Udini wainyemelea CCM?

Ni vema ungetoa Orodha ya Viongozi wote badala ya kutumia mfano wa wachache hawa kisha kutoa tuhuma za Udini ndani ya CCM......Hivi watu kama Pius Msekwa,John Chiligati,Amos Makalla,Bernard Membe(Wajumbe wa Skretariat ambayo ndo safu ya uongozi wa juu wa CCM ni waislamu??),au watu kama Martin Shigella,Beno Malissa(UVCCM) n.k ni Waislamu???????.........
Mimi nimeuliza isitoshe hiyo orodha ni ya wale walioteuliwa jana na NEC CCM si orodha ya zamani ya kina Msekwa na wenzake labda kama una orodha nyingine ya walioteuliwa hivi karibuni na NEC CCM tunaiomba
 
THE National Executive Committee of the Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) has proposed Ms Amina Nassoro Makilagi for the vacant post of General Secretary of the party’s Women wing (UWT).

The statement signed by the Party’s Publicity Secretary Mr John Chiligati said Ms Makilagi has been proposed to the wing’s Executive Committee to replace Ms Husna Mwilima, who was recently appointed District Commissioner for Tandahimba District, Mtwara Region.

In another development, the Party also shortlisted Mr Harun Mkalimoto, Mr Juma Rajab Simba and Mr Salim Mwaking’ida for the post of Dar es Salaam Regional CCM Publicity Secretary.

It also approved Ms Mwajuma Athman Labia, Mr Alhaji Salim Simba and Colonel (rtd) Tajil Mwinchumu for the post of Shinyanga Urban District Party Chairman.

Luteni, look yourself in the mirror..hapa wewe ndio Mdini
 
Keep on crying you poor (walalamishi, wanafiki, wapenda dezo) christians
 
Udini ninavyoelewa mie ni kutumia kigezo cha dini kupendelea kundi moja na kukandamiza kundi jingine la dini tofauti. Yaani dini inatumika kama sifa ya kumpatia mtu maslahi ama manufaa fulanifulani, na hapohapo dini pia inatumika kumnyanyasa mwingine.

Lakini huu udini wanaolalamikia watu hapa JF kuhusu CCM na serikali ya sasa au zote zilizopita si wa kweli. Sijawahi kuona jitihada zozote zinazosimamiwa na serikali ama chama chochote hapa Tz za kuhakikisha watu wa dini fulani ndio wanaopata manufaa na eti wa dini nyingine wanakandamizwa. Nasikia tu makelele ya 'ooh serikali ina watumishi au viongozi wengi wa dini xyz!', lakini hatusikii kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata dini zao badala ya sheria ya nchi, au wanapendelea watu wa dini zao tu katika huduma.

Hivi ukienda hospitali ukakuta madaktari wote ni waislamu huo ni udini? Jibu lingekuwa 'ndiyo' iwapo wangekataa kumtibu mtu wa dini nyingine kwa kuwa tu si wa dini yao. Lakini kama katika kutelekeza majukumu yao hawana ubaguzi, basi hakuna udini hapo, imetokea kwamba walioomba kazi hapo ni waislamu na ndio waliopata. Au kuna mtu angetegemea watu wapewe tu kazi bila kuiomba?

Kwa kifupi, makelele karibu yote ya udini tunayosikia humu hayana mantiki.
 
Mlaria Sugu, udini ni ubaguzi unaojielekeza kwenye dini fulani na wala sio wingi wa watu wa dini fulani. Ubaguzi huu, ndio hushabikiwa kama kigezo cha mwelekeo wa mtu au taasisi husika, mathalan, asilimia 98 ya wakaazi wa Zanzibar ni Waislamu, hivyo wanachama wa chama chochote cha siasa Zanzibar ni lazima watakuwa Waislamu, lakini bado chama hiki hakiwezi kuitwa cha kidini, kwasababu Uislamu sio kigezo cha uanachama, lakini chama hicho hicho kama CUF, kwa upande wa Bara, Wakristu ni Asilimia 60% na Waislamu asilimia 40%, lakini wanachama wa CUF bara nao bado ni Asilimia 98%, then, chama hicho kinaweza kubebeshwa shutuma za udini, hata kama hakuna kigezo chochote cha kidini kujiunga na chama husikasa.

