Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

Majibu na kejeli zako zinaonyesha unakijua kilichomkuta huyo Shekh. Hakuna marefu yasiyo na ncha.

Unajua nilichokisema hakina ubishi na huna data kupinga nilichokiandika. So? Unakimbilia kuita kejeli!
 
Mzee Said,
Awali ya yote nieleze neno linalotumika katika medani ya vita. Neno hilo ni 'shoot any moving object'.
Kauli hii inatumika majeshi yanapokuwa katika wakati mgumu, ya kwamba mbinu zote zimeisha na hakuna mkakati. Nitafafanua wakati nahitimisha maelezo yangu.

......"

When there are no rules of engagement, anything is fair!
Nguruvi3,

Umesema maneno mazuri sana.

Ila ukiyatazama mambo kwa juu juu hutoweza kuona kile kilichojificha.

Nadhani kwa sasa tushafahamiana pakubwa kiasi cha kufanya mjadala mzuri wa kustarehesha.

Hali unayodhani ilivyo sivyo kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Karibu tena ... Kaka yetu .. mwalimu wetu.. Mohammed said.. darasa lako huru sikuzote linaeleweka pamoja na mashambulizi uyapatayo

Ahsante sana mdogo wangu,

Katika ukumbi huu tungelifanikiwa kuwa na adabu za mijadala yaani kushindanisha hoja kwa hoja bila kejeli, matusi nk. hapa lingelipatikana darsa zuri sana na miaka mingi baadae sisi hatupo wataokuja kutusoma wangesema, "Palipita watu JF hebu angalia usomi huu wa hali ya juu."
 
Mbona mashehe wengi tu wanapita hapo airport bila kusumbuliwa? Kwanini iwe ni wewe tu? Hili halihusiani na uislamu bana. Wewe bora utueleze ukweli.
 
Hivi kuonyeshwa inconsistencies zilizopo kwenye hadithi yako ni matusi na/au kejeli?

Kuonyesha inconsistencies ndiyo usomi wenyewe na unatoa changamoto kwa mwenzako arejee katika maandiko yake ajieleza upya.

Hebu soma tena ulichoandika.

Si umeona umeniuliza swali na mimi nimekupa jibu.

Sasa futa kejeli onyesha migongano katika nisemayo tuendelee na mjadala.
 
Mohamed Said,

..mimi nadhani haya mauza-uza yanayokupata yamesababishwa na sept 11.

..kama ugaidi ungeishia na mashambulizi ya dsm na nairobi tu, basi mpaka leo hii tusingekuwa na sheria ya ugaidi Tanzania.

..tangu sept 11 usafiri wa anga umekuwa wa usumbufu sana, na wapo wengi wanasumbuliwa wakati hata siyo Waislamu.

..pia how do u explain your situation, pamoja na ya mufti wa Yemen, wakati wakuu wa vyombo vya usalama vya Tanzania ni Waislamu??
 
Ahsante sana mdogo wangu,

Katika ukumbi huu tungelifanikiwa kuwa na adabu za mijadala yaani kushindanisha hoja kwa hoja bila kejeli, matusi nk. hapa lingelipatikana darsa zuri sana na miaka mingi baadae sisi hatupo wataokuja kutusoma wangesema, "Palipita watu JF hebu angalia usomi huu wa hali ya juu."

Hapa ni JF mkuu, sio kila kitu ni NDIO. Lazima ubishiwe na uombwe maelezo.
 
Mbona mashehe wengi tu wanapita hapo airport bila kusumbuliwa? Kwanini iwe ni wewe tu? Hili halihusiani na uislamu bana. Wewe bora utueleze ukweli.

Ukwerli gani Majebere, kuwa nauza unga na siku yangu ilikuwa imewadia?

Nimesafiri sana dunia hii nimgekuwa mtu a unga weshanikamata siku nyingi.
 
Ukwerli gani Majebere, kuwa nauza unga na siku yangu ilikuwa imewadia?

Nimesafiri sana dunia hii nimgekuwa mtu a unga weshanikamata siku nyingi.
Na katika hizo safari zako ulikuwa unaondokea airport gani? Kama ni Dar mbona hukusumbuliwa kwenye hizo safari?
 
Mohamed Said.

Karibu tena Jamvini tunaitaji darsa kutoka kwako na munakasha kutoka kwa Great Thinkers.
 
Last edited by a moderator:
Kuonyesha inconsistencies ndiyo usomi wenyewe na unatoa changamoto kwa mwenzako arejee katika maandiko yake ajieleza upya.

