Udhaifu wa rais jk mwingine huu hapa.

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,274
9,911
RAIS Jakaya Kikwete amezidi kuandamwa. Sasa
anaitwa “dhaifu na anayetishwa na wasaidizi
wake.”
Mtandao wa WikiLeaks unaoibua taarifa za siri
za kibalozi duniani, umeandika kuwa Rais
Kikwete aliwahi kumwogopa mkuu wake wa
majeshi, Jenerali Mwita Waitara.
Kinachoitwa udhaifu wake ni hatua ya kukatalia
Marekani kuweka nchini kituo cha majeshi ya
ushirikiano – Africa Contingency Operations
Training Assistance (ACOTA).
Taarifa zinasema Kikwete alighairi ahadi yake ya
kuwa na mradi huo kwa kuwa ulikuwa ukipingwa
na Jenerali Waitara.
Rais Kikwete anaelezwa kuwa alikuwa
amekubali, mara baada ya kuingia madarakani
Desemba 2005, mpango huo wa Marekani
unaodaiwa ungesaidia wanajeshi wa Tanzania
kupata mafunzo ya kulinda amani katika ukanda
wa Afrika na serikali kunufaika kwa misaada
kifedha.
WikiLeaks inamnukuu aliyekuwa balozi wa
Marekani nchini, Michael Retzer akisema
kukwama kwa mpango huo kulitokana na
Jenerali Waitara “kuuwekea ngumu.”
Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki moja
baada ya Balozi Retzer kunukuliwa na mtandao
huo akisema Rais Kikwete, alilipiwa na Ali
Albwardy, raia wa Nchi za Falme za Kiarabu
(UAE) nauli ya kwenda Uingereza na kurudi.
Alinukuliwa akisema pia kuwa Rais Kikwete
“aliwezeshwa” kiasi cha dola milioni moja za
Kimarekani (sawa na Sh. 1.6 bilioni), kwa ajili ya
shughuli za kutafuta urais mwaka 2005.
Ali Albawardy, ambaye ni mmiliki wa hoteli
maarufu jijini Dar es Salaam, Kilimanjaro-
Kempinski.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Salva Rweyemamu alikana madai hayo akisema,
“Rais Kikwete hakuwa akikusanya fedha” za
chama chake.
Ikulu ilimwita Balozi Rezter mzushi, muongo
na ikasema Rais Kikwete hajawahi kufadhiliwa
na bilionea mmiliki wa Kilimanjaro-Kempinski.
Taarifa zinamnukuu Balozi Retzer akisema
utawala wa Kikwete ulikuwa unapitia katika
wakati mgumu kati ya raia na jeshi, kutokana na
hatua ya mkuu wa majeshi “kuzuia” rais na
waziri wa ulinzi kuchukua hatua ya kuanzishwa
kwa mafunzo hayo.
Hata hivyo, Balozi Retzer anasema, “Lakini
hatukukata tamaa kwa kuwa mkuu wa majeshi
alikuwa anakaribia kustaafu, 31 Julai 2006 na
Rais Kikwete aliahidi kuanzishwa mafunzo hayo
baada ya Waitara kuondoka.”
WikiLeaks inasema tarehe 2 Mei 2006,
aliyekuwa waziri wa ulinzi, Profesa Juma Kapuya
aliomba kukutana na balozi ambapo aliomba
radhi kwa kucheleweshwa mafunzo hayo.
Profesa Kapuya amenukuliwa akimhakikishia
Balozi Retzer kwamba mafunzo ya ACOTA
yangeanza muda wowote baada ya Waitara
kustaafu.
“Kama ilivyodhaniwa, utawala wa Kikwete
unakumbana na mvutano wa kiraia na kijeshi.