Sambamba na Chadema, nguvu kubwa ya chama hiki, imejikita kanda ya Kaskazini ambalo ni eneo la Wakristo wengi, na Kigoma ambao ni Waislamu wengi. Zitto ambaye ni Mwislamu alipotaka kugombea uenyekiti na Mbowe, alipigwa zengwe na hatimaye kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho. Habari za chini chini zikavuma kuwa Zitto amepigwa zengwe kwa sababu Muslamu kamwe hawezi kuongoza Chadema, hizi ni shutuma za udini, hata kama sio za kweli lakini huo ndio mwelekeo.

CCM imetokana na TANU na ASP, vyote ni vyama vilivyokuwa na waislamu wengi. Baada ya uhuru, Nyerere ambaye ni Mkristo aliwapa uongozi watu wengi walikuwa na elimu nzuri, bahati mbaya ikatokea wengi ni Wakristu, shutuma za Udini pia zilimwangukia.

Mzee Mwinyi alipoachia ruksa kwenye kila eneo, ikatokea Waislamu wengi ndio wenye ndugu Arabuni waliomwagika kwa wingi na kununua karibu majumba yote Kariakoo viwanja sehemu za heri, hivyo nae akabebeshwa tuhuma za udini kuwapendelea Waislamu.

Alipoingia JK kwa kuanzia CCM, alimpiga chini Mangula (Mkristu) kumpa ulaji Makamba (Mwislamu). Kwenye teuzi mbalimbali akawapachika Waislamu akiwemo IGP, Saidi Mwema, Mkurugenzi wa TISS, Rashid Othman, Ramadhani Khalfani (BET). etc. etc. Wale waliokuwa wakizimezea mate posti hizo, ndio wa kwanza kupiga kelele za kichinichini 'udini', 'udini', lakini Wakristu wote walio kwenye posti zote za ulaji miakla yote hawaonekani.

Uchaguzi wa rais, nao unanyemelewa na turufu ya udini, kama vyama vyote vya upinzani wataamua kumsimamisha Dr. Slaa, kuna wana CCM, watampigia kura kwa sababu ya Ukristo wake tuu, wakijisemea kimoyo moyo, huyu ndie mcha Mungu. Na Waislamu vya vyama vyenye mrengo huo, watampigia JK hata kama wao ni CUF, wakijisemea, bora kumpa Mwislamu mwenzao kuliko Kafir.

Matokeo yeyete atakaibuka mshindi, ni kicheko kwa kundi moja na kilio kwa kundi jingine na ndipo mbegu ya chuki za kidini itakapokuwa imepandwa na kuanza kumea, matokeo yake siku zote, huishia kwenye umwagaji wa damu.
 
Asante ndugu kwa mawazo yako yaliyojaa busara.

Binafsi, dini ya mtu hainisumbui... kuwa mkristo au muislam ni chaguo la mtu binafsi au kazaliwa kajikuta ana dini hiyo.Na haiwezekani watu wanaoteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali wasiwe na dini. Labda ni Kingunge tu aliyeamua kutokuwa na dini na hiyo ni exception katika jamii ya watanzania yenye dini mbili kubwa ukiacha animists ambao ni wachache.

Nini cha kufanya?

Endapo uta observe kuwa dini fulani imebahatika kuwa na wateuliwa wengi kuliko nyingine, wewe mezea tu. Fuatilia utendaji wa wahusika. Kama una kasoro kwa maana ya kushindwa kutekeleza majukumu au kuacha kufanya kazi aliyopewa na badala yake kuwa busy kueneza dini yake ama kupitia maamuzi au vitendo vingine, wewe kusanya data tu kisha anika uovu huo bayana hata hapa JF.

Hii itasaidia kujenga case imara ya kulalamikia udini kuliko kupiga kelele zisizo na mwelekeo wala basis.
 
Mlaria Sugu, udini ni ubaguzi unaojielekeza kwenye dini fulani na wala sio wingi wa watu wa dini fulani. Ubaguzi huu, ndio hushabikiwa kama kigezo cha mwelekeo wa mtu au taasisi husika, mathalan, asilimia 98 ya wakaazi wa Zanzibar ni Waislamu, hivyo wanachama wa chama chochote cha siasa Zanzibar ni lazima watakuwa Waislamu, lakini bado chama hiki hakiwezi kuitwa cha kidini, kwasababu Uislamu sio kigezo cha uanachama, lakini chama hicho hicho kama CUF, kwa upande wa Bara, Wakristu ni Asilimia 60% na Waislamu asilimia 40%, lakini wanachama wa CUF bara nao bado ni Asilimia 98%, then, chama hicho kinaweza kubebeshwa shutuma za udini, hata kama hakuna kigezo chochote cha kidini kujiunga na chama husikasa.

Sambamba na Chadema, nguvu kubwa ya chama hiki, imejikita kanda ya Kaskazini ambalo ni eneo la Wakristo wengi, na Kigoma ambao ni Waislamu wengi. Zitto ambaye ni Mwislamu alipotaka kugombea uenyekiti na Mbowe, alipigwa zengwe na hatimaye kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho. Habari za chini chini zikavuma kuwa Zitto amepigwa zengwe kwa sababu Muslamu kamwe hawezi kuongoza Chadema, hizi ni shutuma za udini, hata kama sio za kweli lakini huo ndio mwelekeo.

CCM imetokana na TANU na ASP, vyote ni vyama vilivyokuwa na waislamu wengi. Baada ya uhuru, Nyerere ambaye ni Mkristo aliwapa uongozi watu wengi walikuwa na elimu nzuri, bahati mbaya ikatokea wengi ni Wakristu, shutuma za Udini pia zilimwangukia.

Mzee Mwinyi alipoachia ruksa kwenye kila eneo, ikatokea Waislamu wengi ndio wenye ndugu Arabuni waliomwagika kwa wingi na kununua karibu majumba yote Kariakoo viwanja sehemu za heri, hivyo nae akabebeshwa tuhuma za udini kuwapendelea Waislamu.

Alipoingia JK kwa kuanzia CCM, alimpiga chini Mangula (Mkristu) kumpa ulaji Makamba (Mwislamu). Kwenye teuzi mbalimbali akawapachika Waislamu akiwemo IGP, Saidi Mwema, Mkurugenzi wa TISS, Rashid Othman, Ramadhani Khalfani (BET). etc. etc. Wale waliokuwa wakizimezea mate posti hizo, ndio wa kwanza kupiga kelele za kichinichini 'udini', 'udini', lakini Wakristu wote walio kwenye posti zote za ulaji miakla yote hawaonekani.

Uchaguzi wa rais, nao unanyemelewa na turufu ya udini, kama vyama vyote vya upinzani wataamua kumsimamisha Dr. Slaa, kuna wana CCM, watampigia kura kwa sababu ya Ukristo wake tuu, wakijisemea kimoyo moyo, huyu ndie mcha Mungu. Na Waislamu vya vyama vyenye mrengo huo, watampigia JK hata kama wao ni CUF, wakijisemea, bora kumpa Mwislamu mwenzao kuliko Kafir.

Matokeo yeyete atakaibuka mshindi, ni kicheko kwa kundi moja na kilio kwa kundi jingine na ndipo mbegu ya chuki za kidini itakapokuwa imepandwa na kuanza kumea, matokeo yake siku zote, huishia kwenye umwagaji wa damu.

Heshima mbele Mkulu.
Haya maelezo yako yameeleweka kabisa kwangu,hali hii uliyo ieleza hapa ndio haswa inayo endelea kwenye vichwa vya Watanzania wengi,si lazima uwe na elimu sana kupata kutambua hili.
Sasa,,,,!tunafanyaje ili tusiwe na dhana kama hizi vichwani mwetu?????
 
Keep on crying you poor (walalamishi, wanafiki, wapenda dezo) christians
Tumain
Whatever names you call them but the message is open and clear, kuna baadhi ya wengi humu wamekuja na sababu za historia ya TANU kuwa ilianzishwa na waislam ndiyo maana hali imefikia hapa sasa tuendelee kuilea hali hiyo kwa vile ni ya kihistoria zaidi au tuipuuze
 
Hii ni obvious small minds ziko hivyo wao hawaoni beyond mabega yao, na ndio maana pamoja na yote kuondoka kwa Lowassa kumewafurahisha kwa kuwa mbele yake wasingeweza kufanya huo upumbavu wao.

Tatizo ni unafiki wa wa kina Chiligati hawawezi kukemea kwa kuwa wanajiona hawakustahili hizo position walizonazo, na kwa vile chama kimajaa wanafika hakuna atakae thubutu kuhoji hilo angalia UVCCM wamejaa wakina nani?

Tutake tusitake lazima tutamwaga damu kikwete anatupeleka huko expeditiously na sisi tunamuangalia tu hatutaki kumtoa.

Mimi naomba Mungu usiku na mchana Lowassa arudi maana ndio kupona kwetu jamani wameshashika kasi hawa watu hawarudi nyuma, hawana haya wala aibu, angalia walivyogeuza mashirika yetu, ndio maana yanazidi kufa, huwezi kuongoza nchi hii na dini moja JK utake usitake huwezi kuligeuza hilo.

ACHA KUTUHARIBIA NCHI YETU WEWE UMEPEWA NAFASI USIYOSTAHILI SHUKURU MUNGU PITA TUACHE SALAMA MUOGOPE MUNGU UNAYOYAFANYA YATAMWAGA DAMU ZETU WATOTO WETU WATAGEUKA MAYATIMA TUMZUIENI JAMANI CHONDE CHONDE

Apo pekundu pananichefua,lakini sipendi sana kuongelea udin au ukabila ni adui wa amani sana,unajua tukianza ivyo atari yake kubwa sana.
 
i nadhani badala ya kubishana nani mkristo,nani muislamu,nani Mu hindu n.k katika chama au serikali tujiulize tu je hao wanaoshika nafasi za uongozi wana sifa za kiuongozi na wana nia njema na watanzania wote???

Yah, Makamba ni mchapa kazi mzuri tu!!!!!!!!!
 
Lisemwalo lipo.Ni kawaida siku hizi,mtu akiraise issue ya Uislam,anaambiwa mdini.Au mtu akisema kuwa Wahindi ni mafisadi anaitwa mbaguzi wa rangi.

Suala la Udini ,angalia kama mkoa wa Shinyanga,CCM.Tunajua kuwa Mkoa huu,majority sio waislamu,wengi wao ni waarabu ambao ni wachache sana.
Mwenyekiti CCM-Khamis Ngeleja
Katibu CCM-Mohamed Mbonde
katibu CCM Shy vijijini- Mr Mussa Omella

Kuna agenda ya CCM mkoani Shinyanga kuundermine watu hasa wa upinzani.CCM imeweza kubrainwash wananchi wengi mkoani humo,kama tujuavyo wengi ni very very poor na uneducated.CCM inafanya kila njia kuua upinzani ,kwa kuwatumia hawa mamluki.

Nimeona picha ya Ngeleja hapo ikulu akikabidhi Tshs 1.4 millioni kwa ajili ya kuchukulia fomu Rais.What a mockery!
Ukitembea vijijini Shinyanga utaona poverty ya kujutia.Hizo pesa wangekusanya na kununua madawati .
 
Ila kwa kina Amina kunatisha kinyamaaaaa!!!!!!!!!!!!
Be careful ooooooooooooooooooooo
 
lakini kwa upande mwingine, kwa kuwa DINI ni mpango wa mwadamu

kumwelekea mungu! na si mpango wa Mungu kwa wanadamu

ukristo ni hatua ya mtu kutawaliwa na kuongozwa na roho wa Mungu,

wala ukristo si majina ati pengine mtu kuitwa Yohana, Petro n.k

kwa mtazamo wangu unaweza ukute tangu kundwa kwa taifa la Tanzania

halijawahi kuongozwa na Mkristo hata siku moja, ila na waislamu, hasa

kwa sababu waislamu wanatambulika kwa majina, kuvaa kanzu, kuota sigida n.k

kwa namna moja ama nyingine hao ndiyo wanaoitwa watu wa DINI, yaani

watu wanaojiongoza kwa akili zao 100%

hivyo kwa mtazamo wangu mimi unapozungumzia udini ni kuzungumzia uislam,

na si ukristo, kwa unaweza ukaitwa Edward Lowasa na ukawa muislam, ukaitwa

Benard Membe na ukawa muislam tu,
 
Mkuu ni kama nimekuelewa na kwa lugha uliyotumia ni wachache watakuelewa!
 
