Udhaifu Wa JK: Tafsiri Yangu

a very hypocritical journalist.....ndio sababu wewe huwezi kupata safu kwenye gazeti kama Raia Mwema....because you are a hypocrite.....Seems kuna kitu unatafta toka kwa watawala....you are a very very desperate journalist...very sorry for you...ungekuwa unarudi kujibu michango ya watu humu ningekuonyesha how hypocritical you are....lakini kwa vile hutarudi kujibu michango ya watu humu...i'm just sorry for you....

Ndugu yangu Nderingosha,

Mosi, mimi nina safu kwenye Raia Mwema tangu toleo namba moja. Pili, inashangaza kuwa unaongelea Raia Mwema wakati husomi Raia Mwema. Na haya unayosema hapa huenda umesukumwa na chuki binafsi. Ni tatizo lako.

Maggid
 
Ndugu yangu Nderingosha,

Mosi, mimi nina safu kwenye Raia Mwema tangu toleo namba moja. Pili, inashangaza kuwa unaongelea Raia Mwema wakati husomi Raia Mwema. Na haya unayosema hapa huenda umesukumwa na chuki binafsi. Ni tatizo lako.

Maggid

Hebu Jibu hoja namba 18 wacha Kushambulia ukiambiwa Ukweli Faiza Foxy hayupo wa Kukusifia
 
Tatizo la kauli kama hiyo ni kwamba imetamkwa ndani ya BUNGE. Ujue alimwongelea Rais kama taasisi, akiwa ndani ya BUNGE. Maneno yale hayawezi yakawa mepesi namna hiyo, ati uyatamke BUNGENI, na yaingie kwenye Hansard ya BUNGE, na wewe usitakiwe kuyafuta. Nje ya BUNGE, ruksa. Hatahivyo ndiyo imekuwa kazi ya wanaotaka kuingia serikalini (IKULU) kwa kila mbinu, hata kama ni kwa kujipiga risasi miguuni wakisema 2potelea mbali, nitajitibu India baada ya kuingia IKULU" au something similar. Ni uendawazimu kuidhoofisha taratibu ambayo baadaye wewe mwenyewe unataka uitumie kufanikiwa. Kwa mtazamo wangu, mtu anayediriki kufanya hivyo basi anaashiria kuwa yeye atakuwa DICTATOR. Mh. Mnyika alimwongea Rais kama TAASISI, tena akiwa BUNGENI akijadili "The most important instrument of governance - The Budget". Umaarufu wa mtu kama Mh. Mnyika kwa dharau ya bayana ya TAASISI ya Rais, akiwa BUNGENI, ni akiba kwa Watanzania wenye kutafakari. Lakini nimefuatilia maoni ya baadhi ya wanaodhani ilikuwa sahihi kwa Mh. Mnyika kusema hivyo, sikuona kama wametambua kwamba angweza kusema hivyo ndiyo, lakini NJE YA BUNGE. Kama alidhamiria, kama ilivyotokea hata baada ya kugoma kufuta usemi, basi ama ni kutoelewa taratibu, ama alitaka kujiongezea umaarufu wa bei ya chini, ama utoto tu.

Kwa kweli nitashangaa sana kama Kamati ya Uongozi ya BUNGE, chini ya Spika, watamwacha Mh. Mnyika bila kumjadili kwa kauli na kitendo hicho cha kutumia 'nyumba adhimu' ambayo ni MHIMILI mmoja, kudhalilisha 'MHIMILI' mwingine.
 
Umenifurahisha mno Mjengwa pale unapompa JK jina jipya ... Kigong'onda.
 
Tatizo la Maggid ni kujenga hoja na kisha kuziboa bomoa mwenyewe.

Katika makala hii, sina hakika kama imenisaidia mimi na labda wasomaji wengine kufikia hitimisho kama Kikwete ni Rais dhaifu au la.

I wishi mwandishi angekaa upande mmoja akaeleweka...naona anaendeleza mchezo ule ule wa Watanzania kutotaka kuonekana wabaya na hvyo kubaki wamekaa juu ya fensi!!
 
Kuna hoja mezani juu ya udhaifu wa JK, imetokea Bungeni. Yumkini, kama mwanadamu, JK ana mapungufu na udhaifu wake, nani asiye na mapungufu na udhaifu? Lakini, tukimzungumzia JK kama taasisi ya ' Urais', namwona Rais anayejipambanua na waliomtangulia. Ni kwa kujitahidi kufanya yale yalo nafuu na yenye manufaa kwa nchi yetu kwenye mfumo dhaifu uliopo.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
[/QUOTE]

Kwanza nikupongeze kwa tafakari yako mwanana Bw. Mjengwa.
Hata hivyo umezungumzia hoja kubwa mbili bila kuzitenganisha, jambo ambalo naamini ni muhimu kwa wengi wa wasomaji wako. Hoja zenyewe ni:
(i) Maneno yale kuwa yametamkwa BUNGENI, na
(ii) Haki ya Mh. Mnyika, au yeyote yule kusema chochote alimradi havunji sheria.

Tatizo la kwanza, ambalo ndilo naamini lilimfanya Mh. Spika kumtaka Mh. Mnyika afute kauli, ni kwamba ametamka hayo akiwa ndani ya BUNGE. Yaani, 'amedhalilisha' mhimili mmoja akiwa katika kikao rasmi cha mhimili mwingine. Neno 'amedhalilisha' bado ni laini kulitumia hapa, ingawa kwa Mh. Mnyika kugoma kufuta matamshi yale ili yaonekane katika Hansard kwamba yamefutwa, na kwamba hayakuwa suala la mjadala, inakaribia kuwa 'Treason'. Nasema inakaribia kuwa uhaini. Kwa maana hii inakuwa kama 'uhaini' wa BUNGE, Mh. Mnyika akiwa Kiongozi wa UHAINI huo. Kama utakavyoona, sakafu ile ya BUNGE ni takatifu kwa maana kamili ya neno hilo. Huwezi kutumia patakatifu kufanya uovu na ukaachiwa tu, labda kama sasa hapo kuna 'kundi la shetani' tu. Hiyo ni hoja ya kwanza muhimu ambayo nilidhani wasomaji wako tulitamani tuone kuwa nawe umeiona bayana.

Sasa, hoja ya pili ni uhuru wa mtu yeyote kusema chochote, alimradi havunji sheria. Mh. Mnyika ana haki na mtazamo na tafakari yake, hata 'quantification' yake. Kama asingekuwa amegoma kufuta usemi ule akiwa BUNGENI, ningetoa mawazo yangu kuhusu hayo matamshi. Kwa sasa ninasita kuendelea ili nisimpe uhalali, akiwa MBUNGE, kuvunja sheria bila kuadhibiwa.
Kwa kweli ninasubiri kusikia KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE, chini ya Spika, itatoa adhabu gani chini ya mipaka ya sheria ya uhuru wa MBUNGE akiwa BUNGENI (katika sakafu takatifu).

Wasalaam.
 
Dar City
Ni vigumu kutokubaliana nawe walau kwa asilimia chache juu ya hamsini. Kwa mapungufu ya tafakari ya Mjengwa, kwa nini isiwe ni uwezo wake unaotakiwa kuongezeka katika kuzamia hoja, na madhara ya hoja yenyewe mthili ya hiyo ya Mh. Mnyika? Hilo naona ndiyo tatizo letu kubwa sana tulio wengi. Umakini wa tusemayo kwa vinywa vyetu huupatia mtazamo wa haraka haraka .....

Tatizo la Maggid ni kujenga hoja na kisha kuziboa bomoa mwenyewe.

Katika makala hii, sina hakika kama imenisaidia mimi na labda wasomaji wengine kufikia hitimisho kama Kikwete ni Rais dhaifu au la.

I wishi mwandishi angekaa upande mmoja akaeleweka...naona anaendeleza mchezo ule ule wa Watanzania kutotaka kuonekana wabaya na hvyo kubaki wamekaa juu ya fensi!!
 
Maggid bado uandishi wako uko biased...

1. Unataka kuchora picture kuwa serikali ya awamu ya kwanza ilikuwa ya ki-dictator. Je, ni kweli hivyo ndivyo? Hizo ni harakati za kuunga mkono madai ya watu fulani fulani kwa sababu zao na zako pia. Hapa hujaeleza tatizo la nchi hii bado unazunguka kichaka ..

