Udom posts selection hakuna vimemo.... Udsm watemwa!!!!

mleta thread hii umefanikiwa ktk lengo lako, maana nyavu imekamata waliotakiwa na wasiotakiwa
 
Kijana ukumbuke walipewa mtihan mmoja ili kuwaweka kwenye mizani sawa na wenzao ili kuonyesha wanastahili nafasi hizo ukiona hovyo kuna vijana walioiva zaid yao kutoka vyuo vingine ndo maana wameshindwa ku8wa among the best, idadi yenu isiwadangaye angalia ubora wenu ukoje na kwa taaarifa yako kuna interview ya writting tulifanya na wana UD walikuwa 40% kwenye oral waliitwa watu 10 walioingia top 10 kugombania nafasi 1 na UD hakuchomoza hata mmoja na niko kazin sasa na nina GPA mbovu.

Hukutumia kimemo wewe?
 
Wadau kule udom interview za nafasi mbali mbali zinaendelea usiku na mchana!!!
Amini usiamini son of peasant naye kapigiwa simu kwenda kuchapa interview ya admin. Officer lkn habari chini ya kapeti zinasema udsm hakuwepo hata mmoja kwenye hiyo makitu!!! Sasa mimi nashindwa kujua imekuwaje au wanaogopa challenge, lkn wajue vijana wachuo kile wameiva sana sisi tunao watumia ndio tunajua uzuri wao, msiogope ufaulu wao mdogo wapeni kazi muone mziki wake!!


Poleni udsm..... Kazeni buti nyinyi ni vichwa.

mbaazi ukikosa maua husingizia jua, maneno ya mkosaji, kilio cha samaki, hakina machozi machozi juenda na maji..........
 
kweli bado sana,watanzania hatujaelimika.hivi watu mmesoma lakini bado mnaubiri ushabiki wa vyuo?.mi ata GPA za Tz hazinisumbui,jambo la msingi ni uwezo wa mtu husika
 
Ok tuachane na hayo, hayana mashiko, tuache kubaguana,posti zingine kama wahasibu n.k nao wanaitwa lini, manake naona wanaitwa wengine tu au tayari nao walishaiwa kitambo,manake nikiingia kwenye website yao sioni chochote, kimya tu
 
Ni matatizo ya esteem tuu kwa wale nje ya UD wana kahasira kwa kukosa(rejection) na UD km kawaida yao huwa wanajisikia wao ndio chuo....Na mbaya zaidi hadi leo wanaamini hivyo. Ni kitabia cha UD hata kati yao wenyewe.Na hata watokao UD wakipata nafasi(zamani walipokuwa km standard) walikuwa wanapeleka culture yao.Msihofu dunia ya ubunifu na utendaji somewhere uwezo binafsi utajipambanua.
 
Enyi vijana wa Kitanzania: Mnapaswa kuachana na fikra mgando sasa ili muijenge nchi yenu kwa umoja wenu. Mnasikitisha sana kwa mambo mnayopoteza muda na kuyajadili. Miaka nenda rudi mtakuwa mnahukumiwa kwa kuwa hamjui majukumu yenu.. Wazee wenu ni masikini sana, mnasomeshwa kwa pesa za mkopo wa walipa kodi ambao ni masikini wa Tanzania hii, mnapata shahada zenu, hamfanyi mijadala ya maana ila mnajadili chuo kipi kinatoa watu bora? .....ni utumwa mkubwa sana wa kifikra mlio kuwa nao. Elimu yenu HAITASAIDIA KAMWE kulikomboa Taifa kama vijana. Hiyo UD imekuwa Chuo kikuu hapo Tanzania kwa miaka mingi sasa, Idadi kubwa ya viongozi wote Tanzania wamesoma hapo. Idadi fulani ya viongozi wa Africa wamesoma hapo, Ni hao viongozi ambao tunawalaumu kila siku kwa Ufisadi na ubovu wa uongozi wao wametoka hapo. Chama cha CCM mnakilaumu kila uchao. Viongozi wao wametoka hapo. Kama wao ni wabovu basi tuseme CHUO WALIMOTOKA NDIO CHANZO, hivyo UD tunaweza kujumuisha kuwa huzalisha wasomi Chapwa kwa mtaji huu. Lakini Enyi vijana, mkumbuke pia kuwa hatungeweza kusoma wote UD, lazima wengine sasa waende katika vyuo vingine kwani nchini mwetu sasa kumekuwa na hitaji kubwa la vyuo. Au mlitaraji tuwe na CHUO KIKUU KIMOJA TU? Hivyo sio wakati wa kujisifia Ki Uvyuo. wako watanzania wamesoma na wanaendelea kusoma katika vyuo vikubwa sana hapa Ulimwenguni, wengine wamatoka ktk familia za kawaida sana, sasa hao nao wajisifie kwa vyuo vyao? au tukae kwa pamoja tujenge nchi yetu? Hamna tofauti na wakati ule ukifika Form v mnaanza kujitenga kulingana na shule mlizosoma, mf wa Mkwawa, Ifunda, Tabora nk.. kama wote mlifanya form vi mkafanya vema huko kusoma UD ndio kuna jipya lipi? Na kwa taarifa tu hapo UDOM mnapopasakama hao wahadhiri wengi ama wamesoma na pia waliwahi kuwa wahadhiri na viongozi wa UD, leo wawaogope wanafunzi wa UD, mna nini kipya basi nyie ambao mnaisoma leo hiyo UD? wote ni walewale tu tulioibia mitihani na kupata vialama tukapata hiyo shule...... Achaneni na UD hapa kwani wala hamjui wana JF wengine waliko ama wanaposoma.......


Mkuu umejibu vizuri ingawa naona una kahasira fulani hivi!
 
Back
Top Bottom