Udini: Uchambuzi wa Mobhare Matinyi

Status
Not open for further replies.

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Naomba nichangie hapa kama Mtanzania - na si kama mwislamu au mkristo au mpagani.

1. Kwanza ni kweli kwamba kitabu cha yule padri mzungu kinaleta shida sana mawazoni mwa watu, Dkt. Sivalon. Lakini turejee kwenye ukweli wa kisomi, kwamba huwezi kuhitimisha jambo zito kwa kutumia chanzo kimoja. Hatuna maandiko mengine ya watu wasiokuwa na upande yanayothibitisha aliyosema bwana huyu. Hakuna utafiti wowote. Aidha, ni muhimu pia kuchunguza kujua alisema hivyo katika mazingira gani. Kuna Mkenya mmoja London aliwahi kuzuliwa na wenzake kwamba ni shoga na akatengwa kabisa. Aliyemzulia siku moja akamwambia Mkenya mwingine ninayemfahamu, kwamba anajua fika kuwa bwana yule si shoga lakini alifanya vile kumlipizia kisasi cha ugomvi wao. Uongo ulibadilishwa kuwa ukweli. Je, tuna hakika na maneno ya huyu mwandishi padri? Najua ukivutia upande mmoja itabidi useme uhakika upo kwa sababu kuna uthibitisho mwingine, lakini hali halisi inagoma. Nitaeleza.


2. Pili, ingawa Mwalimu Julius Nyerere analaumiwa sana na waislamu au watetezi wa waislamu, lakini kiukweli kama si yeye, hali ya kielimu ya waislamu nchini ingekuwa mbaya sana. Tusisahau kuwa, tulipopata uhuru serikali ya Mwingereza hakituachia shule za kutosha. Wakristo na dini za Waasia wakiwemo Wabohora Waismailia na Wahindu walikuwa na shule lakini Waislamu hawakuwa na shule. Sasa ukumbuke pia kuwa, wakoloni wa Ulaya walikuja Afrika Mashariki kwenye karne ya 19 wakati wakoloni wa Uarabuni walikuwa tangu karne ya 13. Kwa miaka Waarabu 600 hawakujenga shule hata moja; bali walijenga madrasa kwa ajili ya masomo ya dini. Shule za kwanza zilijengwa Tanganyika na Mjerumani zikiwa ni za darasa la kwanza hadi nne kwa kutumia Kiswahili. Zanzibar zilijengwa sana sana na Mwingereza.

Tafuta maana na historia ya maneno haya:
i)Darasa/Madarasa
ii) Shule
iii) Skuli.

Kimsingi, Nyerere ndiye aliyezitaifisha shule za wasiokuwa waislamu ili na watoto wa waislamu waende kusoma kwa sababu walikuwa wanakwepa kubadilishwa dini na kulishwa nguruwe ingawa wakristo wengine kama wasabato hawali nguruwe.

3. Nchi yetu ikapiga hatua zaidi na tukaanza kujenga shule za msingi. Nyerere akajenga shule kwa juhudi kubwa zaidi kwenye mikoa iliyokuwa nyuma, ambayo mingi ilikuwa ni ya pwani waliko waislamu wengi zaidi. Haikutosha, baada ya Nyerere kuibana mikoa mingine, ambayo wananchi wake waliamua kujijengea wenyewe, akaweka nafasi maalum kwa watu wa makabila ambayo hayakuwa na watoto wengi shuleni, yaani hayakuwa yanataka shule. Waliofaidika zaidi ni makabila ya pwani ambako shule ilikuwa kama kituo cha polisi kwao. Dini yao wengi wao tunaijua. Mwalimu akiwa anaongoza TANU na CCM akajenga shule za jumuiya ya wazazi kwenye mikoa ya pwani na hata alipopata msaada kutoka Kuba (Cuba), aliiachagua mikoa ya Pwani pia kujengewa shule, na ndipo tukapata shule kama Kibiti, Ruvu, n.k. Hata ile ya Waswidi ilijengwa Kibaha. Alifanya hivi kuwasaidia hao mnaowaita waislamu (mimi nawaita Watanzania). Kule kwingine kama Kilimanjaro, wakaamua kujenga shule za
binafsi zao wenyewe na ndio maana hadi leo wanazo nyingi. Serikali ya Nyerere haikujenga shule za sekondari kule bali ilijenga kwenye mikoa yenye waislamu wengi. ndio ukweli huo ila watu hawataki kuutafuta. Rekodi zipo, tafuta shule zote uone.

