi na vilevile kusaidia vyuo vingine kufikia ngazi ya kutoa digrii.

Katika mjadala huu inaonekana kabisa UDSM imekuwa kikwazo kwa vyuo vingine.

Vilevile kutumia kigezo cha ku-publish paper kama ni kigezo vya kupandisha cheo kwa vyuo vichanga ni makosa makubwa. Vyuo vyote Tanzania pamoja na UDSM ni vyuo vya undergraduate na sio research institutions, hivyo walimu hawatakuwa na paper nyingi za ku-publish. Na kama ku-publish paper ni kigezo mbona hatuoni maprofessor wa UDSM katika majarida mbalimbali ya kimataifa?

Na kutokana na kukua kwa mtandao maprofessor wengi wanaweka kazi (paper) zao kwenye mtandao. Mbona niki-google majina ya professor mahiri wa UDSM sipati kitu. Au bado wanatumia type-write kuchapisha paper zao.
 
Hiki ni kisa cha ajabu: I remember one day "DR" WA MZUMBE walitaka kumfanyia promotion ya kuwa Associate Prof. kwa hiyo wakaleta publications zake kwa jamaa azifanyie review pale UD....guess what? the guy had three published papers...(naomba nisiendelee maana anaweza kuwa anapita humu)..kifupi ni mbili alipublish Mzumbe na moja Dodoma chuo cha....!!! Yalaaaabiiiiii this is the guy who wanted to be Associate Professor!!! Well obvisous jamaa alimlima vibaya mno na AKAIKARIPIA BOARD ya Mzumbe kwa kutokuwa makini..The rest is history. Ingawa jamaa aliitwa mnoko..

Personally Iam a UDSM graduate, I do admit UD has its own probs. But as a nation we cant afford to proliferate "degree mills", jamani hawa ndo wanaenda kuwa wataalamu, kutuwakilisha huko duniani..au mnataka watu wawe na degree for the sake of degree? Camon people lets be real! wote humu ni wasomi. Jamani hii globalization mtu wa DIT AU IFM anashindana na Harvard na OXFORD....sasa tusipojizatiti, tutaambulia kitu kweli?

Bwana Mkamap nakusoma ila nadhani UDSM siyo chuo kibaya as we tend to think. Hivi vyuo vinahitaji kuinvest katika raslimali watu. huwezi kuwa na university yenye PhD tatu au tano ukaniambia kwamba hicho ni chuo kikuu! Its a disagrace.

Masanja sina uhakika sana na stori yako ya huyo Dr wa mzumbe kama sijakosea ili mtu aitwe associate profesa lazima awe ame defendi paper kati 20 na 25.
Masanja
udsm sio chuo kibaya ila maudhuhi yake yamefeli na kiungwana mtu kubadirika lazima ajue udhaifu wake na aukubali ndipo mtu hufanya mabadiriko ya kweli Lakini hii ni tofauti na udsm udsm haikubali kuchemka kwake na kukumbatia uozo unaoligharimu Taifa.

TZ sio nchi masikini kwa uhalisia ila umasikini wetu unatokana na kufeli kwa elimu ya juu na kufeli huku kunasababisha pia uchumi kufeli.

Tatizo hii ajenda watu wanaifanya kua ni binafsi eti kwa vile wamepita hapo udsm ila nashukuru kuna waelewa wamepita hapo udsm na bado wanaitolea jicho kali udsm.

Kwa ugumu wa mentality ya wengi wao ndio nikapendekeza kijengwe chuo kingine shindani na udsm .
 
Hiki ni kisa cha ajabu: I remember one day "DR" WA MZUMBE walitaka kumfanyia promotion ya kuwa Associate Prof. kwa hiyo wakaleta publications zake kwa jamaa azifanyie review pale UD....guess what? the guy had three published papers...(naomba nisiendelee maana anaweza kuwa anapita humu)..kifupi ni mbili alipublish Mzumbe na moja Dodoma chuo cha....!!! Yalaaaabiiiiii this is the guy who wanted to be Associate Professor!!! Well obvisous jamaa alimlima vibaya mno na AKAIKARIPIA BOARD ya Mzumbe kwa kutokuwa makini..The rest is history. Ingawa jamaa aliitwa mnoko..

Personally Iam a UDSM graduate, I do admit UD has its own probs. But as a nation we cant afford to proliferate "degree mills", jamani hawa ndo wanaenda kuwa wataalamu, kutuwakilisha huko duniani..au mnataka watu wawe na degree for the sake of degree? Camon people lets be real! wote humu ni wasomi. Jamani hii globalization mtu wa DIT AU IFM anashindana na Harvard na OXFORD....sasa tusipojizatiti, tutaambulia kitu kweli?