Hebu soma tena ulichoandika.

Si umeona umeniuliza swali na mimi nimekupa jibu.

Sasa futa kejeli onyesha migongano katika nisemayo tuendelee na mjadala.

Sasa mzee wangu, kejeli gani tena ninazotakiwa kuzifuta? Ningependa ujibu hoja za Nguruvi3 (ukitilia maanani kuwa wewe mwenyewe umekiri kuwa maneno yake ni mazuri)!
 
Mohamed Said,

..mimi nadhani haya mauza-uza yanayokupata yamesababishwa na sept 11.

..kama ugaidi ungeishia na mashambulizi ya dsm na nairobi tu, basi mpaka leo hii tusingekuwa na sheria ya ugaidi Tanzania.

..tangu sept 11 usafiri wa anga umekuwa wa usumbufu sana, na wapo wengi wanasumbuliwa wakati hata siyo Waislamu.

..pia how do u explain your situation, pamoja na ya mufti wa Yemen, wakati wakuu wa vyombo vya usalama vya Tanzania ni Waislamu??

Umesema kweli lakini juu ya hayo wapo watu wanabughudhiwa pasi na sababu.
Ziko prejudice nyingi na nina uzoefu mkubwa.

Nilipata kuzuiwa Heathrow mwaka 1991 kwa karibu saa mbili.
Kisa?

Pasi yangu ilikuwa imeingia na kutoka Mozambique, Swaziland, Sudan, Egypt, Kenya kwa vipindi vifupi vifupi. Walitaka niwaeleze kwa nini nasafiri sana.

Ilikuwa kazi sana kuwaeleza.
Zama hizi hazikuwa za ugaidi lakini huyu Mswahili mbona anasafiri hivi kuna nini hapa?
 
Umesema kweli lakini juu ya hayo wapo watu wanabughudhiwa pasi na sababu.
Ziko prejudice nyingi na nina uzoefu mkubwa.

Nilipata kuzuiwa Heathrow mwaka 1991 kwa karibu saa mbili.
Kisa?

Pasi yangu ilikuwa imeingia na kutoka Mozambique, Swaziland, Sudan, Egypt, Kenya kwa vipindi vifupi vifupi. Walitaka niwaeleze kwa nini nasafiri sana.

Ilikuwa kazi sana kuwaeleza.
Zama hizi hazikuwa za ugaidi lakini huyu Mswahili mbona anasafiri hivi kuna nini hapa?

Mohamed Said,

..Heathrow wana mtizamo hasi kuhusu wa-Tanzania.

..wao wanafikiri kila Mtanzania anayetua pale ana nia ya kuzamia.

..lakini pia kuna udhalilishaji mkubwa sana hasa ktk ofisi za ubalozi wa mataifa ya magharibi.

..mimi niliwahi kutibuana na walinzi, wa-Tanzania wenzangu, wa ubalozi wa EU, kutokana na tabia yao ya kunyanyasa wananchi wanaokwenda kuomba visa.

..kwa upande mwingine hali ya maisha nchini kwetu ndiyo inayosababisha vijana kutafuta kila njia kutoroka nchini na kuzamia nchi za watu. hilo nalo linasababisha hata wale wenye shughuli zao legitimate watumbukizwe ktk kapu moja la wazamiaji.


NB:

..lakini kukuchokoza tu, mimi naomba siku moja ulete hapa JF mjadala usiohusiana na dini au masuala ya historia.
 
Pole kwa yote yaliyokukuta,hata hivyo elewa watanzania ni wamoja na wanatawaliwa kwa kufuata katika na sheria.Ila uzingatie kuwa suala za vurugu za Mwembe chai na kuvunja mabucha ya nguruwe yasingekubalika katika serikali ya nchi yoyote. Inabidi uwe/muwe wavumilivu katika kuepusha dini na siasa katika misikiti. Wewe umesema ulikuwa ktk mkutano kuusiana na ugaidi Afrika mashariki hususani TZ,ila haujasema ni wa dini au siasa?.

Hata hivyo elewa kuwa watu wenye mamlaka ni waoga sana wakijua au kupata taarifa kuwa fulani anajihusisha na siasa nje ya nchi ktk vikao au mikutano mbalimbali,maana anahatarisha maslahi yao.Kwa walichokufanyia wako sawa kabisa hata wewe ungesikia kama ungekuwa kwenye mamlaka usingenyamaza,ila baada ya kujiridhisha umeachiwa.

