Hukumuzuku
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 6,666
- 4,999
TATIZO SI UISLAMU BALI UARABU WA GHUBA. Anayebisha hongera zake.
UTAMADUNI WA WAARABU WA GHUBA. Hakuna mwislamu anayeonewa wala
anayenyimwa shule.
Pamoja na kwamba Mwandishi M. Matinyi amefanya kazi nzuri kwenye uchambuzi wake hapo juu, lakini amekosea kabisa kwenye premise yake kuu kwamba tatizo ni "WAARABU WA GHUBA". Ameshindwa kuelezea tofauti ya msingi kati ya nchi kama "Moroko, Algeria, Tunisia, Misri na zile za Uturuki, Siria, Iraki na Yodani" ambazo hazina rasilimali ya mafuta, na kwa upande wa pili nchi zile anazoziita "nchi za ghuba" kama "Saudia Arabia, Yemeni, Kuwaiti, Omani, Katari, Imarata na Bahraini" ambazo zina utajiri mkubwa wa mafuta.
Ama baada ya kusema hayo, kwa ujumla utakuta kwamba nchi za Kiarabu za Ghuba zilizojaliwa mafuta, Wananchi wake wengi wameneemeka kiasi kwamba hawana haja kabisa ya kusoma (kwa maana ya elimu ya Kimagharibi au ya kisasa) ili waweze kuishi maisha ya raha na starehe bila kufanya kazi yoyote kwa sababu tu nchi hizi zina uwezo wa kuwalipa professionals kutoka nchi zenye Wasomi wengi (haswa zile za Kiislamu na za Kiarabu) wawafanyie kazi zote hata zile za kufikiri.
Lakini cha msingi ni kwamba utajiri wa mafuta wa nchi hizi uligundulika mwanzoni mwa karne iliyopita, ambayo ni zaidi ya karne mia moja tokea historia ya Waarabu wa Ghuba nchi za Afrika Masharaki na Kati ilipoanzia. Kwa hiyo kwa kweli mtazamo na uchambuzi wa Mwandishi kwamba Waislamu wa Tanzania hawajali elimu eti kutokana na influence ya "WAARABU WA GHUBA" una walakini kwa kukosa uchambuzi yakinifu wa sababu gani zinafanya "WAARABU WA GHUBA" kama tunavyowafahamu leo hii kukosa au kutokujali elimu ya kisasa, ilhali Mwandishi amekiri kwamba "WAARABU WA GHUBA" wa karne mia moja iliyopita walikuwa wakiongoza kwenye nyanja ya elimu ya kusoma na kuandika.