4. Serikali ya Tanzania haikuishia hapo. Wakati wa Rais Mwinyi waislamu wakiongozwa na Waziri Kighoma Malima walilalamika sana. Zikafanyika juhudi nyingi ikiwemo kumweka Malima kwenye sehemu kama elimu ambapo alianzisha awamu mbili za kwenda shule, lengo likiwa kuongeza idadi ya watoto wa kiislamu wanaoingia sekondari ingawa na wakristo pia waliongezeka. Pia Tanzania ikapata nafasi za masomo kwenye mataifa ya Misri, Algeria, Iran, na Uturuki, maalum kwa ajili ya waislamu tu. Marafiki zangu walikwenda huko na walinithibitishia kwamba hii ilikuwa maalum kwa waislamu tu. Bado Waislamu waliendelea kwenda nchi zingine zisizokuwa za kiislamu bila tatizo. Huu ulikuwa msaada mkubwa.

5. Ikaja serikali ya Ben Mkapa na yenyewe ikaweka rekodi ya kuipa dini moja majengo ya chuo kikuu. Leo hii kipo chuo kikuu cha waislamu Morogoro kwa kutumia majengo ya serikali. Serikali ya JK imejenga shule nyingi sana za sekondari nchi nzima na sijasikia ubaguzi kwa upande wa mikoa yenye waislamu wengi. JK pia amehakikisha waislamu wanaongoza wizara ya elimu ili kuondoa malalamiko, na si kweli kwamba eti asiyekuwa mwislamu akiwa waziri wa elimu, basi waislamu wanashindwa kusoma. Hakuna ukweli hapa.

6. Najua kuna malalamiko mengi kuhusu shule na hata hospitali za misheni, lakini tuzitendee haki. Hizi ni za kuhudumia Watanzania wote, na ndiko Kikwete na binti yake waliposoma, hata Mzee Makamba. Tuweni wakweli kwenye hili. Waislamu wanatibiwa kote huku, na ruzuku ndiyo mkombozi wa Mtanzania mnyonge.


WAISLAMU KWENYE VYEO NA ELIMU

7. Labda, tuje kwenye hili moja: KWA NINI HATUNA WAISLAMU WENGI KATIKA NAFASI ZA JUU SERIKALINI? Hili jambo ni la kweli lakini inabidi tujiulize swali jingine zaidi: KWA NINI KUNA MADAI KWAMBA WAISLAMU HAWAJASOMA?

8. Nianze na historia yetu. Waarabu walipokuja kwenye karne ya 13 walileta vitu kadhaa vikuu vikiwa ni dini nzuri ya Kiislamu na pili utamaduni wao wa kishenzi. Ndiyo walileta utamaduni wa kishenzi. Utamaduni wa Kiarabu siyo dini ya Kiislamu na dini ya Kiislamu siyo utamaduni wa Kiarabu. Uislamu ndio ulioongoza elimu duniani kwenye karne ya saba na nane na hata vyuo vikuu vya kwanza duniani vilikuwa vya Waislamu, lakini si Waislamu wote hupenda elimu, kama ilivyo kwa dini zote zingine pia. Ukienda kwenye nchi za Maghrebu na baadhi ya Mashariki ya Kati, yaani Moroko, Algeria, Tunisia, Misri na zile za Uturuki, Siria, Iraki na Yodani, kuna waislamu wengi wenye elimu. Hapa Marekani wanaheshimika, mathalani, wahandisi mahiri hutoka Uturuki, Pakistan na India kwenye majimbo yenye waislamu.

9. Hali ni tofauti kabisa kule Ghuba kwenye nchi za Saudia Arabia, Yemeni, Kuwaiti, Omani, Katari, Imarata na Bahraini. Ghuba watu hawataki shule. Hawa wa Ghuba ndio walioletea ushenzi wao huu Afrika Mashariki kuanzia kule Somalia hadi Msumbiji kaskazini - kote huku kuna watu wenye utamaduni wa Ghuba wa kukataa shule. Hili liko wazi. Kwa kuwa Waarabu wa Ghuba ndio walioleta pia Uislamu, basi watu hujumuisha kwa pamoja tatizo la kukosa elimu kwa sababu za kuiga utamaduni wa Ghuba na dini nzuri ya kiislamu ambayo inajali elimu sana. Saudia watu ni vilaza watupu kiasi kwamba kuna Wamisri milioni moja na zaidi wanaofanya kazi za kisomi. Kote huko Ghuba kasoro Yemeni na Omani (kwa sababu ya umaskini wao) kuna wageni wengi ndani ya nchi kuliko wenyeji kwa sababu watu hawataki shule.

