UDA Scandal Files: Part I (Revealing)

Ki ukweli kama tungekuwa tuna sheria kali na kuzisimamia ipasavyo I don't think kama mambo ya kijinga kama haya yangekua yanatokea, I wish to be a Sniper!
Its very intersting seing people wanna be me.....
 
Huo unyanganyi ukitaka laana yake tambua ya kuwa inaanzia mbali sana Invisible

Na hii ndo shida ya Uhuru wa kugeiwa na wakubwa.
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu hawakawii kusema aliyeiuza UDA kihuni huni ni Nyerere maana wao wana usafi wa malaika...anayedhani amesimama aangalie asianguke, PERIOD!
 
Tumetoka huku kwa wanaojadili vitu kama ni vipya vile. JK alisema za kuambiwa changanya na zako.
 
ccm bila kuomba msamaha kwa udhulumati mlioufanya Tz hii dhambi ya udhulumati huu itawaandama mno na kuwatafuna.
Msione aibu, simameni mbele ya 'madhabahu' na muombe msamaha kwa kukiri ile dhambi na kuijutia.
 
Nikiona leo hadi Machadema wanaungana na "watu" fulani na kusema walikuwa safi unaweza kuzimia kabisa. Watu wakiamua kurudisha yale madudu mbona tutakimbiana humu.
 
Kuna taarifa za uhakika kwamba Robert Kisena alikwenda kwenye ofisi za UD na askari wa Ultimate Security na kuvunja milango kuchukua ofisi baada ya kukataliwa na bodi kukabidhiwa shirika hadi atakapokamilisha malipo. Polisi waliarifiwa na kukamata waliokutwa wakivunja milango wakiwamo askari wa Ultimate. Baadae Robert akaenda polisi kuwawekea dhamana ndipo na yeye akakamatwa. Alipokamatwa mchezo ndio ukaanza maana alitolewa na yeye kuwadhamini wenzake na kutoka polisi moja kwa moja wakaenda tena UDA kuchukua ofisi.

Consolidating Holding Corporation CHC ambao walikuwa wakisimamia uuzwaji wa UDA wakabaini kuwapo jinai katka tukio hilo ikiwamo kuvunja milango na pia kuona kuna forgery katika barua aliyodai Robert imetoka UDA ikimuelekeza kupeleka fedha kwenye akaunti ya Mwenyekiti. Cha kushangaza hakuna hatua zilizochukuliwa kuhusiana na jinai hizo hadi sasa.

Jambo lingine ni kwamba CHC hadi sasa wanashangaa kuona kwamba waliingia mkataba na Simon Group February 2011 na kutoa ratiba ya malipo kwa ununuzi wa hisa na malipo ya awali yalikuwa hizo milioni 280 ambazo zililipwa vyema. Simon walitakiwa kulipa malipo ya pili kabla ya kukabidhiwa shirika na baadaye malipo ya tatu yangelipwa kwa awamu lakini ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Kwa maelezo hayo CHC na menejimenti ya UDA ikashangaa imekuaje Simon wadai kwamba walilipa fedha za mkupuo wa pili mwaka 2009 kwenye akaunti ya Mwenyekiti wakati mkataba ni wa mwaka 2011 na malipo ya awali yalilipwa mwaka 2011 inakuaje ya pili yalipwe kabla ya hata mkataba haujasainiwa? Hiyo jeuri ya kusema hayo maneno Simon wameipata wapi? Unless tunapata maelezo mengine mapya na yenye maelezo ya kina, tunashawishika kuona kwamba hapa hata wabunge wetu akiwamo Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Haule Filikunjombe, walikurupuka na walipaswa kuchunguza kwanza kabla ya kutoa tamko linalotuhumu watu na linaloonyesha kumtetea Simon kana kwamba alionewa.

Kwa kweli ni vyema Bunge likachyukua hatua za makusudi kujisafisha ili tusiendelee kuona yaliyotokea kwenye Kamati ya Mrema kule Tanga baada ya Kafulila kuibua kashfa ya rushwa na ya Jairo pamoja na mengine ambayo kwa kweli si vyema chombo nyeti kama Bunge kikapoteza uaminifu wake kwa jamii. TUNALIAMINI BUNGE NA WABUNGE WENGI na ni vyema wale wachache wakadhibitiwa.
Tulikuwa huku .... soma hili andiko la Halisi
 
Since the story of UDA became part of public discourse, there has been a lot of confusion as to the true facts of what happened. In the process, the truth became a victim of politics. This document you see here is part of an effort to put the facts out there for the public record ahead of political posturing. Hopefully, as a consequence, a rational, non-reactionary conversation about this issue can emerge...

NOTE: This' just part I, follow the series...


UDADocs_2Themeetingdissolvingtheboard_Page_1.jpg


Aiseee
 
Sasa hapa Simon Group wanahudhuria kama nani wakati hawajakabidhiwa rasmi na inakuwaje wakati bado kuna utata kuhusu malipo maana hata baadhi ya doccument alizotumia Simon Group ni forged?

Those days......
 
Hebu tujikumbushe jinsi Meya wa jiji la Dar es Salaam alivyopatikana. Wagombea ubunge wa Dar es Salaam kupitia CCM walikua wakienda kuunga foleni na wagombea udiwani wao kusubiri laki tano bila aibu na sasa matokeo yake ndio haya na itafuatia sasa Coco Beach ambayo Masaburi atataka anayeendesha anyang'anywe apewe Manji.

Tusisahau Yussuf Manji ni mmoja wa wafanyabiasharawaliokua wakitaka kuinunua UDA na hajakata tamaa hadi sasa na hata huyo Simon Group asidhani yuko salama kwa hili hata kidogo na tayari kuna dalili atakosa na Manji ataichukua UDA kiulaini.

Yusuf Manji 'anunua' madiwani Dar

• Amwaga 500,000/- kwa kila mgombea


na Betty Kangonga Tanzania Daima jumatano, 22 septemba 2010


MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuph Manji, anadaiwa kuwahonga fedha wagombea wa nafasi za udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuhakikisha wanamchagua mmoja wao kuwa meya wa Jiji la Dar es Salaam, kuziba nafasi ya Adam Kimbisa, aliyemaliza muda wake.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya duru za CCM, vilidai kuwa mfanyabiashara huyo amekuwa akigawa sh 500,000 kwa kila mgombea udiwani wa CCM ili kuhakikisha mtu anayempigia chapuo, anashika nafasi hiyo nyeti jijini Dar es Salaam kwa masilahi yake binafsi.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata zilisema kuwa mbali ya kutaka mtu wa karibu yake apate nafasi ya umeya wa jiji, pia anadaiwa kuwasaidia baadhi ya madiwani kushinda nafasi za umeya wa halmashauri za wilaya za jijini Dar es Salaam.

Habari zinasema kuwa Manji amekuwa akiwapata wagombea hao wa udiwani kupitia baadhi ya wagombea ubunge wa majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam ambao wamekuwa wakionekana katika ofisi za mfanyabiashara huyo mwenye asili ya Kiasia.

"Huwezi amini ninachokisema, kama unataka fika ofisini kwa Manji, utashuhudia haya ninayozungumza. Kuna msafara wa foleni utafikiri kuna mkutano ndani ya ofisi hizo, kumbe watu wanachukua pesa," kilisema chanzo hicho na kuongeza kuwa ameahidi kuwapa zaidi awamu nyingine.

Baadhi ya wagombea udiwani waliopata fedha hizo ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sasa, walilithibitishia Tanzania Daima Jumatano kupokea fedha hizo na kuongeza kuwa sambamba na fedha hizo, Manji amewapa majina ya watu wanaofaa kuwania umeya wa jiji na halmashauri za wilaya.

Hata hivyo hatua hiyo imelalamikiwa na baadhi ya wana CCM kwamba si ya kiungwana na haipaswi kuvumiliwa kwa kuwa inavunja demokrasia nchini.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia ya simu, Manji kwanza alihoji chanzo chetu cha habari hizi. Hata hivyo mfanyabiashara huyo baadaye alikiri kutoa fedha hizo.

Alisema amekuwa akitoa fedha hizo mbele ya baadhi ya wagombea ubunge wa CCM wa majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam na amekuwa akifanya hivyo kutokana na mapenzi yake kwa CCM.

Alisema mara nyingi amekuwa mstari wa mbele kusaidia wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa CCM kwa ajili ya kuhakikisha wanashinda nafasi nyingi za uongozi na kuvibwaga vyama vya upinzani.

Alifafanua kuwa katika ugawaji wa fedha hizo, wapo baadhi ya wagombea wa udiwani ambao hawakufika katika mgawo huo, lakini aliwaomba wasubiri mpaka atakaporudi kutoka katika safari yake anayotarajia kuondoka leo. Hata hivyo hakufafanua.

"Sioni tatizo kutoa fedha kwa ajili ya chama changu ili kipate ushindi wa kishindo. Ni kweli nilitoa kiasi hicho cha fedha lakini sikuwa peke yangu, nilikuwa na wagombea wa nafasi ya ubunge ambao ndio walifika na madiwani na nikaahidi awamu ya pili nitawapa baada ya wiki mbili nikitoka safari," alisema Manji.

Hata hivyo alikataa katakata kwamba wakati akiwapa fedha hizo hakutoa majina yoyote ya watu anaotaka wawe mameya, ingawa wapo baadhi yao waliomuomba awasaidie ili waweze kupata nafasi hizo.

"Siwezi kukataa, ni kweli najua baadhi ya wagombea udiwani ambao wamekuja kwangu na kuomba niwasaidie fedha kwa ajili ya kupata umeya, lakini nitakuwa si mzalendo iwapo nitaamua kuingilia suala hilo, kwa kuwa hata hiyo nafasi ya udiwani wanaweza wasishinde, sasa itakuwaje wapite kwenye umeya?" alihoji Manji.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa (CCM), Yusuf Makamba, alisema taarifa hizo ndiyo kwanza anazisikia, lakini kamwe chama hakimkatazi mwanachama wake kukichangia, ili mradi afuate utaratibu uliowekwa.

Hata hivyo Makamba aliwashangaa wagombea udiwani wanaohangaika kusaka viti vya umeya wakati hata Uchaguzi Mkuu haujafanyika.

"Hii taarifa inatia aibu. Hawa wagombea wanachekesha sana, maana wanaamini vipi watashinda nafasi hizo wakati hata uchaguzi bado? Utaratibu wa kugombea umeya unafahamika, ukifika wakati wake watatangaziwa wachukue fomu," alisema Makamba.

Eti eeeh
 
Duh! kweli bongo tambarare, kwa namna sakata hili lilivyokuwa linaendelea ilikuwa rahisi kufikiri haya mambo yalikuwa ni kati ya bodi ya wakurugenzi UDA na Dar City Council.

Lakini ukisoma hiyo barua ya SGL kopi zilipelekwa kwa Waziri wa fedha na katibu mkuu wake, waziri wa uchukuzi na katibu mkuu wake. That means walikuwa wanajua na pengine walishakatiwa chao mapemaa otherwise hao vigogo muda wote huu wamefanya ufuatiliaji upi kuhusiana na hili sakata????

Barua ni ya tarehe 16/06/11 na the deal has been on at least by115 days before that date. Hivyo basi kisingizio cha kutokufahamu ni kichekesho!!!!!

Hatari sana
 
Nimezisoma documents zote naweza kusema kitu kimoja kuna mtu behind Simon Groups aliyekuwa anasuka mpango wa kuchukua UDA jumla. Simon haikuwa na haki ya kuitwa mwanahisa kwani hadi Juni, 2011 haikuwa imelipa senti tano ya hisa walizokuwa alloted zilizokuwa na thamani ya zaidi ya Tshs 200 milioni. Sasa Simon ilikuwa kama nani katika mkutano huo batili wa extra ordinary meeting???

Pia nakubaliana na mwanasheria Lyimo kuwa Dr Masaburi alitakiwa atoe kibali kilichomruhusu kuitisha mkutano huo kutoka kwa macouncilor wa jiji la Dar-es-Salaam. Dr Masaburi haongozi shirika lake binafsi ni Meya wa jiji na hivyo alitakiwa kupata kibali kutoka kwa councilor wa jiji kuitisha hicho kikao tunaomba atuambia hicho kikao aliitisha lini na kwa nani? Bila ya hivyo hakuwa na mandate ya kuitisha kikao cha wadau wa uda.

Tatu kuiengua bodi kunatakiwa ruhusa ya majority shareholders or shareholders approval. Simon walikuwa hawana shares mpaka walipoitisha kikao chao na hivyo shareholders wa mwanzo bado ndio walikuwa wamiliki halali je ni kina nani na kwanini hawakushirikishwa. Na sheria ya Company law inasema ni muhimu minority shareholders washirikishwe katika maamuzi hayo je kwanini hawakushirikishwa?

Kunaonekana kuna mchezo mchafu ulikuwa unataka kutokea wa kubandika na kubandua watu wameshaanua matanga na kuendelea na shughuli zao. Dr Masaburi hapa amechemka namuonea huruma kama hizi document ni authentic!!! Shukrani Invisible na bado tunasubiria zile Trilioni 3 sijui Trilioni 7 kwani kila mmoja mjini anazungumzia lake nakuaminia sana mkuu.

Hatari sana
 
Back
Top Bottom