Udini ni ubaguzi, upendeleo kufuatana na imani ya mtu na si uwezo au sifa nyingine ya mtu huyo.

Mdini ni mtu mwenye ubaguzi kwa misingi ya dini (na kwa kawaida anapendelea watu wa dini yake). Ni mbaguzi wa watu wasio wa dini yake. Hata kama wana uwezo na sifa ya kufanya kazi au kushika ofisi fulani lakini wataachwa na mkuu kwa sababu si watu wa dini (imani) yake.

Kwa hiyo udini ni nadharia iliyowekwa kwenye vitendo kwa makusudi na mtu mdini. Kama mtu huyo hakufany ahivyo kwa makusudi (yaani hakufanya ubaguzi kwa uchaguzi) kufuata dini basi huwezi kumuita ni mdini hata kama wale aliwachagua ni watu wa dini yake. Hapa kigezo atakachokuwa ametumia si dini bali uwezo wa mtu.

Kwa jinsi hii kusema mtu ni mdini lazima kuangalia mambo mengi mpaka kufikia hitimisho hilo.
 
lakini kwa upande mwingine, kwa kuwa DINI ni mpango wa mwadamu
kumwelekea mungu! na si mpango wa Mungu kwa wanadamu
ukristo ni hatua ya mtu kutawaliwa na kuongozwa na roho wa Mungu,

wala ukristo si majina ati pengine mtu kuitwa Yohana, Petro n.k

kwa mtazamo wangu unaweza ukute tangu kundwa kwa taifa la Tanzania

halijawahi kuongozwa na Mkristo hata siku moja, ila na waislamu, hasa

kwa sababu waislamu wanatambulika kwa majina, kuvaa kanzu, kuota sigida n.k

kwa namna moja ama nyingine hao ndiyo wanaoitwa watu wa DINI, yaani

watu wanaojiongoza kwa akili zao 100%

hivyo kwa mtazamo wangu mimi unapozungumzia udini ni kuzungumzia uislam,

na si ukristo, kwa unaweza ukaitwa Edward Lowasa na ukawa muislam, ukaitwa

Benard Membe na ukawa muislam tu,

Naona UDINI umekujaa mpaka unakumwagika!
 
Lisemwalo lipo.Ni kawaida siku hizi,mtu akiraise issue ya Uislam,anaambiwa mdini.Au mtu akisema kuwa Wahindi ni mafisadi anaitwa mbaguzi wa rangi.

Suala la Udini ,angalia kama mkoa wa Shinyanga,CCM.Tunajua kuwa Mkoa huu,majority sio waislamu,wengi wao ni waarabu ambao ni wachache sana.
Mwenyekiti CCM-Khamis Ngeleja
Katibu CCM-Mohamed Mbonde
katibu CCM Shy vijijini- Mr Mussa Omella

Kuna agenda ya CCM mkoani Shinyanga kuundermine watu hasa wa upinzani.CCM imeweza kubrainwash wananchi wengi mkoani humo,kama tujuavyo wengi ni very very poor na uneducated.CCM inafanya kila njia kuua upinzani ,kwa kuwatumia hawa mamluki.

Nimeona picha ya Ngeleja hapo ikulu akikabidhi Tshs 1.4 millioni kwa ajili ya kuchukulia fomu Rais.What a mockery!
Ukitembea vijijini Shinyanga utaona poverty ya kujutia.Hizo pesa wangekusanya na kununua madawati .
Kufanya uteuzi kwa upendeleo wa kigezo chochote kile iwe dini ukabila nk nafikiri lengo si kuua upinzani tu bali watakuwa wanaua vipaji vya watu wenye uwezo walio na imani tofauti au wanaotoka sehemu tofauti
 
Kuteua mtu wa dini fulani kushika madaraka si udini, maana rais habanwi na masharti ya dini katika uteuzi. Huyu aliyeleta hii hoja ni mwenye fikra finyu na potofu kabisa.
Ni bora leo uniite nina fikra potofu kwa kukemea kitendo hichi mapema kuliko kusubiri kesho uniite mjinga wakati tutakapoanza kuuana kama Somalia
 
Back
Top Bottom