10. Waislamu wa pwani ya Tanzania, kama wenzao wote wa Somalia yote, Lamu, Malindi, Mombasa, Zanzibar, Mafia, Kilwa, Lindi na Pemba ya Msumbiji, wana utamaduni wa Waarabu wa Ghuba wa kugomea shule. Tofauti na wenzao, waislamu wa Tanzania walioko Machame na Usangi mkoani Kilimanjaro, au Bukoba, na hata wale wa kabila la Waganda (Baganda), wao wanapenda shule. Maeneo yote waliyokaa Waarabu, kuanzia Bagamoyo nenda hadi Tabora/Nzega, na Ujiji, shule si mali kitu. TATIZO SI UISLAMU BALI UARABU WA GHUBA. Anayebisha hongera zake.

11. Tafiti mbili ninazozijua, nitazisaka baadaye, zinasema kwamba kwenye miaka ya nyuma kama ya 1990, pale UDSM waislamu walikuwa ni kati ya 14 - 15% ya wanafunzi wa shahada ya kwanza wote. Hiki ni kiasi kidogo mno lakini ni kidogo cha kiasi gani? Lazima tujue hili nalo, hata kwa makadirio tu.

12. Nyerere aliamua tuachane na sensa ya kupekua dini za watu kwa sababu nzuri kabisa - alitaka Watanzania tusitambuane kwa dini zetu (na makabila pia). Hivyo, ili kuweka usawa tukaanzisha msemo huu: Tanzania sisi nusu ni Waislamu na nusu ni Wakristo. Huu ni msemo tu na hauna usahihi. Pili, hata kama sensa ya zamani ilionesha kwamba waislamu ama wakristo au wapagani ndio wengi, haina maana yoyote leo wakati taifa letu lina watu milioni 45 hivi. Tulipata uhuru tukiwa milioni 12 na baadaye Zanzibar ikaongeza laki tatu. Watanzania hatukuwa na kelele za asilimia ngapi ni dini hii na ile. Leo zimerudi.

13. Kwa mujibu wa taarifa za kitafiti (siyo mimi), Waislamu nchini Tanzania ni theluthi moja ya watu wote. Naomba Nasser na Salim muende mkamuulize rais wetu, Jakaya Kikwete, kwamba kwa nini alipoteua mawaziri mwaka Novemba 2010 aliweka theluthi moja waislamu, na kisha manaibu akafanya hivyo hivyo? Pia, muulizeni, kwa nini alipoteua mawaziri hii juzi, aliweka 1/3 waislamu na kwenye manaibu akafanya hivyo hivyo? Kabla hamjaenda, chukueni rekodi zenu kwanza muone. Rais Kikwete, nijuavyo mimi, anajaribu sana kuliangalia hili suala la kelele za dini ili asiharibu nchi yetu. Anakuwa mwangalifu sana, hata kama kuna wakati anateleza. Je, mahesabu yake haya yana maana gani? Nina hakika anajua anachokifanya na kamwe hawezi kuwaonea waislamu wenzake ambao ni Watanzania kama yeye. Hawezi kufanya uonevu.

14. Zifuatazo ni taarifa zinaonesha idadi ya waumini wa kiislamu nchini Tanzania:
(i) 35% = Muslim Population in World Population Ranking.
(ii) 29 - 35% = List of countries by Muslim population - Wikipedia, the free encyclopedia or The Future of the Global Muslim Population (Pew Research Center), The Future of the Global Muslim Population - Pew Forum on Religion & Public Life.
(iii) 35% = Tanzania

15. Hiyo taasisi ya kwanza ni ya kiislamu. Sijaweka za Wakristo kwa sababu sitafuti ushindani na siamini kama idadi ina maana yoyote, lakini kwa kuwa watu mnataka kupigia kelele, basi mzigo huo hapo. Mwaka jana mwanaharakati mmoja wa Tanga alikuja Marekani na akasema mkutanoni kwenye chuo kikuu kimoja kwamba waislamu ni 70% ya Watanzania wote, na pia kuna mwislamu mmoja mwenyeji wa Songea aliandika makala ya kitaaluma na akasema kwamba waislamu Tanzania ni 55% lakini akashindwa kueleza wanaishi wapi. Huyu wa 70% alishindwa pia kusema wanakaa wapi ambako hawaonekani. Pointi ni kwamba madai haya ni ya kijinga. Makala nyingine iliyoandikwa na msomi huyu Mtanzania ilisema kwamba Uganda wapo 45% na Kenya 33% na Msumbiji 40% (kama sijakosea). Hakuna popote duniani, hata kwenye mashirika ya kimataifa ya kiislamu zinapotajwa namba hizi za 55% kwa Tanzania na hao wengine wa Afrika Mashariki. Mashirika ya kiislamu yanasema kwamba Tanzania ina 30 - 35% tu. Ili kuleta amani, naomba tuseme kwamba Tanzania haina Wakristo kabisa, hata mmoja hayupo isipokuwa wale wenye madaraka serikalini. Tukumbuke pia, marais wetu wote watano wa sasa (kule Zenji na kwenye Muungano) ni waislamu.

