UDA imebinafsishwa ili iingie Biashara na DART - Siri ya kuuzwa Bei Chee

[h=3]Uuzwaji wa UDA watinga mahakamani[/h]
Na Rachel Balama (Majira)

KAMPUNI ya Simon Group imefungua kesi ya madai dhidi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na Consolidated Holding Coorporation kupinga kukatishwa mkakaba
baina yake na mdaiwa wa kwanza.

Kesi hiyo ambayo imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Biashara iliahirishwa jana ili kuona kama kuna uwezekano wa suala hilo kumalizwa nje ya mahakama.

Juzi, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Didas Masaburi alitangaza kuvunja Bodi ya UDA na kusimamisha uongozi wake kutokana na ubadhirifu wa mamilioni ya fedha, huku akiunda Kamati kuchunguza mkataba wa kuuziana hisa kati ya shirika hilo na kampuni hiyo.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Bishara, Bi. Agnes Bukuku, ilitajwa jana na kupangiwa tarehe nyingine ya kutajwa, Septemba 7, mwaka huu.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mahakama iliahirisha kesi hiyo ili kuona kama suala hilo linaweza kumalizwa nje ya mahakama kati ya mdai na wadaiwa.

Kampuni ya Simon Group imefungua kesi mahakamani ikiomba itamke kuwa yeye anastahili kumiliki hisa zote ambazo hazijatolewa za UDA na kuwa kukatishwa kwa mkataba baina yao ni kosa kisheria.
 
[h=3]Uuzwaji wa UDA watinga mahakamani[/h]
Na Rachel Balama (Majira)

KAMPUNI ya Simon Group imefungua kesi ya madai dhidi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na Consolidated Holding Coorporation kupinga kukatishwa mkakaba
baina yake na mdaiwa wa kwanza.

Kesi hiyo ambayo imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Biashara iliahirishwa jana ili kuona kama kuna uwezekano wa suala hilo kumalizwa nje ya mahakama.

Juzi, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Didas Masaburi alitangaza kuvunja Bodi ya UDA na kusimamisha uongozi wake kutokana na ubadhirifu wa mamilioni ya fedha, huku akiunda Kamati kuchunguza mkataba wa kuuziana hisa kati ya shirika hilo na kampuni hiyo.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Bishara, Bi. Agnes Bukuku, ilitajwa jana na kupangiwa tarehe nyingine ya kutajwa, Septemba 7, mwaka huu.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mahakama iliahirisha kesi hiyo ili kuona kama suala hilo linaweza kumalizwa nje ya mahakama kati ya mdai na wadaiwa.

Kampuni ya Simon Group imefungua kesi mahakamani ikiomba itamke kuwa yeye anastahili kumiliki hisa zote ambazo hazijatolewa za UDA na kuwa kukatishwa kwa mkataba baina yao ni kosa kisheria.

Hii kampuni ya SGL mmiliki wake anatokea Maswa?..Tajiri ambaye anayemiliki kiwanda, usafiri etc, swali ninalojiuliza je alinunua enzi za Chenge (Bariadi) akiwa waziri wa Ujenzi na Usafirishaji? kama SGL ina hisa kubwa na pia ilifuta bodi ya kwanza ni vipi Masaburi leo aivunje? je hapo hakuna mchezo wa kuandaa kesi ya makusudi ili SGL aje alipwe bure bure kwa mtindo ule ule wa Dowans? kati ya mdai na mdaiwa ni nani aliyeomba wakayamalizie nje ya mahakama?
 
Hii kampuni ya SGL mmiliki wake anatokea Maswa?..Tajiri ambaye anayemiliki kiwanda, usafiri etc, swali ninalojiuliza je alinunua enzi za Chenge (Bariadi) akiwa waziri wa Ujenzi na Usafirishaji? kama SGL ina hisa kubwa na pia ilifuta bodi ya kwanza ni vipi Masaburi leo aivunje? je hapo hakuna mchezo wa kuandaa kesi ya makusudi ili SGL aje alipwe bure bure kwa mtindo ule ule wa Dowans? kati ya mdai na mdaiwa ni nani aliyeomba wakayamalizie nje ya mahakama?

template yao ya ufisadi ni ile ile; wanaingia mkataba "kihalali" halafu wanazua zogo, wanadai mahakamani na kulipwa. Ni ile ile waliyotumia kwenye ATCL n.k
 
Kuna site moja inaitwa Adam Smith International (ASI). Kwenye site yao wanasema "ASI were engaged by the World Bank to develop and implement a privatisation strategy for UDA, the Dar es Salaam bus company." Kwa hiyo ina maana World Bank imehusika katika ku privatise UDA? Hii kampuni ina ofisi Uingereza, India na Kenya. Site yenyewe: Privatisation of UDA Bus Company | Adam Smith International

Maneno ya Zitto.

Reacting to the issue, the chairman of the Public Organisations Accounts Committee (POAC), Mr Zitto Kabwe, said [on 11 July] that the privatisation of UDA was being supervised by his parliamentary oversight committee. "As far as I know UDA has not yet been privatized. If there is any agreement purporting to show that the public transport firm has been privatised, that agreement is null and void," said Mr Zitto. The Kigoma North MP on the ticket of opposition Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) said the UDA board of directors had reportedly sold the unallocated shares without observing laid down procedures.

Maoni ya mtaalamu

An expert with privatisation of public firms wondered why the alleged new investor has illegally occupied the headquarter offices of UDA if there was a pending case in court, warning: "CHC should be serious in addressing this issue. The case was filed on December 22, 2010 and the investor forced himself into UDA offices on June 21, 2011, raising more questions than answers," said the expert who preferred anonymity lest he was reprimanded since he is a government official.
 
[h=3]Uuzwaji wa UDA watinga mahakamani[/h]
Na Rachel Balama (Majira)

KAMPUNI ya Simon Group imefungua kesi ya madai dhidi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na Consolidated Holding Coorporation kupinga kukatishwa mkakaba
baina yake na mdaiwa wa kwanza.

Kesi hiyo ambayo imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Biashara iliahirishwa jana ili kuona kama kuna uwezekano wa suala hilo kumalizwa nje ya mahakama.

Juzi, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Didas Masaburi alitangaza kuvunja Bodi ya UDA na kusimamisha uongozi wake kutokana na ubadhirifu wa mamilioni ya fedha, huku akiunda Kamati kuchunguza mkataba wa kuuziana hisa kati ya shirika hilo na kampuni hiyo.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Bishara, Bi. Agnes Bukuku, ilitajwa jana na kupangiwa tarehe nyingine ya kutajwa, Septemba 7, mwaka huu.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mahakama iliahirisha kesi hiyo ili kuona kama suala hilo linaweza kumalizwa nje ya mahakama kati ya mdai na wadaiwa.

Kampuni ya Simon Group imefungua kesi mahakamani ikiomba itamke kuwa yeye anastahili kumiliki hisa zote ambazo hazijatolewa za UDA na kuwa kukatishwa kwa mkataba baina yao ni kosa kisheria.

Compare hapo kwenye red na hii taarifa. Try to connect the dots.

Embattled UDA Boss Now Fears for His Life


The general manager of state-owned Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Mr Victor Milanzi, reiterated yesterday [26 Julai 2011] that the new investor in the public transport firm had 'invaded' the firm's headquarters at Kurasini without paying fully for the 51 per cent majority shareholding. He said Simon Group Limited, the new investor, only paid Sh285 million which was only 51 per cent of the 51 shares whose total value is Sh1.4 billion.

Mr Milanzi told a news conference in Dar es Salaam that the investor locked him out of his office last month with the help of the city's mayor, Mr Didas Massaburi. He said the mayor was cooperating with the owners of Simon Group Limited to tarnish his image because he was reluctant to let the new investor acquire UDA's majority shareholding as the company was yet to pay the required amount of money as directed by its board of directors. The government owns 49 per cent shares of UDA.

Mr Milanzi said he was receiving death threats through his phone from anonymous people, following the controversial privatisation of the state-owned firm, which has assets worth Sh12 billion."I received messages threatening me with death if I don't hand UDA's ownership over to Simon Group Limited," claimed Mr Milanzi adding that he had already reported the matter to the Chang'ombe Police Station. But when contacted by The Citizen through his mobile phone for comment, Mr Massaburi hung up his phone after the reporter introduced himself. Subsequent calls went unanswered.

However, during the press conference Mr Milanzi argued that the legal owners of the company could be Dar es Salaam City Council which has 51 per cent shares, followed by the Treasury Registrar with 49 per cent. The company was given four months to pay the second installment, but failed to do so, which consequently gave UDA management the power to forfeit money and sell the shares to another investor. "The mayor and owners of Simon Group Limited, who have a close link with a long-serving minister, held a meeting and made the decision without consulting a full council meeting," Mr Milanzi claimed. However, he called on councillors to take a bold action against the controversial ownership of the firm for the public's benefit.

Source: The Citizen
 
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, ameingilia kati mvutano ulioko kati ya Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi na Meneja wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Victor Milanzi, akisema hakuna mwenye haki ya kumnyooshea mwingine kidole, kwani wote wawili ni sehemu ya matatizo yanayolikabili shirika hilo.
“…wote wawili wameshiriki kwa kiwango kikubwa katika kukiuka sheria, kanuni na taratibu kwenye uendeshaji wa UDA bila kuzingatia kwa ukamilifu maslahi ya wasafiri na walipa kodi,” alisema Mnyika katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa kupitia mtandao wa kompyuta jana.


Amemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuchukua hatua stahiki za kuiongoza serikali kupitia upya mkataba ulioingiwa na kutekelezwa kinyume cha sheria, kanuni na maslahi ya wananchi kati ya Jiji, UDA na Simon Group Limited, kubatilishwa maamuzi yaliyofanywa na Dk. Masaburi na vikao vya Jiji na UDA, na kupitia upya maamuzi ya Bodi ya UDA kwa miaka kadhaa.
Pia Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuingilia kati kupitia Msajili wa Hazina na Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kunusuru hisa za serikali kuu katika UDA na mali zake, pia Kamati za Bunge za Miundombinu na ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ziingilie kati kwa kushirikiana na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mamlaka ya Kudhibiti Manunuzi ya Umma (PPRA) na wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam.


“Hatua hizo zitaokoa mali za umma, kuweka msingi wa kuboresha usafiri katika mkoa wa Dar es Salaam na kuwezesha hatua za kisheria na kinidhamu kuchukuliwa kwa wahusika wote waliofikisha Jiji na taifa katika hali hiyo,” alisema.
Alisema Dk. Masaburi na Milanzi, kwa nyakati tofauti walishiriki katika kuachia maamuzi ya kifisadi ya kuuzwa kwa bei chee hisa za UDA bila ya kuzingatiwa sheria, kanuni na taratibu.
Alisema Milanzi alishiriki kuanzia hatua za mwanzo za mkataba kati ya UDA na Kampuni ya Simon Group mwaka 2009 wakati Dk. Masaburi alishiriki katika kubariki utekelezaji wa mkataba huo wa kifisadi mwaka 2011 bila kuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya wananchi wa Dar es Salaam.


Mnyika alisema Milanzi na bodi ya wakurugenzi wa UDA chini ya uenyekiti wa Iddi Simba, walishiriki katika kuingia mkataba mbovu na wa kifisadi wa mauzo ya kampuni hiyo, huku sehemu ya fedha za malipo zikiingizwa kwenye akaunti za watu binafsi.
Alisema Dk. Masaburi alitekeleza mkataba huo kinyume cha sheria, kanuni na maslahi ya umma kwa yeye binafsi kuhamisha umiliki wa UDA kwa Simon Group baada ya malipo ya Sh. milioni 285 tu sawa na asilimia 12.5 ya mauzo ya hisa hizo kupitia maamuzi yake ya Juni 10, mwaka huu wakati shirika lina mali zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 12.
Mnyika alisema baada ya kufanya maamuzi hayo, Dk. Masaburi alijaribu kujikosha kwa maamuzi batili ya vikao haramu vya Kamati ya Fedha na Uongozi vya Juni 29 na Baraza la Madiwani la Julai 20, mwaka huu.
 
Watu kama kina Mnyika na wabunge wengine wa Dar kwanini wasifunge safari kwenda kujifunza Public Transportation inayomilikiwa na serikali inavyofanya kazi ili wafikirie namna ya kuiboresha UDA?
 
Watu kama kina Mnyika na wabunge wengine wa Dar kwanini wasifunge safari kwenda kujifunza Public Transportation inayomilikiwa na serikali inavyofanya kazi ili wafikirie namna ya kuiboresha UDA?

mkuu hata hapa british council ni hakika wanaweza kuwasaidia mambo kama haya
wanaweza kuita mtaalamu mmoja kutoka moja ya council za UK hakawapiga msasa
ni wazo zuri lakini wafanye hapa nyumbani ili wengi wauzulie na kuwe na midahala ya wataalamu wa mambo
haya kama miwili mitatu

mimi nadhani tatizo ni uzalendo viongozi wanacheka na wamiliki wa daladala lakini kiukweli tungekuwa mbali
 
Tarehe 27 Julai 2011 vyombo mbalimbali vya habari vimemnukuu Meya Wa Jiji la Dar es salaam Dkt. Didas Masaburi akieleza kilichoitwa maamuzi ya Baraza la Madiwani wa Jiji kuhusu kuvunja uongozi wa Shirika la Usafiri Dar es salaam (UDA) na kuunda kamati ya kuchunguza matatizo katika shirika hilo.

Tarehe 28 Julai 2011 vyombo mbalimbali vya habari vimemnukuu Meneja wa UDA, Victor Milanzi akimjibu Meya Masaburi kwa pamoja na mambo mengine kugoma kuondoka katika nafasi hiyo na kukanusha tuhuma zilizoelekezwa juu yake kuhusu ubadhirifu wa fedha za mauzo ya hisa za shirika hilo.

Kwa nafasi yangu ya ubunge ni mjumbe katika Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es salaam ambalo lina hisa 51% katika Shirika hilo na pia nawajibika kushiriki kuisimamia serikali kuu ambayo ina hisa 49% katika kampuni hivyo inanibidi kutoa kauli kuhusu upotoshaji unaondelea kufanywa na Meya Masaburi pamoja Meneja Milanzi kuhusu kashfa hii kupitia vyombo vya habari.

Naomba wakazi wa Dar es salaam na wananchi watanzania kwa ujumla wafahamu kwamba Meya Masaburi na Meneja Milanzi wote wawili ni sehemu ya matatizo ya UDA kwa kushiriki kwa kiwango kikubwa katika kukiuka sheria, kanuni na taratibu kwenye uendeshaji wa shirika bila kuzingatia kwa ukamilifu maslahi ya wasafiri na walipa kodi.

Meya Masaburi na Meneja Milanzi wote kwa nyakati mbalimbali wameshiriki katika kuachia maamuzi ya kifisadi ya kuuzwa kwa bei chee kwa hisa za kampuni ya UDA bila ya kuzingatiwa kwa sheria, kanuni na taratibu. Meneja Milanzi ameshiriki kuanzia hatua za mwanzo za mkataba kati ya UDA na Kampuni ya Simon Group mwaka 2009 wakati Meya Masaburi ameshiriki katika kubariki utekelezaji wa mkataba huo wa kifisadi mwaka 2011 bila kuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya wananchi wa Dar es salaam.
Meneja Milanzi na bodi ya Wakurugenzi chini ya uenyekiti wa Iddi Simba wameshiriki katika kuingia mkataba mbovu na wa kifisadi wa mauzo ya kampuni hiyo huku sehemu ya fedha za malipo zikiingizwa kwenye akaunti za watu binafsi.

Meya Masaburi ametekeleza mkataba huo kinyume cha sheria, kanuni na maslahi ya umma kwa yeye binafsi kuhamisha umiliki wa kampuni ya UDA kwa Simon Group baada ya malipo ya milioni 285 tu sawa na asilimia 12.5 ya mauzo ya hisa hizo kupitia maamuzi yake ya tarehe 10 Juni 2011 wakati UDA ina mali zenye thamani ya zaidi ya bilioni 12.

Baada ya kufanya maamuzi hayo kinyume cha sheria, kanuni na maslahi ya wananchi Meya Masaburi amejaribu kujikosha kwa maamuzi batili ya vikao haramu vya kamati ya fedha na uongozi cha tarehe 29 Juni 2011 na Baraza la Madiwani la tarehe 20 Julai 2011.

Kwa nafasi yangu ya ubunge ni mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi na pia ni mjumbe wa baraza la Madiwani na tarehe 20 Julai 2011 nilieleza mbele ya waandishi wa habari kwamba vikao hivyo vyote viwili vilikuwa batili kwa kuwa viliitishwa bila kuzingatia sheria na kanuni pia vilifanya maamuzi haramu ambayo hayakuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya wananchi wa Dar es salaam.

Kama nilivyoelekeza kusudio siku hiyo, nitatoa waraka kwa wananchi wa Dar es salaam na mamlaka husika wenye kueleza msingi wa kupiga kura ya HAPANA siku hiyo kwa maamuzi yote haramu yaliyofanywa na vikao hivyo batili na kueleza kwa kina vifungu vya sheria, kanuni, mkataba na taratibu zilizokiukwa pamoja na kuwataja wa majina wahusika na kiwango cha fedha kilichotolewa. Hata hivyo, kabla ya kutoa waraka huo nimeona nitoe taarifa hii kwa umma ili mamlaka zote zinazohusika ziingilie kati na kuchukua hatua za haraka kunusuru mali na mwelekeo wa shirika la UDA.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda anapaswa kuingilia kwa kuchukua hatua stahiki za kuingoza serikali kupitia upya mkataba ulioingiwa na kutekelezwa kinyume cha sheria, kanuni na maslahi ya wananchi kati ya Jiji, UDA na Simon Group Limited. Maamuzi yaliyofanywa na Meya Masaburi na vikao vyake haramu vya jiji na vya UDA yanapaswa kubatilishwa. Aidha maamuzi ya bodi ya UDA chini ya uenyekiti wa Iddi Simba kwa miaka kadhaa yanapaswa kupitiwa upya kwa kuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya umma.

Waziri wa Fedha Mustapha Mkullo anapaswa kuingilia kati kupitia Msajili wa Hazina na CHC ili kunusuru hisa za serikali kuu katika UDA pamoja na mali za shirika kwa ujumla wake. Izingatiwe kwamba tarehe 28 Februari 2011 ofisi ya Waziri Mkuu iliandika barua yenye kumbukumbu namba CAB. 185/295/01/27 ambayo Katibu Mkuu Hazina anayo nakala yake yenye kueleza bayana kwamba uuzwaji wa hisa ambazo hazijagawiwa (unallocated shares) uliokuwa ukifanywa na UDA haukuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma na kuagiza mchakato huo usitishwe na CHC kushirikishwa. Izingatiwe kwamba katika maamuzi haramu yaliyofanywa na Meya Masaburi tarehe 10 Juni 2011 Wizara ya Fedha (hazina) na CHC wote hawakushiriki kwenye kikao kilichoitwa cha wana hisa wa UDA wakati serikali kuu imekuwa na hisa 49%.

Kamati husika za Bunge hususani ya Miundo mbinu na ya Hesabu za Mashirika ya Umma ziingilie kati kwa haraka kwa kushirikiana na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mamlaka ya Kudhibiti Manunuzi ya Umma(PPRA) na wabunge wa mkoa wa Dar es salaam.

Hatua hizo za haraka zitaokoa mali za umma, kuweka msingi wa kuboresha usafiri katika mkoa wa Dar es salaam na kuwezesha hatua za kisheria na kinidhamu kuchukuliwa kwa wahusika wote waliofikisha jiji na taifa katika hali hiyo.

Ikumbukwe kwamba masuala ya Mashirika na Makampuni yaliyo chini ya jiji la Dar es salaam nilianza kuyahoji katika vikao hususani vya kamati ya fedha na uongozi mara baada ya kuingia katika utumishi wa umma kwenye Halmashauri ya Jiji kupitia mikutano ya mwezi Machi na Mei 2011.

Hata hivyo, badala ya Mstahiki Meya Masaburi kuchukua hatua stahiki kama ilivyoazimiwa katika vikao hivyo akaenda kufanya maamuzi binafsi ambayo yameongeza ukubwa wa matatizo badala ya kuyapunguza.

Kutokana na hali hiyo mwezi Juni nikaamua kutumia fursa za kibunge katika kushughulikia hatma ya UDA na usafiri mkoani Dar es salaam kwa ujumla wake.

Hivyo, wakati wa mjadala wa Azimio la kuliongezea muda Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) tarehe 23 Juni 2011 nilihoji kwa maandishi kuhusu mauzo ya hisa na mali za kampuni ya UDA na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa kwa kurejea pia ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) . Hata hivyo, Waziri wa Fedha Mustapha Mkullo kwenye majumuisho yake hakutoa kauli wala kuchukua hatua za haraka pamoja na kuwa hatma ya hisa 51% za shirika hilo zinahusu Wizara yake kupitia Msajili wa Hazina.

Nikarudia tena kuhoji kwa maandishi wakati wa mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyowasilishwa tarehe 23 Juni 2011 nikipinga uuzwaji wa hisa za UDA bila maslahi ya usafiri wa wananchi wa Dar es salaam kuzingatiwa na kutaka kuwe na uhusiano baina ya hatma ya UDA na Mradi wa Mabasi yaendayo kwa Haraka (DART) ambao unaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Nilihoji suala hilo kama sehemu ya hitaji la kuwa na mfumo thabiti wa Usafiri wa Halaiki wa Umma (Mass Public Transit) ambao utachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza adha ya usafiri katika jiji la Dar es salaam.

Hatahivyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika majumuisho ya bajeti yake tarehe 1 Julai 2011 hakutoa kauli wala kuchukua hatua za haraka za kunusuru hali ya mambo pamoja na kuwa yeye ndiye mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hivyo ana wajibu wa kufuatilia masuala ya kisheria, kinanuni na kimikataba ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kama ilivyo kwa halmashauri zingine.

Baada ya hapo ndipo kashfa ya UDA ikaanza kujitokeza kwenye vyombo vya habari tarehe 11 Julai 2011 ikiwa katika sura ya mzozo baina ya Meneja Milanzi na Mkurugenzi Kisena wa Simon Group Limited katika hatua za kulazimishana kuondoka ofisini.

Kufuatia hali hiyo tarehe 15 Julai 2011 baada ya majibu ya swali la msingi nililouliza Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu ukaguzi maalum wa mahesabu na ufisadi katika kituo cha Mabasi cha Ubungo (UBT) niliuliza swali la nyongeza kuhusu kashfa ya kampuni ya UDA kutokana na uhusiano wake na mradi wa DART ambapo maeneo ya UBT na UDA yatahusika. Katika swali langu nilitaka hatua za haraka kuchukuliwa na serikali kutokana na mauzo hayo kuendelea bila kuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya wananchi hata hivyo Naibu Waziri Aggrey Mwanri hakutoa majibu ya kuridhisha wala kuchukua hatua zinazostahili kufuatia suala hilo hali ambayo ilitoa mwanya kwa Meya Masaburi kuendelea na mchakato haramu.

Katika muktadha huo nitaendelea kushirikiana na madiwani wenzangu wenye kutanguliza mbele maslahi ya umma ikiwemo wabunge wa mkoa wa Dar es salaam ambao mimi ni katibu wao pamoja na mamlaka zingine za kiserikali na kibunge katika kushughulikia suala hili. Natoa mwito kwa wananchi wa Dar es salaam kutuunga mkono katika kulifuatilia kwa karibu suala hili na kuchukua hatua zinazostahili kila mmoja kwa nafasi yake.

Wenu katika utumishi wa umma,

John Mnyika (Mb)
Bungeni-Dodoma
31 Julai 2011

 
Why This Secrecy in UDA Privatisation?

The Consolidated Holding Corporation (CHC) is in the news again for the wrong reasons. This time around the public is raising eyebrows over the role of the agency charged with the liquidation of public enterprises, divestiture, monitoring and evaluation of privatised entities, among other responsibilities, in the reported privatisation of the Dar es Salaam public transport company, UDA.

Questions are being asked on how a private firm managed to take over the UDA management after paying a measly Sh285 million for acquisition of 51 unallocated shares of the transport firm that has an asset base of Sh12 billion. The uncertainty clouding the future of the 37 year old firm is a result of unnecessary secrecy in which its privatisation is shrouded. It is this kind of secrecy which raises suspicion whenever the State enters into divestiture agreements with private investors. This habit of keeping details of privatisation under wraps invariably leads to the theft of hundreds of millions of shillings of taxpayers' money.

The UDA issue reminds one of the many questionable contracts the country has been stuck in as a result of unwarranted secrecy. The IPTL, Richmond and Buzwagi agreements are but a few of the contracts that have generated a lot of controversy in recent years. It seems that lessons have not been learnt even after it became apparent that billions of shillings have been siphoned from public coffers in dubious contracts signed between state agencies and private firms.

Transparency is the only way that questions such as those being asked about the UDA privatisation can be avoided. UDA has been struggling for the better part of the last two decades or so, and few would dispute the fact that the firm badly needs a fresh injection of capital and new ideas. However, any move to privatise the company must take into consideration the interests of the public as well as those of the potential investor. The sound performance of some privatised firms such as Tanzania Breweries Limited leaves us without doubt that the placing in private hands of some state-owned entities is desirable, but transparency is paramount in such agreements to ensure that Tanzanians are not shortchanged.

Source: The Citizen
 
mkuu hata hapa british council ni hakika wanaweza kuwasaidia mambo kama haya
wanaweza kuita mtaalamu mmoja kutoka moja ya council za UK hakawapiga msasa
ni wazo zuri lakini wafanye hapa nyumbani ili wengi wauzulie na kuwe na midahala ya wataalamu wa mambo
haya kama miwili mitatu

mimi nadhani tatizo ni uzalendo viongozi wanacheka na wamiliki wa daladala lakini kiukweli tungekuwa mbali

Wamiliki wengi wa daladala sio hao hao viongozi? Hivi hii kampuni iliyouziwa share kiaina, huwa inajishughulisha na usafirishaji?
 
Wamiliki wengi wa daladala sio hao hao viongozi? Hivi hii kampuni iliyouziwa share kiaina, huwa inajishughulisha na usafirishaji?
Yes lakini ni wa mahindi na nafaka nyingine, ndio wamekula dili kinyemela kutoa mazao nadhani iringa kuleta DAR
Kwa hiyo walio uza hizo hisa kinyemela kwenye ili kampuni wanatufananisha na mahindi
wapuuzi sana hawa watu
huyu MEYA wa jiji huyu ni kawaida yake kala sana kwenye ugavi na ununuzi na chuo cha IFM sasa kaja
kwenye siasa tumekwisha
ni rafiki wa karibu sana wa MAKONGORO MAHANGA
MAHANGA na kikwete nadhani kila mtu anajua ni macomradi
hii kampuni ya SIMON unaweza kukuta wana hisa wengi ni wakazi wa OFISI yetu ya MAGOGONI pale kwenye tausi waliouzwa na mama siti
 
Jamani.. naona nimemiss swali kuhus UDA na DART; nimeona sehemu ya mwisho waziri akijibu na inaonekana ni Mnyika aliuliza.. any details?

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ambayo Mnyika ameitoa leo juu ya suala la UDA.

"Kufuatia hali hiyo tarehe 15 Julai 2011 baada ya majibu ya swali la msingi nililouliza Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu ukaguzi maalum wa mahesabu na ufisadi katika kituo cha Mabasi cha Ubungo (UBT) niliuliza swali la nyongeza kuhusu kashfa ya kampuni ya UDA kutokana na uhusiano wake na mradi wa DART ambapo maeneo ya UBT na UDA yatahusika. Katika swali langu nilitaka hatua za haraka kuchukuliwa na serikali kutokana na mauzo hayo kuendelea bila kuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya wananchi hata hivyo Naibu Waziri Aggrey Mwanri hakutoa majibu ya kuridhisha wala kuchukua hatua zinazostahili kufuatia suala hilo hali ambayo ilitoa mwanya kwa Meya Masaburi kuendelea na mchakato haramu."
 
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ambayo Mnyika ameitoa leo juu ya suala la UDA.

"Kufuatia hali hiyo tarehe 15 Julai 2011 baada ya majibu ya swali la msingi nililouliza Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu ukaguzi maalum wa mahesabu na ufisadi katika kituo cha Mabasi cha Ubungo (UBT) niliuliza swali la nyongeza kuhusu kashfa ya kampuni ya UDA kutokana na uhusiano wake na mradi wa DART ambapo maeneo ya UBT na UDA yatahusika. Katika swali langu nilitaka hatua za haraka kuchukuliwa na serikali kutokana na mauzo hayo kuendelea bila kuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya wananchi hata hivyo Naibu Waziri Aggrey Mwanri hakutoa majibu ya kuridhisha wala kuchukua hatua zinazostahili kufuatia suala hilo hali ambayo ilitoa mwanya kwa Meya Masaburi kuendelea na mchakato haramu."


haya ni maagizo kutoka IKULU
hiyo kitu ya mnyika nimeetunza kwenye PC yangu kwa kumbukumbu
kuna watawala wanalilia kwa machozi ya mamba, kila maliasi ya serikali wanataka kufanya ya familia
MUBARAK type

kwa tafakari yakina SIMON GROUP hawana uwezo wa kufanya waliyofanya bila SUPPORT ya vi MEMO kutoka kwa wazee
hawa jamaa we hacha mimi nina imani kama nitakuwa hai kuna siku nitakwenda kumsalimia KAKA mkuu ukonga/segere kwa maovu yake/familia au marafiki kupitia vi memo vyake ZOMBE kajitanga mfuu huyu ni mfungwa mtalajiwa kabla ya kujizombe
 
Walionunua hisa za serikali UDA wateta.

WINGU zito bado limeugubika mkataba wa uuzwaji wa hisa za Serikali ndani ya Shirila la Usafiri Dar es Salaam (Uda), kufuatia wanaodai kuwa wamiliki wake kujitokeza hadharani tangu kuanza kwa mvutano ambao umekuwa ukizihusisha pande tofauti. Wamiliki hao ni Kampuni ya Simon Group Ltd ambao jana waliwambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa umiliki wake umekidhi vigezo vyote katika kumiliki Hisa kwa asilimia 52.53.

Hata hivyo, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) jana hiyohiyo ilirusha kombora na kusema kuwa mkataba huo ni batili na kwamba fedha zote zipo kwenye akaunti ya kada wa Chama Cha Mapinduzi na mwanasiasa wa siku nyingi (jina tunalihifadhi kwa sasa). Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simon Group, Robert Kisera alisema kampuni yake ilifuata vigezo vyote vilivyotakiwa na kwamba imejidhatiti kuliendesha Uda bila wasiwasi. Kisera alisema kuwa hadi sasa kampuni yake imekwishawekeza kiasi cha Sh760 milioni na kwamba kiasi kilichobaki cha Sh500 kinatarajia kulipwa kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Msimamo wa POAC

Kwa upande wake, Mwenyekiti POAC, Zitto Kabwe aliitisha mkutano wa Waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge na kueleza kuwa mkataba wa Uda na Simon ni kizungumkuti na kutahadharisha kuwa aliyeingia mkataba huo amejiingiza matatani mwenyewe. Zitto alisema kuwa kilichofanyika ndani ya mkataba huo ni ufisadi mtupu na akaeleza kuwa tayari kamati yake ilishabaini kuwa yako madudu makubwa hivyo ikaomba Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kuingilia kati kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwa kina. "Taratibu hazikufuatwa,na uamuzi wowote utakaofanyika ni batili kwa kuwa tayari sisi tumeshaanza mchakato wa kubaini kilichopo ndani ya mkataba huo ikiwa ni pamoja kumuagiza CAG na tayari Spika ana taarifa hizo,''alisema Zitto.

"Kutokana na hilo, hapa jamaa kaingia choo cha kike na kwa vyovyote vile lazima ametapeliwa na wajanja kwa kuwa kamati ilishamwambia mapema lakini anashindwa kuelewa kuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma ndiyo yenye jukumu la kubinafsisha mashirika zaidi ya hapo ni hakuna.''
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Deo Filikunjombe (Ludewa-CCM) alisema kuwa kinachoyatafuna mashirika ya umma ni Msajili wa Hazina ambaye ameshindwa kutimiza wajibu wake kwa zaidi ya miaka 10.

Filikunjombe alisema kuwa kwa zaidi ya Miaka 10 Msajili ameshindwa kuteua bodi jambo linaloonyesha kuwa uwezo wake ni mdogo sana ambao hata kwa dawa asingeweza kujinusuru zaidi ya kusababisha migogoro kila kunapokucha. Alisema kutokuwapo kwa bodi kulifanya uamuzi kufanyika kiholela holela jambo ambalo limeifanya Kamati hiyo kuwa na shaka. Mbunge huyo alisema kuwa kuna uzembe ndani ya serikali ambao umekuwa ukisababisha baadhi ya wachache kuendelea kutafuna mali za umma wakati nchi ikibaki maskini.

"Kwa mfano angalieni tarehe hizi 2/9/2009 ziliingia Sh 250,00 milioni ziliingia Benki M', Makambako tarehe 26/11/2009 ziliingizwa Sh 20 milioni Benk M' Songea kabla ya tarehe 9/12/2009 kuingizwa kiasi cha Sh 30 milioni katika tawi la Mlimani City zote zikiwa ni akaunti za (anamtaja mwanasiasa huyo),".

Alisema kumekuwapo maneno ya kuichafua kamati hiyo kwamba inafanya kazi chini ya mwamvuli wa vigogo walioko ndani ya Serikali jambo alilokanusha. "Kwanza Watanzania naomba watambue kuwa Simon haijanunua Uda, bali kilichopo ni kwamba Simon ilinunua zile hisa ambazo hazikuwa zimelipiwa na kuwa hakuna kigogo yeyote nyuma ya kampuni hii na huyo wanayemtaja mimi simfahamu," alisema Kisera.

Shutuma nyingi alizirusha kwa Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambaye alisema kuwa kuwa ndiye amekuwa akiichafua Simon Group na kumtaka mbunge huyo kufunga mdomo ili asiingilie mambo yoyote kuhusu mkataba huo. Kwa mujibu wa Kisera, kitendo cha Mnyika kuandika barua kwenye ukusara wa ‘face book' akielekeza shutuma kwa Simon ni kitendo cha uonevu na manyanyaso kwa mwekezaji mzawa.

Mnyika aliingilia kati mvutano ulioko kati ya Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi na Meneja wa Uda, Victor Milanzi, akisema hakuna mwenye haki ya kumnyooshea mwingine kidole, kwani wote wawili ni sehemu ya matatizo yanayolikabili shirika hilo. "…Wote wawili wameshiriki kwa kiwango kikubwa katika kukiuka sheria, kanuni na taratibu kwenye uendeshaji wa Uda bila kuzingatia kwa ukamilifu maslahi ya wasafiri na walipa kodi," alisema Mnyika katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa kupitia mtandao wa face book.

Wingu zito lazidi kutanda UDA
 
haya ni maagizo kutoka IKULU
hiyo kitu ya mnyika nimeetunza kwenye PC yangu kwa kumbukumbu
kuna watawala wanalilia kwa machozi ya mamba, kila maliasi ya serikali wanataka kufanya ya familia
MUBARAK type

kwa tafakari yakina SIMON GROUP hawana uwezo wa kufanya waliyofanya bila SUPPORT ya vi MEMO kutoka kwa wazee
hawa jamaa we hacha mimi nina imani kama nitakuwa hai kuna siku nitakwenda kumsalimia KAKA mkuu ukonga/segere kwa maovu yake/familia au marafiki kupitia vi memo vyake ZOMBE kajitanga mfuu huyu ni mfungwa mtalajiwa kabla ya kujizombe

Kuna kada wa Chama Cha Mapinduzi na mwanasiasa wa siku nyingi ametajwa na akina Zitto lakini vyombo vya habari vimeficha jina.
 
Nadhani kuna issue mbili ambazo ni muhimu kuziangalia. Mwananchi/Citizen kama watu wengine wamelichukulia suala hili kwa mwanga wa "kutouzwa halali" kana kwamba ingeuzwa kwa bei ya juu na halali basi kusingekuwa na issue. Kwangu mimi, tatizo ni zaidi ya kuuzwa kwa bei ya chini, tatizo langu ni kwanini UDA haikuchukua majukumu ya DAR na kubadilishwa kuwa huo wakala wa Usafiri wa Haraka? Kiakili na kimantiki haikubaliki kuona kwamba UDA iiliyoundwa kusimamia usafiri wa umma jijini la Dar haikubadilishwa na kuifanya iwe ndio DART - yaani angalau wangeweka iwe UDART kuonesha mabadiliko hayo. Tatizo langu ni kuwa kwa jiji kama Dar lenye wakazi milioni karibu 4 wengi wao wakiwa ni wa kima cha chini na kati usafiri wa umma ndio suluhisho sahihi kwa wakazi hao. Haiwezekani kila sikuw awatu wanalalamikia usafiri na congestion lakini hawaoni kwamba kwa mtindo uliopo sasa wanalazimisha watu wengi kuwa na magari yao hata kama si lazima kiuchumi.

Ningefurahi sana kama kungekuwepo na watu kule Mwananchi/Citizen ambao wangeweza kuarticulate hii issue kwa mwanga huo. Tatizo siyo bei ya UDA ilivyouzwa bali gharama ambayo wananchi wanalipa na taifa linalipa hasa jijini Dar kwa UDA kuuzwa.
 
Back
Top Bottom