Endelea kufanya kazi ya mungu wako utapata thawabu,maana ninavyojua mimi hakuna mtu aliyewahi kufanya vita na mungu akashinda labda unayemtumikia siyo MUNGU wa kweli.
 
Ndugu yangu M. Said unachofanya wewe ndicho ambacho sisi wengine tunakiona kwa Wamarekani weusi. Ndugu zetu hawa hujiona kwa mtazamo wa rangi sana kiasi kwamba lolote linalowakuta reaction yao ya kwanza ni "Because I'm Black". Akisimamishwa na askari mweupe jambo la kwanza wengi huhisi ni kwa sababu wao ni weusi. Matokeo yake ni kuwa akikataliwa kazi anahisi kwa sababu ni mweusi.

Msingi wa hisia hizi ni slavery legacy. Ndugu zetu walitambulishwa na kujitambua kwa rangi yao kiasi kwamba hata kama mtu kafanikiwa kiasi gani suala la rangi linajitokeza - rejea kisa cha Prof. Louis Gates Jr wa Harvard na Rais Obama katika kasheshe lililoishia kwenye "Beer Summit". Prof. Gates alijua kabisa kama raia anapohojiwa na polisi anatakiwa kuwapatia taarifa zote muhimu lakini yeye aliamua kuwa kichwa ngumu na akaona kuwa alikuwa anabanwa na maafisa wale (weupe) kwa sababu yeye ni mweusi - japo nyumba ilikuwa yake.

Hii mentality ni mentality ya kivictim.. Miezi kadhaa huko nyuma nilisafiri kwa ndege kutoka Houston kurudi Detroit. Pale Houston nilijikuta natolewa na kuwekwa pembeni kwa "special screening" wenyewe wakidai kuwa ni "random" choice. Mwanzoni kwa kweli nilikuwa offended maana katika wote pale ni mimi tu nikajihisi labda kwa sababu jina langu limekaa kiafrika! au kwa vile naelekea Detroit mahali ambapo "Underwear Bomber" kutoka Nigeria alitaka kulipua ndege kama mwaka mmoja na nusu nyuma. Kwa vile sikuwa na kitu chochote kuficha nilisubmit wholly and totally kwa ukaguzi wao wa kupapasapapasa mwili kila nchi! Nikiwa na hasira nikakuta wamemchagua bibi wa kizungu kufanyiwa ile "special search" nami ndio nikatulia na mara nikaona wamefanya hivyo kwa mzungu mwingine...nikatulia.

Umeshajitrain kiakili kuwa ukiulizwa, kusimamishwa, kukataliwa au hata kubishiwa na mtu mwingine yeyote ni kwa sababu wewe ni "Muislamu". Jambo lililokukuta wewe pale Airport yumkini linawakuta waislamu na wakristu wengi tu na hata labda watu wasio na dini. Hawa wote yawezekana waliamua kusubmit kwa sababu hawakuwa na cha kuficha lakini walipotoka hawakufikiria wamefanyiwa vile kwa sababu ya dini zao. Ndio maana niliuliza kama wale waliokuzuia walisema lolote juu ya dini yako, jina lako, au hata Mtume ili kuonesha walikuwa na kitu kingine. Unasema wewe ulijua hicho nje ya tukio lenyewe!

Ndugu yangu umekaribisha na kuendeleza hii "victim mentality" kiasi kwamba Mohammed Said hatakiwa kusimamishwa na serikali ya Tanzania, hatakiwi kuulizwa, na hatakiwi kukaguliwa! Akisimamishwa, akiulizwa, akiambiwa aonane na afisa wa polisi kupata maelezo hisia yake ya kwanza ni "wananifanyia hivi kwa sababu mimi ni Muislamu". Hakuna ushahidi wowote ule ulioutoa zaidi ya maneno yako kuwa ulitendewa vile kwa sababu ni Muislamu! Hakuna kauli ya waliokukamata, hakuna kauli ya wakubwa wa polisi, na wala hakuna mahali popote ambapo umeweza kuonesha kusimamishwa kwako kulikuwa ni kwa sababu wewe ni Muislamu! Ingekuwa kweli kama ungekuwa ni Muislamu pekee kupita pale..

