Uchunguzi tuhuma za Jairo ngoma nzito

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Uchunguzi tuhuma za Jairo ngoma nzito
Send to a friend
Monday, 08 August 2011 21:30


Ramadhan Semtawa
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amesema uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, unaendelea na siku kumi zilizotolewa hazitoshi.

Awali, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, akizungumzia hatua za haraka za Serikali kushughulikia kashfa hiyo, ilisema uchunguzi huo dhidi ya Jairo ungetumia siku 10, lakini Julai 31, ambayo ilikuwa ni siku ya kumi, CAG Utouh alisema ndiyo kwanza alikuwa na siku ya tano tangu kuanza ukaguzi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Utouh alisema uchunguzi siyo kuandika ripoti, kwani kuna mambo mengi ya msingi ya kitaalamu yanapaswa kuzingatiwa.
Kwa mujibu wa Utouh, dhamira ya Ikulu na ofisi yake ni kuhakikisha uchunguzi unaofanyika unatoa matokeo mazuri, ambayo yataonyesha undani wa tuhuma zenyewe na suala siyo kuandika ripoti kama inavyoweza kufikirika na baadhi ya watu.

"Muda is not an issue (muda siyo hoja), jambo la msingi ni kufanya uchunguzi utakaoleta tija kwa kile kilichokusudiwa. Siyo kwamba tunakaa na kuandika ripoti tu, tunafanya uchunguzi wa kina kupata majibu ya msingi ambayo Watanzania wataona matokeo ya uchunguzi wetu," alisema Utouh.
Utouh alisema katika uchunguzi huo kuna kupitia nyaraka mbalimbali za msingi na kwamba, licha ya nyaraka, wanahitaji kufanya mahojiano na watu mbalimbali waliotuhumiwa.

Hata hivyo, CAG alisema uchunguzi huo kwa sasa uko hatua za mwisho, lakini alipoulizwa ni lini unaweza ukawa umekamilika rasmi alijibu: "Hilo siwezi kukwambia."

"Unachopaswa kujua ni kwamba uchunguzi uko hatua za mwisho, sasa kukwambia ni lini siwezi. Jua tu tunakamilisha kazi na jambo la msingi tuje na matokeo mazuri. hivi ninavyokwambia (jana) hapa nipo ofisini ingawa leo ni Nanenane,” alisema na kuongeza:
“Leo ni sikukuu ya Nanenane, lakini kuna kazi zingefanyika nje, nyingine tunazifanya hapa hakuna kupumzika licha ya kwamba ni sikukuu. Ni kwa sababu ya jambo hilo."

Kauli ya Ikulu kupitia Luhanjo
Julai 21, Luhanjo alitangaza uchunguzi huo ambao ulionekana ni hatua za haraka za serikali kushughulikia tatizo hilo, ambalo liligusa hisia za wabunge na watu wa kada mbalimbali nchini, wakiwamo viongozi wa dini.

"Nimeanzisha uchunguzi wa awali (Preliminary Investigation) kwa lengo la kupata ukweli kuhusu tuhuma hizo. Wakati uchunguzi huo ukiendelea, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, amepewa likizo ya malipo kupisha uchunguzi wa awali (Relieve of duties administratively pending preriminary investigation)... hatua zitakazochukuliwa hapo baadaye zitategemea matokeo ya uchunguzi huo," alisema Luhanjo.

Luhanjo alisema ikiwa uchunguzi wa CAG utabaini Jairo ana makosa ya nidhamu, atapewa taarifa za tuhuma husika (Notice) ambayo itaambatana na hati ya mashtaka (charge), ambayo itaeleza kwa kifupi makosa hayo na jinsi yalivyotendekea.
 
[h=4]Comments [/h]


0 #10 kutokakijijini 2011-08-09 18:05 ukishaona mkaguzi mkuu [CAG]nae amekua mtu wa longolongo ujue wananchi tunaonekana [NENO BAYA].ila wawe macho wakiendeleza huo u[NENO BAYA] wao hii nchi haitatawarika.kikwete na hao wenzake waanze kutafuta magereza maana chadema hawaji kutuletea hulu wa kweri pekee bali pia kuwabuluza mahakamani mafisadi wote wa ccm kwa kudhulumu mali zetu.
Quote









0 #9 majmaj 2011-08-09 17:56 Kumchunguza Jairo ni kunchunguza Kikwete. Huyu bwana na JK ni damu damu, alikuwa msaidizi wake binafsi kisa akampandisha cheo akawa Katibu Mkuu kwenye wizara ya kula, kulala na kuiba (Madini na Nishati) ili naye ajitafutie zake. JK, Lowassa, Rostam, Chenge, Ridhwan nk wao walishajitwalia zao mapema. Isitoshe ni utamaduni wa wizara zote kutoa pesa za kupitisha bajeti kila mwaka. Jairo kadakwa tu na kundi la akina Lowassa ili kumuadabisha Kikwete maana kawaruka wezi wenzake ili aonekane mwema kwa wananchi, so na wao wameamua kumkomoa ili waone atashughulikia namna hili gamba la nduguye na rafiki kipenzi chake huku kwa upande mwingine akiwadhalilisha akina Lowassa.Ngoma ya Jairo si mchezo maana ndiyo itampasua Jk na kumwondoa kiherehere chake. Akina CAG huu ni usanii mtupu, Jairo ni mwizi sawa na walivyo makatibu wakuu wote. hata Luhanjo akiwa katibu mkuu wa Wizara ya mamabo ya nje chini ya Kikwete ndi mtindo wamekuwa wakitumia miaka nenda rudi, so hakuna kificho hapo - ni ufisadi mtindo mmoja. Ama kweli chama legelege huzaa kiongozi legelege ambaye pia huzaa serikali legelege.

