UDSM campus rename Mlimani Campus to JK Nyerere

This country needs me........Nyerere Road, Nyerere Airport, Nyerere grounds (Sabasaba), Nyerere Memorial Academy (Kigamboni) now Mlimani and what comes next?
Bill itapelekwa bungeni ile iwe sheria kuwa kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atakaezaliwa nchini Tanzania aitwe Nyerere.
 
Kuita Tasisi jina la mwasisi wa Taifa si vibaya..ila sasa naona hili jina lipo karibu kila mahali. Kwanini kwa hekima tusichague Taasisi moja na tukaipa hilo jina na si kila taasisi??? Leo sijui kiwanja Nyerere, Chuo Nyerere, Campus Nyerere dah...hadi jina litakosa mvuto
 
hawa watu wana matatizo kweli... !

Matatizo hasa, maana hata huko kumuenzi sijui nisemeje
  1. Pugu Road = Changed to Nyerere Road
  2. Dar es Salaam International Airport = JKNIA
  3. USDM Mlimani = UDSM Nyerere
  4. Viwanja vya maonesho ya sabasaba Kilwa Road = Viwanja vya mwalimu Nyerere
  5. ....
  6. ..... You name it
Sasa tunakoelekea ni kubadili jina la nchi kutoka United Republic of Tanzania = United Republic of Julius Nyerere

Kila sehemu sisi tunaweka sias tu. Sikatai kumuenzi muasisi wa Taifa ni jambo jema sana, Ila sasa siyo kila kitu tunabadili tu na hata kupoteza historia kabisa. Nchi nyingi huamua kuchagua site moja tu na kuipa jina la mtu wanayemuenzi, kiasi kwamba mtu akisikia jina la mtu huyo anajua exact ni nini au wapi panaongelewa, sisi sasa mpaka tunachanganyana. Maana itafikia mahali sasa hata google maps tutashindwa kuzitumia.

Haya ndiyo matatizo ya kuweka siasa kila mahali. Kuhusu Location ya UDSM Mlimani inanichanganya sasa maana niliisha wahi sikia kuwa aliye propose Location ni Al Marhum Rashid Mfaume Kawawa, Labla Nyerere anastihili kwa ku- Approve location. Hapo ndipo tunaona umuhimu wa kuweka historia sahihi.
 
kila kitu Nyerere, Nyerere, Nyerere hata mkibadilisha majina yoote hapa TZ na kuyaita Nyerere kama hamumuenzi yeye kwa matendo na kufuata aliyofundisha na kuyaamini ni bure na huu ni unafiki uliokubuhu. Anyways hivi kwa kawaida kabisa mashujaa huadhimishwa siku zao ktk tarehe walizozaliwa how com tunamuenzi Nyerere siku aliyokufa????????

you may be having a point here.

lakini kama hawa watawala waliopo hawatekelezi legacy ya mzee wetu kwa vitendo, je si bora basi hata hii consolation ya kupata even a fraction of it thru renaming after him all these outstanding landmark facilities? (msisitizo upo hapo kwenye bold & undeline maana nimesoma hapa watu wanaongelea guest houses - kitu ambacho naona ni tusi kubwa zaidi kuliko hata hii hatua ya akina Mkandara & co wanayoipinga kwa nguvu zote).

afterall, it's good that in the long run hili jina likionekana mahala pengi linaweza kuw-haunt hawa watawala wa sasa to such an extent that it may drive them back into sobreity.
 
Hapo wanaonesha walivyo na fikra fupi kwani ni vitu vingi sana vinaitwa nyerere lakini ufisadi unazidi kuongezeka. Hatuhitaji vitu kuitwa nyerere tunataka kuona maisha ya watanzania yanbadilika na kuwa boira zaidi si vinginevyo, airport, kivukoni, pugu road, noti za 1000, sasa hata campus ziwe nyerere imetosha tuone mabadiliko katika maisha ya watu
 
jamani acheni wabadilishe ili vijana wetu wakigoma kwa uhuni wa serikali yao wawezi kuimba vizuri ule wimbo wao wa kama sio juhudi zako mwalimu na sisiemu ingekuwa wapi,hahahahahaha,lakini pia naomba ushauri wa kisheria hapo kwani sizani kama wamewahusisha wanafunzi kwa hilo na kama hawajafanya hivyo sheria inasemaje hapo!
 
Ni ujinga mkubwa kwa rwekaza mukandala kuondoa jina "mlimani campus" na kuwa "mwl.jk nyerere campus".
 
C dhan km mchakato wa kubadilisha jina ulihusisha maoni ya wadau wa UDSM{including students,graduates}.huu ni upuuz m2pu!imetosha jaman!kila k2 bas 2takiita nyerere.ipo cku ht TZ itabadilishwa iitwe nyerere.sion logic kbsaaa.kwan jna la mwl tayar lina2mika pale chuo kigambon,hyo ingetosha.SIASA kitu kibaya sana.MKALIA NDALA cjui km anatumia vzr taaluma yke,nadhan watu wa magamba wanamuendesha kwa remote control.UPUMBAV M2PU.KCHEFCHEF K2PU!

Si wanafunzi tu, hata Wafanyakazi (Waalimu na Waendeshaji) hawakuulizwa maoni yao juu ya hilo. Ni University Senate ndio ilokaa na kuamua hilo. Katika yanayokera si hili tu, Subirini siku ya Alhamis mtasikia LINALOKERA NA KUCHAFUA MTIMA ZAIDI.. Another Bogus uamuzi toka senate.
 
Unafiki mwingine huo! na uvivu wa kufanya tafakuri za kina kuhusu mustakabali wa nchi yetu. Hata kama kila landmark ikiitwa JKN hakutabadili chochote kwa mustakabali wa nchi km wananchi kwa ujumla wao na hususan viongozi, hawatakuwa wazalendo wa kweli kwa matendo na kifikra, hawatajivua gamba la ugiligili wa kuweka maslahi binafsi mwanzo, ufisadi, uonezi, unafiki na kupenda vitu vya mteremko pasi na kuvitolea jasho. Historia itatusuta. Si kila kitu kizuri kimeasisiwa na nyerere...kuna watu waliojitolea mhanga kwa nchi yao lakini hawakumbukwi....Siafiki jambo hilo ingawa najua haitabadilisha chochote.
 
Back
Top Bottom