UDSM, Kitu kidogo kinarudisha mambo nyuma!

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Nimemaliza degree yangu ya kwanza mwaka 2006 katika chuo kikuu cha mlimani, Ninajaribu kuendelea na shahada ya pili, moja kati ya mahitaji ya chuo ninachoomba ni kwamba nipeleke barua kutoka chuo nilichosoma kuthibitisha kwamba degree yangu ilifundishwa kwa kingereza, na kama degree yangu haikufundishwa kwa kingereza basi inabidi nipeleke cheti kuthibitisha nimejifunza kingereza, hiki cheti kinajulikana kama TOEFL.

Sasa, kwa hali ya kawaida, kwa sababu degree yangu ilifundishwa kwa kingereza ilikua rahisi tu kupeleka barua kutoka chuo changu. Nikafunga safari hadi mlimani na nikaelekezwa niende kumuona Mr Mwetemi (ni Dr au Prof sikumbuki, enzi tunasoma tulikua tunamuita Don King kutokana na style yake ya nywele), nilipofika ofisini kwake nikakuta msg mlangoni kwake kwamba yuko hospitali na kama mtu ana shida ya kiofisi aende kwa secretary ofisi namba 7.

Hapo ofisi namba 7 ndio nilipokuta vituko. Kwanza yule mama akakataa katakata kuandika barua, ila akaniambia wao huwa wana vimitihani vyao (mradi wao) ambapo natakiwa kulipa elfu 40, ila kama ninataka sana hiyo barua basi nilipe hiyo 40 halafu yeye atanifanyia huo mpango, niwe kama nimefanya mtihani, atanijazia hiyo marks sijui A tupu sijui nini (anajua mwenyewe alitaka ajaze nini) halafu nitapata hicho cheti chao na barua ninayoitaka

HAPA NDIPO CHUO CHETU Kilipofika!

Ni kweli masecretary wa udsm kila kitu wanataka kitu kidogo bila hivyo hupati huduma mbona ni mambo ya kawaida hapo tushayazoea.

pole sana aisee,ndo tanzania hiyo,...
kama vipi waahidi kuwapa afu waite takukuru uende nao kijanja

Kama vipi Kafanye TOEFL achana nao ukishapass TOEFL nenda UDSM na TAKUKURU uwakamatishe
utakuwa umakomesha huu mchezo na utakuwa umesadia wengi kama wewe na mtanzania mpenda maendeleo ya wenzako

Piga simu za takukuru uwakamatishe,jifunzeni kupata haki zenu na acheni ujinga.kila siku mnaelimishwa na hamuelewi.wakamatishe hao then wengine watajifunza na utakuwa umeikomboa nchi.kila siku mnaimba ukombozi na hii pia ni aina ya ukombozi na utakumbukwa daima hapo chuoni.fanya haraka.

Tz bwana mpaka nashindwa kuzuia kucheka. Tatizo UDSM tulishawazoeza hivyo miaka nenda rudi, sasa tumlaumu nani? Mtu ana degree mbili af hata kujua haki za msingi hawezi. Then education for what?

kweli mkuu!

Vile visecretary vinapenda sana rushwa,nenda kuchukua cheti au transcript watakwambia subr wiki 2,hapo wanataka rushwa,ukieleweka unapata within one hour..i hate that place kw sbb ya rushwa!

Even transcript ukiitaka kwa haraka wewe toa pesa,badala ya 14 days,utaipata ndani ya 14 minutes

Chuo kwa hakika sio kisiwa. Hayo ndiyo yaliyopo katika ofisi nyingi za serikali, mahakama, polisi, hospitali n.k.

Sitaki nikuamini moja kwa moja. Kwa nchi ambazo lugha kuu si kiingereza lazima ufanye hiyo mitihani yao pale linguistic au ufanye hiyo TOEFL, kila ofisi zina utaratibu wake kama wewe ulikwenda na haraka zako then lazima wakuombe kitu kidogo ili nao waishi mjini fresh kama unataka haki basi skagonge pepa pale G. Tulip hiyo TOEFL

Hapa hatutakiwi kukupa pole ila tunatakiwa kukulaumu na ikiwezekana kukulaani!
Unashindwa nini kutafuta TAKUKURU?

Kama vipi Kafanye TOEFL achana nao ukishapass TOEFL nenda UDSM na TAKUKURU uwakamatishe
utakuwa umakomesha huu mchezo na utakuwa umesadia wengi kama wewe na mtanzania mpenda maendeleo ya wenzako

nilifikiri hivi lakini TOEFL ni zaidi ya usd 200 kufanya, ningekua nalazimika kufanya sawa, lakini nilipe zaidi ya usd 200 tu kwa sababu kuna kaSecretary hakataki kuandika barua, halafu alivo wa ajabu akasema nisitangaye eti ye ananifanyia tu msaada, yaani mwanamke ni mtu wa ajabu sana

Sitaki nikuamini moja kwa moja. Kwa nchi ambazo lugha kuu si kiingereza lazima ufanye hiyo mitihani yao pale linguistic au ufanye hiyo TOEFL, kila ofisi zina utaratibu wake kama wewe ulikwenda na haraka zako then lazima wakuombe kitu kidogo ili nao waishi mjini fresh kama unataka haki basi skagonge pepa pale G. Tulip hiyo TOEFL

hapana chief, kama degree yako ulifundishwa kwa kingereza unahitaji tu official confirmation kutoka chuo walichotoa hiyo degree (hii ni kwa chuo nilichoomba, sasa sijui huko kwingine) kama si hivyo basi TOEFL

Udsm chemchem ya taaluma,hahahah ELIMU KWANZA,HEKIMA NI UHURU,,,,,,,,,,,THE HILL,,,,,,MAJINA YOOOTE HAYO,,,,ETHICS NDO TATIZO,,,,

Halafu kudadadadadecky Tz kama mazezeta vile,yani katika social network kama hii JF wanatakiwa hata watu wa organs muhimu kama PCCB na usalama wa taifa wapate mambo yanayoendelea ktk jamii af wayafanyie kazi,but hili tatizo litaendelea kudumu milele duh!nchi ya ktu ndogo!

Back
Top Bottom