Bwana Mkamap nakusoma ila nadhani UDSM siyo chuo kibaya as we tend to think. Hivi vyuo vinahitaji kuinvest katika raslimali watu. huwezi kuwa na university yenye PhD tatu au tano ukaniambia kwamba hicho ni chuo kikuu! Its a disagrace.

masanja should be crazy, totally crazy. i am always specific with faculty of law for that is my specification. UDSM utaratibu waliojiwekea unaasema ili mtu awe lecturer lazima awe na PHD, na senior lecturer ni Prof.

ila mbona wapo watu kitivo cha sheria wana masters na bado ni masenior lecturers,na wengine ni malecturers. mbona sisi tumepita kwenye kozi hiyohiyo na kufundishwa na watu hao hao. mbona hatukupiga kelele? kwanini vyuo vingine visiwe na watu kama hawo ilimradi wako caipable kama UDSM?. kwa nini mnaudanganya umma.kwa nini tunakuwa wanafiki? kwa nini tunakuwa na roho mbaya? ufisadi mpaka kwenye elimu?

kimataifa pia wapo watu wana masters na bado ni masenior lecturers na wameandika vitabu vingi tu vinavyopendelewa sana.

Pia wakati tunasoma kuna C. Binamungu wa MU, kaandika vitabu vingi sana, licha ya kuwa na masters. tulikuwa tunaabiwa hapo chuoni na malecturers wetu kuwa vitabu vyake tusivitumia maana havifai. ila tulikuwa tunavitumia sababu alikuwa anafanya references nyingi na ilikuwa inatusaidia. ila kama ungeweka material yake kwenye paper yako ambayo hujamacknowledge, utapata sana 'excellence'. ila ukimacknowledge hao hao malecturers hawakupi. pia C Binamungu amebaniwa sana kupata udaktari na hawa maprof. kama ilivyokuwa kwa Walter rodney. simply because of superiority n.k, utasikia eti hoo, your reseach is good but the language used is not english, what we hear is noly the introduction so go on, wakati bwana anamalizia paper yake, na vituko vingi tu. sasa kama ni publications mbona anawapiku walimu wetu hapo UDSM.

sisaliti chuo changu, ila lazima tuwape moyo hata wale wanaosoma vyuo hivi vingine maana hata wao ni watanzania wenzetu. we should call a spider a spider.

iayekataa publications za binamungu aclick kwenye google na aone.
 
Hiki ni kisa cha ajabu: I remember one day "DR" WA MZUMBE walitaka kumfanyia promotion ya kuwa Associate Prof. kwa hiyo wakaleta publications zake kwa jamaa azifanyie review pale UD....guess what? the guy had three published papers...(naomba nisiendelee maana anaweza kuwa anapita humu)..kifupi ni mbili alipublish Mzumbe na moja Dodoma chuo cha....!!! Yalaaaabiiiiii this is the guy who wanted to be Associate Professor!!! Well obvisous jamaa alimlima vibaya mno na AKAIKARIPIA BOARD ya Mzumbe kwa kutokuwa makini..The rest is history. Ingawa jamaa aliitwa mnoko..

Personally Iam a UDSM graduate, I do admit UD has its own probs. But as a nation we cant afford to proliferate "degree mills", jamani hawa ndo wanaenda kuwa wataalamu, kutuwakilisha huko duniani..au mnataka watu wawe na degree for the sake of degree? Camon people lets be real! wote humu ni wasomi. Jamani hii globalization mtu wa DIT AU IFM anashindana na Harvard na OXFORD....sasa tusipojizatiti, tutaambulia kitu kweli?

Bwana Mkamap nakusoma ila nadhani UDSM siyo chuo kibaya as we tend to think. Hivi vyuo vinahitaji kuinvest katika raslimali watu. huwezi kuwa na university yenye PhD tatu au tano ukaniambia kwamba hicho ni chuo kikuu! Its a disagrace.

masanja unapoongea kitu halisia taja ili tuwajue, uaanza stori za abnasi, oho watu fulani waloyoka UDSM walifanya vizuri na wa DIT walifail, , that is why i dare call you a crazy guy. THIS IS A PLACE TO TALK OPENLY. usituaibishe watu wa UDSM hapa. kama uwezi usilonge.
 
Back
Top Bottom