16. Kwa nini idadi inakuwa muhimu hapa, achilia mbali kelele? Ni kwa sababu tunataka kuielewa ile 14-15% ya UDSM ambayo huenda hivi leo imeshabadilika kwa kuwa tuna vyuo vingi nchini. Tunahitaji maelezo, kwamba hao waislamu wengine wameishia wapi? Jibu lake linarudi kwenye ule UTAMADUNI WA WAARABU WA GHUBA. Hakuna mwislamu anayeonewa wala anayenyimwa shule. Mimi nimekulia na kusomea Dar es Salaam kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita, na JKT kabisa. Waislamu wote marafiki zangu waliokuwa wakali darasani waliendelea na elimu ya juu. Shule ya msingi tulikuwa watoto wanne machachari, mimi, Waziri, Salum na Izihaki, na wote tulifaulu. Vijana wa mwaka mmoja nyuma yetu pale Azania walikuwa na Mpemba aliyepata pointi SABA. Alikwenda tena Tambaza akawa nyuma yetu na akapata pointi TATU. Akaenda Ulaya. Hakunyimwa nafasi yoyote. Hao wanaonyimwa wako wapi?

17. Kwa hiyo, kama 1/3 tu ndio waislamu, na pia wengi wao wako pwani kwenye utamaduni wa Ghuba usiotaka shule, tunashangaa nini wakienda wachache vyuo vikuu, tuseme 20%? Je, watakuwaje sawa serikalini na Wakristo ambao walianza utamaduni wa elimu tangu enzi hizo?

OMBI

Tufanye juhudi kuwakomboa wale wote walio nyuma kielimu Tanzania. Wako wengi, kwa dini na makabila, lakini wote ni Watanzania. Walio nyuma wasiseme kuna uonevu, bali waondoe kilichowakwamisha. Hatuwezi kulinganisha utamaduni wa elimu wa watu wa Kilwa, Mafia, Rufiji na Pangani, na watu wa Moshi, Kyela, au mkoani Kagera. Tuwe wakweli. Mwenyezi Mungu hapendi waongo. Kwa nini shule za binafsi hazina pia waislamu wengi? Nani anawazuia waislamu kujenga shule Tanzania? Je,
kama kweli unataka mtoto wako apate elimu safi, na amekosa nafasi ya shule ya serikali, utampeleka wapi? Pale Kinondoni Muslim? Tuseme ukweli.

Naamini tunao uwezo wa kuyatatua matatizo yetu ya kihistoria na kitamaduni na si kukaa chini kupanga vurugu kwa madai ya kuonewa. Waislamu wa Saudi Arabia hawajasoma licha ya utajiri wao. Je, hao nao waziri wao wa elimu na baraza la mitihani ni ya Tanzania? Mbona waislamu wa Uturuki, Tunisia, Misri, Senegal na Afrika Magharibi yote wana elimu?

Tutafute chanzo cha kweli cha tatizo, halafu wote tushirikiane kulitatua; wote kabisa.


Matinyi.
 
ooooooh information is power ni kusoma kila kitu kisha unachambua pumba na mchele
 
usimuamshe aliyelala,we waache waendelee kuvua,kulima,makonda, kuuza masokoni,kucheza bao,kupiga ramli,kucheza ngoma,roho za kisasi na roho mbaya.watajua baadae kama maharage ni mboga au/
 
Mapogolo
mkuu umetuchambulia mambo makubwa, inapendeza kuwa na watu wenye uelewa kama wewe.

Sipendi ushabiki lakin kuhusu wanaomsema na kumsakama mwalimu kwa mantinki ya kumchafua umewapa darasa tosha. Kibaya zaidi hawajengi hoja yoyote zaid ya kutubwagia data na reference za kipuuzi au video za kichovu na uchochezi.

Sasa wasubilie wale vijana wapinzan feki na hoja za kichochezi watoa reference na video feki ambazo wao wenyewe pia hawajazisoma wala kuzisikiliza walau hata kuzitafakali.
 
Ahsante sana kwa uchambuzi wa aina yake. Wenye kununa wanune tu lakini ukweli ndo ushausema.
 
Huu uchambuzi utakuwa ni thesis ya PhD si bure. Jamaa anatembelea utamaduni na historia ya uislamu na uarabu kama alivyokuwa akifanya Pfof. Haroub Othman (RIP) kuhusu historia ya ukoloni na mapambano ya uhuru kwa nchi za Afrika!
 
usimuamshe aliyelala,we waache waendelee kuvua,kulima,makonda, kuuza masokoni,kucheza bao,kupiga ramli,kucheza ngoma,roho za kisasi na roho mbaya.watajua baadae kama maharage ni mboga au/


safiiiiiiiiiiiiiiii
 
Umewambia ukweli lakini kumbuka wanavichwa vigumu sana.
 
