UDSM & DUCE kuna nini?

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
666
421
Wadau ni mwezi wa tatu huu hatujapokea mshahara sisi wafanyakazi wa UDSM na DUCE, tunaongea na uongozi wa Chuo wanashindwa kutupa jibu Sahihi. Mishahara yetu imeenda wapi? Mtu yeyote anayejua ukweli atujuze? familia zetu zinakufa njaaa,tumekopa vya kutosha!
 
umemeajiriwa lini......mkuu. ungefunguka vizuri tungekupata, na tuweze kuchangia
 
Wadau ni mwezi wa tatu huu hatujapokea mshahara sisi wafanyakazi wa UDSM na DUCE, tunaongea na uongozi wa Chuo wanashindwa kutupa jibu Sahihi. Mishahara yetu imeenda wapi? Mtu yeyote anayejua ukweli atujuze? familia zetu zinakufa njaaa,tumekopa vya kutosha!

Aisee hebu clarify vizuri hii claim yako. Mimi ni mfanyakazi wa hapo na ninalamba salariii kama kawa.
 
Nashukuru mkuu ndio wameniingizia na mimi mchana wa leo mishahara ya miezi mitatu. Asante kwa ushirikiano weno wa kutaka kunisaidia.
 
'Kama mshahara wa mwezi huu utakuwa ule ule ambao hauna nyongeza ya mshahara,tunagoma. Hebu angalia,wenzetu wote wameshapata mishahara yao tena yenye nyongeza tangu Mwezi wa saba kwanini sisi bado? Hadi leo tarehe 3/10/2012 hatujapata mishahara. Tunafanyaje kazi? Nadhani tunataniana hapa.Safari hii tunagoma kweli kweli. Ngoja uone'

Ni maneno ya ukali na ya kutia huruma ya Profesa mmojawapo wa UDSM ambaye alinipigia simu leo 'kuniazima' hela ili auanze mwezi huu. Nimemuonea huruma yeye,Wahadhiri wengine na wafanyakazi wa UDSM kwa ujumla. Mkuu wa Kaya yuko nje anakula maisha. Kwanini lakini mambo haya?
 
Huyu Prof. analalamika kuchelewa kwa mshahara na kutopewa nyongeza ya mshahara ya mwaka 2012-2013. Hii ni tofauti na jamaa hapo juu anayedai kutopata mshahara kwa mwezi wa tatu sasa, which I think is a misconception. Ingekuwa mishahara haijatoka kwa miezi mitatu UDSM kungewaka moto
 
Actually kuna kashifa kubwa sana UDSM.
1. Iligundulika orodha ya wafanyakazi fake kibao,wengine waliokufa..akiwemo Prof Nzali,
2. Mishahara ilikuwa Fake, namaanisha kuwa kulikuwa na Mapanga ya hali ya juu kwenye mishahara ya watumishi pale, Mf,Unakuta mshahara unalipwa SIYO kiwango ambacho kinaidhinishwa na Hazina. Hii imefikia Watumishi pale kutaka Salary Slip zinazotolewa na Hazina moja kwa moja,siyo zile zinazotolewa na Bursar wapo pale.
3. Unakuta baadhi ya ma-Technician analipwa zaidi ya Lecturer..hasa kama ni wa'"kwetu" kule...
4. Prof Mgaya anatuhuma kibao,na anapaswa kula Likizo ya kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.
Habari ndo hiyo.
 
Kwanza wafanyakazi wa UDSM wameanza kupokea mishahara ya mwezi uliopita tangu jana tarehe 4/10/2012 saa sita mchana. Wameanza wafanyakazi wenye akaunti katika benki ya Makabwela yaani 'National Microfinance Bank-NMB'.

Katika mishahara hiyo, wapo watumishi waliopata ongezeko la mishahara. Wapo pia pia wasiopata ongezeko.Hawa wamepata mshahara wao wa kawaida kabla ya ongezeko. Vilevile wapo walioshushwa mishahara.

Hakuna sababu zilizotolewa na Serikali wala Chuo. Nyaraka za mishahara zinaonesha hivyo. Taarifa zinaonesha kuwa Utawala wa UDSM umeziba pengo la walishushwa mshahara ili kuzuia mgomo wa wafanyakazi wa aina hiyo.

Hali ni tete. Lolote laweza kutokea pale...
 
Mbona haueleweki mkuu, kwa hiyo wafanyakazi wameli
pwa mshahara mpya au wa zamani?

Back
Top Bottom