Uchumba wa Mahesabu

Petu Hapa

JF-Expert Member
Jan 2, 2008
714
55
Jana tulikuwa na mjadala mkali juu ya mambo ya uchumba. Watu wazima walidai vigezo vya kuchagua wachumba vimebadilika sana siku hizi. Zamani, watu walikuwa wanaangalia sana tabia, uzuri, kabila, familia aliyotoka binti na mapenzi kwa ujumla wake. Mara nyingi, mwanaume ndie alikuwa mchaguaji, lakini, kinamama wakapinga wakasema "mwanamke ndio huchagua ama kuamua kwanza, wakadai, kama mwanamke hakutaki hutampata"

Vijana wakadai, uzuri peke yake haulipi wala jina la familia kwa mazingira ya sasa – labda mwanzoni mnapotokeana. Bali, watu mpaka kuamua uchumba maswala ya kiuchumi yanapewa uzito sana siku hizi kwa pande zote mbili, huku maswala ya elimu na ajira ndio kama msingi wa mahusiano.

Duh! ya kweli haya? Yaani mapenzi ya kudumu kuangaliwa kama kitengo cha uchumi?
 
Kwangu mimi msichana akiwa na wowowo na rangi ya kunde anatosha mengine nitavumilia tuuuuu
 
Back
Top Bottom