Huu uchambuzi utakuwa ni thesis ya PhD si bure. Jamaa anatembelea utamaduni na historia ya uislamu na uarabu kama alivyokuwa akifanya Pfof. Haroub Othman (RIP) kuhusu historia ya ukoloni na mapambano ya uhuru kwa nchi za Afrika!

wala huhitaji hata form 2 kujua ukweli huu.mimi nawajua wanafunzi wangu watatu wa kiislam waliomaliza form six mwaka huu ambao walikuwa bright tangu primary nilipowafundisha wote wamepata one ya single digit masomo ya sayansi tena shule za serikali.makosa yanafanyika pale necta mengi tu, mimi nilikuwa na rafiki yangu wa kiislam mtihani wa taifa alipata B Kwenye somo ambalo hakulisoma wala kulifanyia mtihani. mimi nachokiona ni kwamba baadhi ya waislam waliotiwa nguvu na jk wakati wa uchaguzi , baadhi ya vyombo vya habari vya kiislam na baadhi viongozi wa kiislam wanapanda mbegu mbaya ya si tu waislam kuwachukia na kuwabagua wakristo lakini zaidi wakristo kuanza kuwabagua waislam, kuwachukia na kuwadharau.dalili kubwa ya kwamba wakiristo wameanza nao kupotoka kutokana na chuki hizi za kijinga zinazopikwa na baadhi ya waislam bila shaka wenye nia mbaya ni GENERALIZATION ya udhaifu wa waislam kutokana na makosa au udhaifu wa muislam mmoja au wachache.
maoni yangu: tuliombee taifa letu liepukane na laana ya kubaguana na unafiki,aidha pia tuwakeemee wale
wanaoendeleza vitendo hivi bila aibu wala kujali ni wenzetu katika dini.
 
Ndugu zangu

Naomba niseme kwa kifupi tuu, hapa nilipo nipo nchi za watu, toka niingie kazini sijasikia bwana asifiwe wala asalaam aleikhum, ni hi hi basi. Watu wanachapa mzigo professionally kujenga mifuko yao na nchi yao.

Jamani hebu for once tuache masihara, tujenge nchi, hizi dini ni muhimu ila zikianza kuwa kikwazo tufikirie mara mbili. Hapa nimekunywa juisi imetoka kenya, imesafiri mbali kufika hapa, kwa nini isitoke Tanzania ? hivi tunahitaji hizi dini kuprocess juisi ? Au kuna aya au mstari katika biblia au Quran unaotufundisha jinsi ya kumchoma mtu sindano ?

Mimi ninao ndugu zangu waumini wazuri tuu wa dini ya kiislam, ila kwa upeo wao mdogo wanawaozesha mabinti zao wakiwa 16 or 17 years badala ya kuwapeleka shule,na hao mabinti wanalazimishwa, sio ridhaa yao, sasa hapa utamlaumu nani ? Jamani sometimes tuache masihara, tuwe wakweli, tusiburuzwe na vipofu, tujielimishe, tujenge nchi yetu.Opportunity zipo nyiingi tuu.

Respect !
 
Ndugu zangu

Naomba niseme kwa kifupi tuu, hapa nilipo nipo nchi za watu, toka niingie kazini sijasikia bwana asifiwe wala asalaam aleikhum, ni hi hi basi. Watu wanachapa mzigo professionally kujenga mifuko yao na nchi yao.

Jamani hebu for once tuache masihara, tujenge nchi, hizi dini ni muhimu ila zikianza kuwa kikwazo tufikirie mara mbili. Hapa nimekunywa juisi imetoka kenya, imesafiri mbali kufika hapa, kwa nini isitoke Tanzania ? hivi tunahitaji hizi dini kuprocess juisi ? Au kuna aya au mstari katika biblia au Quran unaotufundisha jinsi ya kumchoma mtu sindano ?

Mimi ninao ndugu zangu waumini wazuri tuu wa dini ya kiislam, ila kwa upeo wao mdogo wanawaozesha mabinti zao wakiwa 16 or 17 years badala ya kuwapeleka shule,na hao mabinti wanalazimishwa, sio ridhaa yao, sasa hapa utamlaumu nani ? Jamani sometimes tuache masihara, tuwe wakweli, tusiburuzwe na vipofu, tujielimishe, tujenge nchi yetu.Opportunity zipo nyiingi tuu.

Respect !

