Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,249
UDHALILISHWAJI WA WAISLAM NA VYOMBO VYA DOLA VYA TANZANIA

Utangulizi

Sheikh wa kwanza kudhalilishwa na serikali ya Tanzania alikuwa Mufti wa Tanzania kwa wakati ule Sheikh Hassan bin Amir ambae kwa amri iliyotolewa na Julius Nyerere alikamatwa nyumbani kwake usiku wa manane akiwa kavaa khanga tu na akachukuliwa hivyo hivyo hadi uwanja wa ndege na kurejeshwa "kwao" Zanzibar. Kisa cha yeye kufukuzwa Bara ni kirefu na kwa sasa hapa si mahali pake kueleza. Nimekiweka kisa cha Sheikh Hassan bin Amir mwanzo kwa kuwa kina nafasi ya pekee katika historia ya Waislam na mapambano yao na serikali toka uhuru upatikane mwaka 1961. Lakini mwaka wa 1964 masheikh wengi waliwekwa kizuizini kwa amri ya Nyerere hiki nacho ni kisa kingine kinachohitaji wakati maalum kuhadithiwa. Baada ya haya ndipo kwa mara ya kwanza moto wa makumbi ukajitokeza juu na Waislam wakapambana na serikali katika mitaa ya Dar es Salaam mwaka 1993 na mabomu ya machozi na risasi zikapigwa. Haya ndiyo yalikuwa maandamano ya kwanza kufanywa na Waislam baada ya uhuru. Hili lilikuwa sakata la kuvunjwa mabucha ya nguruwe. Damu ya Waislam ilimwagika. Masheikh kumi na moja wa Wilaya ya Kinondoni walikamatwa pasi na adabu usiku wa manane majumbani mwao, wakapigwa pingu na kutupwa katika malendrova ya polisi kama majambazi. Lakini haya yote si kitu tokeo lililotokea siku ya Jumatano tarehe 4 Julai lilifurtu ada. Sheikh Nurdin Kishki akiwa na ugeni wa masheikh wenzake kutoka Yemen ndani yao akiwapo Mufti wa Yemen walivamiwa na askari waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia wakiwa njiani wakitokea Tanga na wakagaragazwa chini huku wakionyeshwa mitutu ya bunduki. Hii ilikuwa habari kubwa lakini vyombo vyote vya habari kama ilivyo ada kwa mambo yanayowahusu Waislam vyombo vyote muhimu vilipuuza stori hii.

Baada ya utangulizi huu naeleza kisa kilichonifika mikononi mwa vyombo vya dola miaka sita iliyopita:

Mkasa Wangu wa Kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Nyerere, Dar es Salaam Mwaka 2006

Mohamed Said

"Mwaka 2006 Radio Tehran walipendekeza jina langu rehekwa Wizara ya Mambo ya Nje Iran wanialike katika hawli ya Imam Khomeni. Sababu ya ya mie kualikwa ni kuwa mara kwa mara nilikuwa nikifanya mahojiano na Radio Tehran Idhaa ya Kiswahili kuhusu siasa za Tanzania hususan wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 na ikatokea kuwa yale mahojiano yangu yakawa yanapendwa na wasikizaji wa Afrika ya Mashariki na Kati na sehemu za Emirati. Nilkwenda Iran na waalikwa walikuwa kutoka dunia nzima na wa kila aina, waandishi, wahadhiri wa vyuo vikuu, wasomi wa kawaida, mawaziri wa serikali kutoka nchi tofauti na watu wengine wengi. Msafara wetu wa wageni kwenda mahali ulikuwa ni msururu wa mabasi zaidi ya kumi yakisindikizwa na kimulimuli cha polisi. Kutoka Tanzania nilikuwapo mimi pamoja na waandishi kutoka Daily News na Kituo Cha TV cha Channel Ten. Nikiwa Tehran niliingia studio za Radio Tehran Idhaa ya Kiswahili na tukafanya mahojiano na mtangazaji wao mashuuri Abdulfataa Mussa na wenzake na vilevile kurekodi vipindi vingi kuhusu hali ya Waislam Tanzania.

