Udhaifu na changamoto kwa wafanyakazi

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Wanajamvi

Vijana/wafanyakazi wengi wengi mofisini iwe serikalini, makampuni binafsi tuko kwenye nafasi za kati au chini kitendaji.Lakini kuwa katika level ya chini ya utumishi au kazi haimaanishi huwezi kuwa kiini au chanzo cha mabadiliko.

Kumekuwa na tatizo moja la sisi vijana/wafanyakazi kukaa na mawazo, maoniau mapendekezo yetu kichwani tu, au kuyasema sehemu isiyotakiwa bila jitihada za kuwashauri wahusika. Huu ni udhaifu

Hata mimi nilikuwa nao lakini toka nimebadilika nimegundua kitu. Ndio maana naleta hii mada kama changamoto kwetu sisi wafanyakazi mahali popote tulipo

Mfano kampuniXYZ kitengo DDD tuko vijana wane na watu wengine wa umri mkubwa pamja Incharge ambaye ni mtu wa makamu. Kuna tatizo wote fulani wote na wote tumeliona lakini hakuna kati yetu aliyewai kushika kalamu na kuandika dokezo/ memo lenye kutoa pendekezo au Idea kwenda kwa incharge wetu . Hatukuwai kumshauri kwa offfcial communication channel. Mara chache tuliliongea katika informa/Unofficial communication channel(mdomo) kati yetu na Incharge. This was never documented.

Tatizo lingine ni kusikia maneno wafanyakazi wengine wasio kuwa creative. Ukiwapa wazo kuwaambia unataka kumwandikia incharge/ boss kitu fulani wanakuambia “ahhhhhh unajisumbua yule hasikilizi ushauri wa mtu.” Mwisho wa siku unakuta una kitu unataka kupendekeza tena kizuri tu lakini kwa sbabau umekatishwa tamaa unatulia unaendelea kudeal na mambo kama ulivyoyakuta.

Tusifanye assumption kuwa Boss/incharge Fulani yuko hivi tena in a –ve way. Jaribu ku prove kwa ku document mawazo yako.

NB:
Wazo lako kukataliwa au kutofanyiwa kazi sio sign ya fauliure wala weakness.

Haya ni baadhi ya maneno aliyoniambia incharge wangu. Baada ya kudocument views zangu na kuziwassilisha kwake. Nilishangaa response niliyopata tofauti na niliyokuwa nasikia na kuambiwa juu yake.

Changamoto za kujiuliza vijana/wafanyakazi wenye mawazo mapya

  • Je umewai kuandika official memo kwa incharge au boss wako ya kutoa pendekezo, ushauri au wazo fulani.? If no Why?


  • Je kutokana na postion au majukumu yako kiofisi unadhani yako unadhani hakuna mabadiliko yanayotakiwa.?Umefanya nini?

Tusisubiri change zitoke juu. Hata maboss/ ma incharge wetu watatushukuru tukiwasaidia kuona mabadiliko chanya yanayotakiwa. Kwa hili hatutakiwi kuogopa hata kama utaonekana unajipendekeza.

Wahasibu, madereva Masecretary wa kizazi kipya wote tuna mchango na nafasi wa kuwa chanzo cha mabadiliko katika ofisi tunazofanya kazi.

Kwahiyo sisi wafanyakazi na vijana tujitambue ni sehemu ya tatizo maofisini, makazini na vibaruani.

Nawasilisha kwa mjadala
 
Jamani ehee tuwe tayari kujikosoa pia. na kutammbua mapungufu yetu .Sisi sio malaika wala hakuna aliye perfect.Katika kazi zetu za kila siku what are our weaknesses.
 
Back
Top Bottom