Mkuu ulichoongea ni cha kweli kabisa!! nina karibu mwaka na nusu kwa watu pia, tena ulaya....sioni mihadhara kama ya kama ya kina mwakasege au shehe ponda.. sioni watu kujishughulisha na makanisa wala misikiti!! wao ni mzigo tu... wakati mwingine wanachapa mzigo mpaka jumapili.... lakini ajabu sisi tulioletewa dini na hawa waasisi wetu ndo tunaona pepo ipo karibu zaidi... tumefikia wakati tunatishiana amani na kutaka kunyukana sisi kwa sisi... Hivi uarabuni au vatican wananyukana nao? tuache mambo ya ajabu.. tufanye kazi na tuachane na uvivu... muda wa kuweka mihadhara na matamasha tungeutumia kuzalisha tungekuwa mbali
 
Kwanini popote wanapozungumziwa waislam au muislam akifanya jambo flani mnaita udini..? Udini ni nini? Kuwa muislam ni udini? Kuwa mkristo si udini? Kichwa cha thread yako kwa nini umeita udini? Kama nia yako kuwachambua waislam huku pata heading iliyokaa sawa mpka ukaita udini? Huyu mubhare ni Nani ? Ni dini gani?
Naomba ujibu hayo maswali kabla hatujaingia kwenye contents..
 
Kimsingi, Nyerere ndiye aliyezitaifisha shule za wasiokuwa waislamu ili na watoto wa waislamu waende kusoma kwa sababu walikuwa wanakwepa kubadilishwa dini na kulishwa nguruwe ingawa wakristo wengine kama wasabato hawali nguruwe.

3. Nchi yetu ikapiga hatua zaidi na tukaanza kujenga shule za msingi. Nyerere akajenga shule kwa juhudi kubwa zaidi kwenye mikoa iliyokuwa nyuma, ambayo mingi ilikuwa ni ya pwani waliko waislamu wengi zaidi. Haikutosha, baada ya Nyerere kuibana mikoa mingine, ambayo wananchi wake waliamua kujijengea wenyewe, akaweka nafasi maalum kwa watu wa makabila ambayo hayakuwa na watoto wengi shuleni, yaani hayakuwa yanataka shule. Waliofaidika zaidi ni makabila ya pwani ambako shule
ilikuwa kama kituo cha polisi kwao. Dini yao wengi wao tunaijua. Mwalimu akiwa anaongoza TANU na CCM akajenga shule za jumuiya ya wazazi kwenye mikoa ya pwani na hata alipopata msaada kutoka Kuba (Cuba), aliiachagua mikoa ya Pwani pia kujengewa shule, na ndipo tukapata shule kama Kibiti, Ruvu, n.k. Hata ile ya Waswidi ilijengwa Kibaha. Alifanya hivi kuwasaidia hao mnaowaita waislamu (mimi nawaita Watanzania). Kule kwingine kama Kilimanjaro, wakaamua kujenga shule za
binafsi zao wenyewe na ndio maana hadi leo wanazo nyingi. Serikali ya Nyerere haikujenga shule za sekondari kule bali ilijenga kwenye mikoa yenye waislamu wengi. ndio ukweli huo ila watu hawataki kuutafuta. Rekodi zipo, tafuta shule zote uone.

4. Serikali ya Tanzania haikuishia hapo. Wakati wa Rais Mwinyi waislamu wakiongozwa na Waziri Kighoma Malima walilalamika sana. Zikafanyika juhudi nyingi ikiwemo kumweka Malima kwenye sehemu kama elimu ambapo alianzisha awamu mbili za kwenda shule, lengo likiwa kuongeza idadi ya watoto wa kiislamu wanaoingia sekondari ingawa na wakristo pia waliongezeka. Pia Tanzania ikapata nafasi za masomo kwenye mataifa ya Misri, Algeria, Iran, na Uturuki, maalum kwa ajili ya waislamu tu. Marafiki zangu walikwenda huko na walinithibitishia kwamba hii ilikuwa maalum kwa waislamu tu. Bado Waislamu waliendelea
kwenda nchi zingine zisizokuwa za kiislamu bila tatizo. Huu ulikuwa msaada mkubwa.

8. Nianze na historia yetu. Waarabu walipokuja kwenye karne ya 13 walileta vitu kadhaa vikuu vikiwa ni dini nzuri ya Kiislamu na pili utamaduni wao wa kishenzi. Ndiyo walileta utamaduni wa kishenzi. Utamaduni wa Kiarabu siyo dini ya Kiislamu na dini ya Kiislamu siyo utamaduni wa Kiarabu. Uislamu ndio ulioongoza elimu duniani kwenye karne ya saba na nane na hata vyuo vikuu vya kwanza duniani vilikuwa vya Waislamu, lakini si Waislamu wote hupenda elimu, kama ilivyo kwa dini zote zingine pia. Kote huko Ghuba kasoro Yemeni na Omani (kwa sababu ya umaskini wao) kuna wageni wengi ndani ya nchi kuliko wenyeji kwa sababu watu hawataki shule.

10. Waislamu wa pwani ya Tanzania, kama wenzao wote wa Somalia yote, Lamu, Malindi, Mombasa, Zanzibar, Mafia, Kilwa, Lindi na Pemba ya Msumbiji, wana utamaduni wa Waarabu wa Ghuba wa kugomea shule. Tofauti na wenzao, waislamu wa Tanzania walioko Machame na Usangi mkoani Kilimanjaro, au Bukoba, na hata wale wa kabila la Waganda (Baganda), wao wanapenda shule. Maeneo yote waliyokaa Waarabu, kuanzia Bagamoyo nenda hadi Tabora/Nzega, na Ujiji, shule si mali kitu. TATIZO SI UISLAMU BALI UARABU WA GHUBA. Anayebisha hongera zake.

11. Tafiti mbili ninazozijua, nitazisaka baadaye, zinasema kwamba kwenye miaka ya nyuma kama ya 1990, pale UDSM waislamu walikuwa ni kati ya 14 - 15% ya wanafunzi wa shahada ya kwanza wote. Hiki ni kiasi kidogo mno lakini ni kidogo cha kiasi gani? Lazima tujue hili nalo, hata kwa makadirio tu.
Mkuu, niruhusu ninukuu sehemu ya maelezo yako ili nami nichangie mawili matatu. Unaweza usiwe sahihi katika maoni yako lakini kwa sehemu kubwa mambo uliyoeleza yana ukweli wake.

Hata hivyo ningependa kutoa ulinganisho wa elimu kati ya eneo moja na lingine zaidi kuliko kutumia dini. Kama ulivyoeleza Waislam wa Kagera, Usangi na Machame mathalani wamekwenda shule zaidi ya wenzao wa maeneo mengine. Ningependa pia uangalie ukweli huo kwa upande wa dini ya Kikristo, unawasemaje Wakristo walioko mikoa ya pwani? Kwa mfano unaweza kulinganisha uwingi wa Wakristo wa Lushoto katika kusaka elimu na Waislam wa Bukoba? Ukristo ulianza zamani sana maeneo ya Muheza na Korogwe, je kuna uhusiano gani na Wakristo wa maeneo hayo kupata au kuipenda elimu? Mimi ninafamu kuwa wilaya ya Kilosa ni moja ya maeneo ambayo elimu ilianza zamani sana sambambsa na dini ya Kikristo lakini mpaka leo elimu ni duni hujapata kusikia hata miongoni mwa Wakristo. Kuna wasomi kiduchu kwelikweli kutoka maeneo yale.

Kwa hiyo mimi ninakubaliana zaidi na suala la utamaduni wa kishenzi (au kwa usahihi zaidi niuite utumwaduni) wa eneo kuwa na athari zaidi kuliko dini maana kama ni dini na utamaduni sidhani kama walioeneza Uislam Uthangi na wale wa Pangani walikuwa tofauti. Mikoa ya pwani ina utumwaduni wake ambao unakinzana sana na dhana ya kwenda shule uwe mkristo, muislam au mpagani. Nikitolea mfano wilaya (yangu) ya Kilosa, kule sifa ni kuoa na kuolewa (haijalishi kama ni wa dini gani). Sifa kwa mwanaume ni matumizi ya uume wake. Atasifiwa sana mwanaume kwa kumpa ujauzito msichana. Shule ipo tena hapo? Starehe ni sehemu inayovutia sana kwa watu wa maeneo haya, hivyo ngoma, muziki na vinavyofanan na hayo ni muhimu kabisa kuliko elimu. Wachache sana wanao utashi wa kujinyima hayo ili kuitafuta elimu. Mazingira mengine ni ya ushirikina ambapo wale waliosoma hawawezi kurudi ya kuishi miongoni mwa watu wao ili kwa kuona ubora wa maisha unaopatikana kwa kusoma wawatie shime wadogo zao kusoma. Naamini kuwa mazingira ya Kagera, Uthangi na Machame hayana matatizo ya ushirikina kwa kiwango kilichopo Kilosa. Kwa upande wa Kilosa pia kuna tatizo la matumizi makubwa sana ya pombe (ingawa najua mbege ipo kule Moshi). Utumwaduni huu umechangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya watu wa eneo lile kutokwenda shule na kuwa masikini wa kutupwa. Wanaweza kulalamika kuwa wanaonewa lakini ukweli unabaki palepale kuwa wako chini ya utumwaduni.