Kusema kuuwa uliwasema sana Wamarekani ndio maana hayo yakakukuta labda huwajui sana Wamarekani. Wamarekani hawatishwi sana na maneno tu. Kati ya haki zao kubwa za msingi ni haki ya kujieleza. WAmarekani wanafuatilia maneno ya mtu pale tu anapotoa "clear threat" siyo anapotoa maoni. Wewe si wa kwanza kubeza Patriot Act au kubeza sera mbalimbali za Wamarekani. Na wewe siyo Muislamu wa kwanza kuwaambia wamarekani ukweli kuhusu sera zao usizokubaliana nazo. Ninapoishi mimi hapa Detroit, mji mdogo karibu ni wa Dearborn - una concentration kubwa zaidi ya Waarabu nje ya Middle East! Kuna misikiti na kuna watu wanazungumza na kupinga sera za Wamarekani bila kuhisi wanatishiwa kwani wanatumia haki ya kutoa maoni.

Sisemi kwamba haiwezekani kutokea hilo la hasha kwani ni sawa na kusema kuwa Polisi wa Marekani hawaangalii kabisa rangi ya mtu wanayemsimamisha - si kweli. Ninachosema ni kuwa hujatoa hata uwezekano kidogo wa kuonesha kuwa lililokukuta linatokana na dini yako. Ulichosema kwa ufupi ni "inference" tu ya hisia zako. Kwa sababu najua kwa msomi kama weewe kitu kama hicho kingekutokea ungeandika hata kwa Said Mwema (Muislamu) kumlalamikia au aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani (nadhani alikuwa Muislamu wakati huo). Usiache vitendo kama hivi kupita miaka mitano mbeleni ndio uviseme vilitokea na sisi hatuna namna ya kuuliza.

Labda walichokuambia kuhusu uuzaji unga ndicho hasa walichoamini; si tumesikia serikali hii hii ikisema wapo "viongozi wa dini" wanaojihusisha na biashara hiyo? Tumesikia maaskofu wa Kikatoliki wakikaguliwa siyo TZ tu hata nje ya nchi; ndiyo sifa mbaya ya nchi yetu hiyo.
 
Pole kwa maswaibu yaliyokukuta sheikh. wengi naona wanachangia kwa kebehi tuu. lakini haya mambo mpaka yakukute wewe ndio utaielewa vizuri hii hadithi.

HATUMCHAGUI MTU KWA SABABU YA DINI YAKE, NA HATUTAMUACHA KUMCHAGUA MTU KWA SABABU YA DINI YAKE!!!!
Kama una akili utayapata Majawabu ya hoja zako/zenu humu.
 
Anazungumzia kilichotokea BAADA ya uchomwaji wa mabucha ikimaanisha waliingizwa hata wasiohusika!
Mimi binafsi siwaoni na hatia waliochoma mabucha (lakini hilo ni suala jingine unaweza kulifungulia thread ukitaka, nitakuja huko)Hapa inabidi ututhibitishie kwanza kuwa ni Waarabu Waislamu ndio walioleta utumwa Tanganyika.Hawa "wanaolialia" na kupanda majukwaani na kuelezea hisia zao au wanaoandamana ni watu wazuri Mkuu, ogopa wale wasio lialia!
Kama wote tutakuwa na mtazamo kama wako, basi na sisi tutasema: Hatuwaoni na hatia waliochoma Koran kule Mbeya. Je unaionaje hiyo? Imekaa vizuri ee? Ni kweli kwamba hawana hatia kwa kuchoma Koran kwa vile tu mtu fulani anaamini hivyo kwasababu ya udini wake? Achaneni na udini, ni sumu mbaya, hauna tofauti na ukabila na ubaguzi wa rangi. Kuweni na dini lakini udini uepukeni kwa gharama zozote zile.
Ili kujua waliowafanya waafrika watumwa walikuwa ni watu wa dini gani, rejea historia ya Tanzania na usome kuhusu sultani wa Zanzibar na utajua imani yake ni ipi. Hata leo hii yeye ya
familia yake yote kule omani ni waislamu. Hiyo ni reference nimekupa. Ila naomba na wewe unithibitishie Jinsi kanisa lilivyohodhi Bunge. Ukiweza kunionyesha ni wapi na lini kiongozi walau mmoja wa kanisa hapa Tanzania aliingia bungeni na kutengua maamuzi ya bunge, kiasi kwamba spika pamoja na bunge lake hawakuwa na mamlaka yoyote zaidi ya kutii amri, nitakubaliana na hoja ya kanisa kuhodhi bunge na hata serikali nzima.
 
Back
Top Bottom