Udom posts selection hakuna vimemo.... Udsm watemwa!!!!

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,474
12,710
Wadau kule udom interview za nafasi mbali mbali zinaendelea usiku na mchana!!!
Amini usiamini son of peasant naye kapigiwa simu kwenda kuchapa interview ya admin. Officer lkn habari chini ya kapeti zinasema udsm hakuwepo hata mmoja kwenye hiyo makitu!!! Sasa mimi nashindwa kujua imekuwaje au wanaogopa challenge, lkn wajue vijana wachuo kile wameiva sana sisi tunao watumia ndio tunajua uzuri wao, msiogope ufaulu wao mdogo wapeni kazi muone mziki wake!!

Poleni udsm..... Kazeni buti nyinyi ni vichwa.
 
ha ha ha ha ha ha umejuaje bana ...UDOM nadhani wanawaogopa sana watu wa UDSM kuanza hata wanafunzi wa pale wanawaogopa wadau wa UD kwa utafiti mdogo uliofanyika
 
Kijana ukumbuke walipewa mtihan mmoja ili kuwaweka kwenye mizani sawa na wenzao ili kuonyesha wanastahili nafasi hizo ukiona hovyo kuna vijana walioiva zaid yao kutoka vyuo vingine ndo maana wameshindwa ku8wa among the best, idadi yenu isiwadangaye angalia ubora wenu ukoje na kwa taaarifa yako kuna interview ya writting tulifanya na wana UD walikuwa 40% kwenye oral waliitwa watu 10 walioingia top 10 kugombania nafasi 1 na UD hakuchomoza hata mmoja na niko kazin sasa na nina GPA mbovu.
 
ha ha ha ha ha ha umejuaje bana ...UDOM nadhani wanawaogopa sana watu wa UDSM kuanza hata wanafunzi wa pale wanawaogopa wadau wa UD kwa utafiti mdogo uliofanyika

achen kasumba zenu za enzi za mwalimu za kuabudu majina na rank ya chuo kuna vijana wengi tu bora wa kutoka taasisi mbalimbali za elimu wanafanya vizuri kuliko nyinyi, kazeni buti mshindane nao na si kelele tu za kulalamika wakati vichwani weupe tu. Mmeshindwa kuwa vinara kwenye pepa ndo maana idadi yenu ndogo.
 
binafsi naamini swala la kazi siku hizi ni bahati na nauhakika hao watu hawakuzingatia au kuweka vigezo tunawapa watu kazi kwa vyuo ! tusiwe wajinga buy da way walio kuwepo kwenye panel zaidi ya asilimia 70 wamesoma ud tubadilike!
 
Enyi vijana wa Kitanzania: Mnapaswa kuachana na fikra mgando sasa ili muijenge nchi yenu kwa umoja wenu. Mnasikitisha sana kwa mambo mnayopoteza muda na kuyajadili. Miaka nenda rudi mtakuwa mnahukumiwa kwa kuwa hamjui majukumu yenu.. Wazee wenu ni masikini sana, mnasomeshwa kwa pesa za mkopo wa walipa kodi ambao ni masikini wa Tanzania hii, mnapata shahada zenu, hamfanyi mijadala ya maana ila mnajadili chuo kipi kinatoa watu bora? .....ni utumwa mkubwa sana wa kifikra mlio kuwa nao. Elimu yenu HAITASAIDIA KAMWE kulikomboa Taifa kama vijana. Hiyo UD imekuwa Chuo kikuu hapo Tanzania kwa miaka mingi sasa, Idadi kubwa ya viongozi wote Tanzania wamesoma hapo. Idadi fulani ya viongozi wa Africa wamesoma hapo, Ni hao viongozi ambao tunawalaumu kila siku kwa Ufisadi na ubovu wa uongozi wao wametoka hapo. Chama cha CCM mnakilaumu kila uchao. Viongozi wao wametoka hapo. Kama wao ni wabovu basi tuseme CHUO WALIMOTOKA NDIO CHANZO, hivyo UD tunaweza kujumuisha kuwa huzalisha wasomi Chapwa kwa mtaji huu. Lakini Enyi vijana, mkumbuke pia kuwa hatungeweza kusoma wote UD, lazima wengine sasa waende katika vyuo vingine kwani nchini mwetu sasa kumekuwa na hitaji kubwa la vyuo. Au mlitaraji tuwe na CHUO KIKUU KIMOJA TU? Hivyo sio wakati wa kujisifia Ki Uvyuo. wako watanzania wamesoma na wanaendelea kusoma katika vyuo vikubwa sana hapa Ulimwenguni, wengine wamatoka ktk familia za kawaida sana, sasa hao nao wajisifie kwa vyuo vyao? au tukae kwa pamoja tujenge nchi yetu? Hamna tofauti na wakati ule ukifika Form v mnaanza kujitenga kulingana na shule mlizosoma, mf wa Mkwawa, Ifunda, Tabora nk.. kama wote mlifanya form vi mkafanya vema huko kusoma UD ndio kuna jipya lipi? Na kwa taarifa tu hapo UDOM mnapopasakama hao wahadhiri wengi ama wamesoma na pia waliwahi kuwa wahadhiri na viongozi wa UD, leo wawaogope wanafunzi wa UD, mna nini kipya basi nyie ambao mnaisoma leo hiyo UD? wote ni walewale tu tulioibia mitihani na kupata vialama tukapata hiyo shule...... Achaneni na UD hapa kwani wala hamjui wana JF wengine waliko ama wanaposoma.......
 
Kazi kweli kweli, akili ya mtu haiwezi kuhesabiwa kutokana na chuo alichosoma, wanasayansi wengi hawakuwa maarufu kwa sababu ya vyuo walivyosoma bali walikuwa talented(gifted). Sasa tumeshaona udini, ukabila n.k havina umuhimu tena tunahamia UCHUO. Namuunga mkono sana Makole. Tuwe na fikra za kisomi, fikra endelevu na zinazoleta ukombozi.
 
Back
Top Bottom