Udokozi unawaponza Wabongo kupata ajira

kila kijana TZ anataka kuwa fisadi. kuwa fisadi bongo ni sifa, vijana wanaona viongozi wanavyopata utajiri wa haraka na wao ndio wanataka huo utajiri wa haraka...

kila mtu bongo anakuambia sitegemei mshahara, unadhani anamahanisha nini...
wengine wanasema serikali mshahara kidogo lakini dili kibao....
ukiwa umeotoka nje unatafuta kazi unataka mshahara mkubwa marafiki zako wanakuambia mshahara si kitu bwana we chukua tu kazi ukifika hapo mara unaanza kupata vidili kibao...
huyo kapuya anasema watu wanaiba vitu vidogo kwa hiyo anafurai wale wanaoiba vitu vikubwa

sababu ya wageni wengi ni kuwa makampuni ya kigeni hayataki ku-train local people, ulaya wenyewe wanatrain graduates wao kwa nini bongo hawataki...

ukitaka kukomesha uwizi mdogo lazima ukomeshe uwizi mkubwa kwanza na uvivu, hii ni dhairi kabisa kapuya ni mvivu na ametafuta kisingizio

TZ hamna work ethics kwa ajili ya rushwa, mtu yupo kazini kwa ajili ya mtu fulani...
kama akijua uzembe utamfanya afukuzwe kazi lazima atajikaza tu..
"angalia dereva wa daladala lazima apeleke hesabu kwa bosi jioni kila siku anajua kama hesabu haijatimia kazi anayo"
 
Ahsante jamani.

Naomba tulijadili kwa kina. Hapa nilipo nimesistitisha mradi niliokuwa niuanze kwakuwapatia wadogo zangu mshiko lakini imekuwa ni lawama baada ya kujiondoa.

tatizo la kuiba au ufujaji wa mitaji watu wanayopewa kusimamia ni sugu na siye tulio majuu tunapata lawama eti hatuwapi mikopo ndugu zetu kumbe ndo kabisaa hawafai kwa sababu hata akiula huwezi kunfunga kwani ndugu wanaweza wakaandamana.

Plz any one with idea? Ukweli umaskini uliopo bongo binafsi unaniuma sana.

Yaani ukisikia ndugu lawama .... ndio hayo hata mimi yamenikuta, nimefunga Food cafe na saluni yangu kubwa tu kwakuliwa mtaji wote, ukisema uweke kijana asimamie nae anataka ainukie hapohapo...uaminifu ni zero bongo kila kitu inabidi usimamie mwenyewe kitu ambacho hakiwezekani.
Nilichokifanya nimekamata biashara moja naisimamia mwenyewe na ndugu wote nimewapiga chini cha moto wanakiona..
 
Ninaomba nirejee hitimisho au suluhisho alilolitoa Alh. Prof. Mh. Waziri kuwa Wizara yake imewasiliana na VETA ili somo la uaminifu liingizwe kwenye mtaala. Sasa swali langu ni kuwa ni vijana wangapi wanaopitia mafunzo ya VETA ili hilo somo liwasaidie? Kama tatizo la udokozi lipo kwenye sekta zote za ajira, mtaala wa uaminifu VETA hautasaidia. La msingi ninaloliona ni kuwa na sheria kali zitakazowabana wale watakaobainika wameiba kwenye sekta walizoajiriwa, ili waadhibiwe vikali kiasi kwamba hata wengine wakifikiri kudokoa waamue kuacha.
Kuna wakati "wachagga" walikuwa wanaonekana watu hatari wanapoajiriwa maeneo mbalimbali kuwa ni wezi au wapenda hela, kumbe ni janga la kitaifa.....
 
Huu ni upuuzi kuna nchi nyingi sana watu wake walevi na wadokozi lakini haiwi sababu ya kutoajili watu kwa sababu hiyo.Hiyo sababu ni ya kipuuzi sana.Kwani Mtanzania mmoja akiiba basi wote ni wezi.Mnataka kutuambia kwamba wazungu wote wabaguzi?

Viongozi wetu ni magarasa tena Joker na wanatoa sababu za kipuuzi kuhalalisha ujinga wao.
 
Teh teh teh teh
Kwa hiyo mnakili kuwa tatizo la ufisadi si tatizo la chama fulani bali ni kwa sisi watanzania wote.

Ndiyo maana tunapigia kelele tatizo la ufisadi wa sasa liishe ili tumulike ufisadi mwingine kama huu. Hivi ni wangapi ambao wanawaza kujenga jumba kubwa Mbezi hata kama hana uwezo huo. Matokeo yake ni kama vile tunapiga kelele ufisadi uliopo ili waondoke halafu na sisi iwe zamu yetu.
ni haki wawekezaji walete watu kutoka kwao maana wanatujua kwa miezi michache wanapofika nchini. Kuna baadhi ya hoteli nchini unakuta zimeandikwa "Beware you're in Africa". Mgeni anatahadharishiwa alinde vitu vyake aisifikirie kwamba hotel aliyofikia ni kubwa kwamba hakuna wizi.
Hivyo ufisadi ni vita pana kuliko tunavyofikiri.
 
Ndugu zangu sio kazi zote sinahusu pesa na ni rahisi kuiba.Mimi nimefanya kazi Tanzania kama Mhasibu na nakuhakikishia sio rahisi hata kidogo kama watu wanavyofikiri kuiba kwani kuna mlolongo wa hatua (Red Tape) mpaka uwezi kuiba hizo hela.Mfano itabidi uwashirikishe watu 15 kuiba million moja sasa hata ukiweza kuiba hiyo hela mtagawana shillingi ngapi ngapi kila mmoja.Hivi ni watanzania wangapi wanafanya kazi kwenye sehemu nyeti na hawaibi hizo hela.Imefika wakati kukataa kila kitu tunachoambiwa kwa sababu itakuwa zambi kuwajumuisha watanzania wote kama ni wezi kwa makosa ya wachache na ndio iwe sababu ya kutoajiriwa.

Kumbukeni sio kila kazi watu wataweza kuiba kiurahisi.kwani ikiwekwa misingi ya kazi imara wizi hautakuwepo kabisa.

Unapuzungumzia swala la ndugu kula hela haliendani kabisa na misingi ya kazi kwenye mashirika au makampuni hilo ni swala binafsi kati yako na ndugu yako na inategemea misingi na malezi ya hao ndugu zako
 
  • Ndugu zangu lazima tukubaliane kuwa hili ni tatizo kubwa sana katika nchi yetu, na limelelewa kwa muda mrefu hata limeshakuwa sugu. Watz wengi wanapenda maisha ya mkato, yaani akifanya kazi kidogo awe na kila kitu, ndio maana wale wanaoitumikia nchi kwa uaminifu wanaishia kuwa na maisha ya shida na wale wezi ndio wanapeta kwenye nafasi za uongozi.

  • Wale wanaofanya kazi kwa kufuata maadili wanaishiwa kuundiwa zengwe la kuondolewa kazini au kufukuzwa kwa hila (kila mmoja wetu anaweza kuwa na mifano)

  • Bahati mbaya dhana hii imejikita sana kiasi kwamba wizi ni sifa mtaani, ukiiba kazini na kujenga nyumba nzuri na usafiri wa maana wewe ndio mjanja.

  • Uaminifu ni sifuri kwa watz walio wengi, si jamii ya wasomi wala wasio wasomi.Fuatilia visa vingi vya uongozi katika taasisi mbalimbali ndio utagundua hilo, hata vyuo vikuu vyetu vingi vinaendeshwa na watu ambao kwao maadili ni msamiati usio na maana.

  • Nasikitika kusema kuwa mshahara kidogo sio hasa tatizo, hili ni tatizo la mfumo mzima, kwani mshahara gani ni mkubwa? kila mshahara utakaopewa utataka ungepewa zaidi, kutibu hili ni vyema tukajaribu kuwa na mitaala toka shule za msingi, tatizo hata walimu wenyewe ndio haohao, wanafanya ualimu kwa kuwa hawana chaguo jingine. Shule za sekondari, vyuo vikuu kote huko watu waelezwe umuhimu wa kuheshimu mali ya watu wengine na ya jamii yote. Tukianza kuwa wazalendo inawezekana.

  • Lakini hili tatizo ni kubwa kuliko tunavyolichukulia, unapoona mpaka waziri anafoji stakabadhi za malipo hawezi kuishia kulaumu anayeiba vitu vidogo vidogo, Kapuya alitakiwa atamke wazi kuwa ni tatizo lilomea mizizi hata ndani ya wabunge na baraza lote la mawaziri. Nasikitika kama yalivyo matatizo yetu mengi nchini hatuna mikakati yoyote ya kutokomeza, mtu aliyesoma kwa kuiba mitihani unategemea aache kuiba cement stoo na kuuza? unategemea awe waziri asiyecollude na watendaji kuiba? sijui wizi upo kwenye genes au ni nini? tusaidiane maana Kapuya kaangalia kwa mtazamo mdogo mno...
 
da hapo mmegusa mahali pake,kweli mishahara hailipi yaani hata kidogo,huduma na job security ni mbaya sana bongo sio siri watu wafanyeje?yaani uibe usiibe yote sawa tu hakuna atakaye kusifia kwamba jamaa haibi ila utachekwa na machungu ya maisha utayaona wakati wenzio wanapiga dili wanachekelea,ni kuiba tu mwanzo mwisho mpaka kieleweke ukipigwa chini kazi poa unatumia ulizoiba mpaka upate kazi ingine,huyo kapuya mwenyewe aulizwe kama mali zote alizonazo mpaka anawalea wazaire kibao kwake pale na biashara zisizoeleweka ni kwa ajili ya mshahara wake tuu?hii ndo tabu yetu wabongo kukumbatia wageni ndio dili,anatetea kama hao wageni waaminifu wakati ndo wanakwepakodi na wanajaza dola kwenye viloba wanapeleka kwao.yaani tanzania ni katastroph kabisa kama kiongozi anatetea haya mambo badala ya kutafuta mbinu mbadala ya kupunguza hao wageni ili wazalendo wapate kazi!!hii inakatisha tamaa kabsaaaa kurudi home
 
Nimefurahi kwakuwa JF sasa tunaanza kuwa objective kwenye maswala ambayo yana ukweli ndani yake. Tanzania kila mtu ni fisadi kwa level yake kwani ndio mfumo tulioujenga kwa wananchi wetu, hili sio la kushangaza na sio vijana tu hata watu wazima wanaiba wakati mwingine vitu vidogo ambavyo hata kazi navyo saa nyingine hana lakini ameiba.

Tanzania ni fashio kumuibia mwajiri wako kila kinachowezekana na ndio maana hata tunapoongelea ufisadi watu wengin wanakwambia hayo maneno yenu tu kwani nyinyi mkipewa nafasi hamtaweza kuiba, yaani kusema furani mwizi unaonekana kama una fitna, wivu n.k.

Nakubaliana na mchangiaji mmoja hapo juu kuwa serikali hiweke somo la uaminifu kwenye mitaala ya elimu zote kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu kuokoa work ethics.

Kea wenzetu swala la ethics ni muhimu sana na ndio maana wanafanya search kila mtu anapotaka kuajiriwa na zinatekelezwa sio hapa kwetu ambapo hata data base ya kujua mtu furani aliachishwa na kampuni furani kwa wizi hatuna.
 
Kapuya alishirikiana na Mkapa kuiba rasilimali za tanesco kupitia kwa net group solution. Mbona yeye hajisemi? Akumbuke kauli yake ya mwisho aliyoitoa hadi macho kumtoka kutishia wafanyakazi wazalendo wa Tanesco ambao walijitolea kupinga ufisadi ule. Kiko wapi leo na Net Group ile?

Anyway, suala la udokozi ni Hulka ya mtu na si ku generalise kama afanyavyo kapuya na kuungwa mkono na baadhi yetu humu.

Serikali ishughulikie mambo ya msingi yanayowakwaza watanzania na si kuleta longolongo hizi. kapuya na wenzako amkeni!!!!!
 
What I like about this wanton and shamefully condenscending soliloquy on the part of our leaders, is the fact that we can see their true colors.

What I don't like is the colors I see.
 
Udokozi unawaponza Wabongo kupata ajira

Na Ramadhan Mbwaduke
20th July 2009

Serikali imesema tatizo la uaminifu kwa vijana walio wengi nchini linachangia kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira nchini kwani huwafanya baadhi ya wenye makampuni kulazimika kuja nchini na watu wao walio na moyo safi na kuwaajiri.

Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, amesema hivi sasa, kuna matukio mengi ya aibu yahusianayo na wizi wa pesa, mali na vifaa vya makampuni, ambayo hujikuta yakiingia hasara kubwa.

Kwa sababu hiyo, Waziri Kapuya akasema wahusika wanaoendesha kampuni hizo hulazimika kuajiri watu wa kwao ili kushika nafasi ambazo Watanzania wangeweza kuzitumikia kwa uwezo sawa au hata zaidi ya wageni wanaowaleta.

"Inafikia mahala hata kijisimu tu (cha mkononi) kinaposahauliwa kidogo tu, kinakwapuliwa... Kwa kweli hili ni tatizo ambalo limeanza kuwa kubwa na linasikitisha sana," akasema Waziri Kapuya, huku akitaja sekta mojawapo inayokumbwa zaidi na tatizo hilo kuwa ni ya huduma za hoteli.

Akitolea mfano zaidi, Waziri Kapuya ameema hata Wachina wanaoendelea na ujenzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma wamekuwa wakikumbana na matatizo ya kuibiwa mali zao na vifaa vya ujenzi kila kukicha, hali ambayo inawafanya walalamike kila mara kutokana na hasara wanayoipata.

"Nenda pale UDOM (Chuo Kikuu cha Dodoma)... Wachina wanaibiwa stoo kila siku. Je, Mchina Mjenzi akisema anataka meneja anayesimamia vifaa awe Mchina mwenzie kwa sababu waliopo sasa wanamuibia sana, halafu we ukiwa Waziri utasemaje? Ni tatizo kubwa kwa kweli," akasema Waziri Kapuya.

Aidha ameongeza kuwa hivi sasa, Wizara yake imewasiliana na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi nchini, VETA ili iweze kuongeza somo la uaminifu katika mtaala wake ili walau kupunguza tatizo hilo ambalo linaleta athari kubwa katika sekta ya ajira.

"Nashukuru kwamba baada ya kuzungumza na VETA, hivi sasa suala hilo limekubaliwa na litawekwa katika mitaala yao ili kuondokana na tatizo hili la uaminifu," akasema Waziri Kapuya.

- Haya ni maneno ya kusikitisha sana knowing kuwa yamesemwa na kiongozi mwenye capacity ya Minister of state, shame on Kapuya tena Professor mzima, badala ya kuongelea sababu inayowafanya vijana wawe wezi kwamba wanaiga tu tabia za kifisadi za viongozi kama yeye, na wengine wengi yeye anajaribu kukwepa responsibility na kujiosha in the process na kuna wananchi tunaokubali kwamba he is right, oh my my my my Tanzania nchi yangu, hivi ulimkosea nini Mungu?

- Kapuya, huwezi panda mihogo ukavuna mahindi wananchi ni wezi kwa sababu viongozi wao wewe included ni wezi, usingekua usingeweza kumiliki mgodi kwa mshahara wa uwaziri tu, na habari za mgodi wako zingekuwa ziko wazi kwa public na sio kusubiri upate ajali huku kukiwa na mjadala wa Zitto na migodi, hakuna anayejua kama mgodi ulinunuliwa kwa halali, unalipiwa kodi, lakini here is the man akitupia lawama vijana as if sisi wabongo wote ni mambumbu!

Can somebody tell this man to shut up!, I mean enough! kila mwananchi ataiba kwa urefu wa kamba yake!

Respect.

Kamanda FMEs!
 
- Haya ni maneno ya kusikitisha sana knowing kuwa yamesemwa na kiongozi mwenye capacity ya Minister of state, shame on Kapuya tena Professor mzima, badala ya kuongelea sababu inayowafanya vijana wawe wezi kwamba wanaiga tu tabia za kifisadi za viongozi kama yeye, na wengine wengi yeye anajaribu kukwepa responsibility na kujiosha in the process na kuna wananchi tunaokubali kwamba he is right, oh my my my my Tanzania nchi yangu, hivi ulimkosea nini Mungu?

- Kapuya, huwezi panda mihogo ukavuna mahindi wananchi ni wezi kwa sababu viongozi wao wewe included ni wezi, usingekua usingeweza kumiliki mgodi kwa mshahara wa uwaziri tu, na habari za mgodi wako zingekuwa ziko wazi kwa public na sio kusubiri upate ajali huku kukiwa na mjadala wa Zitto na migodi, hakuna anayejua kama mgodi ulinunuliwa kwa halali, unalipiwa kodi, lakini here is the man akitupia lawama vijana as if sisi wabongo wote ni mambumbu!

Can somebody tell this man to shut up!, I mean enough! kila mwananchi ataiba kwa urefu wa kamba yake!

Respect.

Kamanda FMEs!

Kamanda FMES ume capture mawazo yangu kwenye hili, waingereza hili wanaliita "blaming the victim". "Give a dog a bad name, then kill it" style.

Kabla ya kulaumu hawa wahanga, waziri anaweza kueleza sababu kwa nini watu hawajui kiingereza? Kuna library ngapi? Vipato vya watu vinaruhusu kununua vitabu?

Hiyo inhuman per capita GDP wanayopewa watu hata wakiiba kuwalaumu itakuwa ni kwa sababu za ethics tu, lakini practically ndiyo mishahara wanayopunjwa hiyo.
 
Well mnaposema vijana wadokozi kwani hakuna sheria? Huyu Waziri ni mdokozi vile vile. Ni wapi hapa ulimwenguni ambako hakuna wadokozi? Hii ni tabia tu na kama hakuna sheria kama ilivyo Tanzania huu udokozi utaendelea. Lowasa alidokoa na anaendelea kudokoa kwa sababu sheria hatutaki kuzifuata. Jakaya Kikwete ni mdokozi anatumia pesa ya walipa kodi bila ridhaa ya bunge halafu anakuja kuomba ridhaa. Rostam Aziz ni mdokozi ambaye anaifadhili CCM - Matokeo yote haya yako wazi sasa kwa nini muanze kusema ati vijana wadokozi? Semeni viongozi wa Tanzania ni wadokozi. Mkikubali hilo ndio mnaweza kuondoa tatizo sio kukimbilia kwamba ati vijana wadokozi.
Kwani hayo makampuni hayadokoi? Au udokozi ni wa toilet paper tu?


Ni hayo tu nimeona niwaamshe kidogo.
 
Tatizo la mawaziri wetu hawana taaluma sahihi katika nafasi husika, hivi kapuya ni professa wa nini? isijekuwa ni professa wa wanyama pori hivyo anaona kila karacta ya mtu ni kama ya chatu au sokwe! hao wabulgaria wamezaliwa kinondoni?

Tunaomba Kapuya atupe list ya makampuni yanayosema yakiajiri watz yataibiwa tufanye HRM case study nadhani hii inaweza kuwa "statement of the problem" nzuri ya kufanyia research.

Rais wa nchi ni mtz, mkuu wa majeshi, spika wa bunge ni mtz, yaani mihimili yote ya dola ni watz, kama kuna mbeba box anaona watz hawafai akafanye biashara Laxenburg, makampuni yaliyoona watz hawafai yaliondoka pamoja na Gavana Twining!
 
Waziri kwa kifupi kawatukana Watanzania, na kama nchi ingekuwa na press inayojua kushikisha watu adabu, anekuwa anajiuzulu sasa hivi.
 
Hii kauli ya mkoloni mweusi vipi? Mwingereza alileta Makarani na madereva wa malori (karisinga)kutoka India kisa hatukuwa tunajua kiingereza, Mjerumani alileta wahima kutoka falme za Bunyoro waje kutawala washubi na watwa (wahaya). yeye anataka wachina wawe substitute ya watz, hii kebehi sasa.
 
Hili siyo tatizo la ethics za kazi peke yake, ni tatizo la kumong'onyoka kwa maadili ya maisha kwa ujumla katika nchi. Uliona wapi nchi ambako wezi, mafisadi, wala rushwa, majambazi na majangiri ndo wanasifiwa kuliko watu waadilifu??
Chama tawala kimekuwa genge la mafisadi, wizi kuanzia wa kura, maliasili zetu, mikataba ya kishenzi, mpaka fedha taslimu benki (EPA nk), na wanaona hivyo ndivyo nchi inapaswa kuongozwa!
Unategemea waongozwaji watakuwaje? Baba wa familia akiwa "panja" unadhani hiyo familia itakuwaje?
Tuna tatizo kubwa sana la kimaadili, tusipoziba ufa sasa tutajenga ukuta.
 
Hili ni tatizo kubwa wala sii Udokozi.. Mbongo ukimwachia duka basi akili yake kesho afungue la kwake na mtaji utatoka dukani kwako..Hivyo chimbuko lake limetokana na kuuvamia Ubepari..

We acha kabisa. Mimi pia nimegombana sana na vijana wanaouza pale Mlimani City. Wakiona unataka kununua kitu cha thamani kubwa kidogo wanakufuata...oohh boss sasa, tuongee, sisi tunaweza kukupatia kwa bei nzuri na sisi utuangalie. Ukiwauliza kivipi, wanakwambia tutakutolea bila receipt kwa bei chee. Sasa kama mimi nilikuwa nataka kitu cha bei chee si ningeenda Kariakoo, kwani sijui wanapounza bei chee? Ninawaambia nyie vijana ni wajinga hamjui mnalolifanya; huyu mwenye duka akipata hasara kila siku atafunga duka lake na kuliamishia nchi nyingine, na nyie ndiyo mtakaoumia maana mtakosa kazi.

It is really terribly pathetic, yaani roho za watu zimekaa kuibaiba tu. Hili ni tatizo kubwa sana katika nchi yetu, na msingi wake ni watu kupenda vitu vya dezo. Yaani unaweza ukampa mtu kitu cha bure anapokea bila hata kujiuliza kwa nini huyu mtu ananipa hiki kitu. Ile kujua kwamba hiki kitu sio cha kwangu hatuna. Na hili ni tatizo la zaidi ya umaskini. It is something that is increasingly becoming enshrined in our culture. Ndio maana hata maviongozi yetu mengine hayaogopi kutuibia; kumbe yataogopa vipi kama yalianza kuiba tangu yalipokuwa madogo? Jana tulikuwa tunajadili jambo hilihili, kijana moja akasema "kila mtanzania ni mwizi tu, isipokuwa kuna wengine hawajapata nafasi ya kuiba"!!! Nilimkatalia sana, lakini ukitulia kidogo, utaona kwamba kuna ukweli mwingi sana kwenye hii sentensi ya huyu kijana kuliko uongo.
 
Nimejaribu kupitia mawazo ya wachangiaji wengi katika thread hii nakuona kuwa wengi wa wachangiaji wanauelewa mkubwa wa athari ya wizi unaotendeka katika sehemu za kazi. Kuna baadhi ya wachangiaji wanaliangalia tatizo hili kisiasa zaidi na kuacha kujadili ukweli na athari zake katika jamii yetu ya kitanzania.
Tatizo la wizi katika maeneo ya kazi liko accross the board, ni tatizo linalowakabiliwatanzania wengi kiasi cha kuweza kuathiri maendeleo ya taifa. Leo hii tunasikia jinsi wageni wanavyolalamika juu ya kukithiri kwa vitendo vya wizi kwenye maofisi. Halikadhalika sisi wenyewe tunashuhudia jinsi wazalendo wenye uwezo kwenye nafasi za kazi wakizikosa na nafasi hizo kupewa wageni. Kimsingi wawekezaji ama mashirika ya kimataifa yanapokujakufanya kazi ndani ya nchi yetu hukusanya taarifa zote muhimu juu ya namna gani wataendesha shughuli zao hapa. Pamoja na mambo mengine hawa jamaa wanataarifa kamili juu ya tabia zetu mbaya za wizi, kwahiyo basi mikakati ya nafasi za nyingine kushikwa na wageni hufanywa na hukohuko nje na wanapofika hapa huwa ni utekelezaji tu.
Tusijidanganye kwa kutaka kumtazama Kapuya kama waziri aliyetoa tamko hilo bali tuliangalie tatizo kama tatizo la kitaifa.
Ninajaribu kuorodhesha maeneo mbalimbali ambayo yanakithiri kwa wizi na wengine waorodheshe yale maeneo wanayoyajua na kujaribu kujadili hili tatizo kwa upana zaidi.

1. Wizi wa mitihani - Wizi wa mitihani ni sugu.
2. Wafanyakazi wanaoprint magazeti - Kama usiposimamia uchapishaji wa magazeti yako, nakala zitakazosambazwa asubuhi yake ni za wizi zote.
3. Wafanyakazi wa viwanja vya ndege - Mizigo mingi ya abiria hufunguliwa na kuibiwa kama si kupotea kabisa.
4. Petrol Station's Pump attendant. - Huibia wateja mafuta kama hutakuwa makini kuangalia meter inavyosoma.
5. Mafundi wa magari - Utabadilishiwa vipuli vya gari yako kama hutasimamia mwanzo wagari linapotengenezwa na hadi mwisho.
6. Wauzaji wa simu za mikononi za kanyaboya.
7. Mkabidhi ndugu yako wa damu biashara then kinachofutata ni kuanguka kwa biashara hiyo
8. Uuzaji wa kiwanja kimoja kwa watu zaidi ya mmoja.
9. Upotevu wa mali za wateja katika mahoteli yetu
10. Wizi ulioithiri katika wizara na idara za serikali pamoja na mashirika ya umma.
11. Wizi wa vifaa vya ujenzi unaofanywa na wafanyakazi wa makandarasi wa ujenzi mbalimbali.
12. Wizi wa mafuta (Dizeli na petroli) kwa magari ya serikali.
13. Ubadilishaji wa vipuri kutoka magari ya serikali na kuvifunga katika magari binafsi.

Nimejaribu kuanisha baadhi ya mambo ambayo makampuni na mashirika ya kigeni wanataarifa nayo na wanajaribu kuyaepuka wakati wakiwa wanafanya shughuli zao hapa kwetu.
Ipo haja ya kupambana na jambo hili na wala hatuna sababu ya kumtazama Kapuya na kukwepa kuwajibika, hili si tatizo la kisiasa ni tatizo la kijamii kabisa.
 
Back
Top Bottom