Mambo yalianza wakati sasa narudi Dar es Salaam na ndege ya Emirates iliyokuwa inatua usiku. Inaelekea maofisa wa pasi pale uwanjani walikuwa na taarifa zangu mapema na walikuwa wakinisubiri kwa hamu kubwa kwani nilipotoa pasi yangu kwa afisa wa pasi hapo ndipo shughuli za kunishughulikia zilipoaanza. Mimi sikuwa na hili wala lile. Nikawa namuona yule dada aliyekuwa kwenye kile kizimba akikukurika na pasi yangu akiitia katika mashine na kuitoa mara kadhaa. Fikra iliyonijia kwa haraka ilikuwa mashine ni mbovu na harakati zile zilikuwa ni kurekebisha mitambo. Kumbe sivyo wahusika nadhani walikuwa wanahakikisha kuwa mimi ndiyo huyo waliokuwa wakimwinda na kumsubiri na sasa kapatikana, kaingia mwenyewe kwenye mtego na kanasa. Yule afisa wa pasi akanambia nikae pembeni natakiwa kwa mahojiano na watu wa usalama. Hofu haikuwa imeniingia kwa kuwa nilikuwa natambua kuwa harakati dhidi ya ugaidi zilikuwa zimepamba moto na labda nilitakiwa kwa mahojiano mafupi kutaka kujua nyendo zangu. Sikujua wala kutarajia kuwa mshtuko mkubwa ulikuwa unanisubiri.

Nilichukuliwa hadi kwenye chumba kimoja na hapo niliwakuta maofisa wa usalama watatu wakanikaribisha kwa taadhima kisha wakanambia kuwa niko chini ya ulinzi kwa kuwa zimewafikia taarifa zangu kuwa mimi nasafirisha mihadarati. Mpaka hapa sikuwa na hofu bado ilinijia picha kuwa yawezekana wamefananisha majina. Niliwaambia huenda Mohamed Said muuza madawa ya kulevya siyo mimi niliye mbele yao. Wakaniambia kwa kujiamini kabisa kuwa taarifa zao ni madhubuti muuza unga ni mimi na wamekuwa wakinifuatilia siku nyingi. Hapo ndipo walipotoa pasi yangu na kuniomba niitambue kama hiyo pasi ni yangu au la. Niliwajibu kuwa hakika hiyo ndiyo pasi yangu khasa. Wakaniamuru sasa tutoke twende nikachukue mizigo yangu ili wafanye upekuzi wa mihadarati katika mizigo niliyotokanayo Tehran. Hapo ndipo nilipojuwa kuwa niko katika lindi kubwa la matatizo na ubongo wangu ukaanza kufanya kazi kwa haraka huku nikosoma dua kumuomba Allah ulinzi wake kwani kwa hakika nilijua kama ni njama zimekamilika na leo imefika siku yangu. Nikajiuliza itakuwaje watakapotoa madawa kwenye mizigo yangu. Nikaanza kufikiri vichwa vya habari vya magazeti yatakavyopambwa na habari zangu. Ikanijia yakini kuwa watu wa usalama wameniwekea madawa ya kulevya katika mizigo yangu ili waniangamize na maadui zangu wapumzike na shari yangu.

Nilimgeukia yule ofisa mkuu aliyekuwa ananihoji nikamwambia kuwa sitokubali kugusa mizigo yangu bila kuwapo mashahidi isijekuwa mizigo yangu ishawekewa hayo madawa ya kulevya kwani nilikotoka mizigo ilikuwa imekaguliwa na ilikuwa salama. Hoja yangu kubwa kwao ilikuwa kupata uhakika kutoka kwao kuwa wananijua vizuri kiasi cha kuthibitisha kuwa kweli mie ni msafirishaji wa madawa ya kulevya. Jibu nililopewa ni kuwa wao wanafanya kazi kutokana na taarifa zilizowafikia. Wakasema, "Sisi tunazo taarifa zako kamili kuwa wewe ni msafirisha madawa ya kulevya." Nikawauiza, "Baada ya kupata taarifa hizo zangu nyie mmechunguza kutafuta ukweli?" Wakasema, "Ndiyo maana leo tumekukamata." Nikawaambia, "Si kweli kama kwa sababu mie nafahamika Dar es Salaam takriban kwingi maana ndio nilikozaliwa na kukulia. Hapo Kariakoo ukiwaambia watu kuwa Mohamed ni "Mzungu wa Unga" kila mtu atacheka maana huo kwao ndugu zangu ni mzaha mbaya." Walitaka kujua nilkwenda kufanya nini Iran. Niliwaambia nilialikwa na serikali ya huko kuhudhuria mkutano. Wakataka kujua vipi nilipata mwaliko. Nikawajibu kuwa hilo swali sina jibu labda waiulize serikali ya Iran. Nikawaeleza kuwa mbona siku zote napita hapo uwanjani nikenda sehemu tofauti duniani kwa mialiko na kutoa mada sijakamatwa kimezidi nini katika hii safari ya Iran? Niliwaeleza kuwa miezi michache iliyopita nilikuwa Chuo Kikuu Cha Ibadan kwa mwaliko tena mkutano umefadhiliwa na serikali ya Amerika na wamenipa na tiketi toka Dar es Salaam hadi Lagos na kuniweka hoteli na kunilipa fedha. "Mbona hamkunikamata wakati ule?" Ikawa swali na jibu swali. Nikafungua mlango mwingine nikawaambia, "Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyanyasa Muislam?" Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa naponzwa na dini yangu.

Baada ya kukurukakara nyingi na mabishano makubwa kuhusu mie kukubali kufanyiwa upekuzi wa mizigo yangu alikuja binti mmoja katika wao na yeye akanihakikishia kuwa wao ni serikali na sio wahuni. Hawathubutu kuniwekea dawa katika mizigo yangu hivyo akanisihi sana kwa upole nikubali ili wajitoe wasiwasi na wataniachia endapo hakuna kitu. Niliomba apatikane shahidi wa kushuhudia mizigo yangu kabla ya kufanyiwa upekuzi lakini hakuna mtu aliyekubali kuchukua dhima ile katika maofisa waliokuwa kazini pale uwanja wa ndege usiku ule. Upekuzi ukafanyika hadi mwilini. Hakuna kitu. Wakanipela katika choo maalum cha kutolea madawa kwa njia ya haja kubwa. Nikakataa kujisaidia pale. Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuona choo kama kile. Choo chenyewe ni cha aluminium. Tofauti na vyoo vya pale ambavyo siku zote ni vichafu, hiki kilikuwa kisafi sana kiasi mtu unaweza hata kutengewa chakula na akala bila ya kuhisi kinyaa.

Nilitegemea wataweka ahadi yao kuwa ikiwa hawatakuta madawa ya kulevya katika mizigo yangu watanirejeshea uhuru wangu wataniachia niende nyumbani. Haikuwa hivyo. Wakanirudisha ofisini kwao. Sasa wakaacha madawa ya kulevya wakahamia katika vitabu na "audio cassette" nilzokuwa nimepewa kama zawadi kule Tehran wakaniluliza kwa nini naingiza vitu vile khasa kanda za Khomeni na vitabu vyake nchini. Nikawauliza, "Kwani kanda na vitabu vya Khomeni haviruhusiwi kuingizwa Tanzania? Maana mimi hata nyumbani kwangu hii leo mkifika nina vitabu vya Khomeni na wanafalsafa wengine kama Karl Marx ambao nimesomeshwa pale Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam." Sasa hapo ikaja kejeli. "Ala wewe mtu wa Kariakoo lakini umefika hadi Chuo Kikuu!" Sikujibu kitu. Awali waliponitia mbarani waliniuliza kwetu na nikawaeleza kuwa nimezaliwa Kariakoo.

Hawakunipa jibu kuhusu kuingiza vitabu na cassette za Khomeni. Ikawa sasa kama vile wameishiwa maswali. Nikaona kuwa sasa ni zamu yangu nami kuwapiga maswali. Yule aliekuwa akinihoji nikamwambia, "Mimi wewe nakufahamu vizuri sana kwa sababu ukicheza mpira Simba Sports Club na mie ni mpenzi wa club hiyo toka utoto wangu wakati huo ikiitwa Sunderland na mmoja wa baba zangu alikuwa mchezaji marufu wa club hiyo katika miaka ya 1950 akafiikia hadi kucheza Kombe la Gossage." Nilihisi amepata mfadhaiko kidogo akanambia,"Unanifananisha yule aliekuwa akicheza Simba ni ndugu yangu." Alikuwa anasema uongo lakini mie nikamkubalia. Hapo nikajua kuwa nishampata sasa hana nguvu tena ya kuuliza maswali. Kusema uongo ni dalili ya kujihami. Nikamrushia kombora lingine, "Sasa tuhuma za madawa ya kulevya zimekwisha tuko katika kwa nini naingiza vitabu vya Khomeni nchini?" Akanijibu kinyonge, "Tumeridhika huna madawa." Kufika hapa tukawa tumemaliza mahojiano.

