Udom kwa mtindo huu mtafukuza wengi

Posho City

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
646
415
Chuo kikuu cha Dodoma hadi sasa tangu chuo kifunguliwe tarehe 03/03/2012,kwa semista ya pili hawajatoa pesa za kujikimu kwa wanafunzi na hakuna taarifa rasmi wanatoa lini.Kumbuka mwezi wa kwanza walichelewesha hivyohivyo wanafunzi walipoandamana kwenda utawala,baada ya wiki moja wakafukuza wenzetu 29.bila sababu za msingi.Kuna TETES kuwa hela hizo zipo muda mrefu lakini wanafanya makusudi ili watu wagome wawafukuze wanaowaita wafuasi wa chadema.Lilitoka tangazo la waziri wa mikopo kuwa sababu za kuchelewa zipo nje ya uongozi wa chuo,akimaanisha ni tatizo la bodi ya mikopo,lakini iweje bodi hiyohiyo itoe hela udsm na kwingineko na isitoe kwa udom?!!!!Wakati huo huo wanatulazimisha tulipe ada na hela ya hostel.Tatizo pia hata serikali ya wanafunzi tuliyonayo ni ya kijinga isiyokuwa na upeo na wanaongoza kwa maelekezo ya Mlacha na Kikula.Kiuhalisai mfano huku kitivo cha elimu mimi nilipo hali ni mbaya na kumbuka hakunaga ustaarabu kwa mwenye njaa watu wameshaanza kusema wataingia barabarani liwalo na liwe.

HIYO NDO UDOM CHUO AMBACHO WANASIASA WALISEMA KITAKUWA BORA KULIKO VYOTE AFRIKA MASHARIKI,LAKINI KIUKWELI SIYO CHUO KIKUU NI CHUO KIKUBWA
 
Poleni sana ndiyo maana wahadhiri wengi wanazidi kuhama na wengi wao wako Mandela Institute of Technology
 
vipi hao wanachuo wanaojiita wakereketwa wa sisiemu na wao pia hawakupewa hilo boom?
 
UDOM mbona wepesi kupelekwa pelekwa? Hadi makazini mtakuwa mnanyimwa haki hivyo hivyo kwa kuhofia kuachishwa kazi. "IT BETTER TO FIGHT FOR SOMETHING THAN TO LIVE FOR NOTHING".
 
Hali ni mbaya mabinti huku social nimetoka saa nje saa sita usiku nimekutwa wanasombwa na teksii wakiwa wanatoka nusu u.chi. Wazazi mnajua mabinti zenu wanayofanya? Wapeni pesa ya kujikimu
 
mmeyataka nyie mwenyewe....nyinyi si ndio 2010 mlichangia chama cha sisi.....wetu katika kampani za uraisi,ubunge na udiwani sasa mnalalamika nini........
 
Tugome bana, ,no way out, hata kipind kile walituzngua hv hv,tulipogoma wakatoa tamko, ,
 
Ondokeni chuo!!Sasa mnapokeaje masomo bila kula?.Ondokeni chuo bebeni mabegi mpitie utawala mkawaage kuwa mnaenda nyumbani mmeshindwa kusoma bila kula,kisha kila mtu anaenda kwao!Just simple!!Hapo mnakuwa hamjagoma ila mmeondoka kuhofia kupoteza maisha kwa sababu ya njaa.
 
poleni sana.
Wale vijana wa CCM UDOM ,kama kweli wanaguswa na wenye uhitaji ,kama walivyojitoa kumchangia JK mwaka 2010,sasa wajikusanye tena wawachangie na nyinyi.
 
Mi kinachonishangaza ni wanafunzi wa udom kumvizia Mlacha eti wamwue kwa madai yeye ndo chanzo cha matatizo na rais ameshindwa kumwondoa kwenye nafasi hiyo,akifa lazima atakuja mwingine. Hivi ni yeye kweli au ni bodi ya mikopo?
 
Back
Top Bottom