Udomasa(udom),yatoa msimamo wake juu ya migomo inayoendelea chuoni hapa

Fungo N.

JF-Expert Member
May 20, 2011
252
43
Umoja wa wanataaluma chuo kikuu cha Dodoma(UDOMASA)umetoa tamko na msimamo wake juu ya migomo mfululizo inayoendelea hapa chuoni.Ikumbukwe kuwa mpaka sasa chuo cha sayansi ya jamii na humanitia pamoja na kile cha sayansi ya mawasiliano(informatics)bado vimefungwa baada ya mgomo.Katika msimamo huo UDOMASA inautaka uongozi wa chuo na serikali kutekeleza baadhi ya mambo yafuatayo: 1-katika utatuaji wa migogoro hiyo wahusika wasiegemee upande mmoja wa wanafunzi tu, 2-wanafunzi warudi haraka chuoni kwa pamoja na sio kwa makundi kama inavyotarajiwa kufanywa,3-Viongozi wa kisiasa serikalini wasilete siasa ktk masuala ya kitaaluma, pia viongozi wa chuo wafuate maadili ya taaluma ya kazi zao na si kuendesha chuo kwa misingi ya kisiasa,4-Wamesema migomo inapunguza hadhi ya chuo si tu machoni pa wanajamii bali hata ktk soko la ajira hivyo ni vema kutatua migogoro isiyokuwa ya lazima kwani kufukuza wanafunzi ni kuumiza wazazi wasio na hatia.MADAI YAO YATATULIWE NA SI KUWAFUKUZA.Haki itendeke.
 
Yac wasomi wanazungumza mambo ya msingi,nawapongeza sana kwa hilo wawasaidie vijana warudi fasta kwny buku coz wanachodai ni haki yao.
 
hi imekaa safi maana chuo sasa kimekuwa kama jukwaa la maenyesho ya siasa, kikwete kageuza udom kama place ya kujsfia na ndo vjana wakgoma inawauma na il kutransfer blame kwa wanafunz waonekane wabaya wanaamua kuwafukuza.
 
nimeipenda hiyo uongozi wa chuo umekuwa na roho nyepesi sana kufukuza wanafunzi.
 
tatizo kabinet za vyuo vya serikali wengi ni magamba ndo maana hawapendi kujiaribia,fasta wanatoa maamuzi ya kigumashi bila kufikiria, nan asiejua madent wanadai haki yao! Solidarity daima
 
Back
Top Bottom