Uchumi wa taifa kuanguka kwa asilimia tano

Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,136
TAASISI ya kimataifa inayojishughulisha na tafiti za Utawala Bora, Jopa ( JPF), imesema taifa litakumbwa na anguko la uchumi la asilimia tano katika mwaka huu wa fedha kutokana na tatizo la umeme nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa JPF, Praygod Mmasi, alieleza hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia utafiti waliofanya katika kipindi cha Januari hadi Machi 31, mwaka huu.
Alisema hali hiyo inatokana na shughuli zote za uzalishaji viwandani na zile za kijamii kuathirika kwa zaidi ya asilimia 75 kutokana na mgawo wa umeme.
Aidha, Mmasi alisema mabadiliko ya hali ya hewa na kushuka kwa thamani ya fedha ya Tanzania kwa zaidi ya asilimia tatu, ni miongoni mwa sababu ambazo zimesababisha mfumuko wa bei wa bidhaa zote za viwandani na vyakula.
Mmasi alisema wakati uchumi wa nchi ukiwa katika hali mbaya kwa kiwango hicho, serikali imekuwa ikitumia zaidi ya sh bilioni saba za bajeti yote ya nchi kwa matumizi ya kawaida ya serikali.
Aliongeza kuwa ni kiasi kidogo cha sh bilioni nne tu kimekuwa kikielekezwa katika shughuli za maendeleo.
Alisema kiini cha matatizo yote ya uchumi na utolewaji wa huduma za kijamii uliopo nchini leo ni matokeo ya anguko la utawala bora Tanzania na kushindwa kuwajibika kwa mamlaka ya wabunge




Source: Tanzania Daima.

Kuna siku za nyuma niliwahi kusema kwamba uchumi wa Tanzania ukuaji wake utakua kwa asilimia 4.5% mwaka huu na waziri wetu wa mapesa akasema uchumi unategemewa kukuwa kwa 7.8%. Je mheshimiwa waziri prediction zake za kukua kwa uchumi sasa ziko asilimia ngapi?
 
Jamani si kuna wakati PM alisema mgao wa umeme hautaathiri uchumi wetu sasa nani mkweli hapa!
 
Serikali yakiri mgawo wa umeme umetikisa uchumi
JIBU LA SWALI LA MBUNGE Viti Maalum

na Mwandishi wetu, Dodoma


amka2.gif
SERIKALI imesema kuwa mgawo wa umeme na mdororo wa uchumi nchini ni moja ya sababu zilizofanya kushuka kwa pato la taifa hasa katika ukusanyaji wa kodi.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Grace Kiwelu, aliyetaka kujua jinsi gani pato la mwananchi mmoja mmoja na pato la taifa lilivyoshuka, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Greyson Teu, alisema mgawo wa umeme umesababisha pato kushuka hasa kwa waliokuwa wakitegemea uzalishaji wao kwa sekta ya umeme.
Teu, alisema pamoja na hali hiyo mwenendo wa makusanyo hasa katika kipindi cha mgawo wa umeme kuanzia Desemba hadi Februari mwaka huu, umekuwa wa kuridhisha bila kuonyesha athari za wazi kulingana na makisio yaliyokusudiwa kukusanywa katika kipindi hiki
Alisema makisio ya makusanyo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na watu binafsi (PAY) pamoja na ushuru wa forodha kwa kipindi cha mwezi Desemba hadi Februari yalikuwa ni sh trilioni 1.24, ambapo makusanyo halisi yalifikia kiasi cha sh trilioni 1.22, sawa na asilimia 98 kwa lengo lililokusudiwa.
Naibu waziri huyo alisema hata hivyo bado kuna ugumu kuhusisha mapato kwa asilimia ya mapato kwa asilimia mbili katika kipindi hicho na mgawo wa umeme.
 
Back
Top Bottom