2.Kipanya cha Masoud pia kilikuwa kinapotosha ukweli wa chaguo la wa-Tanzania. Sisi hatuchagui beina ya Dictator na Dhaifu. Tunataka kuchagua serikali na rais mwenye (a) Kuwajibika (b) Hekima (c) si fisadi (d) asiyejihusisha na mtandao wa mchwa na mafisadi wa ndani na nje. Kwahiyo kipanya cha Masoud na makala yako ni mambo ya kujifurahisha tu na kufurahisha baraza.

3.Wewe kimsingi umeandika ili upate fursa ya kuramba viatu vya huyo rais dhaif Mh Dr Col (rt) JMKikwete. Umeokoteza sifa ambazo hata hivyo siyo sifa asilia. Mfano: Umesema kuwa Mh Dr Col (rt) Kikwete "amepanua uhuru wa wa-Tz kuchangia fikra zao bila hofu. Siku zote, hofu haijengi". Hapa unataka kudanganya watoto ili waende kulala. Mimi kwa mtazamo wa haraka naona hivi:

(i) Kikwete ameongeza uhuru wa kuongea majungu katika taifa
(ii) Kikwete ameongeza uhuru wa kuchafuana na kupakana matope
(iii) Kikwete ameleta mitizamo ya kidini na nchi inakoelekea ni kubaya sana kama hali itaendelea kubaki hivi siku zote
(iv) Kikwete wako ameleta ufisadi unaangamiza uchumi wa nchi na hawezi kuchukuwa hatua kudhibiti hali hiyo
(v) Kikwete ameongeza idadi ya safari kuliko rais yeyote aliyemtangulia. Bahati mbaya safari zake hazijaleta kitu chochote cha maana kubwa kwa nchi hii zaidi ya wawekezaji wa Richmond, Symbion na Waporaji wa ardhi yetu nk. Mwisho UWT wamechoka na safari zake wameanza kuiba mabilioni ya safari ili kumkwamisha asisafiri tena
(vi) Kikwete ameleta mtindo wa kutowa ahadi za uwongo kwa taifa hili
(vii) Kikwete amedhoofisha (a) CCM (b) Muungano (c) Serikali (d) Mfumo wa sheria na mahakama, na (e) Bunge

Kumtetea kiongozi wa jinsi hii janga kwa taifa na ufupi wa mawazo. Nimekusaidia kidogo tu...
Maggid ameeleza mtizamo wake binafsi nawe umetoa maoni na maeneo ambayo unaona yanasababisha JK asipate sifa za Maggid,hapa ndo raha ya mjadala.
Binafsi kama nilivyochangia mwanzoni naafikiana na Mjengwa kuhusu udhaifu wa mfumo lakini nisaidie kuchangia katika uliyogusia.
Kikwete ndiye Rais ambaye ameteua Majaji wengi kuliko Rais mwingine yoyote,je hapo amebomoa au amejenga mfumo wa mahakama?
Kikwete ametoa uhuru mkubwa mno wa kutoa maoni,baba zangu aliwekwa rumande kwa kuhoji ujenzi wa shule na alichukuliwa kama mpinga maendeleo.BWM alitoka povu wakti wa kujadili report ya Jaji Kisanga na watu tukafikia hatua ya kumshauri Kisanga atangaze kujiuzulu kwani ulikuwa udhalilishaji wa wazi,unaikumbuka hiyo?
Katika utawala huu tumeona untouchables wakipanda karandinga la Polisi, member wa Saigon club (kaitafue hii) akisimama Kisutu Mahakamani.
Kwa wana CCM (mimi si mmoja wao) inabidi wamshukuru sana kwani anajua ku pre empty,angalia suala la katiba mpya.Tungekuwa na mhafidhina hii ingekuwa issue ambayo si ajabu damu ingeshamwagika na kwa mtindo huu CCM itaendelea kwa muda.
Nakiri ana mapungufu kama binadamu lakini mfumo una mapungufu zaidi.
Tuendelee kujadiliana.
 
Walioiba pesa za EPA wazirudishe by J Kikwete Dhaifu. Hebu Jifikirie umeiba pesa bado unaombwa uzirudishe kama sio Udhaifu ni nini?

KIKWETE NI DHAIFU HAFAI HATA KUWA MJUMBE WA NYUMBA KUMI MTU KAMA HUYU.
 
hakuna haja ya kutafutana uchawi. Kama jk ni dhaifu,hiyo ni kwa sababu watanzania ni dhaifu. Maana watu dhaifu huchagua raisi dhaifu kuongoza nchi dhaifu.
 
Maggid ulivyosema ni sawa. Lusinde, Lema, Wassira, Heche, Slaa, Nape, Nassari, Lowassa na sasa Mwigulu na Mnyika ni typical vuvuzelas.
Mianasiasa ya Tanzania haina respect wala uelewa, sisi watanzania hatutaki ugomvi fanyeni kazi mafala nyie!!
 
Maggid ameeleza mtizamo wake binafsi nawe umetoa maoni na maeneo ambayo unaona yanasababisha JK asipate sifa za Maggid,hapa ndo raha ya mjadala.
Binafsi kama nilivyochangia mwanzoni naafikiana na Mjengwa kuhusu udhaifu wa mfumo lakini nisaidie kuchangia katika uliyogusia.

Kikwete ndiye Rais ambaye ameteua Majaji wengi kuliko Rais mwingine yoyote,je hapo amebomoa au amejenga mfumo wa mahakama? [COLOR="#FF0000[B]"]- AMEIMARISHA[/B][/COLOR]

Kikwete ametoa uhuru mkubwa mno wa kutoa maoni,............. - SAHIHI KABISA, WENGINE NDIYO WAMELEWA

Katika utawala huu tumeona untouchables wakipanda karandinga la Polisi, member wa Saigon club (kaitafue hii) akisimama Kisutu Mahakamani. Ha ha ha haaa

Kwa wana CCM (mimi si mmoja wao -POLE SANA) inabidi wamshukuru sana kwani anajua ku pre empty,angalia suala la katiba mpya. - KUONGOZA NI KUONA NJIA

Tungekuwa na mhafidhina hii ingekuwa issue ambayo si ajabu damu ingeshamwagika - NAKUBALIANA NAWE

........ na kwa mtindo huu CCM itaendelea kwa muda. - TUKIFANYA KAZI YA KUMSAIDIA JK NA SIYO KUMLEMBA LEMBA KWA UONGO NA KUJIPENDEKEZA KWAKE.

Nakiri ana mapungufu kama binadamu (KAWAIDA) lakini mfumo una mapungufu zaidi (YAANI SOTE, TUKIRI HILO).

Tuendelee kujadiliana.

Nimechangia kwenye hizo colored and underlined text
 
kilichotufanya tufike katika hali tulionayo sasa ni pamoja na haya yafuatayo;
  1. vita vya kagera.
  2. harakati za uhuru kusini mwa afrika.mfano Msumbiji.
  3. Misukumo kutoka nje na ndani ya nchi iliyosababisha kuvunjika kwa azimio la arusha.mfano IMF,WB nk.
  4. Utandawazi ambao umesambaratisha mfumo mzima wa kijamaa na kuzalisha matabaka ndani ya jamii.
  5. Mdororo wa Uchumi duniani,Mabadiliko ya Uongozi na tawala katika nchi za Arabuni.
  6. Mabadiliko ya tabia nchi na huaribifu wa mazingira.
  7. Kumomonyoka kwa maadili kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
  8. Majonjwa hatarishi.
  9. Ubinafsi miongoni mwa wenzetu wachache.
  10. Uvivu wa kutokuwajika na tabia za kuchagua kazi.
Hivyo kwa tafsiri yangu si udhaifu wa President JK bali ni mfumo mzima katika dunia ya leo ambapo kila uchao nchi zinatafuta njia mbalimbali za kujinasua kiuchumi,kiutamaduni hata kisiasa.mfano Ugiriki
Hivi leo hii President akiamua kuwa dikteta sidhani kama tutafika mbele ya safari kwani wapo wanaoomba awe dikteta
hili watumie mwanya huo kuleta maasi,vurugu na hata uporaji.Ni vema kila awaye yoyote kuwa na moyo wa kiasi.
 
Mwenyekiti hapa sikubaliani nawe UDHAIFU NI UDHAIFU.Tusitake kuutafutia maana nyingine!Kama mlalahoi yuko hoi na dhaifu kiafya kutokana na hali ya nchi duni ya kimaisha na lishe duni na mlo mmoja,pamoja na sababu kibao haibadirishi ukweli ya kua mtu huyu kiafya ni dhaifu! Hivyo Mh.JK tusijaribu kupotosha UDHAIFU mwingi unatokana na maamuzi yake yasioridhisha katika mambo mengi.

Swala la Ufisadi.kutowajibika kwa watendaji wake,rushwa na kua na kwikwi katika kutatua matatizo mengi ya kero za wananchi.Mfano mzuri ni jinsi alivyolishughulikia swala la EPA n.k.Hapa kuna swala tunalopashwa kuliona tupende tusipende,katika uchaguzi wa mwaka 2010 Kikwete alikua kwanza chaguo la MAFISADI kabla ya kulazimisha kua chaguo la Watanzania na wakatumia michezo michafu na fedha nyingi(Ambazo kwa bahati mbaya ni pesa zetu)Kumpamba na kufanya tuamini ya kua yeye ndiye chaguo la kweli.


Umafia wa mafisadi wanamalengo yao kuiba rasilimali zetu na ili uibe rasilimali zetu lazima utafute kiongozi"DHAIFU"Hivi ndivyo ilivyotokea kwa JK ambae mpaka sasa hajafanikiwa kujinasua katika mtego huo.Mfano mzuri wa mtu alieweza kujinassua katika mtego huo ni Rais wa sasa wa Urusi na aliekua rais wa nchi hiyo hapo kabla,ambapo mafisadi walimchagua na kumweka madarakani mtu ambae hakua anafahamika na wa katumia pesa nyingi ili kuingia madarakani Rais Vladimir Putin wakitegemea ya kuwa watamdhibiti wakidhani ya kua ni dhaifu.

Lakini alipoingia madarakani akawageuka na kutaifisha mali zao na wengine kuishia magerezani waliofanikiwa wakaikimbia Nchi.Kwetu hilo alikutokea Mh.JK alimeza ndoano ya mafisadi na wanaendelea kumkokota wanavyotaka hii NDIYO SISI YA UDHAIFU WAKE! SIO YEYE ANAEONGOZA NI MAFISADI WANAONGOZA NCHI YETU.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

 
Yote yanayosemwa sasa kuhusu serikali na viongozi wake ndiyo yatakayoisaidia Tanzania kuendelea. dialectical materialism inahusu migongano katika jamii yaani ndani ya maisha ya watanzania kwa sasa kuna pande mbili zinazokinzana; thesis na antithesi ambapo kitakachotokea ni synthesi yaani mfumo mpya na hatua mpya ya maendeleo. Huenda Mnyika amekuwa too radicle about kikwete. kusema kweli si kikwete as an individual bali ni tassisi nzima.

Huwezi kusema Kikwete ni dhaifu moja kwa moja au hana udhaifu wowote. this depends on the side of the arguer. Kikwete ameruhusu hayo na yeye hajapiga kelele kwa vile yenajua hayo hayana budi kutokea.


Ninaloweza kusema kwa sasa ni kuwa ingawa watu wanamsema sana kuna wakati watakuja kumkumbuka pia kwa yale mazuri. Hakuna Raisi hata mmoja ambaye hajawahi kusemwa vibaya hapa tanzania Tena Nyerere alisemwa sana hata akaitwa mchonga meno sasa ni baba wa taifa. KUNAPOTOKEA MAPUNGUFU KATIKA NHI NI LAZIMA KIONGOZI ATABEBESHWA MZIGO. MAPUNGUFU NI MENGI KWA SASA SHIDA NI NYINGI UNADHANI RAIS ATAACHA KUSEMWA?
 
Ndugu yangu Nderingosha,

Mosi, mimi nina safu kwenye Raia Mwema tangu toleo namba moja. Pili, inashangaza kuwa unaongelea Raia Mwema wakati husomi Raia Mwema. Na haya unayosema hapa huenda umesukumwa na chuki binafsi. Ni tatizo lako.

Maggid

Well said, well done Mkuu Maggid, mimi nimesoma post yako na mapendekezo yako ya kujenga wala sioni kama kuna kitu umekosea au eti "unajipendekeza!!" wakati mwingine ni vigumu kuelewa kama watu wanatatizwa/kasirishwa na mfumo au wana chuki binafsi tu na muhusika, kwa nini hawataki kuzungumzia vitu +ve ambavyo JK ame-contribute katika awamu yake; nakubali naye ni binadamu kama sisi tulivyo, ana mapungufu yake lakini tusiya-blow out of proportion as if awamu za viongozi walio pita ilikuwa ni holly.

Waingereza usema kama huna jambo jema la kuzungumza kuhusu binadamu mwenzako, basi ni kheri ukae kimya au umseme kwa kumpa ushauri ajirudi.

Mimi natoa RAI kwa Watanzania wenzangu, tunacho takiwa kufanya ni kumpa moyo JK na kumshauri kwa nia njema na siyo kutumia hira na kuanza kukuza kuza mambo mengine ili dunia imuone kama ni liability kwetu, sio vizuri kujaribu kumkatisha tamaa. Hivi tujiulize ni kiongozi gani aliwahi kumfikisha mahakamani Mawaziri au katibu mkuu, kutema rafiki yake wa karibu, kukubari mawaziri wajihuzuru - kwani unafikili angekataa nani angemlazimisha?

Katiba yetu imempa mamlaka ya kuwa Dikteita wa kutupwa kuliko alivyo kuwa STALIN, lakini mimi sijawahi kuona Jakaya anatumia rungu yake HIYO kutoka ndani ya katiba, kwani unafikili anaogopa RAIA?

Mwisho nisema hii tabia iliyo jengeka ya kuwaona watu ambao wanatoa maoni tofauti kuhusu JK, wana hukumiwa kwamba wanajipendekeza kwake sio tabia nzuri hata kidogo - kila mmoja wetu analitakia mema TAIFA letu, haya mambo kwa mfano: yakumpa Jakaya a tall order ya kuwavurumisha watu mahakani/kuwafunga kwa kutumia hisia tu bila ushahidi litavuruga nchi na hakuna ambae atasalimika.

Juzi hapa niliona watu wanazungumzia mambo ya EPA kwa hisia kali wanasema kwa nini JK anawasamehe walio kubari kulipa DENI? Mambo ya ajabu kabisa: Hivi mtu ukikopa fedha mwisho wa siku anapashwa afanye nini hata ukimfikisha kwenye vyombo vya sheria - atahambiwa arudishe fedha alizo kopa, basi! Akishindwa ndio anafungwa au anafilisiwa, je hawa walio kopa hela kutoka EPA (bila kujali mbinu walizo tumia kukopa) si majina yao yanajulikana?

Sasa JK alikosea nini kusema rudisheni hizo pesa la sivyo? Lakini watu wenye agenda zao watataka dunia imuone JK ndiye muhusika namba moja!!! Je wakini Maranda walifikishwa mahakamani kuhusiana na jambo gani? Nani kasema mkono wa sheria utahishia kwa watuhumiwa hao peke yao, mambo mengine tuwe na subira.
 
Maggid ulivyosema ni sawa. Lusinde, Lema, Wassira, Heche, Slaa, Nape, Nassari, Lowassa na sasa Mwigulu na Mnyika ni typical vuvuzelas.
Mianasiasa ya Tanzania haina respect wala uelewa, sisi watanzania hatutaki ugomvi fanyeni kazi mafala nyie!!

MHESHIMIWA MBONA NA WEWE unatukana. hata mavuvuzela pia yana umuhimu wake pale mechi inapopamba moto. siasa za tanzania zimepamba moto pia lazima wawepo watu wa aina hiyo lakini kutukna c vema wacha wananchi waseme maana wangewakataa wasingefika mbali hivo kuwatukana pia unatukana wananchi
 
Back
Top Bottom