Hamna Faculty of ECSE.Mabadiliko ya muundo wa chuo yameondoa faculties.Ipo idara ya ECSE.Kirefu chake ni Electrical,Computer and Systems Engineering.
Kwanini watu hawagraduate in time?Zipo sababu kadhaa.Nitaeleza zile nilizoshuhudia kupitia marafiki ambao ni victims.
1.Hiyo iliyokuwa faculty imekuwa na tatizo la upungufu wa walimu kwa muda mrefu sana.Hii imesababisha baadhi ya wanafunzi wa shahada za uzamili kupewa majukumu makubwa.Upo mfano wa mtu aliyelazimika kufundisha kozi nzima mwanzo hadi mwisho(from lecturing,setting up and marking exams to results)
2.Njaa.Supervisors wana njaa....mishahara midogo.Hivyo wanatoa priority kwa consultancies and well funded researches kuliko supervision ya wanafunzi hao.Hili lina uhusiano na 1 hapo juu.Imagine kitivo kina uhaba wa walimu.Waliopo njaa kali.Idadi ya wanafunzi inaongezeka.Wakati huohuo wapo vijana wawili wanafanya masters.......kwanini wasifundishe ili supervisor apate muda wa kukimbizana na vijisenti mitaani?
3.Kutumiana.Yupo mwanafunzi wa masters mzuri.Anauwezo mkubwa.Hakika huyu ni wa msaada mkubwa sana kwa supervisor katika kazi zake be it research,consultancy or teaching.Kumruhusu huyu amalize masters yake mapema kutamkosesha supervisor cheap labour.
Mama Macha yupo.Kwa taarifa yako sasa amehamishiwa huko huko ECSE.Kama unamgwaya huyu usisogee ECSE kabsa ha ha haaa
BabaJ,
Asante sana kwa ufafanuzi. Hayo mabadiliko ya muundo wa kuondoa faculties nilikuwa sijayapata. Nilijua CoET ina faculties tatu ECSE, MECHE na CEBE??? ECSE ikiundwa na idara tatu tofauti.
Sasa kama hali ndiyo hivyo, hizo pesa zinazotoka kwa wafadhili zinatolewa tu alimradi zipo ama zina malengo gani? Mimi ningetegemea kwamba kila baada ya muda ni lazima ripoti ionyeshe ni wanafunzi wangapi wameweza kumaliza kutokana na scholarships hizo na pia research findings zao ziwasilishwe kwa wahusika katika muda uliowekwa. Sasa kama supervisor anaweza kuwa na mamlaka makubwa kiasi cha kuamua mwanafunzi amalize lini hata kama akisoma Master kwa miaka sita (badala ya 2 au 3), basi kuna tatizo kubwa sana hapo. Au hizo contracts kati ya mwanafunzi na chuo (c/o sponsor) hazionyeshi muda wa mwanafunzi kumaliza program yake?