Wakati huo sasa ni usiku wa manane na nishapeleka SMS kwa sahib yangu mmoja bingwa wa mambo ya mtandao wa kompyuta kumjulisha kuwa nimekamatwa uwanja wa ndege kwa tuhuma za uongo za kuvusha mihadarati na yeye ile kuipata tu ule ujumbe wangu akaifahamisha dunia kuwa nimekamatwa uwanja wa ndege nikitokea mkutanoni Iran na nimebambikiziwa tuhuma za kuingiza nchini mihadarati. Waliponitia mbaroni tu walinionya kuhusu kutumia simu yangu ya mkononi lakini bahati nzuri hawakuninya'ganya. Aliyenipa onyo hili alikuwa mkuu wa kituo cha polisi cha uwanja wa ndege. Huyu rafiki yangu akawa kanisaidia sana maana hadi kumekucha wapenzi wangu wote ndani na nje ya nchi pamoja na vyombo vya habari vinavyonifahamu walikuwa na taarifa za kukamatwa kwangu. (Kwa kipindi takriban miaka ishirini nyuma kwa nyakati fofauti nimekuwa nikifanya mahojiano na radio zote muhimu kama, BBC, VOA, Sauti ya Ujerumani, Sauti ya Iran nk.).

Nikawaomba wale watu wa Usalama waniachie basi nende zangu kulala nyumbani nirudi hapo kesho asubuhi kwa kuwa sikuwa nimebeba madawa ya kulevya. Wakaniambia, "Itabidi tukulaze hapa hadi asubuhi wakubwa wetu watupe amri ya kukuachia. Maana amri ya kukukakamata wewe imetoka juu."
clip_image001.gif
Sasa hapo ikawa nimelipata jingine. Kumbe wauza unga hawakamatwi hadi amri itoke juu. Sasa kama amri haikutoka ndiyo muuza unga atapita aingize sumu zake mitaani? Hili likazidi kunidhihirishia kuwa kukamatwa kwangu hakukuwa na uhusiano wowote na vita dhidi ya mihadarati bali ni vita vile vile vikongwe dhidi ya Uislam.

Nikawa pale usiku kucha. Sasa wakati niko pale wakidhani nimelala. Wakawa wenyewe kwa wenyewe wanazungumza kuhusu hii ‘operation' neno walilotumia ni kuwa 'leo tume-dial wrong number.' Wakawa wanasema, "Huyu bwana mbona hakuelekea kama muuza unga tena huyu mtu bwana kasoma kweli kweli" Wanadhani mie nimelala kumbe ni macho nawasikiliza. (Vipi utalala katikati ya michongoma?). We umeona jinsi alivyokuwa akijibu na kuchambua mambo." Hilo ndilo likawa gumzo lao wakinisifia kwa ufasaha na mantiki lakini wakizungumza kwa sauti ya chini kabisa. Hapa ikanidhihirikia kuwa hawa vijana walikuwa wanatimiza wajibu wao wa kazi tu lakini kiini khasa cha kukamatwa kwangu hawakuwa wanakifahamu.


Walionikamata walikuwa vijana kama wanne na wote walijitambulisha kwa majina ya Kiislam. Nilijua ni waongo kwa kuwa Muislam anonekana katika uso na katika matumizi ya lugha. Lakini yule mchezaji wa Simba ni Muislam na yeye ndiye aliekuwa mkubwa pale akiongoza ile shughuli yote tena kwa kujidai na kujifaharisha sana. Kisa kile kile cha mtumwa anelimishwa na yule anefanya kazi za ndani nyumbani kwa bwana. Ila kitu kimoja lazima nikiri. Wale vijana walikaa na mimi kwa wema na hawakunibughudhi hata kidogo. Hata nilipokuwa nakwenda msalani kijana alienisindikiza alinitaka radhi akasema, "Nakusindikiza kwa sababu ni sheria lakini sisi tunakustahi kwa hiyo utuwie radhi kwa kukufuta hadi msalani."

