Udini wa kutisha UDOM!

Status
Not open for further replies.
sijui lakini nawafahamu lecturers na assistant lecturers wengi waliohama na kukimbilia vyuo vingine kama kule Mazengo (nimesahau jina ya chuo) na taasisi ya maendeleo (IRDS). Sijui shida ni nini kwani si kawaida mtu kukimbia chuo kikubwa kama UDOM na kwenda kwenye Institute ya Rural Development Studies.

Nami nadhani kuna kitu kikubwa tu pale UDOM ila sijui ni nini na sina hakika kama ni udini.

Tatizo linaloendana na hili liliwahikuwepo pale Chuo Cha Ardhi miaka ya 90 ambapokilikuwa kinajulikana kama chuo cha wachaga. Wakaja kusambaratishwa miaka ya 2000 baada ya Prof. Idris Kikula kuwa Principal. Baada ya hapo chuo kinaenda murua kabisa.

Sasa nitashindwa kumwelewa Prof. Kikula kama ataacha mambo ya kibaguzi hapo UDOM. By the way Prof. Kikula ni VC mzuri na ni jamaa mwenye busara sana. Kinachotakiwa mwenye malalamiko ayafikishe, yatashughulikiwa tu. Sidhani kama uongozi umeshindwa, maybe haujang'amua tatizo.
 
Mtoa mada usikae pembeni ukaacha watu wakatoana ngeu bure! Lete data za uhakika ili tuchangie otherwise watu wameshaanza kutoka nje ya mada ambayo inaonekana haina ushahidi wa kumshawishi mtu aamini unayokusudia aamini!
Kwenye suala la mishahara hawezi kurudi maana hana uwezo wa kuleta huo ushahidi. Kwenye academic huna cha kubargain mshahara ni vyeti na mshahara wako unaujua.
 
sijui lakini nawafahamu lecturers na assistant lecturers wengi waliohama na kukimbilia vyuo vingine kama kule Mazengo (nimesahau jina ya chuo) na taasisi ya maendeleo (IRDS). Sijui shida ni nini kwani si kawaida mtu kukimbia chuo kikubwa kama UDOM na kwenda kwenye Institute ya Rural Development Studies.

Nami nadhani kuna kitu kikubwa tu pale UDOM ila sijui ni nini na sina hakika kama ni udini.

Tatizo linaloendana na hili liliwahikuwepo pale Chuo Cha Ardhi miaka ya 90 ambapokilikuwa kinajulikana kama chuo cha wachaga. Wakaja kusambaratishwa miaka ya 2000 baada ya Prof. Idris Kikula kuwa Principal. Baada ya hapo chuo kinaenda murua kabisa.

Sasa nitashindwa kumwelewa Prof. Kikula kama ataacha mambo ya kibaguzi hapo UDOM. By the way Prof. Kikula ni VC mzuri na ni jamaa mwenye busara sana. Kinachotakiwa mwenye malalamiko ayafikishe, yatashughulikiwa tu. Sidhani kama uongozi umeshindwa, maybe haujang'amua tatizo.
Yah umeongea ukweli lakini labda ni kufahamishe kuwa kuhama chuo kikuu kwenda vyuo vidogo si suala la ajabu wengi wanafanya hivyo. Mf chuo kama UDSM kimeshafikia climax na kama wewe ni assistant lecturer huonekani kabisaaaaa. Sasa kuna vyuo vingine ni vidogo ila vina opportunities nyingi za kujiendeleza na maslahi. Kwanini mtu asikimbie vyuo vikubwa. Watu huwa tunarudi kwenye vyuo vikubwa baada ya kuwa upo well equiped na unaweza kuonekana otherwise huwezi kubaki sehem kisa jina la chuo.
 
From UDOM website:
Chancellor :BW Mkapa
Chairman of University Council : Mohammed Ghalib Bilal
Vice Chancellor : Prof. Idris Kikula
Deputy VC Planning,Finance
Administration : Prof Shaaban Mlacha

Tutajaza!!!!!!

Hapa udini unauona kwa wazi kabisa.
 
From UDOM website:
Chancellor :BW Mkapa
Chairman of University Council : Mohammed Ghalib Bilal
Vice Chancellor : Prof. Idris Kikula
Deputy VC Planning,Finance
Administration : Prof Shaaban Mlacha

Tutajaza!!!!!!
acha kuwa bias na jenga hoja kimakini, mbona prof kinabo hujamuweka..deputy academics...acha kuwa mjinga kiakili na mnapo toa mada kama hzi mjue kuna watu wenye elim zao tunaosoma hizi..by the way me ni christian sioni tatizo la udini hapa UDOM
 
Hii taarifa siyo sahihi, nacho amini mimi mishahara ktk vyuo vikuu vya umma inapangwa na hazina/utumishi. TA anaanza na PUTS12 assistant lecturer PUTS15 lecturer PUTS17 n.k. japo sina details zaidi sijui hapo udini unakujaje.

Kama huyo mtumishi siyo mwalimu basi sijui lakini nao wana scale zao za mishahara kulingana na ngazi yake ktk ajira.

Magezi ni kweli unavyosema lakini hizi scales pia zinaendana na experience. Sasa hapo ndo utakuta top management wanazichezea na kuwapa watu wao scales wasizostahili. Kuna kipindi mchezo kama huu ulivuma sana pale UDSM. Pale ulikuwa ni ukabila kuanzia ajira mpaka scale ya mshahara. Watawala wanazichezea sana hizi salary scales wala watu wa utumishi huwa hawafuatilii.
 
acha kuwa bias na jenga hoja kimakini, mbona prof kinabo hujamuweka..deputy academics...acha kuwa mjinga kiakili na mnapo toa mada kama hzi mjue kuna watu wenye elim zao tunaosoma hizi..by the way me ni christian sioni tatizo la udini hapa UDOM

Acha uongo wewe mwislamu kabisa. Maneno yako yanadhihirisha hili wala huwezi kujificha.
 
acha ujinga wewe tukiweka list ya Mzumbe kwa mfano utasemaje mbona wpte ni wakristo UDSM je tusemaje

Muhimbili je watu watasemaje acheni PUMBA kuweni na hoja nzito

Sasa mbona ulidai wewe christian? Si umedhihirisha wazi kuwa wewe mwislamu. Haya bana endelea na mitusi yako.
 
Sasa mbona ulidai wewe christian? Si umedhihirisha wazi kuwa wewe mwislamu. Haya bana endelea na mitusi yako.
MNAPO TOA HOJA TOENI KWA VIGEZO, UMAKINI NA UKWELI na si kuropoka tuuuu, watanzania tukianza mambo ya udini na ukabila hatutafika mbali...nadhani ni misingi ambayo kila mtanzania ndani na nje ya nchi tunajivunia kuwa nchi yetu haina dini wala ukabila lakini watu kama hawa wanaotoa mada hasa mtoa mada hii kwenye thread hii anasikitisha na anatia aibu sana..hana data na anaropoka mpaka eti kusema mishahara inapendelewa wakati mtu wa higher learning ni cheti ndo kinakupa mshahara wako uano julikana....tuwe wabunif na tusiwe wajinga bwana..aaargghhhhhh......disgusted na mtoa hoja KWAKWELI sijategemea..any way tunatofautiana sana KIELIM tanzania..ndo taaaaabuuu kwelikweli....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom