Udhibiti wa fedha zetu

Malipo ya viza na vibali
 
Tatizo kubwa katika Idara ya Uhamiaji ni kutowasilisha
fedha serikalini kwa wakati.
• Karibu sh milioni 124 zilikusanywa lakini hazikupelekwa
benki.

• Ofi si ya Uhamiaji Zanzibar ilikusanya sh bilioni 2.8
lakini haikuzipeleka Makao Makuu Dar es Salaam.


Nani wanakula hii pesa? Je hatua zozote zinachukuliwa?
 
Makusanyo ya Kodi
Kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali, chini ya 50% ya kodi inayopaswa kukusanywa ndiyo hukusanywa. Pia, wakati mwingine kodi inayokusanywa
huwa haipelekwi serikalini:

• Sh bilioni 196 = Hii ni tofauti kati ya fedha ambazo TRA
iliripoti kuwa imezipeleka Hazina na fedha halisi
ilizozipeleka.

• Sh bilioni 81 = Hii ni tofauti kati ya fedha ambazo TRA
ilikusanya na zile zilizorekodiwa kwenye Akaunti Kuu ya
Taifa.

• Sh bilioni 27 = Kiasi cha fedha ambazo TRA ilikusanya
lakini hazikupelekwa hazina.
 
 
Upotevu wa fedha za umma Upotevu wa fedha za umma
uliongezeka hadi kufi kia 52% kwa mwaka uliopita!
Serikali ilipoteza kiasi cha sh bilioni 3.6 ukilinganisha
na shilingi bilioni 2.4 zilizopotea katika mwaka wa
fedha 2006/2007. Ripoti ya CAG inaeleza kwamba
"hali
hii haikubaliki".
  
Mishahara iliyolipwa kwa wale waliofariki
Kama ilivyo katika serikali kuu, serikali za mitaa pia
zimekuwa zikilipa mishahara kupitia benki moja kwa moja
kwa wafanyakazi ambao ama wamekufa, wamestaafu,
wamejiuzulu, wameacha kazi au wameachishwa kazi. Kiasi
cha
sh milioni 178 kililipwa kwa wafanyakazi hewa
mwaka jana, Halmashauri ya Jiji la Tanga ikiongoza
kwa malipo ya sh milioni 39.
  
"Kuna vioja vingi katika barabara zetu"

Katika ujenzi wa barabara "kuna vioja vingi" ambavyo vimetokea. Vioja hivi ni kama vile kukosekana kwa
vocha za malipo, mkandarasi kuukimbia mradi baada ya
kukamilishiwa malipo yake, au ukosefu wa kutopima
viwango vya ubora wa barabara. Karibu
sh bilioni
9 za fedha za mradi wa barabara zimepotea kwa njia
hii wakati sehemu kubwa
ya fedha hizo, sh bilioni 6,
hazikutumika.

Majabu ya serikali ya majambazi
 
Back
Top Bottom