Asubuhi wakubwa wakaja kazini lakini hakuna alienikabili. Walikuwa wakinichungulia kutoka mlangoni kama simba ndani ya kizimba kwenye zoo, nami nikawa najifanya siwaoni. Ndipo akaja mkubwa mmoja tena akaniita kwa jina langu na kwa heshima na bashasha sana, "Bwana Mohamed tuwie radhi sana pamekuwa na makosa kidogo tuwie radhi sasa hivi tutakuruhusu uende nyumbani. " Akatoka nje akawa akipiga simu. Kisha akarudi ndani akaamrisha nibebewe mizigo yangu na gari la polisi linirudishe nyumbani. Kistaarabu kabisa nikakataa gari ile huku nikifanya maskhara kuwa naogopa gari ya polisi asijepiga simu akasema mrudisheni huyo mtuhumiwa. Ofisi nzima ikacheka. Hapo ndipo wale wakamataji wangu wa usiku wakabeba mizigo yangu nami nafuata nyuma tunatoka nje ya uwanja.
clip_image001.gif


Kilichobaki sasa ni kueleza sababu ya mimi kukamatwa. Mwaka wa 2006 Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria kilifanya kongamano la kimataifa hapo chuoni kwao kuzungumza kuhusu Ugaidi katika Afrika ya Mashariki na Maendeleo ya Afrika (Conference on Islam, Terrorism and African Development). Mimi ninlitoa mada iliyokuwa na anuani hii: Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience. Katika mada hii nilijikita mahsusi katika kuisema Marekani kwa udhalimu wao duniani. Nikaeleza kuwa huo udhalimu wao ndiyo unaopelekea wao kuchukiwa dunia nzima. Hapa ningependa kufahamisha kuwa mkutano huu wafadhili wakubwa walikuwa Iran na Marekani. Saudi Arabia ilikataa kuchangia mkutano ule. Wakati nasema maneno haya ya kuwakanyaga wenyewe Waamerika wapo hapo mkutanoni.

Baada ya kuwalani Waamerika sasa nikaigeukia serikali ya Tanzania na kuishutumu vikali kwa kupitisha Sheria ya Ugaidi. Hapa nikaeleza kuwa Waamerika wasione kuwa Tanzania imepitisha sheria hiyo ya ugaidi kwa haraka kwa sababu Tanzania ina tatizo na ugaidi. Nikaeleza kuwa sheria hiyo imepitishwa kwa sababu Bunge la Tanzania limehodhiwa na Kanisa na kupitishwa kwa sheria hiyo hakuna uhusiano wowote na ugaidi ila Wakristo wamepata fursa ya bure ya kupambana na Uislam wakitumia serikali ya Marekani kama upawa wao wa kuopolea chinyango ya moto kwenye chungu kinachotokota. Nikauchekesha mkutano kwa kuwaambia kuwa Wamarekani wamefanywa wajinga na Kanisa kwa kuchonganishwa na Waislam wa Tanzania ambao hawana ugomvi nao asilani. Baada ya kusema hayo nikahitimisha kwa kueleza nguvu ya Waislam Tanzania, kwanza kwa wingi wao na kisha kwa historia yao iliyotukuka iliyodumu takriban miaka mia wakipambana na ukoloni wa Wajerumani kwa silaha (1905 1907), kisha ukoloni wa Waingereza (1929 1961) na kuhitimisha kwa kuleta uhuru na kuanzia 1961 hadi sasa wanapambana na nguvu ya kanisa katika kupiga vita Uislam.

Kufikia hapa ukumbi ukawa umepata joto. Wanigeria wamesimama kutaka niwaeleze vipi Waislam watakuwa wamepigania uhuru kisha wako wengi nchini wanaruhusu wao kufanywa raia daraja la pili. Wakashangazwa kuwa hata historia ya mashujaa Waislam waliopigana Maji Maji na kunyongwa na wakoloni na mashujaa walipigania uhuru wa Tanganyika hawatajwi katika historia ya ukombozi. Nilitoa majibu kadri Allah alivyoniwezesha. Nakumbuka kitu kimoja walichosema wale ndugu zetu Wahausa. Walisema hali hiyo iliyoko kwenu haiwezekani kutokea Nigeria kwa kuwa hiyo itakuwa na sawa na kutangaza vita. Kisha wakanihakikishia kuwa sheria hiyo ya ugaidi haitapitishwa Nigeria hata siku moja.

Wapashaji habari wangu wakajanieleza baadae ni hili hitimisho langu ndilo lililosababisha Wamarekani kuleta taarifa Dar es Salaam kutaka taarifa zangu za "ugaidi" ikawa sasa sababu imeptikana ya mimi kushughulikiwa na vyombo vya dola. Ndipo ikatengenezwa hadithi ya kuku jike na ng'ombe dume (cock and bull story) kuwa Mohamed Said ni Mzungu wa unga kwa hiyo akamatwe.

Mkasa huu ulinifika miaka sita iliyopita lakini hadi leo kovu la mkasa ule limebaki katika pasi yangu. Sielewi pasi yangu inaonyesha nini inapotiwa katika compyuta baada ya mkasa huu kwani kama mara tatu husimamishwa kwa muda na kuombwa nitoe maelezo ya ziada kuhusu niendako kila nisafiripo nje ya Tanzania. Nimeshuhudia hali hii Uwanja wa Ndege Amsterdam na Detroit, Marekani. Berlin, Ujerumani niliambiwa mzigo wangu umepotea lakini hata kabla sijatoka uwanjani nikatafutwa na kukabidhiwa mzigo wangu na kwa hili sikuwa peke yangu nilikuwa na mwenzangu, jamaa wa Kiarabu kutoka Misri. Sijui kama mizigo yetu ilikuwa imebakishwa nyuma kwa upekuzi zaidi. Amsterdam, Uholanzi baada ya kupita sehemu zote muhimu za upekuzi wakati naelekea kituo cha mwisho niingie kwenye ndege inayoelekea Detroit, Marekani nikachopolewa kutoka kwenye mstari na nikawekwa pembeni peke yangu kwa usaili wa ziada. New York kadi yangu ya benki ilikataa kutoa fedha kwa siku nzima hadi siku ya pili. Nilikujafahamishwa baadae kuwa "system" ilikuwa inanichunguza kwanza. Ilikuwa siku ya pili baada ya kuonana na maofisa wa benki ndipo kadi yangu ikaanza kutoa fedha. Geneva, Uswisi kadi yangu ilikataa kutoa fedha katika mgahawa. Sikujua kama ni yale yale au haya yalikuwa mengine. Lakini pasi hii afisa wa uhamiaji wa Tanzania alipoiingiza kwenye compyuta yake alimwita mwenzake kuja kutazama kisha wakawa wanacheka. Waliona nini kwenye pasi yangu Allah ndiye ajuaye."

M
 
Why encouraging the enlargement of the circle of concerns instead of enlarging the circle of influence? Kila siku ni kulia lia tu na kutafuta mtu wa kuwaonea huruma watu wachache wasio na agenda nyingine yoyote zaidi ya Nyerere. Nyerere is gone and we cant change that fact. Kizazi hiki kianze kushughulika na mambo yasiyotuhusu ili iweje? Tukumbuke wa mbili havai moja! Tupigane kutoka hapa tulipokwamba.
 
Mzee Mohamed Said, tatizo la watanzania sio nani anaimani ipi bali tatizo letu ni umaskini unaosababishwa na sera mbovu za uchumi za serikali ya CCM. Baada ya kushindwa kabisa kujenga mazingira ya raslimali za nchi kutumika kwa manufaa ya wote, serikali ya CCM imeamua kutembeza bakuli nje ya nchi na kuwakumbatia wezi kwa jina la wawekezaji. Ili kuficha udhaifu wake serikali inawatumia watu kama ninyi akina Mohamed Saidi kuchochea chuki za kidini miongoni mwa watanzania ili wakalie hayohayo ya waislamu kuonewa badala ya kuungana na kuishikisha adabu serikali legelege. Nakushangaa sana mzee wewe, iweje serikali inayoongozwa na muislam mwenzio ikuhujumu na kukutuhumu kuwa zungu la unga! kwanini isingekosea na kukupeleka msitu wa Pande?
 