Quoting Kahamba:
Tatizo kumchunguza Jairo ni kuichunguza serikali nzima. Hayuko peke yake. Na kimsingi hata Ngeleja alitakiwa akae kando ndiyo uchunguzi huo ufanyike. Nadhani juhudi ni za kutafuta namna ya kuonyesha wengine hawahusiki au kujaribu kumvua kashfa ili kutoa nafuu kwa wizara nyingine. Hii ndo serikali ya Tz.​
Quote









0 #8 big 2011-08-09 17:18 inauma sana tulipofikia CAG longolongo wote wazushi lao moja hatuna ujanja guys inabidi tuitoe hii serikali ya CCM mapema iwezekanavyo kwenye madaraka kwa nja yoyote tukishindwa tufunge mkanda mpaka uchaguzi ujao usifanye makosa kuizika CCM naisikike tena anza kujenga hasira na chuki dhidi ya chama cha majambazi
Quote









+2 #7 husna 2011-08-09 13:10 Wee wasafishe hao jamaa huna jipya unachukua maelezo ya mashahidi na watuhumiwa ya nini na CAG siyo legal investigation agent sasa kama ushahidi wako hauwezi kuwafikisha mahakamani unapoteza muda wa nini wewe tuambie taratibu za matumizi ya fedha zilifuatwa au la wacha longolongo mzee siku kumi zinatosha sana transaction ndogo sana hiyo!
Quote









+2 #6 MABUWE 2011-08-09 12:17 SERIKALI LEGELEGE!!! NOMAAAAA.
Quote









+3 #5 Michael Zunzu 2011-08-09 10:32 Hivi huyu CAG kwa nini naye asifanyiwe uchunguzi juu ya utendaji wa kazi yake, muda si mrefu alikuwa ameshapitia mahesabu ya mashirika ya Serikali, wizara na idfara zake, kama kusingel;ikuwa na watu waliolipua bomu kuhusu mbinu za Wizara ya nishati na madini tungeliyafahamu lini yanayotokea, na p[engine si mchezo wa wizara moja, au alifunika kombe mwanaharamu apite, akaishia kusema katika mahesabu ya mashirika kadhaa hata idara kwamba kuna matumizi yasiyoonyesha dhahiri pesa zilitumikaje, basi na wala hakuna pendekezo lililotolewa la kutaka wahusika waeleze pesa hizo zilikwenda wapi.
Wenzake wamelipua ndiyo anajitapa kusema kufanya uchunguzi kwa uangalifu, kwa nini hitirafu hizo hakuziona mapema?
Quote









+2 #4 Kahamba 2011-08-09 08:36 Tatizo kumchunguza Jairo ni kuichunguza serikali nzima. Hayuko peke yake. Na kimsingi hata Ngeleja alitakiwa akae kando ndiyo uchunguzi huo ufanyike. Nadhani juhudi ni za kutafuta namna ya kuonyesha wengine hawahusiki au kujaribu kumvua kashfa ili kutoa nafuu kwa wizara nyingine. Hii ndo serikali ya Tz.
Quote









+2 #3 lunde 2011-08-09 07:57 huo ni ushenzi tu ,uchunguzi wa nini sasa mtu nyaraka zilisomwa na mbunge wao(CCM),SEMA WANAPANGA NAMNA YA KUTUDIVERT MIND, SHAURI YENU UVUMILIVU UTAFIKIA KIKOMO PATACHIMBIKA,
NASEMA HII SERIKALI NI FULL LEGELEGE NA NIFISADI NINGEPENDA JAIRO,NA WAZIRI NGELEJA PAMOJA NAWABUNGE WANAHUSIKA WANYONGWE HAZARANI AU TUWATUPIE KATIKATI YA BAHARI AU TUWAPIGE MOTO,VIVYO HIVYO ALIYEMNUSURU JAIRO
MLIVYO WASHENZI(SELIKA RI) MNASEMA SELIKALI HAINA HELA YA KUWALIPA WALIMU LAKINI HELA ZA KUHONGANA KUPITISHA BUDGET MNAZO,VERY STUPID
Quote









+4 #2 mzalendo 2011-08-09 05:10 Ushaidi hupi huo, wakati nyaraka zilishatolewa hapo bungeni. Huyu Jairo kwanza agepewa adhabu na mwajiri wake kwakutotumia taratibu stahiki kuhusu fedha za walipa kodi, harafu mambo ya mahakama yakafuata hapo baadaye.
Quote









+3 #1 ahmed00 2011-08-09 04:34 POSHO ina to cost! jambo la kuisha kwa siku moja, watendaji wa serikali ya ccm watatumia week mbili
Quote







Refresh comments list
 
Hakuna lolote tutakalopata kwa sasa zaidi ya kujilimbikizia hasira na chuki dhidi ya watendaji wa serikali, tunachoshukuru ni kuwepo kwa record ya tukio ili hapo baadae waje wajibu tuhuma.
 
Back
Top Bottom