UDSM: Mgomo unaokuja nani alaumiwe?

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Mwishoni mwa semester iliyopita ulitokea mgomo UDSM, kilio kikiwa ni "Kupungukiwa" hela za kujikimu.

Wanachuo Wali poozwa kwa kuahidiwa kuongezewa kiwango cha hela kwani gharama za Maisha ni kweli zimepanda (tumesikia pia bungeni sijui ni kwa kiasi gani)!

Kutuliza hali ya wakati ule,uongozi wa chuo uliamua Kutoa coupon kwa wanachuo ili angalau wapate mlo (hawakuangalia tatizo la nauli kwa Wanachuo wanao ishi hostel na gharama zinginezo tofauti na kula).

Hela walizo kopeshwa kwa style ya coupon zililipwa kwa kukatwa katika hela walizo wekewa mwanzoni Mwa semester ya pili, hapa, tatizo bado lilirudi pale pale,kwa kulipa deni kwa hiyo hautegemei hela zilizo baki baada ya kulipa deni zimfikishe mwisho wa semester ya mwisho.

Kawaida hela ya field (Practical Training) hutolewa kabla ya kuanza kwa mitihani ya kumaliza mwaka.
Lakini mwaka huu,bodi ya mkopo (HESLB) inataka itoe hela baada ya mitihani kumalizika.
(Kwanini kubadili utaratibu bila taarifa rasmi tena kibabe hivi?)

Ikimbukwe pia kwamba,wapo wanachuo wanao wahi kumaliza mitihani hivo kuondoka mapema,… na pia,mitihani inaisha rasmi tarehe 22.07.2011 na field inaanza rasmi tarehe25.07.2011,..yaani kuna Siku mbili tu kati ya kumaliza mitihani na kuanza field,….amazing.

Kwa mtu anae kwenda kufanya field mwanza,kigoma,kagera,mara etc atafika lini huko? Na pia ataamini vipi kwamba atakua amepata hela hiyo tarehe 23 july, na atumie usafiri gani wa haraka,kwa kiwango kidogo cha hela anazopata kuwahi kigoma awahi field ukizingatia kwamba ukichelewa hata siku moja tu umejiondolea kiasi flani cha maksi?

Ni nini kinaifanya serikali kupitia bodi iamini kwamba hela ambazo hazikutosha semester iliyopita zinatosha semester hii ukizingatia kwamba hela hizo hizo zilikatwa deni la coupon la semester iliyo pita?

Kwa kifupi,
hela ya field pamoja na kwamba inawasaidia wale walio wahi kumaliza mtihani kuondoka mapema,ina saidia pia kuwapa support wale ambao wameishiwa hela katika mda mbaya kama huu wa kuingia katiaka mitihani ambapo mtu hahitaji stress za vipi atakula leo.

Jana tumeenda bodi ya mkopo hawa kutusikiliza,leo tumetaka kufanya kikao cha bunge tumenyimwa
Venue, utawala wanajua kabisa kwamba tunataka kubariki mgomo,lakini hawa saidii kitu kutunyima venue,maana tunaipisha tu siku ya leo kama sikukuu na kesho kama wanachuo hawajapewa haki yao basi na tubariki mgomo kupitia revolutionary square,…

Hadi hapo kesho,tunasubiri kudai haki.
Waziri *

soma pia: http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=30900
 
Ndo hivyo serikali inaypopenda kuwageuzageuza wanachuo kama chapati kwenye flaying pan.
 
Haki ya mtz ipo mikononi mwake! Katu serikali hii ya ccm hatotoa haki kwa mtz yeyote yule!
 
Hapo naona mna kila sababu ya kufanya mgomo manake hoja zenu hazisikilizwi kinachofanyika ni kusogeza mbele matatizo badala ya kuyatafutia suluhisho la kudumu.

Hii ni staili ya uongozi wetu, hatutafuti suluhisho la mda mrefu na badala yake tunapenda kutumia ujanja wa mjini hata kwenye mambo ya muhimu kama elimu. Na kwa nini uongozi wa chuo uwanyime venue ya kikao chenu? hawana sababu yoyote ya kufanya hivyo, wangekuwa waungwana wangekaa nanyi mkayaongelea pamoja ayo matatizo.

Poleni sana.
 
Hapo naona mna kila sababu ya kufanya mgomo manake hoja zenu hazisikilizwi kinachofanyika ni kusogeza mbele matatizo badala ya kuyatafutia suluhisho la kudumu. Hii ni staili ya uongozi wetu, hatutafuti suluhisho la mda mrefu na badala yake tunapenda kutumia ujanja wa mjini hata kwenye mambo ya muhimu kama elimu. Na kwa nini uongozi wa chuo uwanyime venue ya kikao chenu? hawana sababu yoyote ya kufanya hivyo, wangekuwa waungwana wangekaa nanyi mkayaongelea pamoja ayo matatizo. Poleni sana.

wamejua kwamba bunge lita halalisha mgomo
ndo maana utawala wame kataa,lakini kesho kutakua na kikao cha wazi
kwa wanachuo wote pale
revolution square ndicho kitakacho amua cha kufanya
 
pig up UDSM! mgome tu maana wanafunzi wa vyo vikuu tz wamekuwa hawaheshimiki na viongozi wa serikali hii ya awamu ya 4, wameonekana ni watu wa kudanganywa kama watoto wadogo. U have a point guys
 
Dah!silipatii picha hlo kunji,cjui nilianzshe mwenyewe huku kitaa mana nimelimic balaa..
 
Msichoke kudai haki zenu. Enzi zetu tukigoma tulikuwa tunamfungia safari na tunapambana na waziri wa elimu ya juu ( Ben Mkapa) na katibu wake (Dr. Bilal) kasheshe ikianza tunaifunga Jamhuri street, then RPC Gewe anakuja na FFU, palikuwa patamu pale Jamhuri St.
 
Wadau kuna kila dalili UDSM wanaweza kuanzisha mgomo na maandamano kuanzia sasa,kwa sasa wanachuo wapo eneo la revolution square wanapeana modalities.

CHANZO cha mgomo ni kutotolewa kwa pesa ya field,ambapo wanafunzi wanatarajia kufunga chuo kwa muda wa wiki mbili zijazo lakini mpaka sasa bodi ya mikopo hawajatoa pesa hizo.
 
Waseme kabisa wazi kuwa hawana pesa ya kumalizia semester siyo pesa ya field. Labda kuna taarifa zaidi ya hiyo uliyotoa.
 
Njaa hizo,kwa kawaida hizi huwa wiki dume,sasa jwani wameambiwa hawapewi hela za field,what i know ni kwamba mara nyingi huwa zinatoka wakati wa mitihani........wanajipotezea muda,,,,,,,,,mambo mengine ukigoma unaonekana huna maana.......
Waseme kabisa wazi kuwa hawana pesa ya kumalizia semester siyo pesa ya field. Labda kuna taarifa zaidi ya hiyo uliyotoa.
 
Hamuitendei haki REVOLUTION SQUARE......
Wadau kuna kila dalili UDSM wanaweza kuanzisha mgomo na maandamano kuanzia sasa,kwa sasa wanachuo wapo eneo la revolution square wanapeana modalities.CHANZO cha mgomo ni kutotolewa kwa pesa ya field,ambapo wanafunzi wanatarajia kufunga chuo kwa muda wa wiki mbili zijazo lakini mpaka sasa bodi ya mikopo hawajatoa pesa hizo.
 
Kwani field mnaanza lini hasa!???? Je bodi wamesema hamtapewa pesa hiyo kabla ya kufunga chuo!? Kama mkianza mgomo mtaendelea nao mpaka siku ya jumatatu ambayo ni siku mtaanza mtihani!!!!!!.........nawatakia kila la heri katika mitihani!!!!!
 
Swali zuri sana kwa wana udsm,yaan nashangaa,wasomi nao wana wajanja wao,maana kama mtu unajua ku-rizon huwez kuukubali huu mgomo,wanini?????bora wafanye mtihani wakapumzike
Kwani field mnaanza lini hasa!???? Je bodi wamesema hamtapewa pesa hiyo kabla ya kufunga chuo!? Kama mkianza mgomo mtaendelea nao mpaka siku ya jumatatu ambayo ni siku mtaanza mtihani!!!!!!.........nawatakia kila la heri katika mitihani!!!!!
 
Waseme kabisa wazi kuwa hawana pesa ya kumalizia semester siyo pesa ya field. Labda kuna taarifa zaidi ya hiyo uliyotoa.
WAZUSHI TU!!!!!! wala watu wanaosoma mwaka wa kwanza na mwaka 1-4(llb) hawawezi kumalizia semester?? au wanatafuta supp na C kwa kupoteza muda!!!
 
Hapa ni kweli watu wamefulia vibaya,, wanapinga nauli kuwekewa grades ambayo wameifanya kama ngaz ya kupandia, ni mgomo usio na nguvu. 3rd year weng wako chimbo wakijiandaa na UE, Pia kuna 1st year hawana field
 
Habari yako ??????asante kwa taarifa
Hapa ni kweli watu wamefulia vibaya,, wanapinga nauli kuwekewa grades ambayo wameifanya kama ngaz ya kupandia, ni mgomo usio na nguvu. 3rd year weng wako chimbo wakijiandaa na UE, Pia kuna 1st year hawana field
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom