UDSM kujadili jinsi ya kuiunda katiba

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
Send to a friend WATAALAMU wa fani mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameamua kujitosa katika vuguvugu la kupigania katiba mpya nchini na wamepanga kukutana ili kuweka bayana namna Watanzania wanavyotakiwa kuiunda.

Hatua ya wasomi hao imekuja wakati ambapo Rais Jakaya Kikwete amekubali mkakati wa kuandikwa kwa katiba na kuahidi kuunda tume itakayoongozwa na mwanasheria aliyebobea ili kuongoza mchakato wa kuelekea kuiunda kwa umakini.

Kwa mujibu wa taarifa kwa gazeti hili iliyotolewa na Jumuia ya Wanataaluma wa UDSM (Udasa) ,wasomi hao watatimiza azma hiyo kwa kuendesha mjadala katikati ya mwezi huu.

Miongoni mwa wanataaluma, nguli wa kisiasa, watakaoongoza mjadala huo ni Profesa Issa Shivji, ambaye ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluama cha Mwalimu Nyerere na Jenerali Ulimwengu, Mwandishi wa Habari Mashuhuri nchini.

Udasa imeeleza kwamba mhadhara huo ambao utafanyika katika ukumbi wa Nkrumah, UDSM, mbali na kuwahusisha wanataaluma hao, pia watakaribishwa watu mbalimbali wakiwepo wanasiasa, wanaharakati pamoja na wananchi, wakereketwa wa katiba.

Vuguvugu la kutaka iandikwe katiba mpya lilitia kasi nchini mara baada ya kumalizika uchaguzi mkuu, Oktoba mwaka jana, likiongozwa na vyama vya siasa vya upinzani.

Udasa imesema kwamba mjadala huo wanatarajia kuufanya katikati ya mwezi huu.

Wakati huo huo, Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), limempongeza Rais Jakaya Kikwete, kwa uamuzi wake wa kuruhusu mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban Simba, alisema jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba katiba ijayo ijumuishe makundi yote ya kijamii na kwamba waislam pia watachangia waliyonayo mengi katika katiba hiyo mpya.
“ Waislam wanayo mengi ya kupendekeza katika mchakato mpya wa katiba mpya kama zilivyo jamii nyingine za Watanzania,” alisema.
Katika hatua nyingine Jumuiya ya Tawala za Mitaa (Alat), imesema Katiba mpya ikipatikana, itatoa fursa katika kujenga mfumo bora wa serikali za mitaa utakaokidhi ndoto za Watanzania katika kupeleka madaraka kwa wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Alat, Habrahamu Shamumoyo kwenye mkutano wa jumuiya hiyo wa kupanga mikakati ya kuukaribisha mwaka mpya 2001.

Alisema Jumuiya hiyo inayoziunganisha halmashauri na mamlaka za miji na wilaya,inaangalia namna inavyoweza kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa kutunga katiba mpya.
 
Back
Top Bottom