Mkuu wa majeshi ya ulinzi Tanzania anazuia rais na waziri wa ulinzi kuchukua hatua ya kuanzisha mafunzo ya kulinda amani chini ya (ACOTA),” linaeleza WikiLeaks, likinukuu Balozi Retzer.Balozi ananukuliwa akisema mafunzo hayo yalilenga “kufundisha vikosi vitatu vya kulinda amani ifikapo 2008, mafunzo ya kwanza yakiwayamepangwa kufanyika Machi 2007.” Hadi Mei 2007, mafunzo hayo yalikuwa bado hayajaanza na Balozi Rezter ananukuliwa akisema, “…ni muhimu kuelewa kwamba Jenerali Waitara anakumbatia sera za ulinzi za kijamaa na amekuwa akizuia uhusiano wa karibu wa kijeshi na Marekani kwa kupendelea Uchina na nchi nyingine za kijamaa.” Kwa upande wake, Profesa Kapuya ananukuliwa akieleza Balozi Retzer, jinsi Rais Kikwete alivyoweka msimamo wake katika suala hilo, tangu 3 Machi 2006 wakati wa ziara ya Naibu Kamanda wa Marekani katika Muungano wa Ulaya, Jenerali William Ward. “Kikwete alisisitiza nia yake ya dhati ya kuunga mkono shughuli za mafunzo hayo…mbele ya wakuu wake wa jeshi. Lakini sasa kuna mkanganyiko kuhusiana na ucheleweshaji huu,” Kapuya ananukuliwa akisema.
Anasema, “Tunajaribu kuzuia mgongano na CDF (Mkuu wa Majeshi) na kuvuta muda wa kama miezi miwili hadi mitatu – ili tuzuie mgongano huo usiweze kutokea." Kwa shabaha ya kueleweka vema, Kapuya anamwambia balozi, “…tunajaribu kueleza hali
halisi ilivyo ili utuelewe. Tupo katika hali mbaya sana. Tunaomba msamaha kwa ucheleweshaji huo na tunakuomba utusaidie kutoa maelezo haya nchini kwako.” “Kwa dhati tupo tayari kuunga mkono jitahada za mafunzo haya ya kulinda amani nchini, na hatupendi kuona ucheleweshaji huu unaharibu uhusiano wetu mzuri uliopo,” anaeleza Profesa Kapuya katika hali ya kubembeleza. Mtandao unamnukuu Balozi Retzer akimhakikishia Profesa Kapuya kuwa wanaelewa madhumuni ya serikali ya kuunga mkono mafunzo hayo pamoja na changamoto zinazomkumba rais na waziri wake wa ulinzi. Balozi Retzer alisema anautambua mkanganyiko huo ulioanzishwa na Jenerali Waitara, na hivyo akamshauri Profesa kuruhusu mafunzo hayo kuanza kabla ya makubaliano kufungwa. Mpaka sasa, ubalozi wa Marekani nchini haujakana maelezo ya Balozi Retzer, jambo ambalo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema, linathibitisha kilichoandikwa na WikiLeaks. “Hizi tuhuma dhidi ya Kikwete, bila shaka zina ukweli. Vinginevyo ubalozi wa Marekani ungekuwa tayari umetoa taarifa.
 
Habari hii ni nyeti.Hata hivyo tunaamini watu wa usalama wa taifa wako kazini na hawawezi kuona nchi yetu inawekwa rehani kwa sababu ya ubinafsi wa wachache.
 
Habari hii ni nyeti.Hata hivyo tunaamini watu wa usalama wa taifa wako kazini na hawawezi kuona nchi yetu inawekwa rehani kwa sababu ya ubinafsi wa wachache.
Kwani wakati nchi ina ingia mikataba ya kipumbavu na isiyo na tija hao unaowaita usalama wa taifa huwa wako wapi?
 
Kwahiyo yale yanayompa sifa na kuwa imara yameliwa na haya Madhaifu mengi
 
Many congrats to Waitara, anajua na alijua maana ya kitendo hicho barabara. Ana akili sana huyu mtu. Tungekuwa hivi watanzania basi nchi hii isingeonekana DHAIFU hata kidogo. We need many more Waitaras. Halafu kule Kigamboni ule mpango wa Wamarekani ni vipi? Nasikia umeota mbawa!!! Wenye taarifa na the so called satellite city Kigamboni watupe!!!! Kweli Tz ni shamba la nyanya (bibi wa bibi).
 
Back
Top Bottom