Uchungu wa Mwana.......

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Dear JF members
Kwa mara ya kwanza ninarusha threads mbili kwa mpigo...............ninawaomba mnisamehe nimechanganyikiwa

Nauliza tu nini maana ya Usemi wa Uchungu wa mwana aujuaye Mzazi..............mzazi huyu ni yupi wa kike au kiume??

Kwa sababu mara nyingi naona uchungu wa mtoto especially akiwa mdogo unahusishwa moja kwa moja na mama yake.....(ndo maana sometimes tunasikia kesi za wamama kuumia wanaponyang'wanywa watoto wao)

Ninajiuliza swali...........je ni weli kuwa wababa hawana uchungu na watoto wao"
Wababa ninawezapata hisia zenu juu ya hili???

(Teamo please.........spare me)
 
uchungu nafikiri uko kwa wazazi wote MJ1,sema there is an extra connection with mama.......:coffee:
 
Natamani kuchangia ila mimi sio mbaba!!!

Wababa saa hizi sijui wako na familia...au guys night out.....ngoja waje kutuambia kama na wao hua tumbo linawakata pindi chochote kibaya kinapotokea kumhusu mtoto/watoto wao!!!
 
mwanajamii japo sina mtoto naomba niseme.....
i have these weired ideas kwamba my kids will have the best father in the world....
sasa linapokuja suala la uchungu inategemea na what kind of uchungu...but i think no one ambaye atakuwa hana uchungu na damu yake!

"A father is a fellow who has replaced the currency in his wallet with the snapshots of his kids."

labda lets hear from the fathers!
 
Natamani kuchangia ila mimi sio mbaba!!!

Wababa saa hizi sijui wako na familia...au guys night out.....ngoja waje kutuambia kama na wao hua tumbo linawakata pindi chochote kibaya kinapotokea kumhusu mtoto/watoto wao!!!
Pamoja na kuwa kwenye bia ya 6 hapa-post via mobile, mi kama baba mtoto akiwa mgonjwa tunapeana zamu usiku kumhudumia masaa matatu matatu.
 
uchungu wanapata wazazi wote MJ1 ila unaweza ukatofautiana kutokana na wamama wengi wapo karibu zaidi na watoto wao na hivyo kuumia zaidi.
 
Ofcourse baba pia anapata uchungu..., lakini when push comes to shove..., mama ndio mwenye uchungu zaidi...., She is ready to die for her Child...., Hata ukiwa Jambazi vipi am sure ukirudi kwa mama ukajirudi lazima atakusamehe..., Sijui ni kwa nini maybe ni ile attachement ya kukaa kwenye tumbo kwa miezi tisa, kuzaa, kunyonyesha na kumuangalia mtoto mpaka anakua....Therefore mothers (awe binadamu au mnyama) they feel more....

Na huu msemo they meant mzazi as in giving birth na sio mlezi...., kwenye huu msemo baba hayupo kabisa
 
Mi naona Kuna gap kati ya baba na mtoto.
Hivyo Sidhani kama mababa huwa wanasikia uchungu kama wanavyosikia wamama.
 
kuna mtu mmoja amepata mwana wa kiume jana, anaitwa "mtu mmoja" anashangilia kama kichaa, sasa kwa upendo huu utasema baba hana uchungu na mwna? la hasha kuna different roles tu lakini uchungu ni kwa wote muhimu kuna upendo wa kweli wa familia. najua mtu mmoja kwa sasa anajibu safi sana kwa utata huu
 
Pamoja na kuwa kwenye bia ya 6 hapa-post via mobile, mi kama baba mtoto akiwa mgonjwa tunapeana zamu usiku kumhudumia masaa matatu matatu.

Utakua baba mzuri sana.....ila sio akiumwa tu!!Wengine wakiskia mtoto analia badala ya kwenda kumwangalia anamwasha mama kumwambia mtoto analia!!!
 
Uchungu vs upendo?

Mama yupi na baba yupi? Wapo ambao:

1. Mama anatoa mimba(anamuma mtoto), amemzaa anatupa vichakani, au ametelekeza, anampiga mtoto afadhali ya mwizi....
2. Baba amemkana mama wakati wa ujauzito, kule mtoto, au anahangaika na wanawake wengi badala ya kushirikiana na mama kumtunza mtoto, anahangaika na ulevi, ....

To me ni ngumu ku-generalize....
 
Mkuu hata wale wanaotupa watoto ni circumstances zinawabana na sio wengi..., huu msemo upo kuonyesha kwamba uchungu aliopata mama kumleta duniani mtoto ni mkubwa na kuna attachment kubwa..., na hii si kwa binadamu tu, bali viumbe vyote hata ambavyo havina akili..., its nature.
 
umeambiwa mzazi.....yeyote yule hata mjomba au shangazi ilimradi
ndie mzazi wa mtoto huyo.....atakuwa na uchungu na mtoto.....

kwa ufupi mtu yeyote mwenye jukumu na mtoto husika atakuwa na uchungu

kwa lolote baya litakalomfika mtoto......
 
Wote husikia uchungu isipokuwa hutofautiana. Mie nimewahi kushuhudia Baba anabeba jukumu lakulea watoto kuliko mama tena anasikia uchungu ile mbaya. Ndo maana wamesema UCHUNGU WA MWANA AUJUAE MZAZI hawakusema Mama wala Baba
 
umeambiwa mzazi.....yeyote yule hata mjomba au shangazi ilimradi
ndie mzazi wa mtoto huyo.....atakuwa na uchungu na mtoto.....

kwa ufupi mtu yeyote mwenye jukumu na mtoto husika atakuwa na uchungu

kwa lolote baya litakalomfika mtoto......
Kwa tafsiri ya kawaida wazazi ni baba na mama tu hao shangazi/mjomba ni walezi tu.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom