Udini watumika kuizamisha CHADEMA mikoa ya kusini

chadema kama wanakanusha hawatumikiikanisa. WAHOJI MATUMIZI YA MOU yanayotolewa na serekali kwa kanisa.
Walioidhinisha hiyo MoU ni CDM au ccm? Kwa Kweli kama ni ccm au cuf ndio wanafanya huo ujinga wa kuwatumia hao wachumia tumbo wanaojiita viongozi wa dini, narudia tena kama ni ccm au cuf hawafai hata kuitwa vyama vya siasa. Hawafai hata kuongoza nyumba kumi. Hivi waislamu hawaoni dini yao inadhalilishwa na watu kama hawa wanaoeneza upuuzi huu? Nadhani ni wakati wanaopenda uislamu kukataa hawa wachumia tumbo wanaotumiwa na wanasiasa.
Jakaya Mrisho Kikwete unapeleka nchi yetu wapi na hizi siasa za kugawa watu kidini unazozipalilia?
 
Nape Nnauye na Julius Mtatiro naomba mkanushe kama hao wajinga hawaenezi chuki za kidini kama njia ya kuokoa vyama vyenu ccm na cuf kisiasa. Nape kama Kweli ccm haihusiki kemeeni upumbavu huu na kama unavoagiza mawaziri, iagize serikali kuchukua hatua. Mnawaziba mdomo.Uamsho huku mkiachia wanaofanya kazi kama ya uamsho kutamba kwa vile wanawasaidia kuzima nguvu ya CDM. Huu ni usaliti wa nchi kwa maslahi ya kisiasa.
 
Nipo Mkoani Mtwara kikazi kwa wiki karibu mbili sasa.
Njia ya kuelekea Masasi mbele kidogo na ile round about yanapopaki magari ya zimamoto mbele kidogo ya njia panda ya airport kuna mhadhara unafanyika wiki ya pili sasa.

Mashekhe hao ambao wamepita katika kila eneo ambalo chadema wamepita na kufanya mihadhara wanapita na wao kueneza chuki na ghiliba za kidini kuwa asili ya chadema ni ukristo na malengo yake ni kustawisha ukristo

Wanakwenda mbali zaidi kwa kusema Adui wa muislam ni mkristo hivyo hakuna haja ya kukishabikia chadema.
Ingawa hawasemi chama gani kiko neutral wala hawasemi wafuasi wao wanatakiwa wafuate chama gani lakini wanawahamasisha wahakikishe kuwa kuna haki na usawa

Kampeni hii ambayo inafanyika katika mwavuli wa mikutano ya dini ambapo huanza kwanza kwa kuikosoa biblia kwa kutumia quran mwishowe humalizikia kwa kuiponda chadema kidini.

Nimefanikiwa kuhudhuria mkutano mmoja na nimesikiliza mwanzo hadi mwisho, kwa kweli wanafanikiwa kupata wafuasi na waamini wengi. Akili za vijana wengi ambao hapo awali tulidhani zimekombolewa kwa ujio wa cdm zimerud kule kule kwenye enzi za ujima na udini
MUNGU INUSURU TANZANIA NA DHORUBA INAYOWEZA KUTOKEA ANY TIME

Dont wor mkuu hawa wanashda na njaa zao wanataka sadaka2 na mawazo mgando yasiyo na tja unauulaani ukristo huku ukifuatilia vzr pengne watoto, dada, shangazi, kaolewa na mkristo sasa cjui mkweo anaweza kuwa adui wako sababu ya dini vivyo hivyo hakuna sababu ya mkristo kumbagua muislaam kwan cku hz dini sio mpaka wala sababu ya kuwatenga watu kimsingi tumuombe mungu awafungue akili hawa wenzetu wenye mawazo mgando yasiyo na tija udini ni upuuz mtupu i hate sana huu ujinga
 
CHADEMA wawapeleke Makamu Mwenyeti Taifa, Mhe. Said Arfi, Mbunge wa Mpanda Kati, Naibu Katibu Mkuu, Mhe. Zitto Zubeir Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini,labda pamoja na Mhe. Mhonga Saidi Mbunge wa Viti Maalum wakathibitishe uzushi wa hawa watu.

mzee umemsahau profesa Safari
 
Back
Top Bottom