Bwana Mohamed
Acha kuficha hoja zako za kisiasa kwenye mgongo wa Uislamu, unatutia aibu na kutufedhehesha; wewe kama ulipekuliwa ni kwa misingi ya kisiasa na sio ya Kiislamu; Waislamu wanagapi wanapita kwenye viwanja vya ndege duniani na hawabughudhiwi itakuwa wewe tu kila siku? Jitangangaze wewe ni mwanasiasa tukujibu kisiasa ni makruhu makubwa kwa waislamu kukashifiana ila ukija kama mwanasiasa tutakuhabarisha; hata leo hii kama pasi yangu ya kusafiria ina muhuri wa Cuba, Korea ya Kaskazini wamerekani watanihoji nini kilinipeleka katika nchi hizo si kwa misingi ya kidini bali kwa misingi ya kisiasa. Ikiwa kama wewe ulikwenda Tehran na wote tunajua fika Iran ni mahisimu wakubwa wa Marekani na Jumuiya ya Ulaya, walikuwa na sababu ya kukusumbua ina tu nataka uelewe usumbufu ulioupata ulikuwa ni kwa malengo ya kisiasa.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu utakuwa umeingizwa kwenye listi ya potential terrorist, hivyo status yako wewe ni high risk kwahiyo everytime you got to be cleared first for security purposes, wengi wa walioko kwenye hiyo listi ni waislam, however wengi wa magaidi ni waislam pia.
 
Ngooja nikirudie tena hiki kisa kabla sija comment zaidi.
 
Pole kwa maswaibu yaliyokukuta sheikh. wengi naona wanachangia kwa kebehi tuu. lakini haya mambo mpaka yakukute wewe ndio utaielewa vizuri hii hadithi.
 
Wangapi wanatiwa hatiani nchi hii kwa tuhuma za kuunda? Wote wanaofanyiwa hivyo ni waislamu? Nguza kafungwa yeye na wanawe kwa tuhuma ambazo hata kwa mtoto mdogo zitatiliwa shaka (ni nani hata akiwa kichaa atashirikiana na wanawe kufanya ngono wakati mmoja? Na kwa nini shahidi mkuu wa serikali ambae "ushahidi" wake ni sawa na kukiri kosa asiadhibiwe?). Mbona waislamu wanazikimbia nchi zao (kama Pakistan na Yemen - achilia mbali Iran na Syria) na kuhamia Marekani na Ulaya? Hata zuzu anajua kuwa si tatizo mtu kujenga msikiti USA na Ulaya lakini ni kujitafutia kifo mtu kukutwa na biblia Indonesia, Pakistan, Saudi Arabia etc? Acheni unafiki nyie watu! Mbona hamuhaimii nchi za kiislamu kama mnavyohamia nchi zisizokuwa za kiislamu?
 

Kwa hiyo unataka aajiriwe mtu yeyote hata kama hajui kuandika bora tu anajiita muislamu? Walioajiriwa hawana sifa za kuajiriwa kwenye kazi walizopewa? Ninajua nchi hii viongozi ni corrupt, na kwa maana hiyo sitashangaa kuona mtu kapewa kazi asiyostahili (kama kina Sophia Simba, Celina Kombani, Stephen Wassira, Mustapha Mkulo n.k), unataka kutuambia walipewa kwa kuwa wote ni wakristo au walipewa kutokana na incompetence ya aliowapa? Acheni uzuzu nyie watu!
 
Mohamed Said, kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho hawa ndugu zetu hutuogopa kwa majina tu ya Kiislaam. Hawana zaidi ya uoga, na uonevu wao wote lakini AlhamduliLllah Uislaam ndio dini inayokuwa kwa haraka kuliko dini nyingine yoyote duniani na hususan hukohuko Merekani, ushahidi huu hapa: Fastgrowing Islam winning converts in Western world - CNN
 
Mohamed Said, kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho hawa ndugu zetu hutuogopa kwa majina tu ya Kiislaam. Hawana zaidi ya uoga, na uonevu wao wote lakini AlhamduliLllah Uislaam ndio dini inayokuwa kwa haraka kuliko dini nyingine yoyote duniani na hususan hukohuko Merekani, ushahidi huu hapa: Fastgrowing Islam winning converts in Western world - CNN

Hata maovu yanazidi kuongezeka duniani, so what does that tell you?
 
Sijaelewa, huyu Mohamed alikatamwa kwa sababu ya dini yake? Na kwenye ndege ni yeye pekee alikuwa muislam?
 

Hans Roger Dibagula, utafiti wako ni dhaifu, kwa sababu umeangalia maeneo machache tu na wala haujaainisha hizo nyadhifa. naomba uainishe, na ulete tafiti kamili, sababu hapo sijaona idara nyingine muhimu. ainisha pia ugawaji wa madaraka kwa ngazi tofauti. otherwise siwezi kuiamini tafiti yako, huenda ulikaa tu, kwa vile una MS Word kwenye desktop yako, basi ukawashwa washa mpaka kuja na pumba hizi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom