Uchunguzi wamnasa Mkurugenzi TANESCO; Bodi ya Jenerali Mbona yatishia kujiuzulu

Hivi huyo anaemtetea Mboma kumuita mzalendo tu sababu alikuwa mkuu wa majeshi nadhani akapimwe akili, excuse ya kusema eti vijana hawana adabu na si utamaduni wa nchi yetu ndio umetufikisha hapa, hivi anajua Mboma alivyokuwa CDF alichuma mali kiasi gani? anajua Mboma alijenga mahekalu kiasi gani au alinunua plots na mashamba kiasi gani?
Uzalendo anaosemea ni uzalendo gani huo?

Mboma ni pilot sasa weledi wa masuala ya umeme anaupata wapi?
 
Kwani Mboma ni nani hata asipewe ukweli wake? Kwanza anahusika kwa tuhuma kibao.... Meremeta, Zabuni za Jeshi wakati ni Mkuu wa Majeshi na nyingine za kutisha. Na kiwanda chake cha Gypsum je???

Wacheni kutetea watu waovu. Don't judge a book by its cover. MBOMA SI MSAFI NG'OOO!
 
Hii tabia ya kutishia nyau siipendi.kama umeamua kujiuzulu jiuzulu na toa sababu zako za kujiuzulu.kama unaona mambo hayaendi vizuri jiuzulu usipojiuzulu utaonekana mganga njaa tuu.
 
Soma Msimamo wa Makamanda, Wapiganaji, Wapinga UFISADI!

Wabunge ambao tayari wameweka misimamo yao wazi kumtetea Mhando ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka. Zitto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, wakati Sendeka ni mjumbe katika Kamati ya Nishati na Madini.

“Siku ya Jumatano (kesho kutwa) kamati imemwomba Spika ruhusa ya kuitisha kikao ili bodi nzima ya Tenesco kuja kutupa maelezo ya nini kimetokea, maana taarifa ya CAG na PPRA haina hizo tuhuma wanazosema watu wa Serikali,” alisema Zitto na kuongeza: “POAC tunahusika na usimamizi wa fedha za shirika, tunataka kujua ubadhirifu na masuala ya kisheria na itahakikisha uwajibikaji na tutasimamia hilo kwa nguvu zote kwani hatutaki uonevu na tutalinda wanaoonewa. Hata hivyo, kauli hiyo ya Zitto inakuja wakati baadhi ya wabunge akiwamo yeye mwenyewe hivi karibuni walishinikiza mawaziri ambao wizara zao zilitajwa kuhusika na tuhuma za ufisadi katika ripoti ya CAG wajiuzu!

Matokeo ya Tume ya Uchunguzi!

Waandishi WetuToleo la 262 10 Oct 2012

  • Bodi ya Jenerali Mbona yatishia kujiuzulu
  • Bandari nako si shwari, mengine yafichuka
….. aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, William Mhando, ambaye naye alisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi, mambo yanazidi kumuelemea, Raia Mwema, limebaini.

Mhando na wenzake walisimamishwa kazi TANESCO ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zikiwamo za matumizi mabaya ya madaraka na hususan kuwapo kwa mgongano wa kimaslahi, uchunguzi ulioendeshwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambao umebaini mgongano wa maslahi kwa kiongozi huyo.

…… Mhando amebainika kuwa na mgongano wa kimaslahi na Kampuni ya MC Donald Live Line Technology Ltd.

…..taarifa ya uchunguzi huo inamuweka katika mazingira magumu zaidi Mhando…….Pamoja na kashfa hiyo .….Raia Mwema umebaini kuwapo pia kwa kashfa nyingine ambayo pia inaonyesha matumizi mabaya ya madaraka, ikiwa nayo inathibitishwa na nyaraka, ikihusu kujipa kazi za shirika analoliongoza hivyo kujiingiza katika mgongano wa kimaslahi.

“Yupi ni mzalendo kati ya Maselle aliyepewa unaibu waziri hivi karibuni na Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Mboma aliyepigania nchi hii?” anahoji mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo na kuongeza:

“Hawa vijana wasilewe madaraka, huwezi kijana umepata unaibu waziri juzi tu unamwambia Jenerali Mboma eti hana uzalendo, hana weledi, hii si sawa. Ni kukosa adabu, huu si utamaduni wetu Waafrika.”.

Ushauri!
Recall: zitto kabwe alitaka kuunda kamati ndogo ya POAC ili kumsafisha mhando,,,sasa ni wakati muafaka zitto kujitokeza hadharani na aombe radhi watanzania kwa jitihada zake za kutaka kumsafisha Mhando:photo::lol::nerd::spy:
 
Wengi wa vijana wa siku hizi ni Kama wavuta bangi tu, mnajadili Mada za kudhalilisha wazee wenu, hivi Masele ni wa kumtusi mboma? Na Bado watu Humu JF mnashangilia, kweli utamaduni na heshima ya Mtanzania imepotea.

Acha mambo ya ajabu aisee, unajiaibisha sana. watu wengi wawezadhani mtu akiwa na cheo fulani inabidi upewe heshima hata kama hiyo heshima huistahili. huyo mboma yawezekana ana uzalendo, lakini uzalendo kwa tumbo lake. tanesco wamefanya madudu, wameleta umaskini hapa nchini, si angejiuzuru mapema kama kweli mzalendo? msisahau matatizo tulonayo hapa tz ni kutopenda kukosolewa au kukosoana. badili mtazamo, mtu akifanya mambo ya kauzu tunampa za uso, bila kuangalia ni koplo au field marshall. ebo!
 
Wanajeshi wengi wastaafu wa zamani hapa kwetu ukiondoa rais wetu wanakuwa na tabia za viburi na jeuri.

Kwa wenzetu wanajeshi ni kina Colin Powel watu wastaarabu watulivu tofauti kabisa.
 
Wengi wa vijana wa siku hizi ni Kama wavuta bangi tu, mnajadili Mada za kudhalilisha wazee wenu, hivi Masele ni wa kumtusi mboma? Na Bado watu Humu JF mnashangilia, kweli utamaduni na heshima ya Mtanzania imepotea.

peleka huko wajinga wenzio! Hata zzk ndo maana mnamsema kwa kuwa umri wake mdogo kukosoa kina lowasa waliojaa mvi? Huyu mboma si alistaafishwa kwa lazima jeshini? Mnafikiri hatujui? Kwa nini walikubali mgao wa kipuuzi uendelee miaka yote? Ili wauze mafuta? Majenereta? Wahongwe? Siwapendi mawaziri wa jk lakini namuunga mkono masele
 
Hivi mtu ameshaonekana kuwa mwizi mnambembeleza? Bodi ivunjwe mara moja na huyo Mhando asogezwe mahakamani na kesi isimamiwe na Wakili mweledi na mzalendo na ukweli ni kuwa huko ataishia kunyea debe maana alitumia madaraka yake vibaya na kulitia hasara shirika la TANESCO
 
Back
Top Bottom