UDA Scandal Files: Part I (Revealing)

Hata hivyo tumechoshwa na habari za skendo za rushwa. Hakuna muda wa kutosha wa kujadili watu wamepanga nini, wameiba sh ngapi n.k. Huu ni muda wa kujenga taifa letu changa lililokwama kwenye wimbi la umasikini.
 
GreatThinkers,
Ahsante sana Invisible kwa kutupatia hekima yako.
Nchi yetu imemalizwa mara kibao na huyo huyo jamaa, unakumbuka ishu ya million 900 aliyoitoa Lyatonga miaka ya Tisini??
I-Simb ni watu hatari sana wanaojifanya wazawa.
 
Hata hivyo tumechoshwa na habari za skendo za rushwa.
Kweli mkuu maana rushwa hizi ndizo zimepelekea umasikini wa watanzania na hata kukata tamaa kwa watanzania walio wengi hata kufikia kukosa imani na serikali yao.
Hakuna muda wa kutosha wa kujadili watu wamepanga nini, wameiba sh ngapi n.k. Huu ni muda wa kujenga taifa letu changa lililokwama kwenye wimbi la umasikini.
Dah, umejichanganya mkuu, hahaha... Wizi unaokataa usisemwe ndio umeletezea umasikini unaotaka kuukomboa.

NOTE:
Wizi hauna chama mkuu, mnapojaribu ku-divert attention (kupoteza watu kwenye discussions) angalieni vema msichanganye. Bado ninaamini una uzalendo ndani yako, hapa hoja si CCM vs CDM!
 
DSCN1888.JPG

Idd Simba

Duh! Idd Simba naye huwa anaonja onja???????????????????
 
Ki ukweli kama tungekuwa tuna sheria kali na kuzisimamia ipasavyo I don't think kama mambo ya kijinga kama haya yangekua yanatokea, I wish to be a Sniper!
 
Hata hivyo tumechoshwa na habari za skendo za rushwa. Hakuna muda wa kutosha wa kujadili watu wamepanga nini, wameiba sh ngapi n.k. Huu ni muda wa kujenga taifa letu changa lililokwama kwenye wimbi la umasikini.

Tulijenge huku wengine wanalibomoa, tena mbaya zaidi ni wale ambao watu wamewaamini na kuwachagua kuwa viongozi.

Dude u must be joking.
 
swali dogo tu,hv ni nani ataunganisha dot na kuchukua hatua kwa mafisadi? Uchafu hauchafuki! Hawa wameshazoea kelele zetu,jioni wanakutana kugonga glass na kutukebehi kuwa kelele za mlango.......?
 
sasa hapa kuna ishu gani? Tayari tunafahamu kuwa hao simon group wamekuwa major shareholderz!

Hizo ni minutes za mkutano wa shareholderz! Ungeleta mkataba or certificates ya hizo share ambapo kwenye hizo certificates kumeonyeshwa vitu vya muhimu kama price per share ndio ningeona umefanya cha maana!
we ni mseeela kweli, unafikiria na meya wa dar
 
Ukiangalia na kufatilia kiundani hii nchi kuna kikundi cha watu wachache sana wanayoitafuna barbara, kila deal zinazotokea majina ni yaleyale yanajirudia, Lakini kuna maswali machache ambayo Watanzania inatupasa kujiuliza
1) Kazi hasa Ya Usalama wa Taifa ni nini hasa? mimi nadhani hivi vitu vyote vinavyotokea wanavijua na wanavifanyia report, sasa ikitokea utekelezaji wa ripoti zao haufanywi wao kazi yao ni kukaa kimya na kuacha nchi iyumbe?

2) Hivi ni kweli Watanzania Hatuna Solution nyingine/Mbadala ya kusolve haya matatizo zaidi ya kuhabarishana kwenye mitandao na kilamtu anaondoka anasonya? Hiyo ndio hatua yetu ya mwisho kabisa

3) Kitu cha Muhimu kwa sasa kwaWatanzania sio kugombea uraisi bali ni kuitoa CCM madarakani kwa NJIA YOYOTE ILE, Tanzania inapaswa kuzaliwa upya, Chadema na watu wote wenye kuitakia mema hii nchi hebu unganeni kwenye hili la kuikomba Tanzania, Ukombozi wa Tanzania ni wamuhimu zaidi ya Siasa, Ukombozi unaanzishwa na Mtu mmoja, Watanzania tunasubiri kauli kama za Mh Lema zenye kutia HAmasa na uzalendo

SAA YA UKOMBOZI NI SASA
 
1. Kutokana na maelezo ya mwanasheria Simon Group wanamiliki 25% tu ya hisa kwakua hawajalipa kiasi kilichosalia cha hisa kwa muda unaokubalika kisheria.
2. Vikao vyote vilivyoitishwa na SG si halali kisheria.

Duuh hizi barua zimejaa spelling mistakes kibao..bongo bwana..!
 
Hata hivyo tumechoshwa na habari za skendo za rushwa. Hakuna muda wa kutosha wa kujadili watu wamepanga nini, wameiba sh ngapi n.k. Huu ni muda wa kujenga taifa letu changa lililokwama kwenye wimbi la umasikini.
Kila mmoja wetu kachoshwa na hizi habari za ufisadi, wizi na ujambazi lakini zinabaki kuwa muhimu kwa sababu ndizo zinalikwamisha taifa katika wimbi la umasikini. Wakati tunaleta fito ili tujenge taifa wenzetu wachache wanazitumia kama kuni kupikia chakula chao. Mwita 25 tuendelee kuleta fito au tujiulize kwanini wenzetu wanazichoma moto? na sijui kuna uwezekano gani wa kujaza maji ndoo inayovuja.

Ungejua ni kiasi gani kinapotea kwa wizi wa watu wasiozidi 20 ndani ya taifa hili, usingethubutu kusema hayo unenayo, swali dogo tu je ni haki watu 20 waibie watu milioni 40 na tukae kimya? Mwenzetu kama una habari njema za maendeleo ziweke hapa tuzijadili ndio utaifa wenyewe,lau kama huna ni kwanini huna na unataka tujadili zipi usizokuwa nazo wewe mwenzetu.

Hivi kujadili kuwa kwanini UDA ife na dala dala za watu binafsi zipate faida sio hoja ya maendeleo! Hebu tupe yako moja ya maendeleo isiyo na ufisadi ili tuichangie kidogo.

Ahsante
 
WanaJF,
nimezisoma documents vema tu, ninapokwazika kuchangia ni pale ambapo sijui mwenyekiti wa bodi ya UDA anapatikanaje. Nisadieni
 
Jana Masaburi (tena kwa ujasiri) alionekana kwenye vyombo vya habari akikagua majengo ya UDA, huku akitoa maagizo mbalimbali. Sijui anapata wapi huo ujasiri? Hata nasubiri kwa hamu kubwa kamati ndogo ya bunge itagundua nini na itatoa mapendekezo gani!
 
Back
Top Bottom