Pengine nitoe hapa uzoefu wa kaka yangu ambaye alisoma na wanafunzi kutoka mkoa wa Tanga katika shule moja huko Moshi (hii ilitaifishwa kutoka chama cha ushirika - KNCU secondary school). Wakati ule wa mgao wa nafasi za kufaulu kwenda kidato cha kwanza wanafunzi wa Tanga wapatao 30 walichaguliwa (sio kwamba walifaulu).

Kaka yangu alishangaa kukuta baadhi yao hawajui hata kuandika vizuri na uwezo wao wa kufuatilia masomo kwa Kingereza ulikuwa mdogo sana. Utumwaduni wa uvivu na utoro (kwenda mitaani/migombani) kunywa pombe, kupenda starehe (hasa vimwana), dharau juu ya elimu, kutamba na kujisifu ulikuwa wazi katika kundi hili. Walihudhuria masomo walipotaka na kujisomea ilikuwa ni fedheha (unaulizwa kama unasomea kijiji na kubatizwa majina mengi ya kashfa). Matokeo yake wengi walifeli (waislamu kwa Wakristo) mitihani ya kidato cha nne. Miongoni mwao 30 ni wawili tu walienda kidato cha tano na mmoja ndiye alivuka hapo na kwenda chuo kikuu. Waliotoka Kilimanjaro walifanya vizuri zaidi (nao Wakristo kwa Waislam). Wote walikuwa kwenye mazingira yale yale na wenzao kutoka mikoa mingine lakini wale wa Tanga waliathiriwa na utumwaduni. Wao ni "Tangaline", hawana shida (hata kama kwao wanatoka vibanda vya nyasi) wana nazi, watakuwa wavuvi, wao si "Wanyika" na mengine mengi.

Uislam wao wala Ukristo wao haukuwa msaada dhidi ya athari za utumwaduni wa kwao. Kwa hiyo unapoangalia athari za dini (ni kweli zipo) pia utazame zile zinazoletwa na mila na desturi za mahali.
 
Kwanini popote wanapozungumziwa waislam au muislam akifanya jambo flani mnaita udini..? Udini ni nini? Kuwa muislam ni udini? Kuwa mkristo si udini? Kichwa cha thread yako kwa nini umeita udini? Kama nia yako kuwachambua waislam huku pata heading iliyokaa sawa mpka ukaita udini? Huyu mubhare ni Nani ? Ni dini gani?
Naomba ujibu hayo maswali kabla hatujaingia kwenye contents..


Kuna mtaalam mmoja humu JF alipokuwa anaeleza kuhusu mtafaruku wa Zanzibar alisema kuwa uislam ndiyo dini na ukristo ni kama imani tu (ukiamini unaokoka basi ni mkristo) na hakuna aliyempinga JF wote. Kwa mantiki hiyo hakuwezi kuwa na udini bila kuwepo na dini. Hii ndiyo maana udini ukaambatanishwa na wenye dini. Lau kama wewe unataka kupingana naye mtaalam na kuthibitisha kwamba ukristo nao kama ulivyo uislam ni dini utakuwa na haki ya kuuambatanisha ukristo na udini.
 
Mimi hupenda sana kusoma mijadala na sipendi cheap intimidations

watu wanatakiwa waje washuke nondo wakikwama waombe break wakajikusanye then waendelee

nimependa sana Matinyi alivyokuja na figures zake sasa kilichobaki ajibiwe kwa facts lakini I dont think that's allowed here kwa sababu tuuu hao viranja waliowekwa humu nao ni WADINI

tuendelee kujadili ccm na chadema haya mambo ya kuleta facts na figures siyo mahala pake hapa
 
Songíto;4020207 said:
Mkuu ulichoongea ni cha kweli kabisa!! nina karibu mwaka na nusu kwa watu pia, tena ulaya....sioni mihadhara kama ya kama ya kina mwakasege au shehe ponda.. sioni watu kujishughulisha na makanisa wala misikiti!! wao ni mzigo tu... wakati mwingine wanachapa mzigo mpaka jumapili.... lakini ajabu sisi tulioletewa dini na hawa waasisi wetu ndo tunaona pepo ipo karibu zaidi... tumefikia wakati tunatishiana amani na kutaka kunyukana sisi kwa sisi... Hivi uarabuni au vatican wananyukana nao? tuache mambo ya ajabu.. tufanye kazi na tuachane na uvivu... muda wa kuweka mihadhara na matamasha tungeutumia kuzalisha tungekuwa mbali
mwarabu na mzungu walileta dini zao ili kutuogopesha na kutugawa ili wabebe resourse zetu vizuri na walifanikiwa sana hadi sasa hivi ina work out ..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom